Thursday, 13 February 2020

AMUUA MKEWE MJAMZITO KWA KUMTENGANISHA KICHWA NA KIWILIWILI

...
Mkazi wa Kijiji cha Mrere wilayani Rombo  mkoani Kilimanjaro Anthony Asenga (33), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji ya mkewe, Happiness Sianga aliyekuwa na ujauzito unaokadiriwa kuwa wa miezi minane.

Asenga anatuhumiwa kumuua mwanamke huyo kwa kutenganisha kiwiliwili na kichwa chake usiku wa kuamkia jana na kisha akajisalimisha katika Kituo cha Polisi cha Mashati.

Tukio hilo limeacha simanzi katika kijiji hicho na Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Salum Hamduni amesema wanamshikilia mtu huyo wakimuhusisha na mauaji hayo.

“Ni kweli kuna tukio la mume kumuua mke wake huko Rombo. Tunamshikilia mtuhumiwa,” alisema Kamanda Hamduni.

“Uchunguzi unaendelea na utakapokamilika hatua nyingine za kisheria zitafuata.”

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sembalo, Kijiji cha Mrere, Faustina Urassa alisema wanandoa hao waliwahi kugombana na kutengana kwa muda mrefu, na kwamba siku ambayo tukio limetokea ndiyo waliyopatana na kuanza kuishi tena pamoja.
Via Mwananchi
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger