Friday, 7 February 2020

Tanzania Yaishauri Ethiopia Kutafuta Kiini Cha Raia Wake Kukimbia Nchini Humo

Tanzania imeishauri Nchi ya Ethiopia kuchukua hatua ya kuchunguza kiini cha raia wake kuondoka nchini humo kinyume na utaratibu na kwa njia zisizo halali jambo linalosababisha   mrundikano wa wafungwa ambao wanakamatwa katika nchi wanazopita kama wahamiaji haramu ikiwemo Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ametoa ushauri huo Addis Ababa Ethiopia anakohudhuria mkutano wa 33 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika na kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia kando ya mkutano huo Dkt. Workneh Gebeyehu na ili kuchukua hatua za kudhibiti idadi ya raia wake wanaoondoka nchini humo na kukamatwa katika mataifa mengine Tanzania ikiwemo.

Prof. Kabudi amesema Mpaka sasa takribani raia zaidi ya 1,300 wanashikiliwa katika magereza mbalimbali nchini Tanzania huku idadi ya wanaoendelea kukamatwa ikiongezeka jambo linalosababisha mrundikano wa wafungwa katika magereza ya nchi hiyo.

Ameongeza kuwa katika mazungumzo hayo Tanzania na Ethiopia zimekubaliana kuchukua hatua za pamoja zitakazowezesha kurejeshwa wafungwa na wahamiaji haramu wanchi hiyo wanaoshikliwa Tanzania kwa utaratibu utakaokubalika baada ya majadiliano ya kina na kitaalamu.

Akizungumza kupitia kwa msemaji Waziri wa mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt. Workneh Gebeyehu amekiri kuwepo kwa tatizo la vijana wanchi yake kuondoka nchini humo kinyume cha utaratibu na kuitumia Tanzania kama mapito wakielekea katika nchi za kusini mwa Afrika na Ulaya na kuongeza kuwa serikali ya nchi hiyo itachukua hatua madhubuti kukabiliana na hali hiyo.

Pia ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano wake katika suala la wahamiaji haramu kwa kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu raia wa Ethiopia wanaoshikiliwa Tanzania na kwamba wana imani kuwa mazungumzo yatakayofanyika yatasaidia kuwarejesha raia hao nchini Ethiopia kwa njia ya pamoja watakayokubaliana.

Kando na masuala hayo ya wahamiaji haramu pia Prof. Kabudi na Dkt. Workneh wamezungumzia masuala mbalimbali ya mashirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia ikiwa ni pmaoja na mashirikiano katika masuala ya anga,miundombinu na ubadilishanaji wa utaalamu kuhusu ujenzi wa mabwawa ya umeme ili kuziwezesha nchi hizo kupiga hatua za kimaendeleo katika nyanja ya Uchumi.


Share:

Programme Office (Labour Migration) Job vacancy at International Organization for Migration

Position Title : Programme Office (Labour Migration) Duty Station : Arusha, Tanzania, United Republic of Classification : Professional Staff, Grade P2 Type of Appointment : Special short-term graded, Six months with possibility of extension Estimated Start Date : As soon as possible Closing Date : 16 February 2020 Established in 1951, IOM is a Related Organization of the United Nations, and as the leading UN… Read More »

The post Programme Office (Labour Migration) Job vacancy at International Organization for Migration appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Wizara Ya Afya Yakanusha Uwepo wa Mtu Anayeshukiwa Kuwa na Virusi Vya Corona Nchini




Share:

Basi la kampuni ya Premier lagongana na lori

Basi la kampuni ya Premier linalofanya safari zake kati ya Mwanza na Mbeya limegongana uso kwa na lori lenye namba za usajili T486 ANU ambalo lilikuwa likivuta tela lenye namba T 775 APT.

Daktari wa Kitengo cha Dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya Dakta Olivia Masoi amethibitisha kupokea majeruhi 10 wa ajali hiyo, ambapo amesema watu 2 waliodhaniwa kuwa wamekufa katika eneo la Ajari wako hai


Share:

Human Resources for Health (HRH) Lead Job at ICAP Tanzania

Deadline Date: Tuesday, 31 March 2020 Organization: ICAP Country: United Republic of Tanzania Position Summary: The Human Resources for Health (HRH) Lead will provide strategic leadership, guidance, and expertise for technical support for all HRH-related activities for ICAP’s proposed CDC-funded project Technical Assistance to Government of Tanzania (GOT) and Public Health Institutions (PHIs) toward Sustained Health Systems Strengthening… Read More »

The post Human Resources for Health (HRH) Lead Job at ICAP Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MOI Yaleta Mitambo Ya Kisasa Ya Upasuaji Ubongo Bila Kufungua Fuvu

NA ANDREW CHALE
SERIKALI ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kwa dhati kuboresha Sekta ya Afya nchini na tayari imeleta mitambo ya kisasa ya Maabara ya upasuaji wa Ubongo bila kufungua fuvu (Angio Suite).

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Taasisi ya Mifupa (MOI), Patrick Mvungi ameeleza kuwa mitambo hiyo imewasili Nchini ikitokea Ujerumani ambapo ni juhudi za Serikali ya kuona wanasogeza huduma za kibingwa hapa nchini.

“Mitambo ya Maabara ya upasuaji wa Ubongo bila kufungua fuvu (Angio Suite) imewasili bandari ya Dar es salaam.

Mitambo, Vifaa vingine pamoja na ukarabati wa Chumba vimegharamiwa na Serikali kwa gharama ya Tsh Bilioni 7.9.” Alisema mkuu wa kitengo cha Uhusiano MOI, Patrick Mvungi.

Na kuongeza kuwa ujio wa mitambo hiyo ya upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu itakuwa msaada mkubwa kwa wananchi na mataifa mengine hapa Barani Afrika wanaofika MOI kwa ajili ya matibabu.

“Taasisi ya Mifupa-MOI pia tunatoa huduma mbalimbali za kibingwa na kibobezi zikiwemo; Upasuaji wa Kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye Ubongo, Upasuaji wa Mgongo kwa kufungua eneo dogo.

Zipo pia huduma za Upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu, Upasuaji wa kupandikiza nyonga bandia, Upasuaji wa kupandikiza goti bandia na Upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo alieleza Mkuu wa kitengo cha Uhusiano MOI, Patrick Mvungi.

Huduma hizo na nyingine katika taasisi hiyo zimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi na mataifa mengine barani Afrika ambapo awali walikuwa wakizifuata nje ya Nchi.


Share:

Majeshi ya Syria yaingia kwenye mji muhimu licha ya Vitisho vya Uturuki

Vikosi vya serikali ya Syria vimeingia kwenye mji wa kimkakati wa Saraqeb ambao ulikuwa ngome ya mwisho ya waasi, baada ya mapambano makali na wapiganaji wa upinzani. 

Operesheni za vikosi vya Rais Bashar al-Assad kwenye miji na vijiji vya kaskazini magharibi mwa jimbo la Idlib zimesababisha zaidi ya watu laki tano kukosa makaazi kwa zaidi ya miezi miwili, hali inayozidisha janga la kibinaadamu kwenye ukanda huo wenye wakimbizi wa ndani.

Hatua hiyo imeikasirisha Uturuki na kuhatarisha kuzuka mapambano ya kijeshi kati ya majeshi ya Uturuki na Syria. 

Mji wa Saraqeb ulioko karibu na mpaka wa Uturuki, umekuwa kitovu cha mapambano makali kwa siku kadhaa. 

Wakati huo huo, wizara ya mambo ya nje ya Urusi, imesema kuwa ujumbe wa nchi hiyo kesho utaelekea Uturuki kwa ajili ya kuijadili hali katika jimbo la Idlib.


Share:

Corporate Sales Executive Job at Britam Mtwara, Tanzania

Corporate Sales Executive Job at Britam Mtwara, Tanzania The job holder will be responsible for the growth of revenues for the branch to meet set annual premium targets for the branch. The role will report to the Branch Manager. Secure new business directly or through intermediaries Service existing business and follow up to ensure renewal Maintain excellent customer… Read More »

The post Corporate Sales Executive Job at Britam Mtwara, Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Human Resources Officer Job at Dar es Salaam Merchant Group (DMG)

Human Resources Officer at Dar es Salaam Merchant Group (DMG)     For extensive Information: https://ift.tt/2S9Y22x

The post Human Resources Officer Job at Dar es Salaam Merchant Group (DMG) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Programme Management Specialist – Consultant – Dar es Salaam at UN Women Tanzania

Programme Management Specialist – Consultant – Dar es Salaam at UN Women Tanzania   Background Grounded in the vision of equality enshrined in the Charter of the United Nations, UN Women works for the elimination of discrimination against women and girls; the empowerment of women; and the achievement of equality between women and men as partners and beneficiaries… Read More »

The post Programme Management Specialist – Consultant – Dar es Salaam at UN Women Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Download App Yetu Kwenye Simu Yako Ili Uweze Kupata Habari Zetu Kwa Haraka Zaidi

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.



Share:

Serikali kuwarejesha Wafungwa wa kigeni nchini mwao

Serikali inafanya mazungumzo na Serikali ya Ethiopia ili kuona namna ya kuwarejesha nchini mwao Wahamiaji 1, 415 ambao wanatumikia kifungo katika magereza mbalimbali hapa nchini.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria nchini, Siku inayoashiria kuanza kwa shughuli za Mahakama kwa mwaka huu.

Rais Magufuli amesema kuwa baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo, atasaini hati ya kuachiwa kwa Wafungwa hao raia wa kigeni ili waweze kurejea nchini mwao.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, lengo la hatua hiyo ya Serikali ni kupunguza msongamano katika magereza mbalimbali hapa nchini.


Share:

Kiongozi wa Al-Qaeda Nchini Yemen , Qasim al-Raymi auawa na shambulio la Marekani

Marekani imemuua kiongozi wa Al-Qaeda katika eneo la Rasi ya uarabuni, Rais Donald Trump ameeleza.

Qasim al-Raymi aliyeongoza kikundi cha Jihad tangu mwaka 2015, aliuawa wakati wa operesheni ya majeshi ya Marekani nchini Yemen, Ikulu ya Marekani imeeleza.

Kiongozi wa wapiganaji wa Jihad amekuwa akihusishwa na mfululizo wa mashambulizi dhidi ya maslahi ya nchi za Magharibi katika miaka ya 2000.

Alichukua madaraka ya uongozi baada ya mtangulizi wake kuuawa kwa shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani.

Kundi hilo la AQAP liliundwa mwaka 2009 kutokana na matawi mawili ya Al-Qaeda nchini Yemeni na Sausi Arabia, ikiwa na nia ya kuangusha tawala za serikali zinazoungwa mkono na Marekani na kuondoa ushawishi wa nchi za Magharibi kwenye ukanda huo.

Tetesi kuhusu kifo cha al- Raymi kwa shambulizi la Marekani zilianza kusambaa mwishoni mwa mwezi Januari. Katika kujibu hilo kundi hilo lilitoa ujumbe wa sauti ukiwa na sauti ya al -Raymi tarehe 2 mwezi Februari ukisema kuwa wao ndio waliotekeleza shambulio la risasi kwenye kambi ya jeshi la wana maji wa Marekani huko Pensacola, Florida.

Shambulio hilo lilifanyika mwezi Desemba, na ujumbe huo huenda ulirekodiwa mapema.

Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani sasa imethibitisha kifo cha al-Raymi lakini haijasema aliuawa lini.

''Kifo chake kinaendelea kudhoofisha kundi la AQAP na shughuli za kundi la al-Qaida, na inatufanya tuendelee kukaribia kuondosha vitisho vya makundi haya yanayohatarisha usalama wa taifa,'' taarifa ilisomeka.

''Marekani, maslahi yetu na washirika wetu wako salama kutokana na kifo chake''.


Share:

Makondo Ataka Mabadiliko Ya Kiutendaji Wizara Ya Ardhi

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo amewataka watumishi wa sekta ya ardhi katika Wizara hiyo kushirikiana ili kuibadilisha Wizara na kuwa na utendaji bora utakaokidhi mahitaji ya wananchi.

Makondo alisema hayo jana wakati akizungumza na watumishi wa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipowasili kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.

Makondo alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Dorothy Mwanyika aliyestaafu kwa mujibu wa Sheria. Kabla ya Uteuzi huo Makondo alikuwa Kamishna wa Ardhi kwenye Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Alisema, mategemeo ya watumishi wa Wizara ya Ardhi mara baada ya kuteuliwa kwake ni makubwa lakini msisitizo wake ni watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kwa kujituma ili kuweza kuibadilisha Wizara.

‘’Kauli ya Wizara kuwa ina ‘madudu’ siyo nzuri hivyo tukimbie ili tuwe na sekta ya ardhi iliyobadilika’’ alisema Makondo.

Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitaka kuthaminiwa kwa mchango wa kila mtumishi wa Wizara hiyo kwa kuwa ndiyo njia pekee itakayoleta mabadiliko na mafanikio ya utendaji kazi wa sekta hiyo.

Kwa mujibu wa Makondo, Kampuni ya utengenezaji magari ya Toyota imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye biashara zake kutokana na kutumia mfumo wa Kaizen unaothamini mchango wa kila mmoja katika utendaji kazi.

Makondo amewataka pia watumishi wa Wizara ya Ardhi kuweka miakakati ya pamoja kwa lengo la kuibadilisha wizara hapo ilipo ili kuonesha kuwa wizara hiyo imebadilika katika utendaji wake.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi walioneshwa kufurahishwa na uteuzi wa Katibu Mkuu huyo kwa kuwa ametokea Wizara hiyo na anaijua sekta ya ardhi vizuri pamoja na watumishi wake.


Share:

Serikali Kuboresha Skimu za Umwagiliaji za Wakulima Wadogo (Small Scale Irrigation Development Project -SSIDP)

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali inatekeleza Mradi wa Kuendeleza Skimu za Umwagiliaji za Wakulima Wadogo (Small Scale Irrigation Development Project -SSIDP) ikiwa ni pamoja na Skimu ya Umwagiliaji ya Nyida.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo Bungeni tarehe 6 Februari 2020 Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe Azza Hilaly Hamad aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itachimba bwawa kwa ajili ya kuboresha Mradi wa Umwagiliaji Nyida?

Mhe Mgumba amesema muwa katika kutekeleza Mradi huo, Kampuni ya Shekemu Construction Ltd inafanya kazi ya ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya kuboresha mfumo wa usambazaji maji mashambani ambapo utekelezaji wa Mradi huo kulingana na Mkataba umefikia asilimia 68 ya kazi zote za ujenzi.
Ameongeza kuwa hadi kufikia mwezi Disemba 2019 jumla ya Tsh. 282, 154,880.68 zimelipwa kwa Mkandarasi kati ya Tsh 466,594,981.81 zilizotengwa kwa ajili ya kuendeleza Skimu ya Nyida.

Hata hivyo Mradi huo kwa sasa umesimama kupisha msimu wa kilimo kwa wakulima na mvua zinazoendelea kunyesha. Hivyo, Mkandarasi ataendelea na kazi iliyobakia kulingana na Mkataba mara baada wakulima kuvuna mazao yao na Msimu wa mvua kumalizika.

Mhe Mgumba amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi na mvua zisizotabirika pamoja na wakulima kuwa na mwamko mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji wa kutaka kuongeza uzalishaji, tija kwa kulima misimu miwili kwa mwaka na kwa kuzingatia kuwa chanzo cha maji cha skimu hiyo ni mto Manonga ambao ni wa msimu na hivyo Serikali iliona umuhimu wa ujenzi wa Bwawa ili kuendeleza skimu hiyo.

Aidha, ili kutekeleza mradi huo, mwaka 2013 Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya ya Shinyanga na Nzega zilifanya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa awali kwenye eneo linalokusudiwa kujengwa bwawa la Nyida eneo la Lyamalagwa litalokuwa na uwezo wa kumwagilia maji mita za ujazo 4,167,825 na gharama ya shilingi 3.5 bilioni kwa wakati huo.

Kadhalika, Kutokana na mabadiliko ya kimuundo ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, na miradi mingi ya umwagiliaji kujengwa chini ya kiwango, Serikali haikuweza kutekeleza mradi huo kwa wakati kutokana kufanya tathmini ya kina ya ufanisi ya miradi hiyo na hivyo kushindwa kutekeleza mradi kwa wakati.

Aidha, kwa kuwa muda mrefu umepita tangu tahtmini hiyo ifanyikke, Serikali itafanya mapitio upya ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili kupata mahitaji na gharama halisi ya ujenzi wa bwawa na athari zake kwa sasa.

MWISHO


Share:

Bashe: Marekebisho Ya Sheria Ya Vyama Vya Ushirika Kutua Bungeni

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Wizara ya Kilimo ipo katika hatua za mwisho  kupeleka Bungeni mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya Maendeleo ya Ushirika yatakayoendana na mahitaji ya sasa ambayo yatahusisha mabadiliko ya mfumo na muundo wa uongozi  ili kuendana na mahitaji ya  teknolojia  na kuleta ushindani wa kibiashara.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma tarehe 6 Februari 2020 wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Mbinga vijijini  Mhe Martini Mtonda Msuha aliyetaka kufahamu serikali ina mpango gani wa kurekebisha Sheria ya Vyama vya ushirika ili kuondoa mapungufu yaliyopo, hususani kwa upande wa uanachama na kuipa serikali nguvu za kisheria juu ya Vyama vya ushirika.

Bashe amesema kuwa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2015 – 2020 (Ibara ya 22 (g)(iv) na 86 (a­­­) inaelekeza  “Kuifanyia mapitio Sera ya Vyama vya Ushirika na kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Ushirika na upatikanaji wa takwimu zitakazosaidia kuandaa mipango na kuleta mageuzi katika Sekta ya Ushirika na kuimarisha uchumi wa Taifa na Kuviimarisha vyama vya ushirika kuwa na uwezo wa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ya ndani na nje kwa kuweka mfumo madhubuti wa ukusanyaji, uchambuzi na uenezaji wa taarifa za masoko na kutoa elimu juu ya uongezaji thamani na biashara“

Amesema kuwa Ushirika ni dhana ya hiari, lakini Serikali ni  msimamizi mkuu wa vyama vya ushirika pale ambapo viongozi wake au vyama vyenyewe havitekelezi malengo yaliyokusudiwa na dhamira ya kuanzishwa kwa sekta ya ushirika.

Serikali inakiri vyama vinakabiliwa na changamoto za kiutendaji, usimamizi, viongozi kutokuwa waadilifu na mapungufu ya kimfumo ya uendeshaji wa vyama vya Ushirika hapa nchini.

Hata hivyo, Bashe amesema vipo baadhi ya vyama vya ushirika ambavyo vinafanya vizuri. Mfano, Chama cha Ushirika cha Chai Mkonge, Mafinga na Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU).

Kadhalika Mhe Bashe ameongeza kuwa Ushirika ndicho chombo cha kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi kwa kuwaunganisha wakulima ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kutoa huduma za ugani, upatikanaji wa pembejeo na kutafuta masoko ya mazao.

MWISHO


Share:

Rais Magufuli Akerwa na Wapelelezi Kuchelewesha Kesi za Watu

Rais John Magufuli amesema wapelelezi wa kesi na wasimamizi wa sheria nchini wanawaumiza mahabusi wengi kutokana na kuchelewa kukamilisha kazi kwa wakati.

Amesema wapelelezi wa kesi ni chanzo cha watu kuwekwa kwenye magereza bila hatia yoyote, huku wengine wakiwekwa mahabusi kutokana na shinikizo la matajiri.

Aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria iliyokuwa na kaulimbiu, Uwekezaji na biashara: Wajibu wa Mahakama na wadau kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji.

Kutokana na hali hiyo, Rais Magufuli aliwataka viongozi wa dini nchini kuwaombea wapelelezi wanaofanya vitendo hivyo wapate laana.

Alisema idadi ya wafungwa waliopo katika magereza nchini ni ndogo kulinganisha na mahabusi waliopo, ambayo alitaja wafungwa ni 13,455 wakati mahabusi ni 17,632.

Alisema idadi ya mahabusi walioachiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) baada ya kubainika kubambikiziwa kesi ni 1,422.

“Lakini niwaombe ndugu zangu wapelelezi, ufalme wa mbinguni utakuwa shida kwenu msipotubu kwa Mungu, kwa sababu roho za wasiokuwa na hatia zinaangamia kule, mnawapa shida sana mahakimu na majaji na roho za watu, ninawaambia ukweli mtaenda kuyalipa badilikeni,” alisema Rais Magufuli na kuongeza:

“Mimi nimeshuhudia ukienda kwenye magereza yetu watu wanalia na wengine ni kesi za kusingiziwa, wapo wengine wamewekwa kule ndani kwa sababu ya matajiri kwamba ni akukomeshe utaenda kwanza mahabusu,” alisema Rais Magufuli.

“Roho za watu wasiokuwa na hatia zinaangamia kule gerezani na wala msiwasingizie majaji na mahakimu kwa sababu hamuwapelekei na saa nyingine hata kupelekwa mahakani ni lazima uhonge ili kesi yako isomwe, mnawapa shida mahakimu na majaji ninawaambia ukweli mtakwenda kuyalipa badilikeni.”

Rais Magufuli alisema idadi ya wafungwa waliosamehewa katika kipindi cha miaka minne ni 38,801 na baadhi yao walikuwa na kifungo cha maisha.

Alisema kwa sasa serikali iko katika mazungumzo ya kuwarejesha wafungwa raia wa kigeni wakiwamo kutoka Ethiopia 1,451 ili warudi kwao.

“Tunafanya mazungumzo na ninafikiri nitasaini hati mapema ndani ya siku mbili tatu ili hawa wafungwa waweze kurudishwa kwao na hii pia itatusaidia kupunguza wafungwa wanaokaa mahakamani,” alisema Rais Magufuli.

Kadhalika, alisema miongoni mwa kero ambazo alizipokea kipindi cha kampeni mwaka 2015 ni pamoja na wananchi wengi kulalamika ucheleweshaji wa kesi, kukithiri kwa vitendo vya rushwa, ubambikizaji wa kesi, ucheleweshaji wa upelelezi.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger