Friday, 7 February 2020

Kiongozi wa Al-Qaeda Nchini Yemen , Qasim al-Raymi auawa na shambulio la Marekani

...
Marekani imemuua kiongozi wa Al-Qaeda katika eneo la Rasi ya uarabuni, Rais Donald Trump ameeleza.

Qasim al-Raymi aliyeongoza kikundi cha Jihad tangu mwaka 2015, aliuawa wakati wa operesheni ya majeshi ya Marekani nchini Yemen, Ikulu ya Marekani imeeleza.

Kiongozi wa wapiganaji wa Jihad amekuwa akihusishwa na mfululizo wa mashambulizi dhidi ya maslahi ya nchi za Magharibi katika miaka ya 2000.

Alichukua madaraka ya uongozi baada ya mtangulizi wake kuuawa kwa shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani.

Kundi hilo la AQAP liliundwa mwaka 2009 kutokana na matawi mawili ya Al-Qaeda nchini Yemeni na Sausi Arabia, ikiwa na nia ya kuangusha tawala za serikali zinazoungwa mkono na Marekani na kuondoa ushawishi wa nchi za Magharibi kwenye ukanda huo.

Tetesi kuhusu kifo cha al- Raymi kwa shambulizi la Marekani zilianza kusambaa mwishoni mwa mwezi Januari. Katika kujibu hilo kundi hilo lilitoa ujumbe wa sauti ukiwa na sauti ya al -Raymi tarehe 2 mwezi Februari ukisema kuwa wao ndio waliotekeleza shambulio la risasi kwenye kambi ya jeshi la wana maji wa Marekani huko Pensacola, Florida.

Shambulio hilo lilifanyika mwezi Desemba, na ujumbe huo huenda ulirekodiwa mapema.

Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani sasa imethibitisha kifo cha al-Raymi lakini haijasema aliuawa lini.

''Kifo chake kinaendelea kudhoofisha kundi la AQAP na shughuli za kundi la al-Qaida, na inatufanya tuendelee kukaribia kuondosha vitisho vya makundi haya yanayohatarisha usalama wa taifa,'' taarifa ilisomeka.

''Marekani, maslahi yetu na washirika wetu wako salama kutokana na kifo chake''.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger