Friday, 7 February 2020

Majeshi ya Syria yaingia kwenye mji muhimu licha ya Vitisho vya Uturuki

...
Vikosi vya serikali ya Syria vimeingia kwenye mji wa kimkakati wa Saraqeb ambao ulikuwa ngome ya mwisho ya waasi, baada ya mapambano makali na wapiganaji wa upinzani. 

Operesheni za vikosi vya Rais Bashar al-Assad kwenye miji na vijiji vya kaskazini magharibi mwa jimbo la Idlib zimesababisha zaidi ya watu laki tano kukosa makaazi kwa zaidi ya miezi miwili, hali inayozidisha janga la kibinaadamu kwenye ukanda huo wenye wakimbizi wa ndani.

Hatua hiyo imeikasirisha Uturuki na kuhatarisha kuzuka mapambano ya kijeshi kati ya majeshi ya Uturuki na Syria. 

Mji wa Saraqeb ulioko karibu na mpaka wa Uturuki, umekuwa kitovu cha mapambano makali kwa siku kadhaa. 

Wakati huo huo, wizara ya mambo ya nje ya Urusi, imesema kuwa ujumbe wa nchi hiyo kesho utaelekea Uturuki kwa ajili ya kuijadili hali katika jimbo la Idlib.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger