Wednesday, 4 December 2019

Breaking : SUMAYE AJIONDOA CHADEMA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye amejiondoa Chadema.

Amesema ni baada ya kutafakari kwa kina na kuona wakubwa wamewashawishi watu wa Kanda ya Pwani kumpigia kura ya Hapana
-
Ametangaza kuwa hajiungi na chama chohote ila yupo tayari kutoa ushauri kwa chama chochote hata CHADEMA akihitajika
Share:

LIVE: Sumaye Anaongea Na Waandishi Wa Habari

LIVE:  Sumaye Anaongea Na Waandishi Wa Habari


Share:

Biteko Alia Na Upungufu Wa Madini Ya Chumvi Viwandani

Na Issa Mtuwa – Dodoma
Upungufu wa madini ya Chumvi kwenye viwanda vya chumvi hapa nchini unamsikitisha waziri wa madini Doto Biteko kutokana na uwepo wa mahitaji (soko) makubwa ya wanunuzi wa madini hayo huku madini hayo yakiwa  hayapatikani kwa wingi kutosheleza mahitaji kutokana na uzalishaji mdogo kutoka kwa wachimbaji wa madini hayo huku wanunuzi wakikosa madini hayo.

Akiongea  tarehe 03/11/2019 ofisi kwake Mtumba jijini Dodoma wakati wa kikao chake na wamiliki wa kampuni wa viwanda vikubwa vya chumvi  hapa nchini Neelkanth Lime anaemiliki; Neelkanth Lime (T) Ltd, Neelkanth Salt(T) Ltd na Rushabh Investment (T) Ltd, Biteko amesema, anasikitishwa na ukosefu mkubwa wa madini hayo huku akiambiwa kuwa kiasi kikubwa cha  chumvi kinachotumika hivi sasa ni kutoka nje ya nchi kutokana uzalishaji mdogo uliopo hapa nchini.

 “Siku zote huwa naumia sana kuona bidhaa au kitu chochote kinacho husiana na sekta yangu (Madini) kikiingizwa kutoka nje wakati uwezo wa upatikanaji wa kitu hicho upo hapa nchini. Kuna wakati tulilazimika kuzui uingizaji wa makaa ya mawe kutoka nje ili kuyapa nguvu masoko ya ndani na leo makaa yam awe yanathamani kubwa. Leo Madini ya Chumvi yanakosekana kwenye viwanda, niseme ukweli naumia sana moyoni.” Alisema Biteko.

Kwa upande wa uongozi wa  Neelkanth Lime (T) wakiongozwa na Ahmed Said Meneja Mkuu akiwa na Rashid Ahmed Mkurugenzi ambao ni wanunuzi wakubwa wa madini ya nchumvi wamesema wanahangaika kupata idadi kubwa ya madini hayo ili kukidhi mahitaji yao hasa kwenye kiwanda chao kilichopo wilayani Mkuranga huku wakiwa wamepandisha bei ya kununua madini hayo hadi Tshs. 160,000/= kwa tani lakini bado mahitaji ni madogo.

“Mhe. Waziri tunahangaika sana kupata haya madini, sisi tumekwenda kila mahali, Lindi, Mtwara na hata hivi majuzi tulikuwa Tanga na tumefanya kikao na wazalishaji wa madini hayo kwenda kuongeza hamasa ya uzalishaji. Nikupe taarifa njema, kuanzia mwezi Februali mwaka huu kiwanda chetu kimeanza kuchakata  tani 1000 kwa siku.” Alisema Rashid Ahmed.

Ahmed, ameongeza kuwa mpaka sasa wastani wa 70% ya chumvi tunayoitumia ni kutoka nje kutokana na upungufu wa uzalishaji wa madini uliopo hapa nchini. Ameongeza kuwa wao wapo teyari kuwaweka wazilishaji wa chumvi kwenye vikundi vidogo vidogo waweze kuunganisha nguvu ili wazalishe kwa wingi huku wakiwawezesha kwa mikopo kama walivyo kufanya huko Mkuranga huku wakimiliki shamba lao la chumvi lenye hekari 2000.

Kutokana na kauli hiyo, kama kawaida Biteko kwa staili ile ile ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli “papo kwa papo” aliinua simu na kumpigia mwenyekiti wa Chama cha Wavunaji Chumvi Tanzania Habib Nour akitaka kuthibitisha kama kweli kuna upungufu wa uzalishaji wa madini ya chumvi na mwenyekiti huyo akapatikana na akamuwekwa “hewani” moja kwa moja mbele ya kikao.

Bila kung’ata maneno, Habib alikiri na kumwambia Waziri kuwa ni kweli kuna upungufu mkubwa wa uzalishaji wa madini ya chumvi hapa nchini huku juhudi za kimkakati wa kuongeza uzalishaji zinaendelea.

Kutokana na hali hiyo Waziri Biteko ametoa wito kwa wachimbaji hasa wadogo kuongeza uzalishaji wao huku akiwasisitiza kukaa kwenye vikundi ili iwe rahisi kupata mikopo kwa ajili ya mtaji ili waweze kuzalisha na kukidhi mahitaji huku  Neelkanth Lime(T) wakisema wako teyari kutekeleza ushauri uliotolewa na Waziri katika kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa mikopo kweye vikundi vyao.


Share:

Wizara Ya Kilimo Yasisitiza Ulazima Wa Kuwa Na Viwanda Vya Mbolea Nchini

 Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro
Serikali imesema kuwa inathamini sana mchango wa Sekta binafsi katika kukuza uchumi kwani ndio chanzo kikubwa cha Pato la Taifa kutokana na mchango wake kupitia kodi, ushuru na tozo mbalimbali.

Kilimo ni moja ya Sekta zinazoongoza kwa ushiriki wa sekta binafsi. Wakulima wote ni sekta binafsi. Ukiondoa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), wafanyabiashara wote wa mazao ya Kilimo ni sekta binafsi.

Aidha, wauzaji wote wa mbolea isipokuwa kampuni ya mbolea Tanzania (TFC) ni sekta binafsi. Vile vile, viwanda vyote 13 vinavyotengeneza mbolea (Fertilizer) na visaidizi vya mbolea (Fertilizer supplements)  vinamilikiwa na sekta binafsi.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 3 Disemba 2019 wakati akifungua kikao kazi cha wadau wa mbolea chenye lengo la  Kuweka Mikakati ya Kutumia Fursa za Uwekezaji katika Viwanda vya Mbolea Nchini kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es salaam.

Mhe Hasunga amesema kuwa ili kuongeza tija katika sekta ya kilimo ni dhamira ya serikali kuhakikisha kuwa inaanzisha viwanda mbalimbali nchini huku akisema kuwa kwa Wizara ya Kilimo msukumo maalumu ni kuhakikisha kuwa viwanda vya kuzalisha mbolea vinaanzishwa hapa nchini.

Amesema kuwa Tanzania ina viwanda 10 vya mbolea ambavyo hutengeneza virutubisho vya aina mbalimbali kwa ajili ya mimea kama vile (Nitrogen - N, Phosphorus - P, Potassium - K, NP, NK, PK, NPK n.k.)

Amesema baadhi ya wafanyabashiara walioko nchini wana mitambo ya kuchanganyia mbolea (Fertilizer Blending) ili kupata aina za virutubisho mahsusi kwa ajili ya mazao (Crop Specific Fertilizer Catalogues) na pia kuwekewa visaidizi vya mbolea kwa ajili ya kurekebisha afya ya udongo (Soil Specific Fertilizer Catalogues).

Amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa viwanda vitatu vya visaidizi vya mbolea (Calcium/gypsum n.k.) ambavyo hutumika kurekebisha hali ya  udongo ili mbolea ichukuliwe vizuri na mmea (optimal fertilizer uptake). Hata hivyo, uzalishaji wa viwanda hivi bado ni mdogo na hivyo kutokidhi mahitaji makubwa ya mbolea Nchini kwetu.

Ili kuimarisha upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kuwa na bei rafiki kwa wakulima ni lazima kuongeza uwezo wa viwanda vya mbolea, viwanda vya visaidizi vya mbolea na mitambo ya kuchanganyia mbolea ili viwe na uwezo wa kutosheleza mahitaji ya wakulima nchini.

Pia amesema inatakiwa kujenga viwanda vipya vya mbolea, viwanda vya visaidizi vya mbolea na mitambo ya kuchanganyia mbolea ili viwe na uwezo wa kutosheleza mahitaji ya wakulima.

Zingine ni kuweka mkakati wa miaka mitano wa kupunguza au kuondoa kabisa uagizaji wa mbolea kutoka nje ya nchi; kuweka mkakati wa miaka miaka mitano wa kupunguza bei ya mbolea kwa mkulima kutokana na utengenezaji wa mbolea ndani ya nchi; na Kuweka mkakati wa kuongeza uuzaji wa mbolea nje ya nchi ili kutosheleza mahitaji ya Nchi hizo na kuiongezea Serikali pato la fedha za kigeni.

Pia, Taasisi zinazotoa huduma kwenye tasnia ya mbolea (fedha, utafiti, elimu, usafirishaji, nishati, vyama vya ushirika) kuweka mkakati wa kuhakikisha kwamba zinaweka mazingira wezeshi ya uwekezaji katika viwanda vya mbolea.

Mhe Hasunga amesema kuwa pamoja na hayo lakini pia Asasi za kiraia (AZAKI) zinatakiwa kuwa mstari wa mbele kufuatilia na kuona kwamba wadau wote wanashiriki katika mchakato wa kuhakikisha viwanda vya mbolea vinakuwepo nchini.

Kadhalika amesema kuwa hizi sio zama za kusubiri matamko ya Serikali na kuanza kuyakosoa bila kupendekeza majawabu. AZAKI zinatakiwa kuwa sehemu ya kutafuta majawabu badala ya kutafuta changamoto bila kutafuta au kupendekeza majawabu.

MWISHO


Share:

Bodi Ya Uratibu Wa Ngos Yatoa Maagizo Mazito Kwa Baraza La NGOs

Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam
Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini imeliagiza Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kukutana ili kuhakikisha wanatatua changamoto za uendeshaji wa Baraza hilo kikamilifu na kutoa taarifa kwa Bodi ndani ya siku 14 jinsi walivyoshughulikia changamoto hizo, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Baraza hilo.

Agizo hilo limetolewa jana  jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Richard Faustine Sambaiga wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kilicholenga kutoa maelekezo mahsusi kwa Baraza ili kukitaka chombo hicho kuzingatia matakwa ya kisheria katika uendeshaji wake.

Dkt. Sambaiga ameliagiza Baraza hilo kufanya mapitio ya Kanuni ya Sheria ya marekebisho Na. 11/2005 na Sheria ya marekebisho Na.3/201 ili kuweza kukidhi mapendekezo ya mapitio ya Kanuni hizo na kuwasilisha kwenye Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ndani ya siku 30 ili kuondoa mkwamo wa kiutendaji wa majukumu ya Baraza la NGOs nchini.

Pia Dkt. Sambaiga ameliagiza Baraza hilo kujielekeza kwenye matakwa ya muda wa kisheria wa kuwa kiongozi wa Baraza hilo ambao ni miaka mitatu toka kuteuliwa kwa Baraza mwaka 2016, na hivyo kuelekeza kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa Baraza jipya ndani ya siku 30.

“Nalielekeza Baraza kupitia upya uwakilishi wa wajumbe wa Mikoa na makundi maalum hasa ikizingatiwa ipo Mikoa mipya na makundi ambayo hayana wawakilishi kwani kumekuwa na changamoto kubwa ya uwakilishi wa wajumbe kutoka mikoani” alisema.

Aidha Dkt. Sambaiga amewataka Viongozi wa Baraza la Taifa kuzingatia uwasilishaji wa taarifa yake ya utekelezaji wa kazi zake kwa Bodi ili kutosababisha Bodi kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kisheria kama yalivyoainishwa kwenye kifungu 7(1) (j) cha Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali kinachoitaka Bodi kupokea kujadili na kupitisha taarifa za Baraza hilo.

Dkt. Sambaiga amelitaka Baraza kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ikiwemo kutetea maslahi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kuwa jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kuhakikisha wanakuwa mwavuli wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika masuala yote yanayohusu uratibu na kutandaa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali; na

“Nawasihi viongozi wa Baraza Kutunga na kusimamia utekelezaji wa Kanuni za Maadili kwa lengo la kuwezesha Mashirika Yasiyo ya kiserikali kujiongoza kwa kufuata misingi ya kimaadili yenye uwazi na uwajibikaji.”

Mweyekiti wa Bodi ya Mashirika Yasika ya Kiserikali ameleza kuwa maelekezo anayoyatoa yanalenga kuhakikisha kuwa Baraza la Mashirika ya NGOs linatekeleza kazi zake kikamilifu, kuimarisha uratibu wa sekta ya NGOs, kuondoa chanagmoto za uendeshaji wa NGOs hivyo Bodi ikalazimika kutoa maagizo thabiti kuboresha uendeshaji wa kazi za NGOs nchini.

Dkt Simbaiga amelieleza Baraza la Taifa la NGOs kuwa ulegevu wa kiutendaji ndani ya Baraza la NGOs unakwamisha utendaji wa kazi za Bodi ya NGOs amabzao wamekasimiwa kuzitekeleza kwa mujibu wa sharia, kanuni na taratibu.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Nicolaus Zachariah ameshukuru kwa hatua iliyochukuliwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NGOs ya kukutana na wajumbe wa Baraza la NGOs na kujadili masuala yenye chanagamoto katika uendesjai wa majukumu ya Baraza. Baraza la NGOs limepokea maelekezo ya Bodi na kukiri kuyafanyia kazi maagizo yote kwa pamoja kama yalivyowasilishwa na Bodi ya NGOs.

Aidha, Baraza la NGOs limeaomba kuendelea kupata ushauri wa kitaalam na msaada wa kisheria ili kuhakikisha kuwa maalekezo yote yanatekelezwa katika muda uliokubainishwa.

Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali iliyoanzishwa chini ya Kifungu cha 6 (1) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya Mwaka 2002 kwa lengo la kuwakilisha Sekta ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ikiwa na jukumu la kusimamia uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini ikiwemo uendeshaji wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.


Share:

MAMA MATATANI KWA KUMUUZA MTOTO WAKE


Gari la Polisi nchini Kenya

Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Sharon Achieng (23) kutokea nchini Kenya, amekamatwa na polisi katika kituo cha Siaya kwa kosa la kutaka kumuuza mwanaye wa kiume aliye na umri miaka mitano.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa kutokea kijiji cha Anduro, ambapo alitaka kumuuza mwanaye kwa mwanamke aliyejulikana kwa jina la Irene, kwa shilingi milioni 2 za Kenya sawa na milioni 45 pesa ya kitanzania.

Joseph Aloo ambaye ni kiongozi msaidizi wa kituo hicho cha polisi amesema, wanamshikilia mtuhumiwa huyo kwa kujaribu kumuuza mwanaye kwa mtu ambaye anafanya kazi ya ulinzi.

Pia anajitetea kwa kusema alikuwa anashindwa kumlea mtoto huyo peke yake kwa kuwa mume wake amemkimbia.

Aidha kwa upande wa Irene ambaye alipelekewa mtoto huyo ili kumnunua ameeleza kuwa, Sharon Achieng alimleta mtoto huyo huku akisema yeye ni yatima na anaishi kwa bibi yake pia hajawahi kuolewa.
Share:

Serikali Yawafichua Watoto 16,000 Wenye Ulemavu Waliofichwa Na Kuwaandikisha Shule

Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa amesema Serikali imewafichua na kuwatambua jumla ya watoto 16,000 wenye ulemavu wa aina mbalimbali waliokuwa na umri wa kwenda shule katika mikoa yote hapa nchini waliokuwa wamefichwa na kuwaandikisha shule kulingana na mahitaji yao ya msingi.

Naibu waziri Ikupa ameyasema hayo Desemba 03, 2019 katika Maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

“Watoto wenye mahitaji maalum waliokuwa wamefichwa Serikali imewatambua na kuwaandikisha shule kulingana na mahitaji yao ya msingi, watoto 16,000 wametambuliwa kutoka mikoa na halmashauri zote nchini isipokuwa Halmashauri tisa tu ambazo hazijafikiwa kwa kuwa zoezi hili ni endelevu kadri bajeti itakavyoruhusu nazo zitafikiwa,”alisema Ikupa.

Aidha akijibu baadhi ya changamoto zilizowasilishwa na  Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) kuhusiana na kutengewa bajeti  ndogo amesema kuwa tayari serikali imetenga milioni 30 kwa ajili ya kuliwezesha baraza la watu wenye ulemavu  kufanya kazi kwa ufanisi, huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kuongeza nguvu katika kuwasaida watu wenye ulemavu hususani walio katika maeneo ya pembezoni.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri  Ikupa ametoa wito kwa vyama vya siasa nchini kutenga nafasi maalum za uwakilishi bungeni kwa watu wenye ulemavu kama kilivyofanya Chama Cha Mapinduzi( CCM), huku akiwasisitiza wenye ulemavu na wao kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi badala ya kusubiri nafasi maalum pekee.

Awali akiwasilisha taarifa ya Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi amesema Simiyu inawathamini na kuwajali watu wenye ulemavu huku akibainisha kuwa Halmashauri zimetenga zaidi ya shilingi milioni 231 katika mwaka wa fedha 2019/2020 kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba kwa watu wenye ulemavu na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo ili wajikwamue kiuchumi.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Bibi. Tungi Mwanjala ameiomba Serikali   kuviwezesha viwanda vya ndani kutengeneza vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu ili kupunguza gharama zitokanazo na kodi ya kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.

Naye mmoja wa Watu wenye ulemavu Bi Nuru Awadh amesema katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano watu wenye ulemavu wameaminiwa  katika nafasi mbalimbali na sheria nyingi zinazowahusu watu wenye ulemavu zitakelezwa kwa vitendo.

Maadhimisho ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu inayosema: “HAMASISHA USHIRIKI WA WATU WENYE UELMAVU NA UONGOZI WAO: TEKELEZA AGENDA ENDELEVU 2030”

MWISHO


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano December 4



















Share:

Tuesday, 3 December 2019

Salesman Job Opportunity at Bonite Bottlers

Salesman Qualification: Applicant should be a holder of form IV/VI with Diploma in Sales and Marketing / Business Administration or any related field from recognized Institution. Key skills & Abilities: Skills and knowledge of customer care and customer services. Ability and skills of route sales. Ability to forecast sales/load to be taken for each day to the location… Read More »

The post Salesman Job Opportunity at Bonite Bottlers appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

3 Sales/Marketing Executive (Corporate) Job Opportunities at Alliance Life Assurance

Sales/Marketing Executive (Corporate) 3 Posts Location: Arusha; Mbeya; Mwanza Alliance Life Assurance Limited is one of the leading Life Insurance companies in Tanzania providing life insurance solutions and services to both corporates and the public. We have exciting openings for Sales/Marketing Executives (Corporate) to be based in Arusha, Mbeya and Mwanza. Reporting to the Sales & Marketing Manager, the… Read More »

The post 3 Sales/Marketing Executive (Corporate) Job Opportunities at Alliance Life Assurance appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

TAKUKURU YAZINDUA KAMPENI YA "VUNJA UKIMYA KATAA RUSHWA YA NGONO"..YAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KAGERA


Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera John Joseph akitoa elimu ya rushwa ya ngono kwa waandishi wa habari mkoani Kagera.

Na Ashura Jumapili - Malunde 1 blog Bukoba

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania (TAKUKURU ) imeanzisha kampeni ya kitaifa ya" vunja ukimya kataa rushwa ya ngono "ili kutoa fursa kwa waathiriwa wa matatizo ya ngono kufunguka.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera John Joseph,wakati akitoa elimu ya rushwa ya ngono kwa waandishi wa habari mkoani humo.

Joseph alisema rushwa ya ngono inamdhalilisha mtu,inasababisha magonjwa maana unaweza kujikuta unashiriki ngono na mtu ambaye ana magonjwa ya kuambukiza na kumuambukiza mwingine.

Alisema upo ulazima wa nchi na wadau mbalimbali kushirikiana ili kuweza kufichua vitendo vya rushwa ya ngono katka jamii.

Alisema matukio ya rushwa ya ngono yanafanyika kwa wingi lakini hayaripotiwi katika mamlaka husika ili ziweze kuchukua hataua stahiki.

Alisema zaidi ya matukio 391 yaliripotiwa takukuru ya kuombwa rushwa ya Ngono hapa nchini kwa mwaka 2017 Hadi 2019 na majalada 46 yalifanyiwa uchunguzi.

Alisema kuwa Takukuru Mkoa wa Kagera unampango wa kuanzisha dawati amaalumu la Rushwa ya Ngono ili jamii iweze kutambua madhara yatokanayo na rushwa ya ngono.

"Nitumie nafasi hii kuwajulisha jamii na jinsi Rushwa ya Ngono jinsi inavyo mdhalilisha mtu na inasababisha magonjwa maana huwezi jua kuwa yule anayefanya Jambo Hilo kuwa ni mgonjwa au la",alisema Joseph

Alisema kuwa Sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11ya mwaka 2007 imetamka kuwa kosa chini ya Kifungu Cha 25 " Mtu yeyote ambaye kwa kutumia nafasi yake au Mamlaka yake katika kutekeleza majukumu yake anadai au analazimisha upendeleo wa Kingono au upendeleo mwingine wowote Kama kigezo Cha kutoa ajira , Kupandishwa cheo, Kutoa haki au upendeleo wowote unaotambulika Kisheria atakuwa ametenda Kosa" ,alisema Joseph.

Alisema kuwa kesi ya rushwa ya ngono zimekuwa zikishindwa mahakamani kwa kukosa ushahidi uliojitosheleza kutokana na jamii kutokuwa na elimu ya rushwa ya ngono.
Share:

Majaliwa Aagiza Ujenzi Wa Machinjio Ukamilike Mwezi Huu Mwishoni Kama Ilivyoamriwa Na Rais Magufuli

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka mkandarasi anayejenga machinjio ya kisasa ya Vingunguti jijini Dar es Salaam ahakikishe kwamba anakamilisha ujenzi huo mwishoni mwa mwezi huu kama alivyoamriwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo leo (Jumanne, Desemba 3, 2019), Mheshimiwa Majaliwa amesema amefurahishwa na hatua ya mkandarasi huyo ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ya kuongeza idadi ya watalaam na mafundi ili kuhakikisha kwamba kazi hiyo inafanyika haraka na kukamilika kwa wakati ulioamriwa na Rais Magufuli yaani Desemba 30, mwaka huu.

Amesema amefurahi pia kuona kwamba mkandarasi huyo ameamua kufanya kazi usiku na mchana, hatua ambayo imeongeza kasi ya ujenzi huo na anaamini kuwa kazi hiyo itakamilika kwa wakati.

Mheshimiwa Majaliwa amemtaka  Mshauri Mwelekezi wa mradi huo ambaye ni M/SCONS AFRIKA LIMITED na FB Consultant wa Dar es Salaam  asimamamie kwa karibu ili  kujiridhisha  kuwa maelekezo yote yaliyopo kwenye michoro ya ujenzi huo yanazingatiwa na mkandarasi.

Amesema Serikali imeamua kujenga machinjio hayo ya kisasa ya Vingunguti baada ya kugundua kwamba wafanyabiashara wa mifugo na mazao yake  katika machinjio hayo, walikuwa wakifanya kazi zao kwenye mazingira duni na  kwamba nyama iliyokuwa ikitoka kwenye machinjio hayo ilikuwa haikubaliki kwenye soko la nje ya nchi.

“Uamuazi wa Serikali kujenga machinjio haya, utaifanya nyama inayotoka hapa ikubalike kwenye masoko ya nje ya nchi, hatua ambayo itaongeza mzunguko wa fedha kwenye eneo hili wakati Serikali na Manispaa watanufaika kwani kutakuwa na ongezeko la makusanyo ya kodi,” aliongeza Mheshimiwa Majaliwa.

Waziri Mkuu pia ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Manispaa ya Ilala wafanye mazungumzo na uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) ili ijengwe reli ya mchepuko kutoka reli ya kati kwenda kwenye machinjio ya Vingunguti ili mifugo iingizwe moja kwa moja kwenye machinjio hayo badala ya kuteremshiwa Pugu halafu ikapelekwa  kwa magari.

Amewahakikishia wafanyabiashara wote wanaoendesha shughuli zao kwenye machinjio hayo kuwa ujenzi wa machinjio ya kisasa  ya Vingunguti hautawafanya wapoteze fusa zao za biashara au kuajiriwa kwenye eneo hilo kwani  machinjio hayo yatafungua fursa zaidi za biashara na ajira kwao.

Amewaagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala wahakikishe kwamba wanaushirikisha uongozi wa wafanyabiashara wa mifugo na mazao yake wa Vingunguti ili wanachama wao wenye sifa za kuajiriwa, waajiriwe na pia wawaandalie mazingira ya kufanya biashara mbalimbali karibu na machinjio hayo.

Akizungumzia soko na bei duni ya ngozi za mifugo nchini, Waziri Mkuu amekemea tabia ya wafugaji ya kuweka alama kwenye ngozi za mifugo yao hasa ng’ombe kwani kufanya hivyo kunashusha thamani ya ngozi za Tanzania na badala yake amewataka waweke alama za hereni kwenye masikio ya mifugo yao ili kulinda ubora wa ngozi za mifugo yao.

Amesema Serikali tayari imekwishampata mwekezaji kutoka Misri ambaye amekubali kuwekeza kwenye kiwanda cha ngozi cha Mwanza hatua ambayo italihakikishia Taifa soko la ngozi.

Mapema, akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri amesema ujenzi wa machinjio hayo ulianza Julai 8, mwaka huu na mkandarasi alitakiwa akamilishe ujenzi huo ifikapo  Januari 6, 2021. Amesema kufuatia agizo la Rais Magufuli alilolitoa Septemba 16, mwaka huu, ujenzi huo unatakiwa ukamilike ndani ya miezi mitatu yaani ifikapo Desemba 31, 2019.

Bw. Shauri amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo itagharimu sh.  12, 498,916,063.00 ambapo sh. 8,528,486,470.00 ni ruzuku kutoka Serikali Kuu na sh. 3, 970,429,593.00 zimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri na kwamba ujenzi wa mradi huo kwa sasa umefikia asilimia 60.

Akisoma risala  ya Ushirika wa Wafanyabiashara ya Mifugo na Mazao yake  wa Vingunguti (UWAMIVI), Mwenyekiti wao, Bw. Joel Meshaki aliiomba Serikali  iwaandalie wafanyabiashara hao eneo mbadala la kufanyia shughuli zao  ili  ajira yao isipotee.

Alipendekeza kwa Waziri Mkuu maeneo matatu yaliyoko karibu  eneo hilo, ambayo yangewafaa wafanyabiashara hao wakati watakapoondoka  kwenye maeneo yao sasa yanapojengwa machinjio ya kisasa kuwa ni Dampo la zamani ambalo kwa sasa halitumiki,  eneo la Wizara ya Kilimo ambalo kwa sasa ni sehemu ndogo tu inayotumika  na jengo la Kilimo ambalo kwa sasa linatumika kama ghala.

Alisema idadi ya mifugo inayochinjwa katika machinjio hayo kwa sasa ni ng’ombe 550 hadi 600 kwa siku za kawaida na siku za sikukuu ni ng’ombe 1,000 hadi 1,500. “Halmashauri yetu ya Ilala  hukusanya  zaidi ya sh.  milioni 118 kwa mwezi  wakati Serikali Kuu hukusanya milioni 117 kila mwezi,” alisema Meshaki.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Share:

Bodi ya Manunuzi na Ugavi Yaagizwa Kuwachukulia Hatua Wanunuzi Waliokwenda Kinyume Na Maadili

Na Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, ameiagiza Bodi ya Manunuzi na Ugavi kuwachukulia hatua waliopelekwa kwenye baraza la maadili  kulingana na uzito wa makosa yao ili taaluma hiyo iendelee kufanya kazi kwa weledi bila rushwa.

Agizo hilo limetolewa Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa 10 wa Wataalamu wa Ununuzi  na ugavi kutoka maeneo mbalibali nchini.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, kuna ununuzi usiozingatia sheria na kanuni na kusababisha kununua bidhaa zilizo chini ya kiwango, ununuzi hewa wa huduma na bidhaa na kutokuwepo kwa kumbukumbu za ununuzi na mikataba hewa licha ya uwepo wa wataalam hao.

“Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi wa Umma kwa mwaka 2018/19 inaonesha mikataba 12 kutoka taasisi tisa za umma yenye thamani ya shilingi bilioni 25.8 ina viashiria vya rushwa kwa kuwa utaratibu wa manunuzi kwa mikataba hiyo haukufuatwa”, alieleza Dkt. Kijaji

Alisema kuwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonesha kuwa ununuzi wa jumla ya Sh. bilioni 16.6 haukuwa kwenye bajeti wala mpango wa ununuzi ulioidhinishwa na Sh. bilioni 24.85 zimetumika kulipa mikataba ambayo haikuwa na hati ya utekelezaji.

Dkt. Kijaji amewataka waajiri wote kutoa ushirikiano kwa bodi za kitaaluma hususan linapojitokeza suala la usimamizi wa maadili kwa wataalamu waliosajiliwa na bodi husika, kwa kuwa hakuna ufanisi bila maadili.

Aidha Dkt. Kijaji, ameupongeza uongozi wa PSPTB kwa hatua zilizochukuliwa za kusimamia mahitaji ya ajira ya kada ya ununuzi na ugavi kwa kuwapeleka mahakamani watu wanaofanya kazi za ununuzi na ugavi bila kuwa na sifa stahiki.

Hivyo akawataka waajiri wote kuhakikisha wanaajiri watumishi wenye sifa zinazotambuliwa na PSPTB na kuzingatia mahitaji yaliyopo kwenye waraka wa Maendeleo ya utumishi wa mwaka 2015.

Naibu Waziri Dkt. Ashatu Kijaji, ameiagiza Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kufanya tathmini ya uwezo na uadilifu wa taasisi za umma zilizobeba dhamana ya ununuzi Serikalini.

Alielekeza kuwa taarifa ya Baraza la Maadili iwasilishwe wizarani mapema ili iweze kupitiwa na kufanya maamuzi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali.

Amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kuunga mkono juhudi za Bodi zinazolenga kuondoa kabisa uzembe na ukiukwaji wa maadili katika fani ya ununuzi na ugavi, kwa kuwa bajeti ya ununuzi wa Serikali ni takribani asilimia 80 ya bajeti yote.

Kwa upande wake Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Dkt. Fredrick Mwakimbinga, alisema kuwa Bodi inafanya jitihada za dhati kuhakikisha taaluma ya ununuzi na ugavi inatoa mchango unaotarajiwa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda kulingana na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano, ili kutimiza malengo hayo bodi imetoa mafunzo mahususi kwa taasisi mbalimbali ambayo yameongeza ufanisi katika taasisi husika.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Bw. Godfrey Mbanyi, amesema kuwa Bodi hiyo imeahidi kufanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na Naibu Waziri Dkt. Kijaji. Amebainisha kuwa licha ya kuwa na Sheria inayowataka watumishi wanaofanya kazi ya ununuzi na ugavi kusajiliwa, bado wapo ambao hawafanyi hivyo, Bodi itaendelea kuchukua hatua stahiki kwa wale wote watakao kiuka sheria.

Mwisho.


Share:

Country Director at Room to Read Tanzania

Room to Read is a global organization transforming the lives of millions of children in low-income communities by focusing on literacy and gender equality in education. Founded in 2000 on the belief that World Change Starts with Educated Children®, our innovative model focuses on deep, systemic transformation within schools during two time periods that are most critical in… Read More »

The post Country Director at Room to Read Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waziri Lukuvi Awataka Wakurugenzi Wa Halmashauri Kujitathmini Katika Utoaji Hati Za Ardhi

Na Munir Shemweta, WANMM IRINGA
Waziri wa Adhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuanza kujitathmini katika idadi ya hati za ardhi wanazotoa kwa wamiliki wa ardhi kwenye halmashauri zao.

Alisema Wizara yake itaanza kutangaza wilaya itakayoongoza katika Upangaji, Umilikishaji na Utoaji Hati za ardhi kwa wananchi ili kubaini hamashauri ambazo ziko nyuma katika kutoa hati za ardhi kwa wananchi.

Lukuvi alisema hayo jana katika mkutano wake wa kusikiliza na kutatua kero za ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Iringa kupitia programu ya Funguka kwa Waziri uliyofanyika ukumbi wa Siasa ni Kilimo katika Manispaa ya Iringa,

‘’Mkurugenzi ajione fahari kuwaezesha wananchi kwa kupima na kuwapatia hati, kama Mkurugenzi huwezi kutoa hati miliki hata mia moja basi wewe hufai’’ alisema Lukuvi.

Kwa mujibu wa Lukuvi, kumilikisha na kumpatia mwananchi hati ya ardhi ni kumuwezesha kiuchumi kwa kuwa anaweza kuitumia hati kwenye shughuli za kimaendeleo na kusisitiza kuwa wakurugenzi wa halmashauri wahakikishe wanapanga na kuwamilikisha maeneo wananchi.

Aidha, Lukuvi alisema kwa sasa wizara yake imejipanga kuhakikisha inasogeza huduma za ardhi karibu na wananchi kwa kuanzisha ofisi za mikoa zitakazokuwa na watendaji wote wa sekta ya ardhi kama vile Wapimaji, Wathamini, Wataalamu wa Mipango Miji pamoja na Wasajili.

‘’Sasa Wapimaji, Wathamini na Wapangaji watakuja hapa Iringa, muundo unaanza mwezi ujao lengo ni kuwapunguzia usumbufu wananchi katika kupata huduma za ardhi’’ alisema Lukuvi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, katika kuboresha huduma za sekta ya ardhi, Wizara yake itatumia mifumo unganishi itakayorahisisha utendaji kazi kwa wataalamu wa sekta ya ardhi ambapo kazi kubwa itakuwa ikifanyika kielektroniki badala ya kutumia makaratasi aliyoaeleza kuwa wakati mwingine husababisha tamaa kwa maafisa ardhi.

Alitolea mfano mkoa wa Dar es Salaama kuwa, ushaanza kutumia mfumo unganishi ambapo sasa wamiliki wa ardhi katika mkoa huo wanapatiwa hati za kielectroniki na kubainisha kuwa lengo la kuwa na mfumo unganishi ni kuondoa urasimu na kurahisisha utendaji kazi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi alieleza kuwa mkoa wake umejitahidi kupunguza kero na migogoro ya ardhi iliyokuwepo miaka ya nyuma kwa kuanzisha utaratibu wa kuwafuata wananchi kwenye maeneo yao kupitia programu ya Iringa Mpya.

Alimueleza Waziri Lukuvi kuwa, kama angekuja mwaka mmoja na nusu uliopita basi ukumbi aliofanyia mkutano wa Funguka kwa Waziri ungekuwa umejaa wananchi wenye kero za ardhi lakini jitihada za mkoa wake zimesababisha mkutano huo kutokuwa na idadi kubwa ya wananchi wenye migogoro ya ardhi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

‘’Muda mwingi nautumia kwenda kwa wananchi na kazi za ardhi zina changamoto kubwa na njia pekee ya kukabiliana nazo ni kutenda haki bila kujali uwezo, kabila ama dini ya mtu’’ alisema Hapi.


Share:

Tanzania kuimarisha, kuendeleza ushirikiano na Falme za Kiarabu (UAE)

Serikali ya Tanzania imeahidi kuendeleza ushirikiano wake na Falme za Kiarabu (UAE) katika sekta za biashara, miradi ya maendeleo, utalii, utamaduni, usafirishaji, kilimo na afya.

Akiongea katika maadhimisho ya 48 ya Falme za Kiarabu (UAE) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kuwa ili kukuza na kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ni muhimu pia kupanua maeneo ya ushirikiano kati ya nchi zetu mbili hyaakiwemo ya utalii, kilimo na miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Tayari tumeanza maandalizi ya mkutano wa pili wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Falme za Kiarabu (UAE) ambao utafanyika hapa nchini Tanzania mwaka 2020, baada ya mkutano wa kwanza wa JPC ambao ulifanyika Desemba 2016 Abu Dhabi wakati ambao, makubaliano hayo yalipo sainiwa”. Amesema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi aliongeza kuwa, makubaliano hayo yaliyosainiwa Abu Dhabi ni pamoja na Mkataba wa Huduma za Hewa za Kigeni (BASA) na Mkataba wa ushirikiano katika sekta ya Utalii. Tunatarajia kupanua wigo wa ushirikiano wetu katika mkutano ujao wa JPC.

Kama moja ya Makati wa uwekezaji, tuko tayari kuhakikisha kuwa wawekezaji wanawekeza Tanzania. Aidha, mbali na maboresho ya mfumo wa udhibiti wa biashara Tanzania (Blue Print)yaliyoanza Julai, 2019, tunafanya mashauriano ya ndani mkataba wa kuepusha na na tozo za ushuru mara mbili; na makubaliano ya mkataba wa pamoja juu ya kukuza na kuendeleza ulinzi wa uwekezaji aambapo kwa makubaliano haya ni chanzo cha Falme za Kiarabu (UAE) kuwekeza Tanzania.

“UAE imekuwa ikisaidia katika ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kusaidia juhudi za Tanzania kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kama vile ufadhili wa ujenzi wa barabara kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi (ADFD). Ni matumaini yangu kuwa Mfuko utaendeleza usaidizi na kuelekeza miradi mingine ya maendeleo”. Amesema Prof. Kabudi.

Kwa upande wake, Kwa upande wake, Balozi wa Balozi wa Falme za Kiarabu kwa nchini Tanzania, Balozi, Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi amesema kuwa Falme za Kiarabu zitaendeleza ushirikiano baina yake na Tanzania kindugu, kidiplomasia, kiuchumi na kuhakikisha kuwa ni wa kudumu.

“Napenda kuwafahamisha kuwa Falme za Kiarabu (UAE) utaendelea kuwekeza hapa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya kukuza uchumi. Tutaendelea kuwaeleza wawekezaji fursa zilizopo Tanzania ili waendelee kuja kuwekeza”. Amesema Balozi, Mohamed Al- Marzooqi.


Share:

Nsato Marijani : Umakini unahitajika tunapohakiki wakimbizi Dar

Na Veronica Mwafisi, MOHA-Dar es Salaam
UHUISHAJI takwimu za wakimbizi waishio jijini Dar es Salaam na mikoa mingine nchini, unapaswa kufanywa kwa umakini mkubwa kwani unagusa usalama wa nchi. 

Mkurugenzi Msaidizi wa Uendeshaji Makambi na Makazi, kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Nsato Marijani, aliyasema hayo jana wakati akifungua mafunzo ya uhuishaji takwimu za wakimbizi. 

Mafunzo hayo yalifanyika kwenye Ukumbi wa Polisi Officer’s Mess, Oysterbay, Dar es Salaam yakihusisha watendaji wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Uhamiaji, Ofisi ya Rais, Polisi pamoja na UNHCR. 

Alisema uhuishaji takwimu utahusisha wakimbizi wote waishio jijini Dar es Salaam wenye nyaraka, walioruhusiwa kuishi nje ya kambi za wakimbizi, maeneo mengine kuanzia kesho (Novemba 4), saa 2 asubuhi hadi Novemba 7, mwaka huu. 

Alifafanua kuwa, uhuishaji huo utafanyika katika Ofisi za Shirika la Relief of Development Society (REDOSO), zilizopo eneo la Biafra, Kinondoni. 

“Matarajio ni kuhuisha takwimu za wakimbizi 243 lakini idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na wakimbizi kutoka nchi mbalimbali ambao watajitokeza. 

Marijani alisema idara zote ambazo zinahusika na uhuishaji takwimu hizo, zinapaswa kufanya uhakiki huo kwa umakini mkubwa kwani zoezi hilo linagusa usalama wa nchi. 

“Jambo la msingi fanyeni kazi kwa ushirikiano na umoja kati ya watendaji wa idara za serikali na UNHCR, hakuna aliye juu ya mwingine,” alifafanua Marijani. 

Alifafanua kuwa, katika uhuishaji huo zinaweza kutokea changamoto ambapo utatuzi wake unapaswa kushirikisha viongozi na watendaji wa pande zote. 

Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Utawala na Makambi kutoka idara hiyo, Stephen Msangi, alisema wanatarajia kuhuisha taariza za wakimbizi 231 waliojadiliwa. 

Alisema pia kua wakimbizi 12 ambao wameongezeka hivi karibuni hivyo kufikia idadi ya wakimbizi 243 walioandikishwa ambao taarifa zao zitahakikiwa na kuthibitishwa. 

Naye Monday Iddi ambaye ni Afisa Hifadhi ya Wakimbizi mkoani Kigoma, alisema lengo la uhuishaji huo ni kufahamu idadi ya wakimbizi waliopo katika mikoa mbalimbali nchini.

“Baada ya uhuishaji, taarifa zao zitakuwa katika mfumo hivyo watashindwa kujiandikisha zaidi ya mara moja, uhuishaji huu utahusisha alama za vidole na macho (mboni),” alisema. 

Mkimbizi yeyote ambaye hatajitokeza wakati wa uhuishaji takwimu taarifa zake hazitahuishwa, usajili wake utasitishwa.
Wakimbizi hao wanatakiwa kufika na nyaraka za utambulisho zikiwemo barua ya uthibitisho wa mkimbizi, usajili, kibali cha kuishi nje ya kambi, vyeti vya kuzaliwa. 

Nyaraka nyingine ni vyeti vya ndoa, hati ya kusafiria, vitambulisho vya kazi, shule, chuo na nyaraka nyingine yoyote inayomtambulisha mkimbizi ambayo inatambulika kisheria. 

Shughuli zote zinazohusiana na uhakiki wa taarifa za mkimbizi na waomba hifadhi zinatolewa bure ambapo uhuishaji huo hautahusisha wakimbizi wa mwaka 1972. 

Wakimbizi hao ni wale wanaotoka makazi ya Ulyankulu, Katumba, Mishano na waishio vijijini mkoani Kigoma.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger