Monday, 11 November 2019

Waziri Wa Kilimo Aagiza Viongozi Wa Chama cha Akiba na mikopo na Chama cha Ushirika wa Ayalabe Dairy Wakamatwe

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameliagiza jeshi la Polisi Mkoani Arusha kwa kushirikiana na Mkuu wa Upelelezi, na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuwakamata viongozi mbalimbali wa Chama cha Akiba na mikopo cha Ayalabe na na Chama cha Ushirika wa Ayalabe Dairy kutokana na ubadhilifu wa fedha za wanachama wa vyama hivyo.
 
Waziri Hasunga ametoa maagizo hayo jana tarehe 10 Novemba 2019 wakati mara baada ya kusikiliza malalamiko ya wanachama wa vyama hivyo wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika eneo la uwanja wa vyama hivyo Wilayani Karatu ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Arusha.
 
Waziri Hasunga ameagiza viongozi hao kukamatwa haraka iwezekanavyo kwani dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya kuanzisha vyama vya ushrika ni kuwanufaisha wananchi kupitia umoja huo.
 
Viongozi hao ni Wajumbe wa Bodi ya AYALABE SACCOS ambao ni aliyekuwa Mwenyekiti Ndg Christopher Kastuli, Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Ndg Yuda Moratha, Waliokuwa makatibu Bi Maria Lohay na Anastazia Evodi pamoja na wajumbe Eustela Kastuli, Faustini Tekko, Ludovick Marmo, Tarsila Visent na Costantine Matle.
 
Wengine ni waliokuwa wajumbe wa Chama cha Ushirika wa Ayalabe Dairy ambao ni aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Yuda Moratha, aliyekuwa Makamu mwenyekiti Faustine Tekko, aliyekuwa katibu wa chama hicho Ndg Yasinta Faustin, na wajumbe ambao ni EufrasiaAntony, Israel Sarwat, Evarist Sulle, Florance Neston na Eustela Kastuli.
 
Waziri Hasunga ameagiza pia kukamatwa viongozi wote wa makampuni yaliyochukua hela kinyume na taratibu za ushirika, kampuni hizo ambazo ni Shimaswa na Teddy Agrovet.
 
Katika hatua nyingine ameagiza Ndg Blanka Michael akamatwe kutokana na kukodisha eneo la Chama cha Ushirika wa Ayalabe Dairy pasipo kufuata utaratibu wa kisheria.
 
Katika mkutano huo pia Mhe Hasunga ameagiza kuwekwa kizuizini viongozi na wajumbe wa kamati ya usimamizi wa Chama cha Akiba na mikopo cha Ayalabe ambao ni aliyekuwa Mwenyekiti Ndg Lazaro Titus Lazaro  na wajumbe Joseph Bayo na Eudesi Jonas.
 
Waziri Hasunga ameuagiza uongozi uliopo wa Chama cha Ushirika cha akiba na mikopo cha Ayalabe kusitisha mara moja kulipa deni la mkopo waliochukua wa shilingi 500,00,000 kutoka Benki ya TIB kwa kutumia hati za majengo ya Ayalabe Dairy mpaka serikali itakapojiridhisha kama mkopo huo ni halali.
 
Ameagiza watuhumiwa hao wote wafunguliwe kesi ya uhujumu uchumi na watakaoweza kurudisha fedha za wanachama waweze kusamehewa. Pia ameuagiza uongozi wa wilaya ya Karatu na Tume ya Maendeleo ya Ushirika kuhakikisha kuwa wanasimamia ukarabati wa kiwanda cha Ayalabe Diary na kufikia mwezi Januari 2020 kianze kufanya kazi.
 
Chama cha Ushirika wa maziwa cha Ayalabe kilipokea kiasi cha shilingi 513,407,077 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Karatu kupitia miradi ya ASDP na DADPS tangu mwaka 2009 hadi 2013 kwa ajili ya ujenzi wa kuboresha kiwanda cha maziwa ambapo hata hivyo baada ya kufanyiwa uchunguzi na ukaguzi kilibainika kuwa na ubadhilifu wa Tshs 147,126,000 huku chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) chenyewe kilikuwa na akiba za wanachama ambazo ni shilingi 11,015,000 na hisa zao zilikuwa Tshs 2,830,000, huku kikiwa kimechukua mkopo wa Tshs 500,000,000 kutoka Benki ya TIB.


Share:

CCM Nao Kutoa Tamko Kesho Kutwa Kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema chama hicho kwa sasa kinaendelea kufuatilia muenendo wa zoezi zima la uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na kinatarajia kutoa tamko lake Novemba 13, 2019.

Polepole ametoa kauli hiyo Leo Novemba 11, 2019 kupitia ukurasa wake wa Twitter, huku zoezi zima la uchaguzi huo likiwa limekumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo wagombea wengi wa vyama mbalimbali kuenguliwa.

Kutokana na changamoto hizo, jana Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo alitengua maamuzi yote na kuamua kuwaruhusu wagombea wote nchini waliochukua fomu na kuzirejesha kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa bila kujali kama walienguliwa isipokuwa kwa wale wasio raia wa Tanzania, hawakujiandikisha au wamejiandikisha mara mbili.


Share:

Obstetrician and Gynaecologist/MD Job at Maternity Africa

Job Description Oversee medical activities in the clinical areas- antenatal, postnatal ward, labour ward, theatres, new born nursery, fistula ward, early pregnancy ward, outpatient clinic, theatres and laboratory as appropriate. Lead the team of local doctors to ensure excellent clinical care is maintained and developed To provide an opinion and assist in management of any […]

The post Obstetrician and Gynaecologist/MD Job at Maternity Africa appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Watu Wasiojulikana Wachoma Moto Ofisi Ya Mtendaji wa Kata ya Soweto katika Manispaa ya Moshi.

Watu wasiojulikana wamechoma moto ofisi ya Serikali ya mtendaji wa kata ya Soweto katika Manispaa ya Moshi.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa watu hao walichoma ofisi hiyo kwa kutumia mafuta ya petroli na kusababisha baadhi ya nyaraka na samani za ofisi kuungua.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira, alithibitisha jana kupokea taarifa za uhalifu huo, muda mfupi baada ya kuzuru eneo la Wailes, lilipo jengo hilo.

Katika taarifa yake, Mghwira ameagiza kufanyika uchunguzi wa kina ili kubaini wahusika wa tukio hilo, huku akisema ni mapema mno kulihusisha na masuala ya siasa.

Watu hao wanadaiwa kuichoma moto ofisi hiyo, Novemba 9, mwaka huu, kati ya majira ya saa 1:30 na saa 2:30 usiku.

“Ni kweli mimi na kamati yangu ya ulinzi na usalama mkoa, nilipokea taarifa hizo jana usiku kwamba kuna watu wasiojulikana wamechoma Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Soweto iliyoko eneo la Wailes, Manispaa ya Moshi na kuunguza nyaraka za serikali.

"Nimesha vielekeza vyombo vya ulinzi na usalama kuanza uchunguzi mara moja ili kubaini kiini cha uhalifu huo. Mpaka sasa kuna watu kadhaa wameshakamatwa na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano."

Kwa mujibu wa Dk. Mghwira, tukio la kuteketezwa kwa ofisi hiyo liligunduliwa na mtu mmoja aishie jirani na ofisi hiyo, ambaye anadai kusikia harufu ya petroli na ya vitu vinavyochomwa moto.

“Jirani huyo alihisi kuna taka zinachomwa ndipo akaamua kuchungulia kupitia dirishani na kuona ofisi ya mtendaji ikiwa imeshika moto, hapo hapo, ndipo alipotoka nje na kupiga kelele, kitendo ambacho kilisababisha wananchi wenzake kutoka nje na kuuzima moto huo na kisha kufanikiwa kupunguza athari zilizoanza kujitokeza,” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Pia Dk. Mghwira alisema wahalifu hao baada ya kutekeleza nia hiyo ovu, waliacha katika eneo la tukio kibiriti na kipande cha msokoto wa bangi.

Alipoulizwa kama nyaraka zilizounguzwa ni zinazohusiana na masuala ya uchaguzi, Mkuu huyo wa Mkoa alisema nyaraka nyingi zilizoteketea ni za masuala ya afya.

Alizitaja baadhi ya nyaraka zilizokuwa karibu na dirisha ambalo lilianza kuteketea kwa moto kuwa zinazohusiana na zoezi la chanjo ya rubella, surua na polio, iliyofanyika hivi karibuni.


Share:

LIVE: Kinachoendelea Bungeni Muda Huu

LIVE:  Kinachoendelea Bungeni Muda Huu


Share:

Mke wa Waziri Mkuu: Watoto Wenye Mahitaji Maalumu Wasitengwe

MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa ametoa wito kwa wazazi na walezi watoto wenye mahitaji maalumu  kutowaficha na kuwatelekeza na badala yake wawape nafasi ya kupata elimu kwa sababu ni haki yao ya msingi.

Mama Majaliwa ambaye pia ni Mlezi wa Umoja wa Wake wa Viongozi (New Mellenium Women Group), ametoa wito huo jana (Jumapili, Novemba 10, 2019), wakati alipokabidhi majengo ya madarasa manne na matundu ya vyoo kumi kwa Kituo cha Watoto Wenye Ulemavu cha Buhangija mkoani Shinyanga yaliyojengwa na umoja huo.

Mama Majaliwa amesema si vyema kuwatenga au kuwakatia tamaa watoto wenye ulemavu kwani wao pia ni watoto sawa na watoto wengine, hivyo wanastahili kupewa haki zote bila kubaguliwa.

Amesema hatua waliyochukuwa akinamama wa umoja huo inaunga mkono jitihada za serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe  Magufuli za kuwapatia watoto wa kitanzanai elimu bure na katika mzingira mazuri.

Mgeni rasmi katika makabidhiano hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako ameupongeza umoja  huo kwa shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuwajali watoto wenye mahitaji maalumu.

Profesa Ndalichako amesema katika  kipindi  cha  mwaka  2019/2020  Serikali imetenga  jumla  ya  sh 3,809,758,460.00  kwa  ajili ya  kununua  na  kusambaza  vifaa  vya  kufundishia na  kujifunzia  pamoja  na  vifaa  visaidizi  kwa  ajili  ya wanafunzi  wenye  mahitaji  maalum  (wakiwemo Albino),  katika  shule  na  vitengo  vya  elimu  maalum. 

Waziri huyo ameongeza kuwa pamoja  na  juhudi  hizo  za Serikali, bado wanafurahi wanapopata  michango  kama  huo uliotolewa leo. "Wito  wangu kwenu tusichoke  kuwasaidia  hawa  watoto  wetu.  Napenda kuwakumbusha  na  kusisitiza  kwamba  Watu  wenye Ulemavu wanahitaji  msaada  mkubwa  kutoka kwenu."

"Tuwasaidie  na  tushirikiane  kuwapatia mahitaji  yao  muhimu  ikiwa  ni  pamoja  na  elimu, huduma  za  afya  na  mazingira  mazuri  ya kuwawezesha  kuishi  bila  ya  matatizo. Serikali  kwa upande  wake itaendelea  kujitahidi kwa  uwezo kutoa  fursa  zinazojali  mahitaji  yao."

Amesema madarasa  pamoja  na  vyoo alivyokabidhiwa  leo kwa niaba ya uongozi  wa  kituo  cha Buhangija na  Kikundi  cha  New  Millenium ni  tunu kwao na  wananchi  wa  Shinyanga  na  ni  sadaka kwa watoto wa Buhangija, hivyo,  ameutaka uongozi wa  Mkoa  na  Uongozi  wa  Kituo  kwa  pamoja washirikiane  kuyatunza  vizuri  ili yaweze  kutumika kwa  muda  mrefu.

Akitoa taarifa ya ujenzi huo kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela amesema fedha zilizotumika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne ni sh. 65m,884,523/= ambapo kila chumba cha darasa kimejengwa kwa wastani wa sh. 16,471,130.

Amesema ujenzi wa vyumba kumi vya vyoo  unaendelea na ukikamilika utagharimu sh.26, 271,922.44 na kwamba vyoo hivyo vitakuwa vya kisasa vikiwa na maji ndani pamoja na masinki ya kunawia ili kukidhi mahitaji ya watoto wenye ulemavu.



Share:

OFISI YA SERIKALI YACHOMWA MOTO...DIWANI WA CHADEMA ASHIKILIWA

Na Daniel Mjema na Janet Joseph, mwananchi
 Nani wamehusika? hili ndilo swali linawaumiza vichwa wapelelezi baada ya watu wasiojulikana kuchoma moto ofisi ya Serikali ya mtendaji wa kata ya Soweto katika Manispaa ya Moshi.

Tukio hilo limetokea wakati mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ambao umekumbwa na utata ukiendelea, lakini baadhi ya watu wamelihusisha na uhalifu wa kawaida.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa watu hao walichoma ofisi hiyo kwa kutumia mafuta ya petroli na kusababisha baadhi ya nyaraka na samani za ofisi kuungua.

Tayari watu kadhaa wanashikiliwa na polisi, akiwamo Collin Myuta ambaye ni diwani wa Kata ya Soweto (Chadema), huku chama hicho kikitaka weledi katika uchunguzi wa tukio hilo. Katibu wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Basil Lema alisema haelewi sababu za polisi kumhusisha diwani wao na tukio hilo na kufanya lionekane ni tukio lenye sura ya kisiasa kuliko jinai.

Alisema ni mapema mno kulihusisha suala hilo na siasa na hawaelewi sababu za diwani huyo kukamatwa.

Hata hivyo, kamanda wa polisi wa mkoa, Salum Hamdani alisema hawajasema kama diwani huyo na wengine wamehusika bali wanashukiwa.

“Jukumu letu ni kuchunguza na kuwapata watu wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine na kuchoma hiyo ofisi. Suala la mtu kukamatwa halina limitation (mipaka),” alisema Hamdani.

“Sisi tumekamata watu kadhaa ambao tunawashuku kuwa huenda wamejihusisha kwa namna moja ama nyingine na tukio hilo. Hatujasema wamehusika. Tunawatuhumu kuwa wamehusika,” alisema.

“Tunaendelea na taratibu za mahojiano na watapewa haki zao za msingi kulingana na sheria. Tunaendelea na upelelezi ila kuna watu kadhaa tunawashikilia akiwamo huyo diwani,” alisema.

Tukio lilivyokuwa
Taarifa iliyotolewa jana na Shaban Pazi kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), inasema usiku wa kumkia jana, jirani anayeishi karibu na ofisi hiyo alihisi harufu ya moshi.

“Harufu ya moshi iliyochanganyika na mafuta ya petroli ilimshitua mkazi mmoja anayeishi jirani na ofisi hiyo ambaye alichungulia nje na kuona jengo la ofisi ya kata likiungua,” alisema.

Via Mwananchi

Share:

MIKOPO YA ELIMU YA JUU YAFIKIA SH. BILIONI 162.8 .....NI KWA WANAFUNZI 46,838 WA MWAKA WA KWANZA KWA MWAKA 2019/2020

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia Novemba 3, mwaka huu, Serikali imekwishatoa mikopo ya sh. bilioni 162.8 kwa wanafunzi 46,838 wa mwaka wa kwanza nchini kote.


“Kwa mwaka 2019/2020, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 450 kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi walengwa 128,285. Na hadi tarehe 3 Novemba, 2019 wanafunzi 46,838 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka 2019/2020, walikuwa wamepewa mikopo inayofikia shilingi bilioni 162.8,” amesema.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumapili, Novemba 10, 2019) wakati akizungumza na maelfu ya waumini waliohudhuria Baraza la Maulid kitaifa katika viwanja vya Benki Kuu (BoT) Capripoint, jijini Mwanza.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli, amesema Serikali inatambua kuwa utoaji wa huduma ya elimu ni gharama na kuwa baadhi ya wananchi hawawezi kumudu gharama hizo, hivyo ikaamua kuanzisha utaratibu wa kutoa mikopo ya elimu ya juu kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

“Mikopo inayotolewa na Serikali, huongozwa na Sheria ya Bodi ya Mikopo (Sura 178) inayotaja vigezo vya wahitaji na wenye udahili lakini wasio na uwezo wa kumudu gharama zote au sehemu ya gharama za mafunzo au kwenye maeneo ya kipaumbele ikiwemo yatima na wanaotoka familia zenye kipato duni.”

“Hata, hivyo Serikali inaendelea kufanyia kazi maoni na mapendekezo ya wadau mbalimbali ili kuboresha mfumo wa utoaji mikopo ya elimu ya juu. Nitumie nafasi hii kuwapongeza sana BAKWATA kwa kuweka mkakati wa kuunga mkono jitihada za Serikali katika eneo hili.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka viongozi mbalimbali watumie maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) kama chachu ya kujiuliza juu ya uongozi wao, na kwa kiasi gani uongozi wao unaacha alama kwa wale wanaowaongoza.

“Kipindi hiki tunachoadhimisha mazazi ya Mtume huyu mbora wa darja, hebu nasi kama viongozi wa waumini tujiulize na tujitathmini, je, ni kwa kiasi gani tunamuenzi kwa kufuata mwenendo mzima wa Mtume Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam. Je, ni kwa kiasi gani uongozi wetu umekuwa ni wenye kuacha athari njema kwenye nyoyo na fikra za waumini?”

Amesema wataalamu, waandishi na watafiti wa masuala ya uongozi walitumia muda mwingi kumsoma Mtume Muhammad (S.A.W). “Sababu kubwa iliyowavutia kumtafiti, kumsoma na hata kumuandikia makala na vitabu mbalimbali ni mafanikio makubwa aliyoyapata katika uongozi wake. Itoshe tu kusema kwamba Mtume Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam alikuwa ni mtu wa familia na kiongozi makini kabisa.”

Aliwataka watambue kwamba mtu anaweza kuteuliwa kuwa sheikh au imamu lakini hawezi kuwa kiongozi bora mpaka pale uteuzi au kuchaguliwa kwake utakapothibiti katika nyoyo na fikra za wale anaowaongoza.

“Nitoe rai kwamba wakati tunapoelekea kwenye uchaguzi wa viongozi wa BAKWATA kwa ngazi mbalimbali baadaye mwaka huu, suala la kumuogopa Allah mtukufu na kufuata mwenendo wa bwana Mtume Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam uwe ndiyo mwongozo wetu wa kuwapata viongozi,” alisisitiza.

Mapema, akitoa salamu za BAKWATA Taifa, Katibu Mkuu wa BAKWATA, Ustaadh Nuhu Jabir Mruma alisema Baraza hilo limeanzisha vikundi 82 vya uzalishaji vinavyojishughulisha na kazi za bustani na shamba darasa.

Kuhusu masuala ya utoaji wa haki na sheria, Katibu Mkuu huyo alisema watu 59,824 walipatiwa msaada wa kisheria na wataalamu wasaidizi wa sheria (paralegals) 79 katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema Desemba mwaka huu, BAKWATA itafanya uchaguzi katika ngazi mbalimbali. “Kupitia chaguzi hizo, tunatarajia kupata viongozi wabunifu, waadilifu na wachapakazi. Ninawasihi Waislamu wenye sifa wajitokeze kugombea nafasi husika.”

Pia alitumia fursa hiyo kuwaomba Waislamu wote wajitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, mwaka huu ili watumie haki yao ya kuchagua viongozi wanaofaa. “Kuacha kupiga kura ni kuwapa wengine fursa wakuchagulie viongozi wanaowataka. Tuepuke kuchaguliwa viongozi tusiowataka,” alisema.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU


Share:

KACU YAISOGEZA PETROBENA KAHAMA,SASA KUANZA KUNUNUA TUMBAKU KATIKA CHAMA CHA MSINGI NGOKOLO


Katika jitihada za kuhakikisha wakulima wa zao la Tumbaku katika msimu wa mwaka 2019/20 wanapata wanunuzi, Chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) kimeanza kutafuta wanunuzi wapya wa zao hilo baada ya baadhi ya kampuni kusitisha ununuzi wa zao hilo katika mkoa wa kitumbaku Kahama na kusababisha usumbufu kwa wakulima.

Akizungumza na wakulima wa Chama cha Msingi Ngokolo kilichopo katika Halmashauri ya Ushetu Mwenyekiti wa (KACU) Emanuel Charahani ameitambulisha kampuni mpya ya ununuzi ya Petrobena ambayo itanunua tumbaku katika chama hicho cha msingi kilo laki 2 na nusu kwa msimu ujao.

Amesema katika mkoa wa kitumbaku Kahama bado vyama vya msingi vitano bado havijapa mnunuzi wa zao hilo na baada ya kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco company (TLTC) kusitisha mkataba wa ununuzi wa zao hilo kwa wakulima kwa mawaka hujao na kusababisha wakulima kutojua mstakabali wao.

Charahani ameiomba wizara ya kilimo kukaa na wamiliki wa kampuni za ununuzi wa Tumbaku ili kupata muafaka wa kodi ambazo kampuni hizi zinazodaiwa ili kunusuru kilimo cha tumbaku ambapo kwa mwaka huu kampuni ya TLTC pekee ingepaswa kununua kilo milioni 14 na laki 5 za tumbaku lakini kutokana na mtikisiko wa zao hilo haitanunua tena.

Kwa upande mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Michael Matomora amesema kutonunuliwa kwa tumbaku iliyozalishwa nje ya mkataba na makapuni ya ununuzi wa zao hilo kumepunguza mapato ya halimashauri hiyo kwa asilimia 50 na kuzitaka kampuni za ununuzi wa Tumbaku kuhakikisha zinawasaidia wakulima ili waweze kulima kwa kisasa ili kuongeza thamani ya zao hilo.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Petrobena, Peter Kumalilwa amekishuruku KACU kwa kukubali kufanya kazi na kampuni hiyo na kuwataka wakulima wa chama hicho kulima kwa kuzingatia kilimo cha kisasa ili kuongeza ubora wa zao la tumbaku na kwa kuanza wataanza na kununua kilo laki mbili na nusu.

Kumalilwa amesema endapo chama hicho kikizalisha kwa ufasaha Kampuni ya Petrobena itaongeza ununuzi na kuwataka wakulima kutowa tumikisha watoto katika kilimo hicho sambamba na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ya kutosha.
Mkurugenzi wa Petrobena Peter Kumalilwa akizungumza na wakulima wa Tumbaku katika Kijiji cha Ngokolo Ushetu Kahama.
Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika kahama (KACU) Emanuel Charahani akikagua shamba la mbegu la wakulima wa chama hicho.
Mkurugenzi wa kampuni ya Petrobena, Peter Kumalilwa akizungumza na wakulima wa tumbaku wa cha msingi Ngokolo hawapo pichani.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ushetu Michael Matomora akiwasililiza viongozi wa kampuni ya Petrobena ofisini kwake
Baadhi ya wakulima wa Tumbaku kutoka chama cha masingi ngokolo katika halmashauri ya Ushetu wakiwasiliza viongozi wa kampuni ya petrobena.
Share:

PROF. KUFUNGUA MKUTANO WA WATAFITI 250 WA SAYANSI KUTOKA NCHI MBALIMBALI


Kushoto ni Meneja tafiti Costech,katikati ni Mkurugenzi mkuu Costech Dr Amos Ningu na Afisa Mtafiti kutokaTume ya Sayansi na Teknolojia NeemaTindamalile (kulia).


Na Hellen Kwavava Dar es Salaam

Waziri wa Elimu,Sayansi naTeknolojiaProfesa Joyce Ndalichako leo jioni anatarajia Kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa baraza la sayansi kanda ya Afrika utakaofanyika hotel ya Sea Clif jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unaohusisha wanasayansi 250 toka nchi mbalimbali na Tanzania ikiwani Mwenyeji wake.

Akizungumzia kuhusiana na mkutano huo Afisa Mtafiti kutokaTume ya Sayansi na Teknolojia NeemaTindamalile alisema mkutano utafanyika wiki nzima na mada mbalimbali zitajadiliwa kila siku ilikuongezeana uelewa katika sayansi uwazi

“Mkutano huu unatarajia kuanza leo Jumatatu Novemba 11,2019 na kuna mada mbalimbali zitajadiliwa ambapo siku ya kesho kutakuwa na mada ya sayansi uwazi katika utafiti na ubunifu kwa ajili ya maendeleo lakini pia kutajadiliwa mada ya Jinsia mbalimbali katika ubunifu”,alisema Neema.

Naye Hulda Gideon alisema lengo la Mkutano huo nikufanya sayansi zote zijumuishe watu alafu ziwe na uwazi iliziweze kuwafikia walengwa kwa ufasaha.

“Tunaposema sayansi uwazi inahusisha mambo tofauti tofauti katika kufanya tafiti kwa uwazi zaidi ambapo inaanzia katika wazo kwa kuliweka wazi,Vifaa vya Utafiti kuwa wazi ili watu wengine wajue pia nanamna ya kufundisha masuala ya Utafiti kwa Uwazi”,alisema Hulda.

Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Costech Dr Amos Ningu aliongeza kwamba kwenye Mkutano huo utaleta ushirikiano zaidi kati ya taasisi mbalimbali toka nje kwa kuboresha kazi baina yao watafiti na kuzifanya ziwe za kiwango cha juu zaidi.

Mkutano huo umeweza kughalimu kiasi cha shiling Milion mia tano na wanasayansi hao wataweza kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini.
Share:

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YARIDHISHWA NA TASAF KATIKA KUONDOA KERO YA UMASKINI NCHINI



Makamu wa pili wa SMZ Balozi Seif Ali Idd akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga (wa pili kushoto juu ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo.



Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga aliyevaa miwani) akisisitiza jambo kwenye mkutano wa viongozi wa SMZ juu ya utekelezaji wa shughuli za TASAF .

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ, Mhe. Mohamed Abood akizungumza kwenye kikao cha kuwajengea uelewa viongozi wa SMZ juu ya utekelezaji wa shughuli za TASAF.


Baadhi ya maafisa wa SMZ (picha ya juu na chini) wakiwa katika kikao cha kuwajemgea uelewa juu ya masuala mbalimbali ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF

***

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii {TASAF} Awamu ya 3 kipindi cha Pili umejikita zaidi kufanya kazi na walengwa katika masuala ya uimarishaji wa Elimu, Afya, pamoja na mafao kwa Walemavu waliomo ndani ya Kaya Maskini kupitia Shehia mbali mbali Unguja na Pemba. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo Nd. Ladislaus Mwamanga alisema hayo wakati akitoa Taarifa ya matayarisho ya kuanza kwa Awamu hiyo katika Kikao cha Wakurugenzi na Maafisa wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar mkutano uliofanyika Vuga Mjini Zanzibar. 

Ndugu Ladislaus Mwamanga alisema Awamu ya Tatu kipindi cha Pili ambayo Fedha za Mfuko huo jumla ya shilingi Trilioni 2.1 sawa na Dola za Kimarekani Milioni 883 zimeshatiwa saini inategemewa kuwafikia Wananchi wote katika Vijiji mbali mbali hadi vile visivyopata huduma ya TASAF na Awamu zilizopita. 

Alisema Uongozi wa TASAF utasimamia vyema miradi yote iliyopendekezwa na Wananchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Mabwawa ya kufugia Samaki pamoja na Miundombinu ya Umwagiliaji Maji kwenye Mashamba ya Wana TASAF kwa lengo la kuongeza uzalishaji. 

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii {TASAF} aliwahakikishia Wakurugenzi na Waratibu hao wa TASAF wa Zanzibar kwamba mafao yote yanayolalamikiwa katika kipindi cha nyuma yatalipwa mapema kabla ya muendelezo wa kipindi cha Pili kuanza rasmi. 

Nd. Mwamanga alifahamisha kwamba yapo mabadiliko ya muundo mzima wa TASAF kipindi cha pili yatakayozingatia zaidi maboresho ya shughuli za mfuko huo ili miradi yake iweze kufanya kazi kwa ufanisi kupitia mfumo wa kisasa wa Mtandao wa mawasiliano katika kutanua wigo wa maendeleo ya Kiuchumi. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii {TASAF} alielezea faraja yake kutokana na mafanikio makubwa ya Awamu zilizopita za Mfuko huo zilizowezesha Wanafunzi 277 wa Kaya Maskini Tanzania wamepata mikopo ya elimu ya juu kutoka taasisi ya HELB ili waweze kuendelea na masomo yao ya Vyuo Vikuu mwaka 2019. 

Wakitoa michango yao katika Kikao hicho cha matayarisho ya kuanza kwa Awamu ya Tatu sehemu ya Pili ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Wajumbe wa Kikao hicho walisema TASAF Awamu ya Tatu Kipindi cha Pili inapaswa kutoa upendeleo zaidi kwa Wananchi wenye mahitaji maalum ili kuwapunguzia utegemezi. 

Wajumbe hao pia wakaelezea changamoto zinazowakumba Watendaji wa Mfuko huo ambazo zinapaswa kutafutiwa ufumbuzi wakizitaja kuwa ni pamoja na ucheleweshaji wa Taarifa, udanganyifu kwa baadhi ya Watendaji pamoja na ufinyu wa Elimu kwa Walengwa. 

Akitoa nasaha zake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed aliushukuru Uongozi Mzima wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii {TASAF} kwa jitihada zake za kuunga mkono Miradi ya Wananchi katika maeneo mbali mbali Nchini. 

Waziri Aboud aliwakumbusha Viongozi na Watendaji wanaosimamia Mfuko huo kuangalia zaidi uimarishaji wa Miradi ya maendeleo hasa katika Sekta ya Elimu, na Kilimo ambayo inasaidia kukwamua Kaya Maskini katika kujiletea maendeleo yao. 

Katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud alimkabidhi rasmi Uenyekiti wa Kamati ya Mfuko wa TASAF Unguja Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Hassan Khatib Hassan. Mapema asubuhi Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii {TASAF} Nd. Ladislaus Mwamanga alikutana kwa mazungumzo ya kubadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar. 

Katika mazungumzo yao Balozi Seif aliwapongeza Viongozi wa Mfuko wa TASAF kutokana na kazi nzuri wanayoifanya hususan kwa upande wa Visiwa vya Unguja na Pemba kwa kuendeleza kuwatumikia Wananchi ili waweze kujikomboa Kiuchumi. 

Aliwataka na kuwashauri Watumishi hao wa TASAF waendelee kutoa Elimu kwa Wananchi kutokana na faida zinazopatikana kupitia miradi na mafao ya TASAF katika kusukuma gurudumu la Maendeleo.Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza ufuatiliaji wa Taarifa sahihi za Wananchi ili kuhakikisha kila mstahiki anapatiwa fursa hiyo na kuitumia ipasavyo. Nao Wananchi kwa upande wao wanapaswa kutoa taarifa zilizo sahihi kupitia Sheha wa Shehia zao ili ziweze kusaidia katika ugawaji wa mafao ndani ya Kaya zao. 
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu November 11

























Share:

Sunday, 10 November 2019

KACU NA PETROBENA WAKUBALIANA KUANZA UNUNUZI WA ZAO LA TUMBAKU KATIKA MKOA WA KITUMBAKU KAHAMA KATIKA MSIMU WA MWAKA 2019/20


SALVATORY NTANDU
Katika jitihada za kuhakikisha wakulima wa zao la Tumbaku katika msimu wa mwaka 2019/20 wanapata wanunuzi, Chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) kimeanza kutafuta wanunuzi wapya wa zao hilo baada ya baadhi ya kampuni kusitisha ununuzi wa zao hilo katika mkoa wa kitumbaku Kahama na kusababisha usumbufu kwa wakulima.

Akizungumza na wakulima wa Chama cha Msingi Ngokolo kilichopo katika Halmashauri ya Ushetu Mwenyekiti wa (KACU) Emanuel Charahani ameitambulisha kampuni mpya ya ununuzi ya Petrobena ambayo itanunua tumbaku katika chama hicho cha msingi kilo laki 2 na nusu kwa msimu ujao.

Amesema katika mkoa wa kitumbaku Kahama bado vyama vya msingi vitano bado havijapa mnunuzi wa zao hilo na baada ya kampuni ya Tanzania Leaf Tobacco company (TLTC) kusitisha mkataba wa ununuzi wa zao hilo kwa wakulima kwa mawaka hujao na kusababisha wakulima kutojua mstakabali wao.

Charahani ameiomba wizara ya kilimo kukaa na wamiliki wa kampuni za ununuzi wa Tumbaku ili kupata muafaka wa kodi ambazo kampuni hizi zinazodaiwa ili kunusuru kilimo cha tumbaku ambapo kwa mwaka huu kampuni ya TLTC pekee ingepaswa kununua kilo milioni 14 na laki 5 za tumbaku lakini kutokana na mtikisiko wa zao hilo haitanunua tena.

Kwa upande mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Michael Matomora amesema kutonunuliwa kwa tumbaku iliyozalishwa nje ya mkataba na makapuni ya ununuzi wa zao hilo kumepunguza mapato ya halimashauri hiyo kwa asilimia 50 na kuzitaka kampuni za ununuzi wa Tumbaku kuhakikisha zinawasaidia wakulima ili waweze kulima kwa kisasa ili kuongeza thamani ya zao hilo.

NaYe Mkurugenzi wa kampuni ya Petrobena, Peter Kumalilwa amekishuruku KACU kwa kukubali kufanya kazi na kampuni hiyo na kuwataka wakulima wa chama hicho kulima kwa kuzingatia kilimo cha kisasa ili kuongeza ubora wa zao la tumbaku na kwa kuanza wataanza na kununua kilo laki mbili na nusu.

Kumalilwa amesema endapo chama hicho kikizalisha kwa ufasaha Kampuni ya Petrobena itaongeza ununuzi na kuwataka wakulima kutowa tumikisha watoto katika kilimo hicho sambamba na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ya kutosha.
Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika kahama (KACU) Emanuel Charahani akikagua shamba la mbegu la wakulima wa chama hicho.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Petrobena, Peter Kumalilwa akizungumza na wakulima wa tumbaku wa cha msingi Ngokolo hawapo pichani.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ushetu Michael Matomora akiwasililiza viongozi wa kampuni ya Petrobena ofisini kwake

Baadhi ya wakulima wa Tumbaku kutoka chama cha masingi ngokolo katika halmashauri ya Ushetu wakiwasiliza viongozi wa kampuni ya petrobena.
Share:

Vilio na huzuni vyatawala tena mgodi wa Imalanguza Geita

Na Issa Mtuwa “WM” - Geita
Majonzi na huzuni vimetawala kwenye mgodi wa wachimbaji wadogo wa Imalanguza wilaya ya Geita kata ya Lwamgasa katika Kijiji cha Imalanguzu, mara baada ya kuwasili Naibu Waziri wa Madini Stanslausi Nyongo mgodini hapo akiwa na viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Madini, uongozi wa mkoa na viongozi wa dini kwa ajili ya kwenda kusitisha shughuli za uokoaji wa wachimbaji wadogo wawili Karos Msukuma Paulo mwenyeji wa Chato na Kulwa Joseph Mahungija mwenyeji wa Busolwa Nyang’wale waliofukiwa kifusi siku ya tarehe 1/10/2019.
 
Usitishaji wa zoezi hilo umefanyika tarehe 9/11/2019 ikiwa ni siku 39 tangu wachimbaji hao wafukiwe na kifusi kutokana na uwepo wa changamoto mbalimbali zilizo jitokeza katika kipindi chote cha uokoaji. Ripoti maalam ya timu ya wataalam wa uokoji imeeleza kuwa kumekuwa na changamoto nyingi wakati wote wa ukoji zilizopelekea kuwa na ugumu wa kuwaokoa wachimbaji hao. 
 
Akiwasilisha taarifa ya wataalam wa uokoaji iliyoishauri serikali kusitisha kwa zoezi hilo la uokoaji kwa Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo,  mkuu wa wilaya ya Geita Josephat Maganga amemwambia Naibu Waziri wa Madini kuwa miongoni mwa changamoto zilizojitokeza wakati wa uokoaji ni pamoja na uwepo wa maji chini ya mgodi, mwingiano wa magogo mbalimbali chini ya shimo la mgodi, na kutokuwa na usalama katika eneo hilo hata kwa vyombo vya uokoaji.
 
Maganga aliongeza kuwa, kulikuwa na wataalam wa makundi mbalimbali ya uokoaji na vifaa vya kutosha kutoka kwa jeshi na uokoaji, mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), na makampuni mengine kutoka kwenye migodi mbalimbali, lakini pamoja na juhudi zote hizo imeshindikana kupatikana kwao.
 
Taarifa hiyo iliendelea kusema kuwa  siku ya tukio hilo, kwenye shimo hilo kulikuwa na wachimbaji 5 ambapo 3 kati yao waliokolewa siku hiyo hiyo na wawili hawakuweza kupatikana hadi zoezi hilo la uokoaji linasitishwa.
 
Kwa upande wake Naibu Waziri Nyongo, akiongea kwa masikitiko na majozi kwenye hadhara hiyo, Nyongo amesema kwanza lililotokea ni bahati mbaya na kwamba serikali imesikitishwa na tukio hilo na kwamba iko pamoja wafiwa na wachimbaji wote.
 
Ameongeza kuwa, serikali inathamini sana hata uhai wa mtu mmoja kuliko dhahabu au madini yote yaliko chini na ndio maana inasisitiza wachimbaji kuchimba kwa kufuata utaratibu na sharia ili wachimbe kwa kuzingaatia usalama ili kuepukana na majanga kama hayo. 
 
Nyongo ametowa kauli ya serikali ya kuhitimisha shughuli za uokoaji na kutoa maelekezo kuhusu eneo hilo ambalo wachimbaji hao wamefukiwa na kifusi.
 
“Na sasa tunakwenda kufanya ibada ya kwenda kuwazika wenzetu, viongi wetu wa dini wako hapa watatuongoza katika ibada hiyo kwa ajili ya maombi. Natamka kuwa, shughuli zote za uchimbaji katika eneo ambalo tunaamini kuwa ndipo wezentu hawa wapo, basi eneo hilo litambuliwe rasmi kuwa ndio kabuli lao na kama kuna undelezaji wa shughuli ya uchimbaji utaendelea katika eneo lingine na kwa utaratibu mwingine.” alisema Nyongo.
 
Nyongo pia alitoa maagizo kwa afisa madini mkazi mkoa wa Geita na timu yake kusimamia usitishwaji wa shughuli za uchimbaji katika eneo hilo mpaka pale hatua za uzingatiaji usalama ziwe zimefuatwa ili kuepusha ajali nyingine.
 
Kwa upannde wake Mchungaji Nuhu Suleman alie ongoza ibada hiyo ya kuwaombea marehemu alisema, hapana budi kumshukuru mungu kwa kila jambo na kila jambo hukusudiwa na mungu. Amewakumbusha waumini wote kumuelekea mungu kwani yeye ndie mwenye upekee na ufalme na kwamba maisha ya binaadamu yana ukomo ni vyema kila mmoja akajiandaa na safari hiyo.


Share:

Tangazo La Kuwarejesha Wagombea Wasio Na Makosa Ya Kikanuni Kwenye Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa 2019

Zoezi la Uchukuaji fomu, Urudishaji fomu, Uteuzi, Pingamizi na Rufaa lilianza tarehe 29/10/2019 na kumalizika tarehe 9/11/2019.
 
Katika zoezi hilo jumla ya wananchi 555,036 kutoka Vyama mbalimbali vya Siasa walifanikiwa kuchukua fomu za kugombea. Na jumla ya wananchi 539,993 sawa na asilimia 97.3 walifanikiwa kurejesha fomu.
 
Wagombea kutoka Chama cha Mapinduzi waliochukua fomu walikuwa 412,872 (asilimia 74), Chama cha Demokrasia na Maendeleo walikuwa 105,937 (asilimia 19), Chama cha Wananchi CUF walikuwa 24,592 (asilimia 4), ACT Wazalendo walikuwa 8,526 (asilimia 1.5), NCCR – Mageuzi walikuwa 2,244 (asilimia 0.4) na Vyama vingine vyenye usajili
wa kudumu walichukua chini ya asilimia 0.1 kwa kila chama.
 
Katika zoezi zima la kuchukua na kurejesha fomu kulikuwa na changamoto kubwa kwa wagombea wengi kufanya makosa mengi ya kikanuni yaliyopelekea wengi wao kutoteuliwa. 

Baadhi ya makosa hayo ni pamoja na kujidhamini wenyewe, kutojaza fomu namba IV, kutofautiana kwa majina, kutojaza fomu kwa ukamilifu, kuandika umri, kukosea umri (mfano amezaliwa mwaka 2019) na makosa mengine mengi mbalimbali. Hii ilitokana na baadhi ya vyama kushindwa kuwajibika ipasavyo katika kuwaelekeza wanachama wao. Kutokana na hali hiyo pingamizi na rufaa mbalimbali zipatazo 15,380 ziliwasilishwa.
 
Hadi zoezi la maamuzi ya rufaa mbalimbali lilipohitimishwa tarehe 9/11/2019, jumla ya rufaa 4,921 (32%) zilipitishwa na zilizobaki zilikosa sifa kwa sababu mbalimbali.
 
Katika mchakato huo wa kuchukua na kurudisha fomu Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kupita bila kupingwa katika maeneo mbalimbali kwakuwa hapakuwa na mgombea yoyote kutoka Chama cha Upinzani. Kwa upande wa Wenyeviti wa Vijiji Chama cha Mapinduzi kimepita bila kupingwa katika vijiji 6,248 kati ya vijiji 12,319 sawa na asilimia 51. 

Kwa upande wa Mitaa Chama cha Mapinduzi kimepita bila kupingwa katika Mitaa 1,169 kati ya Mitaa 4,263 sawa na asilimia 27 Kwa upande wa Vitongoji Chama cha Mapinduzi kimepita bila kupingwa katika Vitongoji 37,505 kati ya Vitongoji 64,384 sawa na asilimia 58. Kwa upande wa Wajumbe wa kundi la wanawake jumla ya wajumbe 64,085 wamepita bila kupingwa na wajumbe kundi mchanganyiko jumla ya wajumbe 75,560 wamepita bila kupingwa.
 
Kwa kuwa imeonekana wazi wananchi kutoka vyama mbalimbali wamekuwa na nia kubwa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi licha ya vyama vyao kutokuweka umuhimu katika kuwaelekeza vyema wanachama wao juu ya ujazaji fomu kwa mujibu wa Kanuni. 

Mamlaka ya Uchaguzi imeona ni vyema wananchi hao kupewa nafasi ya kushiriki katika Uchaguzi kwani imejidhihirisha wazi hata baada ya vyama viwili vilivyojitoa bado wanachama wao waliendelea kuwasilisha rufaa zao ili wapewe nafasi ya kushiriki katika uchaguzi.
 
Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka 2019 Tangazo la Serikali Na. 371 la Mwaka 2019 Kanuni ya 49, Tangazo la Serikali Na. 372 la Mwaka 2019 Kanuni ya 51, Tangazo la Serikali Na. 373 la Mwaka 2019 Kanuni ya 52, na Tangazo la Serikali Na. 374 la Mwaka 2019 Kanuni ya 52 ninatoa muongozo kwamba Wagombea wote ambao walioteuliwa na kudhaminiwa na vyama vyao na kufanikiwa kurejesha fomu zao za uteuzi kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katika kipindi kilichokuwa kimepangwa cha kuchukua na kurejesha fomu kilichoanza tarehe 29*/10/2019 na kumalizika tarehe 04/11/2019 kwa Tangazo hili wanapewa sifa ya kupigiwa kura na wananchi wa Kijiji, Mtaa, au Kitongoji husika kwa ajili ya Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019 isipokuwa tu kama atakuwa amekutwa na mambo yafuatayo:
 
1. Siyo Raia wa Tanzania,
2. Hajajiandikisha katika Kijiji, Mtaa, au Kitongoji husika,
3. Amejiandikisha mara mbili,
4. Amejidhamini Mwenyewe,
5. Hajadhaminiwa na chama chake cha Siasa,
6. Wamerejesha fomu watu zaidi ya mmoja kutoka chama kimoja kwa nafasi inayofanana ya Mwenyekiti wa Kijiji, Mtaa, au Kitongoji kwa Kijiji, Mtaa, au Kitongoji husika. Msimamizi Msaidizi hata wajumuisha wagombea hao katika orodha ya wanaopaswa kupigiwa kura,
7. Amejitoa kwa mujibu wa Kanuzi za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tangazo la Serikali Na. 371 la Mwaka 2019 Kanuni ya 19, Tangazo la Serikali Na. 372 la Mwaka 2019 Kanuni ya 20, Tangazo la Serikali Na. 373 la Mwaka 2019 Kanuni ya 20, na Tangazo la Serikali Na. 374 la Mwaka 2019 Kanuni ya 20.
 
Msimamizi wa Uchaguzi ataanza kupokea ratiba za kampeni kutoka katika Vyama vya Siasa kuanzia leo hii tarehe 10/11/2019 hadi kesho jioni kwa ajili ya kuziunganisha.
 
Tarehe ya matukio na shughuli zingine zote zinazohusu Uchaguzi huu zitaendelea kwa mujibu wa Kanuzi za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2019.
 
Selemani S. Jafo (Mb.)
WAZIRI WA NCHI – TAMISEMI
10 Novemba, 2019


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger