Monday, 5 August 2019

Mbaroni kwa Kumuua Mume Wake kwa BisiBisi

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MWAJUMA Omary Malembeka (28)anadaiwa kumuua mume wake Selemani Kondo (43) mkulima na mkazi wa Chamalale,kata ya Vihingo,Mzenga ,wilayani Kisarawe mkoani Pwani, kwa kumchoma na bisibisi kwenye bega  .
 
Akithibitisha kuhusu tukio hilo,kamanda wa polisi mkoani hapo, Wankyo Nyigesa alisema mwanamke huyo alifanya maamuzi hayo kutokana na wivu wa kimapenzi.
 
Alieleza, kulikuwa na mzozo baina yao ambapo Mwajuma alimtuhumu mume wake kuwa siyo mwaminifu katika ndoa yao.
 
“Selemani aliuawa kwa kuchomwa bisibisi katika bega lake la kushoto na sehemu ya juu na mke wake huyo”alifafanua.
 
Wankyo alisema, kujichukulia sheria mkononi sio jambo la msingi kwani inaweza kuleta madhara kama ya kujeruhi ama kusababisha kifo ,na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.
 
Katika hatua nyingine, huko kijiji cha Lulenga, Ubena ,jimbo la Chalinze polisi walimkamata Kitenye Lumange ,mfugaji wa jamii ya kimasai (24) kwa kosa la wizi wa ng’ombe 13 wenye thamani ya sh.milioni 7.2 mali ya Arisen Hussein mkazi wa kijiji cha Visakazi .
 
Kamanda huyo alibainisha,wanawasaka watuhumiwa wengine walioshiriki kuiba mifugo hiyo.


Share:

Serikali Kupitia Upya Sera ya kilimo Ili Kuwanufaisha Wakulima

Serikali imesema  sera iliyopo ya sekta ya kilimo inayotumika sasa,  ndiyo cha chanzo cha wakulima kuwa masikini kutokana na kuwatumikisha  wananchi kuilisha nchi na  matajiri, huku wakiwa wanakabiliwa na changamoto kubwa.

Kutokana na hali hiyo, imesema sera imepitwa na wakati ambapo wizara  imelazimika kuanza kuipitia upya  na kuondoa  changamoto  na vikwazo kwa wakulima.

Bashe ametoa kauli hiyo  Jumamosi Agosti 3, 2019 wakati akifungua maonesho ya Nanenane  Mikoa ya Kagera,  Geita na Mwanza yaliyofanyika viwanja vya Nyamhongoro jijini Mwanza ambapo aliwapiga marufuku wakuu wa wilaya na mikoa kuwazuia wakulima kuuza chakula chao kwa kuhofia uwepo wa njaa.

Alisema kila mkulima, anajua namna anavyotunza  na kuilisha familia yake hivyo  kama kuna kiongozi anahofia uwepo wa njaa ni vema  akanunua mazao hayo  kwa bei anayotaka mkulima na kuyatunza ili yaweze kusubiria dhana aliyoiweka kichwani kwake, kwamba kutakuwapo na uhaba wa chakula.

"Nataka niwaulize hata kama tumejaza mahindi hiki kiwanja chote kama hamna hela ya kuyanunua hayo mahindi yatawasaidia? Wakulima wanalima mazao ya kilimo, ya chakula na ya biashara ili kupata uwezo wa mifuko yao.”

"Hatuwezi kujenga viwanda wakati wakulima ni masikini, haiwezekani na ili wakulima waweze kupata fedha ni lazima tuwaruhusu kufanya biashara za mazao yao pale ambapo wanaweza kuuza mazao yao,” alisema Bashe

“Sera iliyopo imepitwa na wakati  kabisa,  inawaumiza wakulima   na kuwafanya kubaki  kila mwaka kuilisha nchi na matajiri huku wao wakibaki na umasikini wao  huku kukiwapo na utitiri wa taasisi nyingi ambazo ukichunguza zimeanzishwa kwa lengo la kuwakandamiza, hii haiwezekani kama wizara tumeanza kuangalia ni taasisi gani zinatakiwa  kufutwa na kubaki  chache.

“Fedha ambazo zilikuwa zikielekezwa kwenye utitiri wa taasisi hizo, zitaelekezwa katika mfuko maalum  ambo  wizara tunatarajia kuanzisha  na kazi ya mfuko huo ni kufidia mkulima pale inapotokea mtikisiko wa bei katika soko la dunia, kama serikali hatuna uwezo wa kuthibiti bei ya soko la dunia, mfuko huo ndio utakaokuwa na kazi ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuwafikia wakulima,”alisema.

Alisema Serikali ilikuwa ikipokea fedha nyingi kutoka mataifa ya nje ili kuendeleza kilimo, lakini zilikuwa zikishia katika semina mafunzo kwa  watendaji, huku  asilimia 50 ya fedha zilizokuwa zikipokelewa ndizo  zinafika kwa wakulima.


Share:

WAZIRI UMMY ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA TANGA, ATAKA IKAMILIKE KWA WAKATI WANANCHI WAANZE KUPATA HUDUMA



 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ziara yake wa kukagua na kutembelea Hospitali ya wilaya ya Tanga na Kituo cha Afya cha Mwakidila Jijini Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazazi wilaya ya Tanga Nassoro Makau
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji mara baada ya kutembelea hospitali ya wilaya ya Tanga
 Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ziara hiyo
 MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa ziara ya WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu kulia kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mkoba
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia wakati wa ziara ya kutembelea hospitali ya wilaya ya Tanga inayojengwa eneo la Masiwani na kituo cha Afya Mwakidila
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na wakazi wa Masiwani wakati wa ziara yake kutoka kushoto ni Mganga Jiji cha Tanga CMO
 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akionyeshwa kitu na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga daudi Mayeji wakati wa ziara yake
 Sehemu ya wananchi wa Masiwani wakiwemo wazee wakimsikiliza WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu
 KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange kulia akicheza na wananchi wa Masiwani wakati wa ziara hiyo
 Muonekano wa mmoja ya majengo yaliyopo kwenye Hospitali ya wilaya ya Tanga eneo la Masiwani


 Muonekano wa mmoja ya majengo yaliyopo kwenye Hospitali ya wilaya ya Tanga eneo la Masiwani
 Muonekano wa mmoja ya majengo yaliyopo kwenye Hospitali ya wilaya ya Tanga eneo la Masiwani
 Muonekano wa Majengo kwenye Hospitali ya wilaya ya Tanga eneo la Masiwani Jijini Tanga

Muonekano wa mmoja ya majengo yaliyopo kwenye Hospitali ya wilaya ya Tanga eneo la Masiwani

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Tanga inayojengwa eneo la Masiwani Kata ya Masiwani Jijini Tanga huku akitaka umaliziaji wake umalizika kwa wakati ili wananchi waanze kupata huduma za matibabu.

Kutokana na kazi nzuri iliyofanyika kwenye Hospitali hiyo ya wilaya Waziri huyo alimpongeza Mkurugenzi wa Halamshauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji na wataalamu wengine akiwemo fundi ambao wanasimamia ujenzi huo kutokana na kujengwa kwa ufanisi mkubwa.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipofanya ziara ya kuitembelea na kukagua ujenzi wake unavyokwenda huku akionyesha kuridhishwa nao huku akimuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kuhakikisha vitu vidogo vidogo vya umaliziaji vifanyike kwa haraka.

Licha ya kutembelea hospitali hiyo lakini pia Waziri Ummy alitembelea pia ujenzi wa kituo cha Afya Mwakidila ambapo pia aliridhishwa na kasi yake huku akitaka kikamilika kwa wakati ili wananchi wa maeneo hayo wapata huduma hiyo muhimu.

Alisema kwani amepita sehemu mbalimbali Tanzania akiwa anakagua hospitali hizo huku baadhi akisema wabomboe kwenye baadhi ya maeneo kutokana na kujengwa chini ya kiwango lakini kwenye wilaya hiyo hajasema hivyo.

Waziri huyo aliwataka watumie miezi michache kumaliza kazi zilizobakia ili wananchi waanze kupata huduma hawana muda wa kusuburi hosipitali hiyo imesubiriwa kwa muda mrefu sana jiwe la msingi lililwekwa 2013.

“Maisha mangapi yamepotea kwa kukosa hospitali ya wilaya…wazee wangu na wananchi masiwani niwapongeze kutoka ndani ya moyo wangu kusimama kidete kuhakikisha kwamba hospitali inajengwa na kukamilika,tunawashukuru kwa uvumilivu kwa ushirikianao mkubwa wa kufika eneo hilo"Alisema

"Lakini pia mwenyezi mungu awazidishie heri mmetizima wajibu wenu kama wana Tanga na Tanzania maendeleo sio kama hayajaletwe yanaanza na sisi wenyewe jambo tunalosisitiza ni ushiriki wananchi katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yao yanayowazunguka”Alisema

Aidha alisema kwamba wamekubaliana na Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jafo ndani ya muda mfupi huduma zianze kutolewa ili kuondosha kero za wananchi wa maeneo hayo.

Hata hivyo aliwaomba wakazi wa masiwani kuendeee kumuombea Rais Dkt John Magufuli heri na baraka kwenye suala zao kutokana na kazi kubwa na mapinduzi makubwa aliyoyafanya kwenye sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo za Afya

Awali akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alisema kwamba huwezi kuzungunza jambo lolote la kuisifu nchi ukaacha kumtaja Rais Magufuli iwe sekta binafasi au umma kutokana na kufanya kazi kubwa ya kuwapa maendeleo watanzania.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kwamba ujenzi wa majengo saba kwenye hospitali hiyo yapo kwenye hatua umaliziaji na jengo ambalo limejengwa muda mrefu litajengwa litakuwa la utawala na wameweka utaratubu wa kutenga bajeti kulikarabati ili liweze kufafana na majengo mengine.

Alisema walipokea bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo na mpaka sasa wamekwisha kutumia zaidi ya bilioni 1.4 lakini kazi zote zinazohusiana na ujenzi huo wamewapa watu wanafanya ukamilishaji, milango, aluminiamu, watu wanaweka umeme, kazi zote na vifaa vyake zimekwisha kununuliwa.

Hata hivyo alisema kwamba mpaka sasa madaktari sita tayari wametengwa kwa ajili ya kuanzisha hospitali hiyo na wamekwisha kuandaliwa barua za kuhamishiwa kwenye hospitali hiyo.

Mwisho.
Share:

Rosa Ree Ametuletea VIDEO Mpya Itazame Hapa...Wimbo Unaitwa Nguvu za Kiume

Rapper Rosa Ree anaendelea kushusha madude ni kijidhirisha kuwa ndio Rapper Bora kwa kipindi hichi, Usiku wa Leo ameachia Dude kali linaloitwa nguvu za kiume...


Share:

LIVE: Rais Magufuli Katika Ufunguzi Wa Maonesho Ya SADC

LIVE: Rais Magufuli Katika Ufunguzi Wa Maonesho Ya SADC


Share:

TIGO YAZINDUA MTANDAO WA 3G PANGANI, TANGA

Meneja wa mauzo wa Tigo mkoani Tanga, Robert Kasulwa, akihutubia wakazi wa Madanga wilayani Pangani wakati wa hafla ya kuzindua mnara ulioboreshwa kutoka mtandao wa 2G hadi 3G
***

Kampuni inayoongoza katika maisha ya kidigitali nchini Tanzania, Tigo, imezindua mnara ulioboreshwa kutoka mtandao wa 2G hadi 3G mjini Madanga wilaya ya Pangani ili kuboresha mawasiliano katika mji huo unaojulikana kwa utajiri mkubwa kihistoria na biashara ya uvuvi.

Akiongea katika sherehe za uzinduzi katika mji wa Madanga, Meneja wa mauzo wa Tigo mkoani Tanga, Robert Kasulwa, alisema upatikanaji wa mtandao wa 3G katika eneo hilo utaleta mabadiliko chanya katika ustawi wa mji huo na ni muhimu katika kuleta maendeleo ya uchumi na kuhamasisha utengenezaji wa ajira.

"Kwa kuboresha mnara huo kutoka 2G hadi 3G katika mji wa Madanga, tunawaletea huduma bora zaidi wateja wetu kuweza kufurahia huduma za kidigitali za Tigo zinazo ongezeka kila siku na maudhui ambayo yametengenezwa kwa ajili ya elimu, burudani na biashara. Jambo hili kwa hakika litafungua fursa mpya za kibiashara na kukuza maendeleo ya kiuchumi kwa jamii"

Kasulwa alisema kwamba pamoja na spidi ya Intaneti, mtandao wa 3G una ubora zaidi katika kupiga simu na kiwango chake cha upatikanaji.

"Mteja atakayenunua kifurushi chochote cha intaneti kutoka katika mtandao ulioboreshwa kutoka 2G kwenda 3G atazawadiwa kifurushi cha 100MB kila mara atakapo nunua. Ofa hii itatumika mpaka kufikia siku 30 tangu kuzinduliwa kwa mnara," alisema.

Kuzinduliwa kwa huduma ya Tigo ya mtandao wa 3G mjini Madanga ni muendelezo wa uzinduzi wa mtandao wa aina hiyo katika kila mkoa nchi nzima.

Uzinduzi huu ni wa tisa kati ya maeneo 52 nchi nzima ambayo yako katika orodha ya uboreshwaji kwenda katika mtandao wa 3G au 4G LTE hasa katika kanda ya Kati, Pwani, Kusini, Kaskazini na kanda ya Ziwa.
Share:

TAASISI YA PASS YAMVUTIA MKUU WA MKOA KILIMANJARO KWENYE MAONESHO YA NANENANE ARUSHA

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira(kulia) na Mkuu wa wilaya ya Mbulu mkoa wa Manyara,Celestine Mofuga wakimsikiliza Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa taasisi inayounganisha wakulima na taasisi za kifedha nchini PASS,Hellen Wakuganda alipotembelea banda hilo wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya Nanenane (Kilimo, Mifugo na Uvuvi) kwenye uwanja wa Taso Njiro jijini Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira(kulia) akizungumza jambo alipotembelea banda la taasisi inayowaunganisha wakulima na taasisi za kifedha nchini PASS wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya Nanenane (Kilimo, Mifugo na Uvuvi) kwenye uwanja wa Taso Njiro jijini Arusha.


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa taasisi ya kuwezesha sekta binafsi kuwaunganisha wakulima na taasisi za kifedha nchini PASS,Hellen Wakuganda alipotembelea banda hilo kwenye uwanja wa Taso Njiro jijini Arusha.




Wafanyakazi wa PASS walio katika viwanja vua Taso Njiro jijini Arusha kuwahudumia wakulima kuongeza tija katika shughuli zao.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira ameipongeza taasisi ya Private
Agricultural Sector Support (PASS) chini ya Programu ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini kwa juhudi inazofanya kuwasaidia wakulima kuongeza tija katika shughuli zao.


Ametoa kauli hiyo wakati akifungua maonesho ya 26 ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi maarufu Nanenane katika Kanda ya Kaskazini kwenye viwanja vya Taso Njiro jijini Arusha yanayohudhuriwa na wananchi kutoka mikoa ya Kilimanjaro,Manyara na Arusha.


Amesema utendaji kazi wa taasisi ya PASS hautiliwi shaka kutokana na kupenya maeneo mengi ya vijijini kutoa elimu kwenye vikundi na kuwaunganisha wakulima wa ngazi mbalimbali na taasisi za kifedha huku PASS ikitoa dhamana.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa PASS ,Nicomed Bohay amesema taasisi hiyo inafanya kazi kama kiungo kati ya sekta ya kilimo na sekta za fedha lengo likiwa kuwawezesha kuwawezesha upatikanaji wa huduma za kifedha na kibiashara kwa wajasiriamali binafsi wa biashara za kilimo katika mnyororo mzima wa thamani.


Bohay amesema kuwa walengwa na wakulima binafsi,vyama vya ushirika,makundi ya wakulima wadogo na makampuni yanayojihusisha na kilimo.

Ameongeza kuwa hadi sasa PASS inafanya kazi na jumla ya benki 15 nchini zinazotoa mikopo kwa wakulima na makampuni yanahusiana na kilimo huku jumla ya wajasiriamali 929,172  wamenufaika na mikopo iliyodhaminiwa na taasisi hiyo inayofikia Sh 712 bilioni


Share:

DKT. MWANJELWA : SERIKALI KUPITIA TASAF YAANDAA UTARATIBU MPYA WA KUWAPATA WALENGWA WA TASAF WENYE UFANISI ZAIDI


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Burugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ambako yuko kwenye ziara ya kikazi kukagua utekelezaji
wa miradi ya TASAF na kukutana na Watumishi wa Umma kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wananchi  na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Burugo (hawapo pichani) juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Baadhi ya Wananchi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika katika kijiji cha Lukindo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani).
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa
(Mb) (katikati) akiwa nyumbani kwa mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Burugo Bi. Justa Migini (kulia kwa Naibu Waziri),wa kwanza kushoto ni Meneja wa
Miradi ya Ajira za Muda TASAF Bw. Paul Kijazi 
wakishuhudia nyumba iliyojengwa na mlengwa huyo kwa kutumia ruzuku ya TASAF.
Mmoja wa Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Burugo, Halmashauri ya Wilaya ya
Bukoba Mkoani Kagera Bi. Agnes Kemilembe akitoa ushuhuda wa namna alivyotumia ruzuku kuboresha makazi yake kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb). Picha ya chini ni mlengwa huyo akimuonesha naibu waziri shamba lake analoliendeleza kwa
kutumia ruzuku ya TASAF. 

NA ESTOM SANGA---KAGERA 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa amesema Serikali kupitia TASAF imeandaa utaratibu utakaowezesha kuorodheshwa kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini watakaokidhi vigezo vya umaskini. 

Akiwahutubia Wananchi na Walengwa wa TASAF katika vijiji vya Lukindo na Burugo katika halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Dkt. Mwanjelwa amesema utaratibu huo mpya wa kuzitambua na kuziorodhesha kaya za walengwa kwenye Mpango utahusisha matumizi ya kielektroniki na kupiga picha kwa wahusika ili kuondoa uwezekano wa kuorodhesha kaya zisizostahiki. 

Aidha Naibu Waziri huyo amesema serikali kupitia TASAF inaendelea kukamilisha maandalizi ya uzinduzi wa sehemu ya pili ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao amesema haitawapa mwanya wananchi wenye uwezo kujumuishwa kwenye Mpango huo. 

Amesema Walengwa wa Mpango huo wenye uwezo wa kufanya kazi watawekewa utaratibu wa kutekeleza miradi ya Maendeleo kwenye maeneo yao watakayoibua na kisha kulipwa ujira kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. 

Katika hatua nyingine Dkt. Mwanjelwa amewaagiza wataalamu wa sekta mbalimbali katika halmashauri za wilaya kutenga muda wa kuwatembelea Walengwa wa TASAF na kuona namna wanavyotekeleza miradi yao na kuwashauri namna bora zaidi ya kutekeleza miradi hiyo ili waweze kupata matokeo bora na yenye tija. 

Wakati huo huo ameonyesha kuridhishwa kwake na mafanikio waliyoanza kupata Walengwa wa TASAF katika Nyanja mbalimbali jambo linaloonyesha kuwa mkakati wa Serikali katika kupambana na umaskini unatekelezeka. 

Dkt. Mwanjelwa ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipotembelea vijiji vya Lukindo, na Burugo katika halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera na kukutana na Walengwa ambako amekagua shughuli wanazozifanya kwa kutumia ruzuku wanayoipata kutoka TASAF. 

Naibu Waziri huyo amesema Walengwa hao wa TASAF wameweza kubadilisha maisha yao kwa kutumia ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kwa kuboresha maisha yao hususani katika Nyanja za makazi, uchumi huku wengine wakifanikiwa kujenga nyumba zao bora ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya kupata ruzuku hiyo. 
Share:

NHIF ARUSHA YATOA HUDUMA ZA VIPIMO NA USHAURI WA AFYA BURE VIWANJA VYA NANENANE

Wananchi wakiwa katika banda la Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) kupata huduma za ushauri na kupima afya bure kwenye maonesho ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi maarufu Nanenane viwanja vya Taso Njiro jijini Arusha.

Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) mkoa wa Arusha,Miraj Kisile(kulia) akizungumza na mmoja wa wananchi waliofika katika banda hilo kwenye maonesho ya Nanenane Njiro jijini Arusha.


Mmoja wa wananchi waliotembelea banda la NHIF kwenye uwanja wa maonesho ya Nanenane jijini Arusha akipewa ushauri baada ya kupima afya bure.


Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) mkoa wa Arusha,Miraj Kisile(kulia) akizungumza na wananchi waliotembelea maonesho ya Nanenane na kufika katika banda hilo kwaajili ya kufahamu shughuli za mfuko huo na kupima afya bure.


Mmoja wa wananchi waliofika kwenye banda la NHIF kwenye viwanja vya maonesho ya Nanenane mkoa wa Arusha akifurahia maelezo yanayohusu sekta ya afya.







Share:

WCF MBIONI KUANZISHA MFUMO WA WAAJIRI NA WAFANYAKAZI KUWASILISHA MADAI YA FIDIA KIMTANDAO


 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (watatu kushoto), akizungumza jambo mbele ya Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter (katikati) na Mussa Mwambujule, Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko, wakati alipotembelea banda la WCF kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi Simiyu.
 
 Afisa Uhusiano Mwandamizi WCF, Bw. Sebera Fulgence (kulia) akitoa elimu ya Fidia kwa wafanyakazi
 Mussa Mwambujule, Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), akitoa elimu hiyo.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akisalimiana na mama huyu aliyefika banda la WCF kupata elimu ya Fidia kwa wafanyakazi



NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), hivi karibuni uko mbioni, kuanzisha mfumo wa waajiri na wafanyakazi kuwasilisha madai ya Fidia kwa njia ya mtandao, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Anselim Peter ameyasema hayo jana kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Bw.Peter alisema lengo la kuanzisha mfumo huo ni kusogeza karibu huduma za Mfuko kwa wateja wadau wake na hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma.

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi unashiriki katika maonesho ya Nanenane kwa lengo la kupata fursa ya kuwaelimisha waajiri na wafanyakazi kuhusu shughuli za Mfuko ambazo ni kulipa Fidia, utaratibu gani wa kufuata ili kuwasilisha madai kabla ya kulipwa Fidia.

"Pia katika banda la WCF hapa Nyakabindi, wataalamu wetu watatoa elimu kuhusu Mfuko, kusajiliwa, kuwafahamisha taratibu za michango, kuwafahamisha taratibu za madai ya fidia na pia kupokea maoni ya wadau kuhusu Mfuko. Lakini pia tunatoa huduma kwa vitendo jinsi wanavyoweza kufanya kazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wafanyakazi wake kwenye orodha iliyoko WCF, kuprinti cheti, na pia kulipa michango ofisini kwako.” Alifafanua Bw. Peter.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mtaka, ameupongeza Mfuko huo kutokana na ushiriki wake katika mpango wa Mkoa kujenga kiwanda cha kutengenza vifaa tiba Huu ni utekelezaji kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuanzisha na kuimarisha viwanda ambavyo vitaipeleka nchi kafika uchumi wa kati.

"Nishukuru na kutambua mchango mkubwa wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba na WCF kwa ujumla kwa sababu ni partner (Mshirika) Mkubwa kwenye mipango yetu ya ujenzi wa kiwanda cha Vifaa tiba." Alisema Mhe. Mtaka.

Alisema uongozi wa Mkoa walishirikiana na WCF katika hatua mbalimbali za kushirikiana katika ujenzi wa kiwanda hicho ambapo tayari site clearance imeshafanyika na kwamba hivi sasa wizara iko katika nafasi nzuri ya kutangaza zabuni ili kumpata mkandarasi atakayejenga kiwanda hicho.

"Kwetu sisi kama mkoa WCF imetoa ushirikiano mkubwa katika mipango yetu ya kushiriki katika uchumi wa viwanda wametoa ushirikiano mkubwa." Alisema Mkuu wa Mkoa.

Share:

Rais Maguli Leo Atafungua Rasmi Maonesho ya 4 ya wiki ya viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Dar

Rais Magufuli leo Jumatatu August 5, 2019  anatarajiwa kufungua rasmi Maonesho ya 4 ya wiki ya viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), jijini Dar es Salaam.

Maonesho haya ni utangulizi wa mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi zote 16 za SADC unaotarajiwa kufanyika hapa Dar es Salaam, Agosti 17-18.


Share:

Gari ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima Lapata Ajali Likidaiwa Kuendeshwa na mtu anayedaiwa kuwa ni mtoto wa dereva

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki amesema gari la mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima limepata ajali jana Jumapili Agosti 4, 2019 likiwa linaendeshwa na mtu anayedaiwa kuwa ni mtoto wa dereva wa mkuu huyo wa Mkoa.

Ndaki amesema ajali hiyo imetokea  jana saa 3 asubuhi na kwamba gari hilo lenye namba za usajili STL 5961 lilikuwa likiendeshwa na mtu ambaye taarifa za awali zinaeleza kuwa ni kijana wa dereva wa Malima.

"Mtoto na Baba yake wote wamelazwa Hospitali, Mtoto ana majeraha baada ya kupata ajali na gari ya Mkuu wa Mkoa na huyu baba ambaye ni Dereva wa Mkuu wa Mkoa alianguka kwa Presha tukamkimbiza Hospitali, maana alipata mshtuko bada ya kufika eneo la tukio na kuiona ajali"-Amesema


Share:

Mashambulizi mawili ya risasi Ohaio na Texas Nchini Marekani yaua watu 30

Watu kumi wameuawa kufuatia shambulizi la risasi katika mji wa Dayton, Ohio nchini Marekani. 

Polisi wamesema hayo mapema jana Jumapili na kuongeza kuwa mshambuliaj ni miongoni mwa waliouawa. 

Watu wasiopungua 16 wamejeruhiwa na wamepelekwa katika hospitali mbaimbali kwa matibabu. 

Shambulizi hilo linajiri katika muda wa saa 24, baada ya kutokea mkasa mwengine kama huo ambapo watu 20 waliuawa na 26 kujeruhiwa kwa kufyatuliwa risasi na mtu aliyekuwa na bunduki ndani ya duka moja kubwa eneo la El Paso, Texas. 

Polisi wamemkamata mwanaume anayeshukiwa kuhusika kwenye shambulizi la Texas mwenye umri miaka 21.

Msemaji wa polisi wa El Paso Robert Gomez ameeleza kuwa wengi wa wahanga katika kisa cha Texas walimiminiwa risasi katika duka la Walmart. 

Gomez ameongeza kuwa wakati wa tukio hilo kulikuwa na karibu wateja 3000 kwenye duka. 

Polisi wamesema huenda shambulizi hilo lilichochewa na chuki za ubaguzi wa rangi. 

Jumla ya watu 30 wameuawa kwenye mashambulizi hayo mawili.


Share:

Tanzania Yalaani Mauaji Ya Watu Wasio Na Hatia Marekani




Share:

Jaji Mstaafu Wa Mahakama Kuu Ya Tanzania, Mhe. Jaji Rugazia Afariki Dunia

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Projestus Aloyce Rugazia (pichani) amefariki dunia.

Mhe. Jaji Rugazia amefariki dunia alfajiri ya kuamkia Agosti 04, 2019 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa-Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Msiba upo nyumbani kwake Kinondoni- Dar es Salaam, ratiba ya taratibu za kuaga na mazishi itajulikana mapema Agosti 05, 2019.

Marehemu Jaji Rugazia alizaliwa Agosti 28, 1954 mkoani Kagera, alianza kazi rasmi Januari 01, 1983 kama Hakimu Mkazi.

Marehemu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Machi 28, 2003. Aidha; Marehemu Jaji Rugazia alistaafu rasmi Agosti 28, 2016 akitokea Mahakama Kuu-Divisheni ya Ardhi.

Mahakama ya Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo chake.

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE


IMETOLEWA NA :
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,
MAHAKAMA YA TANZANIA.


Share:

Katibu Mkuu Wizara Ya Fedha Awataka Watafiti Na Wadadisi Kuzingatia Viwango Ukusanyaji Wa Takwimu

Na Mwandishi Wetu, MAELEZO
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James amewataka wadadisi na wasimamizi wa utafiti wa sekta isiyo rasmi nchini kuzingatia viwango vya ubora katika ukusanyaji wa taarifa ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi zenye kubaini mahitaji na changamoto za sekta hiyo nchini.

Akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa Utafiti wa Sekta isiyo rasmi Nchini  jana Jumapili (Agosti 4, 2019) Jijini Dar es Salaam, Bw. James alisema matokeo ya utafiti huo yataisaidia Serikali kufahamu mchango halisi wa sekta isiyo rasmi katika Pato la taifa ikijumuisha ulipaji kodi.

Aliongeza kuwa ni ukweli ulio dhahiri kuwa sekta isiyo rasmi imekuwa nguzo muhimu katika pato la taifa kwani kulingana na utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi uliofanyika mwaka 2014 ilibainika kuwa, asilimia 21.7 ya watu waliokuwa na ajira walikuwa katika sekta isiyo rasmi, na hivyo kuleta kiashiria kuwa sekta hiyo ina mchango muhimu katika pato la taifa.

Bw.James alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejiwekea malengo mbalimbali katika kuinua uchumi wa wananchi wake ikiwemo kubaini changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta isiyo rasmi ikiwemo hali ya upatikanaji wa masoko, fursa za mikopo, ujuzi unaohitajika pamoja na matumizi ya teknolojia kwa nia ya kuongeza tija kwenye uzalishaji.

“Sina shaka na ubora wa takwimu zitakazokusanywa kwa kuwa mnaendelea kufanya kazi hii kwa karibu sana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Benki ya Dunia (WB), tumieni uzoefu wenu ili na sisi Watanzania tunufaike kuifahamu zaidi sekta hii katika kukuza uchumi wa Tanzania” alisema Bw. James.

Kwa mujibu wa Bw. James alisema utafiti wa kwanza wa kitaifa katika sekta isiyo rasmi ilifanyika nchini mwaka 1991 na kufuatiwa na utafiti kama huo katika Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1995, hivyo ni kipindi kirefu kimepita na kufanya kuwepo na mahitaji makubwa ya takwimu zinazoakisi hali halisi ya sasa ya sekta hiyo nchini.

Kwa upande wake, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa alisema hatua ya Serikali ya Awamu ya Tano kufanya utafiti huo ni uthubutu mkubwa kwa Tanzania kwa kuwa ni nchi chache za Bara la Afrika zimeweza kufanya utafiti huo kwa ajili ya kupima sekta yenyewe na upatikanaji wa rasilimali fedha sambamba na kubaini fursa za ajira kwa wananchi wengi wakiwemo wananchi maskini.

“Kama mnayofahamu Serikali kwa sasa inatekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 hadi 2020/21 ambao unahitaji takwimu katika ngazi za chini za utekezaji, ili kuongeza wigo wa hifadhi ya jamii kwa lengo la kufikia lengo la angalau asilimia 40 ya watu wenye ajira ifikapo mwaka 2020” alisema Dkt. Chuwa.

Aidha Dkt. Chuwa alisema Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu na Shirika la Kazi Duniani (ILO) imeshakamilisha maandalizi yote ya kufanyika kwa utafiti huo, unaotarajia kuanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam Mwezi Agosti hadi Novemba mwaka huu.

Dkt. Chuwa alisema muundo wa utafiti huo umegawanyika katika ngazi kuu mbili, ikiwemo ngazi ya ukusanyaji wa taarifa katika ngazi ya kaya na ngazi ya pili ni ngazi ya biashara (uchumi), ambapo katika ngazi ya kaya, utafiti huo umejikita katika maeneo ya taarifa za kidemokrasia, elimu, hali ya ulemavu, ajira, ukosefu wa ajira.

Akifafanua zaidi, Dkt. Chuwa alisema sampuli ya utafiti huo katika ngazi ya kaya pia utahusisha maeneo ya kuhesabia yapatayo 200 yaliyo mkoani Dar es Salaam na kaya zilizochaguliwa zaidi ya 2,400 pamoja na ukusanyaji wa taarifa kutoka kwenye biashara zaidi ya 4,000 na matokeo ya utafiti huo yatawezesha upatikanaji wa taarifa za kitakwimu ambazo ni wakilishi katika ngazi za Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.

MWISHO


Share:

Zoezi La Kupima Utayari Wa Kukabili Ebola La Acha Alama Mkoani Kagera

Na. OWM, KAGERA
Serikali kupitia uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na wadau wa maendeleo,   imefanikiwa kufanya zoezi la kupima utayari wa kukabili ugonjwa wa Ebola katika mkoa wa Kagera katika wilaya tatu za mkoa huo kwa kuhusisha  watoa huduma za Afya katika wilaya hizo za  Bukoba, Misenyi na Ngara.

Zoezi hilo limefanikiwa kuwaimarisha watumishi hao katika maeneo maalum ikiwemo ya uratibu, utambuzi na ufuatiliaji wa wagonjwa iwapo wakipatina, matibabu ya wagonjwa, uchukuaji na usafirishaji wa sampuli na kuthibitisha maabukizi pamoja kuimarisha mifumo ya utambuzi wa masuala ya Afya kwa kila abiria wanaopita kwenye mipaka ya mkoa wa Kagera.

Akiongea kuhusu kuhitimishwa kwa zoezi hilo jana tarehe  3 Agosti, 2019, mkoani Kagera, Mkurugenzi Msaidizi (Utafiti na Mipango), Idara ya Menejimenti ya Maafa,   ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu, ameeleza kuwa watumishi wa sekta ya Afya katika maeneo yote ambayo zoezi hilo limefanyika wameweza kuimarishwa katika suala la  uratibu hususani katika kuhakikisha kuwa rasilimali zote zinazohitajika pindi ikigundulika kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola zinapatikana kwa wakati na kwa kutosheleza mahitaji pamoja na kutumika kwa usahihi.

Aidha, Mratibu wa zoezi hilo toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, ambaye pia ni Mtaalamu wa Afya ya Jamii, Dharura na Maafa,  Dkt. Faraja Msemwa amefafanua kuwa timu ya  wataalamu wa sekta za Afya na Uratibu wa Shughuli za serikali, kutoka Wizarani, Idara na Mashirika ya Kimataifa,   wamefanikiwa kuendesha   zoezi hilo kwa watoa huduma wa Afya kwa wilaya tatu za mkoa huo hususan zilizopo  mipakani.

“Zoezi letu tumefanikiwa  kulihitimisha mkoani hapa tayari kwa kufanya zoezi la kupima utayari wa kukabili ugonjwa wa Ebola kwa watoa huduma wa Afya kwa vituo vya Afya vya  Nshambya, Kabyaile, Kabanga, Bunazi pamoja na Hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Bukoba.Tunaamini kufanikiwa kufanya zoezi hili limeboresha utendeji wa watoa huduma hao katika kukabili ugonjwa wa Ebloa” alisema Dkt. Msemwa

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Marco Mbata amefafanua kuwa kufanyika kwa zoezi hilo mkoani humo kumewawezesha kujua maeneo gani ya kuboresha wakati wa ugonjwa wa Ebola na watumishi  wameelewa kwa vitendo wapo tayari kukabili ugonjwa huo.

“Tunashukuru vifaa tunavyo vya kutumia wakati wa kujikinga iwapo atatokea mgonjwa wa Ebola, hivyo kupitia zoezi hili tumeongeza uelewa wa kujikinga wenyewe, kuwakiknga watu walio karibu na mgonjwa pamoja na jamii nzima. Tumeweza kujifunza jinsi ya kumpokea mgonjwa, kuchukua vipimo hakika zoezi hili limetujenga  ” alisisitiza Mbata.

Naye Mratibu wa Vituo vya Mipakani, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Remedius Kakuru amebainisha kuwa kupitia zoezi hilo limeimarisha utendaji wa maafisa Afya wa mipakani kwa kuzingatia kuwa  tayari serikali imenunua vifaa vya kisasa muhimu vinavyo hitajika kwa ajili ya utambuzi wa abiria mwenye maambukizi ya ugonjwa wa Ebola ikiwemo Vipima  joto la mwili “themo scanners”.Vifaa hivyo  vyenye uwezo wa kupima joto la mwili la abiria wanao pita katika mipaka ya Tanzania vina uwezo wa kupima joto la mwili kwa kuwa ndiyo kiashiria  kikuu kimojawapo kwa mgonjwa mwenye maabukizi ya Ebola .

Kwa upande wake Afisa  anayeshughulika na Magonjwa ya Mlipuko kutoka Shirika la Afya Duniani, hapa nchini, Anthony Kazoka alieleza kuwa Shirika la Afya Duniani linaendelea kushirikiana na serikalai ya Tanzania katika kulinda Afya za watu wake kwa kutoa utaalamu katika zoezi hilo  kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimo hatarini kupata mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Hivyo kwa kufanyika zoezi  hilo kwa mafanikio kutasaidia Tanzania kuwa salama na kuwa chanzo cha kuiweka Dunia salama kwa kutambua maabukizi ya ugonjwa huo mapema iwapo yatatokea.


Kufuatia nchi ya jirani (DRC) kuendelea kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu Agosti mwaka 2018. Tanzania imeendelea kuchukua tahadhari za ugonjwa huo kwa kupima utayari wa Watoa huduma za Afya kwa mikoa ya mipakani ukiwemo mkoa wa Kagera. Mkoa huo ambao unapakana na nchi ya Uganda ambayo  inapakana na DRC lakini pia  imekuwa na wagonjwa kadhaa wa Ebola.

Zoezi hilo linaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo ambao ni WHO, FAO, USAID, HRH2030, na USAID Global Health Supply Chain Programu. Zoezi hilo limefanyika kwa muda wa wiki moja ambapo limekamilika tarehe 3 Agosti mwaka 2019, kwa kufanyika  katika vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo ya mipaka ya  mkoani  wa Kagera.

MWISHO.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger