Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira(kulia) na Mkuu wa wilaya ya Mbulu mkoa wa Manyara,Celestine Mofuga wakimsikiliza Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa taasisi inayounganisha wakulima na taasisi za kifedha nchini PASS,Hellen Wakuganda alipotembelea banda hilo wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya Nanenane (Kilimo, Mifugo na Uvuvi) kwenye uwanja wa Taso Njiro jijini Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira(kulia) akizungumza jambo alipotembelea banda la taasisi inayowaunganisha wakulima na taasisi za kifedha nchini PASS wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya Nanenane (Kilimo, Mifugo na Uvuvi) kwenye uwanja wa Taso Njiro jijini Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira(kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa taasisi ya kuwezesha sekta binafsi kuwaunganisha wakulima na taasisi za kifedha nchini PASS,Hellen Wakuganda alipotembelea banda hilo kwenye uwanja wa Taso Njiro jijini Arusha.
Wafanyakazi wa PASS walio katika viwanja vua Taso Njiro jijini Arusha kuwahudumia wakulima kuongeza tija katika shughuli zao.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira ameipongeza taasisi ya Private
Agricultural Sector Support (PASS) chini ya Programu ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini kwa juhudi inazofanya kuwasaidia wakulima kuongeza tija katika shughuli zao.
Ametoa kauli hiyo wakati akifungua maonesho ya 26 ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi maarufu Nanenane katika Kanda ya Kaskazini kwenye viwanja vya Taso Njiro jijini Arusha yanayohudhuriwa na wananchi kutoka mikoa ya Kilimanjaro,Manyara na Arusha.
Amesema utendaji kazi wa taasisi ya PASS hautiliwi shaka kutokana na kupenya maeneo mengi ya vijijini kutoa elimu kwenye vikundi na kuwaunganisha wakulima wa ngazi mbalimbali na taasisi za kifedha huku PASS ikitoa dhamana.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa PASS ,Nicomed Bohay amesema taasisi hiyo inafanya kazi kama kiungo kati ya sekta ya kilimo na sekta za fedha lengo likiwa kuwawezesha kuwawezesha upatikanaji wa huduma za kifedha na kibiashara kwa wajasiriamali binafsi wa biashara za kilimo katika mnyororo mzima wa thamani.
Bohay amesema kuwa walengwa na wakulima binafsi,vyama vya ushirika,makundi ya wakulima wadogo na makampuni yanayojihusisha na kilimo.
Ameongeza kuwa hadi sasa PASS inafanya kazi na jumla ya benki 15 nchini zinazotoa mikopo kwa wakulima na makampuni yanahusiana na kilimo huku jumla ya wajasiriamali 929,172 wamenufaika na mikopo iliyodhaminiwa na taasisi hiyo inayofikia Sh 712 bilioni
0 comments:
Post a Comment