Monday, 8 July 2019

TFF YAMTUMBUA AMUNIKE STARS

Shirikisho la Soka Nchini Tanzania limetangaza kuachana na kocha wa timu ya taifa Taifa Stars Emmanuel Amunike mara baada ya kufikia makubaliano ya pamoja kwa pande zote mbili kusitisha mkataba baina yao. 

Taarifa ya Shirikisho la Kabumbu Nchini Tanzania kwenda kwa vyombo vya Habari inasema kuwa Kocha atakayeiongoza Stars katika michezo ya CHAN atatangazwa hivi karibuni. 
Makocha wa muda watangazwa baada ya kamati ya Dharura ya kamati ya utendaji (Emergency Committee) itakapokutana Julai 11,2019. 

Huku mchakato wa kumpata Kocha mpya ukiwa umeanza mara moja.
Share:

AGIZO LA WAZIRI JAFO LATEKELEZWA KWA VITENDO WILAYANI PANGANI



KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mkoani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani akiwa na viongozi wengine wa Halamshauri hiyo wakati walipotembelea shule za Msingi Pangani na shule ya Sekondari Funguni kufuatilia utekelezaji wa agizo la Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jaffo la kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa nchini wanaimba nyimbo tatu za uzalendo ikiwemo ule wa Taifa,Tazama Ramani na Naipenda Tanzania
KATIBU Tawala wa KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mkoani Mwalimu Hassani Nyange akiuzngumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani akiwa na viongozi wengine wa Halamshauri hiyo wakati walipotembelea shule za Msingi Pangani na shule ya Sekondari Funguni kufuatilia utekelezaji wa agizo la Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jaffo la kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa nchini wanaimba nyimbo za uzalendo ikiwemo ule wa Taifa,Tazama Ramani na Naipenda Tanzania kulia ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George
Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George kushoto akiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange kulia wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuzungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani wakimsikiliza kwa umakini Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani
KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Funguni
AGIZO La Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jaffo la kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa nchini wanaimba nyimbo za uzalendo ikiwemo ule wa Taifa,Tazama Ramani na Naipenda Tanzania limeanza kutekelezwa kwa vitendo wilayani Pangani mkoani Tanga.

Utekelezaji huo umeanza leo Julai 8 mwaka huu kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo wilayani humo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo kutembelea shule za Msingi Pangani na shule ya Sekondari Funguni kufuatilia utekelezaji huo.

Agizo hilo la Waziri Jaffo alilitoa hivi karibuni wakati akifunga mashindano ya Michezo ya Umoja wa shule za Msingi Tanzania (Umitashumta) yaliyokuwa yakifanyika mkoani Mtwara ambapo aliagiza kwamba wakati wanafunzi watakapofungua shule wanatakiwa kuimba nyimbo tatu kabla ya kuingia madarasani asubuhi Nyimbo hizo ni wimbo wa Taifa,Wimbo wa Uzalendo (Tanzania tanzania) na Tazama Ramani utaona nchi nzuri kwa maafisa elimu Kata na wakuu wa shule wasimamie hilo.

Akizungumza mara baada kikao cha wadau wa elimu kilichohusisha wakuu wa shule za msingi na sekondari,Waratibu Elimu Kata,Watu wa tume ya Utumishi wa walimu wa kudhibiti ubora wa elimu ambacho kilikuwa ni mahususi ya kuona namna ya kuendeleza utekelezaji wa agizo hilo na baadae kutembelea kwenye shule hizo kuona namna wanafunzi wanavyoweza kuimba nyimbo za uzalendo wanapokuwa shuleni na hivyo kujiridhisha.

Alisema kwamba wao kama wilaya wataendelea kulisimamia ipasavyo na kulitekeleza agizo hilo kwa vitendo huku wakianza na hatua ya kwanza kwa kuwaita kwenye kikao hicho huku akimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Isaya Mbenje na Wakuu wa Idara kwa kuweka mikakati ya kuona namna gani agizo hilo linatekelezwa kwa kuhakikisha wanaandika upya kwenye makaratasi na kubandikwa kila darasa wanalosoma wanafunzi.

"Lakini kubwa ni kwamba kila mwanafunzi achague kwenye somo wanayosoma achukue daftari moja aandika nyimbo hizo vizuri kwa nyuma kujikumbusha mara kwa mara kwa lengo la kuweza kuutambua na kuweza kuimba kwa ufasaha zaidi kila wakati ",alisema.

Hata hivyo Katibu Tawala huyo aliwaagiza Waratibu wa kata wahakikishe maelekezo yaliyotolewa yanafanyiwa kazi na kupita kwenye kukagua kuona kama nyimbo hizo zimefundishwa.

Awali akizungumza Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George alisema kwamba wamefika kwenye shule hizo kutekeleza agizo la Jafoi shule zao zirudi kwenye msingi ya kukumbushia nyimbo za uzalendo kwa wanafunzi.

Alisema pia wataendelea kuwajenga vijana kuhusu uzalendo wakiwa wadogo ili kutengeneza Taifa Bora la kesho ambalo litakuwa chachu ya maendeleo kwa watanzania

Naye Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Pangani Isaya Mbenje alisema kwamba ni imani yake kwamba watendaji wa sekta ya elimu watakwenda kufanyia kazi kwa kuweka uelewa wa pamoja.

Alisema kwamba uelewa huo unaweza kuwasaidia kuona namna ya utekelezaji wa agizo hilo la serikali katika kujenga nidhamu,uzalendo wa vijana wa shule za msingi na sekondari za serikali wilayani humo.

Hata hivyo naye pia Afisa Elimu Taaluma wa wilaya ya Pangani Marietha alisema kwamba wanamshukuru Waziri Jaffo ambaye alihuisha uzalendo wa nchi kutokana na kwamba watu walikuwa wamejisahau sana nyimbo hizo miaka ya nyuma zilizokuwa ngao lakini kutokana na kwamba hapo katikati walipotea na kusahau hivyo wanahaidi kufanya vizuri sana
Share:

IGP SIRRO AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE AJALI ILIYOUA WAFANYAKAZI WA AZAM TV

Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro ameagiza kufanyika uchunguzi kubaini chanzo cha ajali ya magari mawili iliyotekea eneo la Shelui mkoani Singida na kusababisha vifo vya watu saba wakiwemo wafanyakazi watano wa kampuni ya Azam Media (pichani).

Akizungumza jijini Mwanza leo Jumatatu Julai 8, 2019 katika ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za polisi eneo la Myamhongolo, IGP Sirro ameuagiza uongozi wa jeshi hilo mkoani Singida kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote atakayebainika kuwa chanzo cha ajali hiyo iliyojeruhi wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa uzalishaji vipindi wa kampuni ya Azam Media, Yahya Mohamed, waliofariki dunia katika ajali hiyo iliyotokea asubuhi ya leo ni Salim Mhando, Florence Ndibalema, Said Haji, Sylvanus Kasongo na Charles Wandwi.

Madereva wa Coaster lililokuwa limewapakia wafanyakazi 10 wa kampuni hiyo, pamoja na dereva wa lori pia wamefariki katika ajali hiyo iliyotokea wakati wafanyakazi hao wakiwa njiani kwenda wilaya ya Chato Mkoa wa Geita nchini Tanzania kuripoti tukio la uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Chato-Burigi.
Share:

Mahakama ya ICC yamkuta Ntaganda na makosa ya jinai ya kivita

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC mjini The Hague imemtia hatiani mbabe wa zamani wa kivita wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bosco Ntaganda kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.

Ntaganda, ambaye alishikilia hana hatia wakati wa kipindi cha miaka mitatu ya kusikilizwa kwa kesi dhidi yake, anakabiliwa na kifungo cha maisha jela baada ya kukutikana na hatia leo katika mahakama ya kimataifa ya ICC. 

Hakuonyesha hisia zozote wakati jaji aliyesimamia kesi hiyo, Robet Fremr, alipopitisha hukumu hiyo. Ntaganda alitiwa hatiani mara ya kwanza mnamo mwaka 2006 na kuwa ishara ya kufanya uhalifu bila hofu ya kuchukuliwa hatua kisheria katika bara la Afrika, akihudumu kama jenerali katika jeshi la Congo kabla ya kujisalimisha mwaka 2013 wakati nguvu zake ziliposambaratika.

Ntaganda mwenye umri wa miaka 45 alishtakiwa kwa kusimamia mauaji ya raia na wanajeshi wake katika eneo linalokabiliwa na machafuko na lenye utajiri wa madini la Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkorasia ya Congo mnamo mwaka 2002 na 2003.

Waendesha mashitaka walitoa taarifa za kina za kutisha za wahanga wakiwamo baadhi waliopasuliwa matumbo na koo zao, kama sehemu ya ushahidi katika kipindi cha miaka mitatu ya kusikilizwa kwa kesi yake katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC mjini The Hague.

Ntaganda, aliwaambia majaji wakati wa kesi yake kwamba alikuwa mwanajeshi na wala sio muhalifu na kwamba jina la utani la "Terminator" halimhusu. 

Mzaliwa huyo wa Rwanda anakabiliwa na mashitaka 13 ya uhalifu wa kivita na mashitaka matano ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa jukumu lake wakati wa machafuko ya kinyama yaliyotokea eneo la kaskazini mashariki mwa Congo. 

Mashitaka hayo yanajumuisha mauaji, ubakaji, kuwasajili watoto kama wanajeshi na kuwanyanyasa kingono, uporaji na kuwalazimisha raia kuyakimbia makazi yao. 

Ntaganda ameyakanusha mashitaka yote dhidi yake katika kesi inayomkabili, ambayo ilianza kusikilizwa mnamo Septemba 2015 mjini The Hague.
 


Share:

Picha : HAWA NDIYO WAFANYAKAZI WA AZAM TV WALIOFARIKI KWENYE AJALI SINGIDA

Wafanyakazi watano wa kampuni ya Azam Media wamefariki dunia leo Jumatatu Julai 8, 2019 katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Shelui mkoani Singida baada ya gari aina ya Coaster walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori.

Mkurugenzi wa uzalishaji vipindi wa kampuni hiyo, Yahya Mohamed amewataja waliofariki dunia kuwa ni Salim Mhando, Florence Ndibalema, Said Haji, Sylvanus Kasongo na Charles Wandwi.

Mbali na wafanyakazi hao, watu wengine wawili wamefariki dunia katika ajali hiyo ambao ni madereva wa Coaster lililokuwa limewapakia wafanyakazi 10 wa kampuni hiyo, pamoja na dereva wa lori.

Wafanyakazi hao walikuwa wakielekea wilayani Chato Mkoa wa Geita katika uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Chato-Burigi.
Share:

Toa Mikunjo Usoni,Michirizi,Makovu, Kuza Nywele zako na Hawa Jamaa

Kessy_product_cosmetics:

            🍅🥒🍒👇

1- Kutoa Mvi Sugu Pia Zakuzala @130,000/

2-Kuza Nywele Na Kuzijaza Bila Kukatika@120,000/

3-Tengeneza Umbo Lako
4-Toa Mikunjo Uson Makonyanz(Ngozi Yakuzeeeka)90,000/

5-Toa Kitambi Na nyama Za pemben

6-Punguza Mwili Mzima @130,000/

7-Ongeza Unene Wa Mwili @100,000/

8-Towa Michirizi (Strech Mark)90,000/

9-Kutoa Alam, Chunusi,makovu Madoa@80,000/

10-Toa Ndevu Na Vinyweleo@100,000/

11-Ongeza Mguu Kam Bia@100,000/

12-Kama Umepoteza Hamu Yakula @100,000/

13-Towa Weusi Mapajani Mikononi@80,000/

14-Pata Mikanda Yakutowa Tumbo Kabisa *wakawaid@100,000/

*wenye Daw@150,000/

*waumeme@200,000/

15-Ngiri Ainazote@90,000/

16-Rudisha Nywele Kichwani(Kipara@15,000

17-Toa Harufu Sehem mbaya kwapani@100,000/

            🍍🍒🥬👇

Akikisha Unaongea Na Kessy Kwa Maelekezo

Tunapatikana Dar, K Koo,posta, Sinza

_+225_

0719955528

0756259180

0785371237

*Delivery  Popote Ulipo


Share:

Nyongo: Serikali Ipo Macho Masaa 24 Kulinda Rasilimali Za Madini

Na Mwandishi Wetu,MAELEZO
NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema Serikali ipo macho masaa 24 katika siku 7 za wiki na itaendelea kuwabaini kuwakamata na kuwatia hatiani watoroshaji wa madini sambamba na kulinda rasilimali hizo, kwa kuwa watoroshaji hao wamekuwa wakiwahujumu Watanzania  na kurudisha nyuma maendeleo yao.
 
Akizungumza katika Kongamano baina ya Wadau wa Madini lililoandaliwa na Tume ya Madini kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Baiashara Tanzania (TANTRADE) leo (Jumatatu Julai 8, 2019) katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Waziri Nyongo alisema kitendo cha utoroshaji wa madini ni kosa kisheria na hivyo Wafanyabiashara wote wanatakiwa kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali.
 
Kwa mujibu wa Waziri Nyongo katika mwaka wa fedha 2018/19 Serikali kupitia Tume ya Madini imevunja rekodi katika  ukusanyaji wa mapato ya madini hatua iliyotokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, ambapo kiasi cha Tsh Bilioni 310 ziliweza kukusanywa hatua iliyotokana na kudhibiti mianya ya utoroshaji wa rasilimali za madini.
 
“Tangu uhuru nchi yetu haikuwahi kukusanya kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni mapato yatokanayo na madini ya kiasi cha Tsh Bilioni 310, hivyo Serikali itaendelea kuweka mkazo kuzuia njia za panya ambazo zimekuwa zikitumiwa na watoroshaji wa madini kutorosha madini yetu na hivyo kuikosesha Serikali mapato” alisema Nyongo.
 
Aidha Waziri Nyongo alisema katika mwaka wa fedha 2019/2020 Serikali kupitia Tume ya Madini imepanga kukusanya kiasi cha Tsh Bilioni 470 na hivyo aliwataka watendaji wa Tume hiyo kuhakikisha kuwa malengo hayo yanafikiwa kwa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu ikiwemo kuendelea kuwafichua na kuwakamata Wafanyabiashara wasiotaka kufuata sheria.
 
Naibu Waziri Nyongo alisema Serikali kupitia Tume ya Madini kamwe haitomwonea mfanyabiashara yoyote anayafanya biashara zake kwa kufuata sheria ikiwemo kuuza madini yake katika masoko yaliyofunguliwa na Serikali kwani kwa kufanya hivyo kutawezesha Serikali kukusanya kodi yake pamoja na kuweza kuongeza  mapato ya serikali.
 
Aliongeza kuwa hadi sasa kuna jumla ya masoko ya madini 29 yaliyofunguliwa katika maeneo mbalimbali nchini na kusema Serikali imeweza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara kuuza madini katika maeneo hayo katika masoko hayo kwa kuwa ni salama kwao na pia yataiwezesha Serikali kutambua kiasi cha madini kinachozalishwa  na kuuzwa nchini.
 
Akifafanua zaidi Naibu Waziri Nyongo aliitaka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuendelea kujenga mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini ikiwemo kuwatafutia masoko na kuwatakutanisha mara kwa mara ili kuweza kutambuana pamoja na kuweza kupeana ujuzi na maarifa mbalimbali.
 
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Zanzibar, Latifa Hamisi alisema Ofisi yake itaendelea kuimarisha ushiriakiano na wadau wote wa sekta ya biashara nchini ikiwemo wadau wa madini kwa kuwajengea uwezo sambamba na kuwafutia masoko ya uhakika wa bidhaa zao ndani na nje ya nchi.
 
Aliongeza kuwa TANTRADE itaendelea kutumia majukwaa yake ya kibiashara ikiwemo mikutano ya mara kwa mara baina yake na Wafanyabiashara pamoja na kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara hao ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa bora zinazokithi masoko ya ndani na nje ya nchi.
 
Naye Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Madini Nchini (FEMATA) John Bina aliiomba TANTRADE kuweka utaratibu wa kuwatembelea wachimbaji wadogo wa madini katika maeneo mbalimbali nchini ili kuweza kuzitambua changamoto zao kwa kuwa kupitia utaratibu huo utawawezesha kutambua mchango wao katika uzalishaji wa madini na nafasi waliyonayo katika kukuza uchumi wa nchi.


Share:

Kigwangalla, January Makamba Waombana Msamaha

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla, amemuomba msamaha Waziri wa Mazingira, Mhe. Januari Makamba baada ya mvutano waliokuwa nao katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Majibizano hayo yalianza baada ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kudai kuwa inatarajia kuanzisha usafiri mpya wa kutumia magari ya umeme yanayopita kwenye nyaya (Cable Cars), kwa ajili ya kupeleka watalii katika mlima Kilimanjaro.

Waziri Makamba aliamua kujibu kwa kuandika, ''inabidi watu wa Mazingira tupitishe na kutoa cheti kwanza kabla hawajaanza. Na tutafanya 'studies' ili kujua madhara kwa mazingira na uthabiti wa 'mitigation measures".

Baada ya hapo, Waziri Kigwangalla alikuja tena na kutoa maelezo ya pili kuhusu TANAPA, "hivi kuna nchi ngapi zimeweka Cable Cars kwenye milima yake?, hizi haziharibu mazingira?, Cable inapita juu inaharibu mazingira gani?. Zaidi ya hekari 350,000/- za misitu zinapotea kila mwaka nchini, ipi ni risk kubwa? ‘Watu wa mazingira’ wamechukua hatua gani zaidi ya makongamano tu?".

Na leo Julai 8, 2019, kupitia ukurasa wake, Waziri Kingwangalla ameamua kumaliza malumbano hayo akikiri kuwa hakukuwa na haja ya kupeleka Twitter mjadala huo.

''Ni Jumatatu njema. Tunaanza upya. Tufunge. Mtani wangu Mhe. January Makamba anajua wazi kuwa kila mradi tunaofanya unafanyiwa EIA, hakukuwa na haja ya kuleta twitani jambo lile, lakini yameisha. All good. Tusameheane kwa yote. Wakimbu wangu walikaa vibaya jana nili-overreact!''

Kwa upande wake, Makamba ameandika, “Ndugu yangu, naomba hili jambo liishe. Tunajenga nyumba moja ya Watanzania. Hii ni kazi ya umma leo upo kesho haupo, tulipoghafirika tusameheane na sasa tutazame mpira #AFCON2019.”



Share:

Kizaazaa : MAITI 'AFUFUKA' AKIZIKWA

Kumeshuhudiwa kizazaa kwenye mtaa mmoja nchini India baada ya jamaa aliyedhaniwa kufariki 'kufufuka' wakati wa shughuli ya mazishi yake.

 Mohammad Furqan, kutoka mtaa wa Uttar Pradesh, alikuwa amelazwa katika hospitali moja mnamo Juni 21, 2019 na akatangazwa kufariki.

Kulingana na gazeti la Hindustan Times, Furqan alikuwa amehusika katika ajali ya barabara iliyomwacha katika hali mbaya.

 Huku akiwa amelazwa kwenye hospitali hiyo, familia yake iliambia usimamizi wa kituo hicho cha afya kuwa hawakuwa na fedha za kugharamia malipo. 

Ni hapo ambapo famili ilijulishwa kuwa jamaa wao alikuwa 'amefariki'. 

Furqan alipelekwa nyumbani na shughuli za mazishi zikaanza. Huku shughuli hizo zikiendelea, 'maiti' alionekana akiamka na kuzua kizazaa huku waombolezaji wakiwa mguu niponye kila mmoja. 

"Tulikuwa tunaendelea na shughuli za mazishi wakati ambapo tuliona maiti akiamka. Alikimbizwa katika hospitali ya Ram Manohar Lohia na madaktari wakasema hakuwa amefariki" nduguye Furqan aliambia gazeti hilo. 

Furqan inaarifiwa yuko katika hali mahututi lakini madaktari wanasema yungali hai. 

Daktari mkuu wa Lucknow Narendra Agarwal alithibitisha tukio hilo na kusema litachunguzwa zaidi. 
Share:

RATIBA YA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA MSIMU WA 2019/20 YATANGAZWA


Afisa Mtendaji Mkuu wa TPBL, Boniface Wambura

Bodi ya Ligi nchini (TPLB) imetangaza ratiba ya Ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20.

Akiongea leo mbele ya wanahabari Afisa Mtendaji mkuu wa Bodi hiyo Boniface Wambura, amesema mchezo wa ufunguzi utapigwa Agosti 23, 2019 kati ya mabingwa watetezi Simba dhidi ya JKT Tanzania.

Wambura amesema wiki moja kabla ya mchezo huo utapigwa mchezo wa Ngao ya Jamii ambao huwakutanisha Mabingwa wa Ligi ambao ni Simba na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho ambao ni Azam FC. Mchezo huo utapigwa Agosti 17, 2019.

"Msimu huu tumezingatia ratiba zote za kimataifa na hatutarajii mabadiliko ya ratiba kwa sababu zizisokuwa za msingi", amesema Wambura.

Kwa upande wa mchezo wa watani wa jadi raundi kwanza utapigwa Januari 4, 2020. Katika mchezo huo Simba watakuwa wenyeji wa Yanga kwenye uwanja wa taifa.
Share:

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI NCHINI MISRI KWENYE ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri Mkuu ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly, wakati akiwasili mjini Cairo Misri kwa ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo, Julai 8.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri Mkuu ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly, baada ya kuwasili mjini Cairo Misri kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, Julai 8.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Share:

RAIS MAGUFULI AWALILIA WAFANYAKAZI WATANO WA AZAM TV,MADEREVA WALIOFARIKI KWENYE AJALI LEO

Share:

Mwakyembe Azungumzia Hatima Ya Kocha wa Taifa Stars Amunike

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison G. Mwakyembe amesema mashindano ya kombe la mataifa barani Afrika mwaka 2019 yanayoendelea kufanyika nchini Misri, yamebeba uzito wa kipekee kwa nchi ya Tanzania baada ya kukaa nje kwa miaka thelathini na tisa(39) na kufuzu kushiriki katika mashindano hayo ambayo Timu ya Taifa ya Tanzania imetupwa nje katika hatua ya makundi  baada ya kupambana na timu za Senegal, Algeria na Kenya.
 
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari tarehe 6 Julai, 2019 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Raia wa Nigeria Emmanuel Amunike katika hotel ya Protea Courtyard Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa bado ana imani kubwa na Kocha huyo kuendelea kufanya vizuri ,kinachohitajika ni swala la muda tu, kwani amemueleza mipango mikubwa ya kiufundi aliyonayo kwa Timu ya Taifa hili iweze kufanya vizuri katika mashindano yajayo.
 
“Ndugu waandishi wa Habari kwanza kabisa niseme tu kwamba, nimefurahi sana kukutana na kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, ambapo lengo la kukutana naye ni kunieleza kilichotokea kule nchini Misri katika mashindano ya Afcon ambayo tumeshiriki baada ya miaka 39 kupita, 

"Mashindano haya yamebeba uzito wa kipekee kwa nchi yetu, na niseme tu kwamba nina imani kubwa sana na kocha Amunike kuendelea kufanya vizuri na yetu, nimeongea naye mambo mengi sana kuhusu mashindano, na tumeona kama Wizara tumpe muda zaidi kwa mipango mizuri ya kiufundi aliyonayo kwa Timu ya Taifa hili iweze kufanya vizuri katika mashindano yajayo,”.
 
“Mimi nimefurahi sana kukaa na mwalimu, na yeye pia amefurahi kukaa na Serikali, ili tujuwe mwenzetu maoni yake ni nini kuhusu timu ya Taifa, tufanyaje kujipanga hili kesho, kesho kutwa turejee tena Afcon lakini safari hii tukirejea kila mtu awe na wasiwasi kuwa hii sio timu nzuri kukutana nayo

"Ametupa mfano mzuri sana, kwamba Uganda mwaka 2015 iliposhiriki mara mwisho haikufanya vizuri hata kidogo, lakini wenzetu wakarudi wakaanza kuyafanyia kazi mapungufu katika mchezo wao, badala ya kukaa mwaka mzima mnalumbana na kunyoosheana vidole, mapungufu kwenye timu ya kiufundi na sisi kwa upande wetu yamejitokeza sana, 

"Mengi sitayasema kwa sababu ni mambo ambayo tutakaa na vyombo vinavyohusika, lakini cha msingi tunafurahi sana mwalimu ana moyo chanya kwamba tunaweza, tumeonyesha watanzania kwamba tunaweza, lakini kiufundi inatakiwa na sisi tujiongeze,” alisema Mheshimiwa Mwakyembe.
 
Aidha Mheshimiwa Mwakyembe amesema Kocha Amunike amependekeza mazoezi zaidi kwa wachezaji wa Timu ya Taifa pamoja na kucheza mechi za kirafiki kimataifa mara Tatu kwa Mwaka hili kuweza kupata uzoefu zaidi katika mashindano ya kimataifa.
 
“Tatizo lililojitokeza ambalo mwalimu anadhani linaweza kutatuliwa ni mazoezi kwa timu ya Taifa,kwamba angalau mara tatu timu ya Taifa kila mwaka ikawa na mechi za kirafiki, wanaitwa leo wanacheza na Zambia , na Afrika Kusini, tumewakaribisha pengine Spain wanakuja na kuangalia mbuga za wanyama, tunajenga imani ya wachezaji wetu, kwenye mashindano haya yaliyopita tumeona kuna wakati wachezaji wetu walikosa kujiamini, unaona mchezo kadri unavyoendelea ndio sasa hata pasi za uwakika ndio zinapigwa, kwa hiyo ni kujiamini lakini vijana wa Tanzania walicheza vizuri sanaa,” alisema Mwakyembe.   


Share:

Wafanyakazi Azam Media wapata ajali wakielekea Chato

Wafanyakazi wa Azam Media wamepata ajali ya gari mkoani Singida leo Julai 8 mwaka 2019.

Kwa Mujibu wa taarifa za awali zinadai kuwa katika ajali hiyo kuna waliopoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Walikuwa wanakwenda Chato kikazi kwa ajili ya kuonesha LIVE moja ya matukio ya Rais Dkt.John Magufuli.


Share:

Breaking : GARI LA AZAM TV LAPATA AJALI..WATU SABA WAFARIKI, WATATU WAJERUHIWA


Watu saba wanasadikiwa kupoteza maisha na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia ajali ya gari la Azam Tv iliyotokea asubuhi hii Jumatatu Julai 8,2019 katika eneo la Malendi wilayani Iramba mkoani Singida.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa gari Hilo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Chato.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Igunga Merichad Magongo amethibitisha kupokea majeruhi watatu katika hospitali ya Igunga.
Tutakuletea taarifa zaidi hivi punde
Share:

Polisi Dodoma wamuua Jambazi Sugu

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limemuua kwa kumpiga risasi mtuhumiwa sugu wa ujambazi aliyefahamika kwa jina la Sostenes Muganyizi  maarufu Rasta aliyeuawa baada ya kujaribu kurushiana risasi na askari polisi katika mtaa wa Ubemebeni wilayani Kondoa ambapo inadaiwa jambazi huyo amefanya matukio ya kiuhalifu katika mikoa  mbalimbali hapa nchini na alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu. 

 “Huyu ni jambazi sugu na kutokana na taarifa njema za raia zikatufikia, hii ni bunduki inayomilikiwa na Serikali na tukikuta mtu binafsi hasa jambazi anamiliki bunduki ya Serikali hakuapa kupewa na mkuu wa nchi ni lazima tumuondoe

“Sasa sadaka aliyoikusanya hapa anakwenda kula moto mbinguni, alikuwa na risasi kumi (10) ndani ya bunduki hii na akapiga tatu (3) saba zimebaki lakini yeye amelala, Askari wetu ni wepesi wanajua mbinu za kupambana na majambazi, watapata tabu sana," Amesema Kamanda wa Polisi Dodoma Gilles Muroto 


Share:

Waziri Lugola Apiga Marufuku Makamanda Wa Polisi Kuyakamata Mabasi Usiku, Asema Nchi Ina Amani, Ataka Yasafiri Saa 24 Bila Kubugudhiwa

Na Felix Mwagara, Mwibara (MOHA)
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amepiga marufuku Makamanda wa Polisi wa Mikoa nchini kuyazuia mabasi yanayotoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa kwenda Dar es a Salaam au kurudi Kanda ya Ziwa kusafiri muda wa usiku kwa kisingizio cha kuofia kuvamiwa na majambazi.

Lugola amesema Jeshi la Polisi lipo imara na kamwe haliwezi kucheka na majambazi wala kuwaonea huruma majambazi na kuanza kutupangia majambazi muda gani mabasi yasafiri na yasisafiri, mabasi hayo yanapaswa kusafiri saa 24.

Akizungumza na katika mkutano wa hadhara Kijiji cha Namibu Kata ya Neruma, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, Lugola amesema mabasi yanayosafiri kutoka Kanda ya Ziwa kwenda Dar es Salaam yasizuiwe Morogoro na yanayotoka Dar es Salaam kwenda kanda ya ziwa yasizuiwe Shinyanga kwasababu zinazodaiwa za kiusalama.

“Mimi ndiyo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, hatuwezi kupangiwa ratiba ya kusafiri na majambazi, Serikali ya Rais Magufuli ipo imara, na Polisi ipo imara, hivyo agizo hili ambalo pia niliwahi kulitoa lizingatiwe ipasavyo, niliagiza majambazi wote wasambaratishwe, asakwe mpaka jambazi wa mwisho, akamatwe kama kuku”.Alisema Lugola na kuongeza.

“Taarifa ya uhalifu zinaonyesha Jeshi la Polisi limefanya kazi kubwa ya kupambana na uhalifu na hasa uhalifu wa majambazi, na niliwahi kuagiza kipindi hiki si cha kuwa na huruma na majambazi ni kipindi cha kuwashughulikia ili wananchi waishi kwa amani”.

Lugola alifafanua kuwa, nchi haiwezi kupangiwa na majambazi muda wa kusafiri, kufanya biashara, hivyo maelekezo aliyoyatoa kwa Jeshi la Polisi liendelee kupambana na majambazi popote walipo nchini.

“Nimeelekeza magari yanayosafiri yasizuiwe Morogoro yanpopita muda wa usiku saa nne usiku na kuendelea, yasizuiwe Shinyanga, ili majambzi wajue popote walipo wapo imara wamejipanga vizuri na mimi Waziri wao nipo imara kuhakikisha Jeshi la Polisi linawashughulikia makambazi mmoja baada ya mwingine ili kuwafanya wananchi katika nchi yao waendelee kushughulika na masuala ya kujijengea uchumi ili Serikali ya Rais Magufuli, iweze kuwa na uchumi wa kati na majambazi wote wakamatwe kama kuku,” alisema Lugola.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger