Tuesday, 28 July 2026

RAIA WANNE WA UHOLANZI MIONGONI MWA WALIONUSURIKA AJALI YA BOTI ZIWA NYASA

...
Eneo la tukio la ajali ya ziwa Nyasa iliyotokea baada ya boti kupinduka na kusababisha manusura wa ajali  bandari ya Mbamba Bay wilayani Nyasa mkoani Ruvuma 
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed akiwa amewasili eneo la ajali iliyotokea ziwa Nyasa katika bandari ya Mbamba Bay wilayani humo

Na Regina Ndumbaro

Nyasa -Ruvuma 

Watu saba, wakiwemo raia wanne wa Uholanzi, wamenusurika kufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kutoka Bandari ya Mbamba Bay, wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma kuelekea nchini Malawi kupata ajali katika ziwa Nyasa. 

Ajali hiyo ilitokea Julai 26, 2026, majira ya saa 4:00 asubuhi, baada ya boti hiyo kupata hitilafu ya injini, kujaa maji kufuatia dhoruba kali na hatimaye kupinduka.

Kwa mujibu wa taarifa za viongozi wa Mkoa wa Ruvuma, manusura hao walikaa majini kwa takribani saa 27 wakisubiri msaada kabla ya kuokolewa salama majira ya saa 10:00 jioni ya Julai 27, 2026.

 Uokoaji huo ulifanikiwa baada ya juhudi za pamoja za wananchi na vyombo vya uokoaji vilivyoshiriki kuwatafuta.

Akizungumza baada ya zoezi la uokoaji kukamilika, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, amewashukuru wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha katika kuokoa maisha ya manusura hao. 

Amesema mshikamano huo umeonyesha umuhimu wa ushirikiano wa jamii wakati wa kukabiliana na majanga.

Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed amesema manusura wote saba wanaendelea vizuri na wanapatiwa matibabu.

 Manusura hao ni Hussein Ajalia Hasa, Shadrack Mpata, Filimon Moyo, Hendrika Verveda, Christian Gerlagh, Lente Maarjse na Mitchel Haring.




Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger