Afisa Mtendaji Mkuu wa TPBL, Boniface Wambura
Bodi ya Ligi nchini (TPLB) imetangaza ratiba ya Ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2019/20.
Akiongea leo mbele ya wanahabari Afisa Mtendaji mkuu wa Bodi hiyo Boniface Wambura, amesema mchezo wa ufunguzi utapigwa Agosti 23, 2019 kati ya mabingwa watetezi Simba dhidi ya JKT Tanzania.
Wambura amesema wiki moja kabla ya mchezo huo utapigwa mchezo wa Ngao ya Jamii ambao huwakutanisha Mabingwa wa Ligi ambao ni Simba na Mabingwa wa Kombe la Shirikisho ambao ni Azam FC. Mchezo huo utapigwa Agosti 17, 2019.
"Msimu huu tumezingatia ratiba zote za kimataifa na hatutarajii mabadiliko ya ratiba kwa sababu zizisokuwa za msingi", amesema Wambura.
Kwa upande wa mchezo wa watani wa jadi raundi kwanza utapigwa Januari 4, 2020. Katika mchezo huo Simba watakuwa wenyeji wa Yanga kwenye uwanja wa taifa.
0 comments:
Post a Comment