Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limemuua kwa kumpiga risasi mtuhumiwa sugu wa ujambazi aliyefahamika kwa jina la Sostenes Muganyizi maarufu Rasta aliyeuawa baada ya kujaribu kurushiana risasi na askari polisi katika mtaa wa Ubemebeni wilayani Kondoa ambapo inadaiwa jambazi huyo amefanya matukio ya kiuhalifu katika mikoa mbalimbali hapa nchini na alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu.
“Huyu ni jambazi sugu na kutokana na taarifa njema za raia zikatufikia, hii ni bunduki inayomilikiwa na Serikali na tukikuta mtu binafsi hasa jambazi anamiliki bunduki ya Serikali hakuapa kupewa na mkuu wa nchi ni lazima tumuondoe
“Sasa sadaka aliyoikusanya hapa anakwenda kula moto mbinguni, alikuwa na risasi kumi (10) ndani ya bunduki hii na akapiga tatu (3) saba zimebaki lakini yeye amelala, Askari wetu ni wepesi wanajua mbinu za kupambana na majambazi, watapata tabu sana," Amesema Kamanda wa Polisi Dodoma Gilles Muroto

0 comments:
Post a Comment