Saturday, 29 December 2018

PICHA: Waziri Mkuu Majaliwa Atoa Pole Kwa Familia Ya Marehemu Ndejembi Jijini Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi Job Lusinde wakati alipowasili nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe nchini, marehemu Pancras Ndejembi  eneo la Kilimani jijini Dodoma kutoa pole kwa familia Desemba 29, 2018. Kushoto ni Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa na Waziri Mstaafu, William Kusila.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mwanasiasa Mkongwe nchini, Pancras Ndejembi, nyumbani kwa marehemu eneo la Kilimani jijini Dodoma, Desemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Bibi  Leah Pancras Ndejembi, Mjane wa Mwanasiasa Mkongwe nchini, marehemu Pancras Ndejembi  wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu  eneo la Kilimani jijini Dodoma kutoa pole kwa familia, Desemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)PMO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole, Edna Ndejembi ambaye ni binti Mwanasiasa Mkongwe nchini, marehemu Pancras Ndejembi wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu eneo la Kilimani jijini Dodoma kutoa pole kwa familia, Desemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na waombolezaji nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe nchini, marehemu Pancras Ndejembi wakati alipokwenda nyumbani kwa maremu eneo la Kilimani jijini Dodoma kutoa pole kwa familia, Desemba 29, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


from MPEKUZI http://bit.ly/2CDDOX4
Share:

Katibu Mkuu CHADEMA Na Viongozi Wengine Wakamatwa Kwa Kufanya Mkusanyiko Bila Kibali

Jeshi la Polisi wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, linawashikilia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji na viongozi wengine watatu wa chama hicho mkoani humo kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya amesema viongozi hao wamekamatwa mchana.

"Ni kweli tumemkamata Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Mashinji, katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema, mwenyekiti wa halmashauri ya Hai, Helga Mchomvu na msaidizi wa mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, Irine Lema kwa kufanya mkusanyiko usio halali," amesema.

Sabaya amesema viongozi hao, leo mchana wamekutwa wakifanya mkusanyiko katika eneo la Boma bila ya kuwa na kibali jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

"Naomba nitoe wito kwa wanasiasa kuheshimu sheria na taratibu, kama mnataka mkutano kuna taratibu hamuwezi kuvamia na kufanya mikutano kiholela," amesema.

Sabaya amesema katika wilaya yake ya Hai kwa sasa hataruhusu mikutano isiyo halali ambayo inalenga kuwapotosha wananchi kuhusu kazi nzuri ambazo zinafanywa na Rais john Magufuli.

"Waiache serikali ifanye kazi zake, kama wanataka siasa zao wasubiri kwenye kampeni, Hai tunataka maendeleo," amesema.



from MPEKUZI http://bit.ly/2SwVHfT
Share:

MADEREVA BAJAJI WAAGIZWA KUFUATA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

Mbeya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora,Dkt Merry Mwanjelwa,amewataka madereva wa babaji jijini Mbeya kuendelea kufuata taratibu na sheria za usalama barabarani ili kulinda maisha yao na ya watu wengine. Aidha amewataka askari wa usalama barabarani kuwaadhibu wale wasiofuata sheria za barabarani na kuacha kuwanyanyasa madereva kwa kuwatukana,kuwapiga na kuwadai rushwa akiita kitendo hicho kuwanyima haki vijana waliojitoa katika kujiajiri wenyewe. Dkt.Mwanjelwa amezungumza hayo leo,alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa ofisi ya chama cha kuweka na kukopa cha Bajaji Saccos jijini Mbeya ambapo…

Source

Share:

WATU KUMI WAHUKUMIWA MIAKA 20 JELA KWA KUHUJUMU UCHUMI

Na,Naomi Milton Serengeti Mahakama ya wilaya ya Serengeti imewahukumu watu 10 kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia katika shauri la uhujumu uchumi 69/2018 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kupatikana na nyara za Serikali bila kuwa na kibali Kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo mwendesha mashtaka wa Jamhuri Emmanuel Zumba aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Juma Chacha(44)Walter Akida(55)Kyaro Jackson(30)Hamis Reuben(35)Nyaisa Mtatiro(38) Wengine ni Adrew Tanu(20)Matiko Msamba(48)Raphael Walter(21)Juma Muhere(45)na Fred Tanu(28) wakazi wa Kijiji cha Nyamatoke wilayani hapa Zumba alisema wote kwa pamoja wanashitakiwa kwa makosa matano…

Source

Share:

VIGOGO WA CHADEMA WAKAMATWA NA POLISI..YUMO KATIBU MKUU MASHINJI

 Jeshi la Polisi wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro, linawashikilia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji na viongozi wengine watatu wa chama hicho mkoani humo kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Desemba 29, 2018 mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na wsalama wilaya ya Hai ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya amesema viongozi hao wamekamatwa mchana.

"Ni kweli tumemkamata Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Mashinji, katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Basir Lema, mwenyekiti wa halmashauri ya Hai, Egra Mchomvu na msaidizi wa mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, Irine Lema kwa kufanya mkusanyiko usio halali," amesema.

Sabaya amesema viongozi hao, leo mchana wamekutwa wakifanya mkusanyiko katika eneo la Boma bila ya kuwa na kibali jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

"Naomba nitoe wito kwa wanasiasa kuheshimu sheria na taratibu, kama mnataka mkutano kuna taratibu hamuwezi kuvamia na kufanya mikutano kiholela," amesema.

Sabaya amesema katika wilaya yake ya Hai kwa sasa hataruhusu mikutano isiyo halali ambayo inalenga kuwapotosha wananchi kuhusu kazi nzuri ambazo zinafanywa na Rais john Magufuli.

"Waiache serikali ifanye kazi zake, kama wanataka siasa zao wasubiri kwenye kampeni, Hai tunataka maendeleo," amesema.

Baadhi ya wanachama wa Chadema wilaya ya Hai walikiri kukamatwa kwa viongozi hao majira ya mchana hata hivyo hawakuwa tayari kufafanua chanzo cha kukamatwa kwao.

"Mimi nimewaona wakipelekwa polisi sijui kilichowakuta," amesema Lilian Shirima ambaye ni mfanyabiashara mjini Boma.

Na Mussa Juma,Mwananchi 
Share:

2019 MWAKA WA NEEMA KWA WANANCHI WA WILAYA YA SERENGETI

Na,Naomi Milton Serengeti. Hospital ya wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara inayojengwa kwa michango ya wananchi kupitia kauli mbiu ya Jenga hospital kwa shilingi 1,000 na fedha kutoka Tamisemi inatarajiwa kuzinduliwa Januari 1 mwaka 2019 Katika taarifa yake Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya wilaya ya Serengeti Juma Hamsin inasema hadi sasa kiasi cha shilingi bilioni 2,347,284,000 zimeshatumika katika ujenzi huo Aidha katika pesa hizo shilingi bilioni 1,4000,000,000 zimetoka Serikalini na pesa iliyobakia ni michango ya wananchi pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Kukamilika kwa hospital hiyo iliyoanzwa kujengwa tangu…

Source

Share:

MCHINA AKAMATWA NA MADINI YA TANZANITE



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hamis Issa amethibitisha kukamatwa kwa madini ghafi mbalimbali ikiwemo madini yanayopatikana Tanzania pekee aina ya Tanzanite ambayo yalikuwa yamebebwa na raia wa kigeni mwenye asili ya China kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Kamanda Hamis Issa amesema tukio la kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo limetokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Kilimanjaro, ambapo madini mengine aliyokutwa nayo ni aina ya Salfa, Ruby, Safaya na Almadite.

Aidha amesema kuwa zoezi hilo limefanikiwa kwa msaada wa mashine za kisasa za kukagulia mizigo na abiria zilizofungwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA), kupitia Kitengo cha Usalama cha kiwanja hicho ambapo madini hayo yalikuwa na uzito wa gramu 1118.

Ameongeza kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 22 mwaka huu, ambapo wakiwa katika ukaguzi wa mizigo ya abiria askari maalumu kitengo cha ukaguzi na usalama walifanikiwa kubaini mzigo wa madini hayo ambao ulikuwa umefungwa kwa umahiri wa hali ya juu ili isiwe rahisi kutambulika.

Imeelezwa kuwa madini hayo yana thamani ya zaidi ya shilingi milioni 40 za kitanzania ambapo mtuhumiwa ametozwa faini ya shilingi milioni nne kama adhabu.
Chanzo - Eatv
Share:

MBUNGE MWINGINE CHADEMA AMTAKA WAZIRI MHAGAMA AJIUZULU SAKATA LA KIKOKOTOO


Baada ya Rais John Pombe Magufuli kufanya utenguzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya mifuko ya Jamii, (SSRA) Dr. Irene Isaka, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amedai kwamba atashangazwa kama Waziri ataendelea kuwepo ofisini.

Heche ameyasema hayo ikiwa ni siku moja kupita tangu Rais alipotangaza kuendelea kutumika kwa sheria ya zamani katika uchukuaji wa mafao.

Kupitia mtandao wa Twitter Heche amesema kwamba "Kanuni inatungwa na waziri, kwa maana nyingine kanuni ni ya waziri. SSRA ni 'regulatory body' nitashangaa 'regulator' kutumbuliwa alafu Waziri kuendelea kubaki ofisini"

Mbali na Heche kupitia mitandao ya kijamii baadhi ya Wabunge wa upinzani wamekuwa wakimyooshea kidole Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kujiuzulu nafasi yake kutokana na kushindwa kutetea maslahi ya wananchi.

Jana akifuta kutumika kwa kanuni mpya Rais Magufuli alisema “Kwanza kustaafu ni heshima na siyo mateso. Mtu amefanya kazi kwa muda mrefu hata zaidi ya miaka 30 na matokeo yake unampa masharti kuwa atapata mafao kidogo. Utampangiaje mtu kuwa sasa utachukua kiasi fulani halafu kingine tutakutunzia, huu ni wema gani?” Hii haiingii akilini hata kidogo kwa mtu yeyote,”.


Share:

JUMA NKAMIA AKOMAA MUDA WA UBUNGE UWE MIAKA 7


Mbunge wa Jimbo la Chemba kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Juma Nkamia amesema kwa 2019 ataanza upya mpango wa kuwasilisha hoja yake ya kufanyika kwa uchaguzi kila baada ya miaka 7, licha ya kubainisha atakutana na ukosoaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya wabunge wenzake.

Kwa mujibu Nkamia mwaka 2019 atahakikisha anazungumza na viongozi wa chama chake cha CCM ili kupata baraka juu ya kuendelea na mpango wake huo juu ya kuendelea au kutoendelea na baadaye kufuata taratibu za kibunge ili suala hilo liweze kujadiliwa ndani ya bunge.

Juma Nkamia amesema msimamo wake kuhusu kuwasilisha hoja ya ukomo wa miaka 7 bado upo palepale na kudai wanaokosoa ni wenye kutaka nafasi ya utawala mapema.

"Msimamo wangu kuhusu miaka 7, uko palepale Mungu akijalia tukiwa hai tutazungumza na chama changu na mamlaka za Bunge kwa mujibu wa taratibu wakiniruhusu nitaupeleka, nilishasema tangu mwanzo. Ila unajua wapingaji wa hoja zangu ni wanaotaka Ubunge haraka na Urais haraka, kiufupi mimi kama unavyonifahamu nikiamua jambo huwa sikwepeshi."

Mwaka 2017 Mbunge huyo wa Chemba alitaka kuwasilisha Bungeni Mswada wa kutaka kusogezwa kwa muda wa kufanya uchaguzi kutoka miaka 5 ya sasa hadi miaka 7 kwa kile alichokidai kuwa nchi imekuwa ikiingia kwenye gharama nyingi za kufanya uchaguzi wa mara kwa mara.

Share:

“DANA DANA” ZA KOROSHO ZAENDELEA,SERIKALI YA JPM YAZIFUNGA AKAUNTI HIZI KISA HIKI

WAKATI Wakulima wa Korosho wakiwa wanailalamikia Serikali kwa hatua ya kuchelewesha malipo yao huku wengine wakikata tamaa ni wazi suala hilo limeendelea kupigwa “dana dana” ndivyo naweza kusema baaada ya Serikali kuibuka na kutangaza  kuzifunga kwa muda akaunti 191 za benki zinazomilikiwa na wakulima wa korosho kupisha uhakiki wa kina wa umiliki wa korosho walizouza. Uamuzi huo unakuja wakati ikiwa imeshaingiza Sh3.8 bilioni kwenye akaunti hizo katika mfululizo wa uhakiki na ulipaji wakulima wa zao hilo unaoendelea nchini. Akizungunza na gazeti la The Citizen, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema…

Source

Share:

KOCHA MKUU SIMBA : KUNDI LETU LIPO WAZI, TUNA NAFASI NZURI YA KUFIKA ROBO FAINALI

Share:

KWA RATIBA HII YA CAF SIMBA KWAO SAFI,MNYAMA ANAWAJULIA VIZURI WAARABU ,”TRY AGAIN” ATOA NENO HILI

NA KAROLI VINSENT WANAOZANI kuwa Mabingwa wa Ligi kuu soka Tanzania Bara,Timu ya Simba kuwa wamefika mwisho kwenye hatua ya makundi basi wajue wamepotoka. Wanamsimbazi hao wakiwa tayari wamewafahamu wapinzani wao katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambao wote wapo kundi (D) ambapo kuna timu za AS Vital, Al Alhy, na JS Saoura, Simba ambayo ni timu pekee hapa nchini ambayo inawajulia waarabu basi kwa hatua ya kukutana nao ni njia nyepesi kuwaondoa baada ya kufanya hivyo miaka ya nyuma. Simba ambao wananolewa na Kocha mwenye “Fomesheni” ya hatari .Mbelgiji Patrick…

Source

Share:

TANZIA: Mwanasiasa mkongwe nchini, Pancras Ndejembi afariki dunia

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Pancras Ndejembi amefariki dunia leo Jumamosi Desemba 29, 2018 majira ya saa 3:30 asubuhi.

Ndejembi amefariki katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alikopelekwa jana Ijumaa baada ya hali yake kubadilika ghafla.

Mtoto wa Marehemu, Edna Ndejembi amesema baba yake alikuwa anasumbuliwa na kifua kubana ambapo alilazwa katika Hospitali ya DCMC ya jijini Dodoma na kuruhusiwa juzi Alhamisi akiwa ameimarika kiafya.

"Lakini jana jioni hali yake ilibadilika ghafla ndipo tukamkimbiza hapo hospitali ya mkoa na leo saa tatu asubuhi mzee ametutoka," amesema Edna.

Mzee Ndejembi aliwahi kuwa mkuu wa wilaya katika wilaya mbalimbali nchini na baadaye akawa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma na mwenyekiti wa wenyeviti wa mikoa kwa miaka 20.

Pia, ni miongoni mwa waliokuwa mawaziri katika utawala wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.


from MPEKUZI http://bit.ly/2CEfJiV
Share:

DIAMOND NA MPENZI WAKE WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI COMORO


Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz amekutana na balozi wa Tanzania nchini Comoro.

Katika hafla hiyo Diamond alikuwa ameongozana na mpenzi wake kutoka nchini Kenya, Natasha.

"Earlier today when i visited the Tanzanian Embassy in Comoros,"ameandika Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram. 
Share:

REPSSI WAANZA KAMPENI KUPAMBANA NA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI


Mkurugenzi mkazi wa taasisi inayojishughulisha na maswala ya kisaikolojia (RESPSSI) Tanzania,Edwick Mapalala akizungumza wakati wa kampeni ya kutokomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni
Mkurugenzi mkazi wa taasisi inayojishughulisha na maswala ya kisaikolojia (RESPSSI) Tanzania,Edwick Mapalala akizungumza wakati wa kampeni ya kutokomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni
Baadhi ya vijana wa boda boda waliochangia mjadala wa kupinga ndoa na mimba ya utotoni

Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na masuala ya
Kisaikolojia nchini (REPPS) limeanza kufanya kampeni ya kupambana na tatizo la mimba na ndoa za utotoni baada ya tafiti nyingi kuonyesha bado tatizo hilo ni
kubwa.

Takwimu za Democratic and Health Survey , zinaonyesha kuwa tatizo la mimba za utotoni nchini limeongezeka kutoka asilimia 23 mwaka 2010 hadi kufikia 27 mwaka 2016/17, kutokana na ukosefu wa huduma pamoja na elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenye
umri kuanzia miaka 15 hadi 19.

Mkurugenzi Mkazi wa Repps, Tanzania Edwick Mapalala amesema kampeni hiyo wanaiendesha kwa kuzungumza na jamii kwenye vijiwe, shambani, maeneo ya masomo na mikusanyiko
yote ili kufikisha elimu ya namna ya kuwalea na kuwatunza watoto kimaadili.

“Tatizo la mimba na ndoa za utotoni lipo kwenye jamii yenyewe, wazazi na walezi wakijua umuhimu wa malezi bora tatizo hili halitakuwepo kabisa,” amesema.

Amesema kama watoto wa kike wataendelea kukatisha masomo yao kwa mimba na ndoa itakuwa vigumu kufikia ndoto ya Tanzania yenye viwanda kwa sababu nguvu kazi inayoachwa njiani ni kubwa.

“Mtoto wa kike akipata elimu na kusoma kwa bidii atatimiza ndoto yake na kuja kuchangia maendeleo kwenye taifa lake,” amesisitiza.

Amesema kupitia kampeni hiyo wanayoiendesha kwa ushirikiano na Shirika lililo chini ya Kanisa la Roman Katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam (PASADA), vijana wameweza kupewa
elimu ya afya ya uzazi na kujitambua itakayowasaidia kufikia ndoto zao.

Kaimu Afisa Mtendaji wa kijiji cha Parang’andam Felisian Magulu amesema kupitia kampeni hizo jamii inapata ufahamu wa madhara ya mimba kwa watoto na kujua namna ya kupambana na tatizo hilo.

Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Mkuranga, Dunia Mabufu alikiri kuwepo kwa kampeni za aina hiyo kunasaidia katika kubadilisha fikra za wengi zinazoendeshwa na mila na desturi
kandamizi dhidi ya wasichana na wanawake.
Share:

Arsenal kutia mchanga kitumbua cha Klopp?

Share:

Kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City leo

Kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City leo

Kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City mechi ya ligi kuu Tanzania Bara TPL ikichezwa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

1.Ramadhan Kabwili
2.Paul Godfrey 
3.Gadiel Michael
4.Abdallah Haji
5.Kelvin Yondan
6.Feisal Salim
7.Ibrahim Ajibu
8.Haruna Moshi ‘Boban’
9.Heritier Makambo
10.Amis Tambwe
11.Mrisho Ngassa

#AKIBA – Klaus Kindoki
– Juma Abdul
– Cleofas Sospeter
– Maka Edward
– Deus Kaseke
– Pius Buswita
– Jaffar Mohammed.

The post Kikosi cha Yanga dhidi ya Mbeya City leo appeared first on KWATA UNIT Sports News.



from KWATA UNIT Sports News http://bit.ly/2Qauspl
via IFTTT
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger