Wakati
wateja na wananchi mbalimbali wakiendelea kunufaika na promosheni ya
Nogesha Upendo ya Vodacom katika kujishindia mamilioni ya fedha kila
siku pindi wanunuapo vifurushi kwenye simu zao, sasa malipo ya faida ya
kutumia M-Pesa ambayo yameanza wiki hii yanaufanya mwanzo wa mwaka mpya
kuwa mzuri zaidi kwa mamilioni ya wateja na mawakala wa M-Pesa.
Awamu
hii ya malipo ya faida ya utumiaji wa M-Pesa inafikia jumla ya Tsh
Bilioni 32/- na itawawezesha watumiaji wa M-Pesa kuuanza mwaka vizuri
ambapo kila mtumiaji atapata sehemu ya gawio kulingana na matumizi ya
akaunti yake ya M-Pesa. Malipo haya yanafanyika kwa awamu na
yatawanufaisha wateja na mawakala wa M-Pesa waliopo kila kona ya
Tanzania. Ikiwa ni mwendelezo wa mtandao huo kuwarudishia faida ya gawio
hilo kampuni hiyo imekwishagawa zaidi ya Tsh Bilioni 39 katika awamu
zilizopita. Hii inamaanisha kwamba awamu hii itakapokamilika, ni zaidi
ya Tsh Bilioni 70 zitakuwa zimewekwa moja kwa moja kwenye mifuko ya
wateja wetu.
“Ugawaji
huu wa faida ya kutumia M-Pesa kwa wateja na mawakala wetu ni
muendelezo wa dhana kuu ya promosheni yetu ya”Nogesha Upendo”. Kila
mtumiaji wa M-Pesa atapata pesa ya ziada kwenye akaunti yake, ambayo
atakuwa na uhuru wa kuitumia vyovyote anavyopenda kama kununua
vifurushi, kulipia huduma na bidhaa au kuwatumia ndugu na jamaa zake.
Mteja mwenye matumizi makubwa kwenye M-Pesa, anapata gawio kubwa “zaidi
la faida” Alisema Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.
Kuona
kiasi cha gawio lako, tuma SMS yenye neno KIASI kwenda 15300. Utapokea
SMS inayoonesha kiasi cha pesa kitakachotumwa kwenye akaunti yako.
Vifurushi vya Cheka, Intaneti na YaKwakoTu vinaweza kununuliwa kwa
kutumia gawio hili la faida. Kununua vifurushi kwa kutumia pesa
uliyopokea, Piga *150*00# chagua NUNUA MUDA WA MAONGEZI/VIFURUSHI kisha
chagua kifurushi unachohitaji.
Promosheni
ya Nogesha Upendo ipo kwenye wiki ya 7 sasa ambapo zaidi ya wateja 200
washajishindia Tsh Milioni 1 pesa taslimu na 600 wengine wameshashinda
Tsh 100,000/- za kila siku. Kuendelea kuongeza nafasi za kushinda zawadi
za siku na wiki za hadi Tsh Milioni 1/- mteja anatakiwa kununua
kifurushi chochote cha Vodacom ambapo ataingia kwenye droo moja kwa
moja.