Tuesday, 6 December 2016
Mbunge wa Ukonga apinga amri iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mbunge
wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) amepinga amri iliyotolewa na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya wafanyabiashara kufunga maduka
yao kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa nne ili
wafanye usafi.
Amesema
amri hiyo ni batili na haitekelezeki kwa sababu inarudisha nyuma uchumi
wa wananchi hususani wafanyabiashara ndogondogo ambao wanategemea
kipato chao cha siku kuendesha maisha yao.
Akizungumza
na wananchi wa Mtaa wa Kivule mwishoni mwa wiki, Waitara alisema yeye
hapingani na watu kufanya usafi katika maeneo yao, lakini amri ya
kufunga maduka kila Jumamosi inaathiri uchumi wa wananchi hivyo ni
batili na haipaswi kuendelea kuwapo.
Siku
chache baada ya kuteuliwa kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda
alipiga marufuku kufungua maduka na biashara zingine kabla ya saa nne
asubuhi ili muda huo utumike kufanya usafi na anayekaidi agizo hilo
hutozwa faini isiyopungua Sh 50,000.
Mbunge
huyo wa Ukonga alisema uchumi wa watu masikini hususani wa mjini
unategemea kile wanachokizalisha kila siku, hivyo amri ya kufunga
biashara kila wiki ni kurudisha nyuma juhudi za wananchi kujiletea
maendeleo yao.
Katika
mkutano huo aliwaambia wananchi hao kujiwekea utaratibu kuhakikisha
maeneo yao yanakuwa safi wakati wote na kila Jumamosi wafungue biashara
zao asubuhi kama kawaida na wasibughudhiwe na mtu yeyote.
“Mimi
naunga mkono utaratibu wa kufanya usafi kila mwezi uliotangazwa na Rais
Dk. John Magufuli ambao upo kwa mujibu wa taratibu, lakini huu wa kila
Jumamosi mimi sina mwongozo nao na hizo faini za kila wiki sizitambui na
ni batili.
“Ninachotaka
kila mtu afanye usafi kwenye eneo lake, hizi faini zinatozwa bila
utaratibu hata kama eneo la mtu ni safi sitaki kuzisikia, wananchi hawa
si wanyama, waelimishwe waachwe wajiwekee utaraibu wao.
“Hivi
mama, baba ntilie anayepika maandazi, vitumbua, chapati afunge
biashara tangu asubuhi mpaka saa nne halafu hiyo chai itanywewa na nani,
huyu mtu unamwambia afunge biashara ili akaibe mtaani?” alihoji mbunge
huyo na kuongeza:
“Watendaji
lazima muwasikilize watu, nasikia kinachofanyika ni mwendo wa
kuviziana, waacheni watu wafanye kazi, hapa ni kazi tu sio faini tu”
alisema Waitara.
Katika
hatua nyingine, Waitara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Kivule alivunja kikundi cha ulinzi kilichokuwa katika ofisi hiyo kwa
tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kuwanyanaysa
wananchi.
Badala
yake, alisema uitishwe mkutano wa hadhara watu wote wanaohitaji kazi
hiyo walete maombi katika ofisi hiyo na baadaye wajadiliwe na wananchi
katika mkutano wa hadhara ili kuepuka kuwapa kazi watu wasiokuwa
waaminifu katika jamii.
Monday, 5 December 2016
Waziri Mkuu Majaliwa Aitembelea Familia Ya Marehemu Sokoine Monduli Juu
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Napono Sokoine (wapili kulia) na
Nekiteto Sokoine (kulia) ambao ni wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu,
Marehemu Edward Sokoine wakati aipokwenda nyumbani kwa marehemu, Monduli
Juu kuisalimia familia akiwa katika ziara ya wilaya ya Monduli
Desemba 4, 2016.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliekuwa
Waziri Mkuu, Edward Sokoine wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu,
Monduli Juu akiwa katika ziara ya wilaya ya Monduli

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokwenda nyumbani kwa
aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine, Monduli Juu kuisalimia familia
akiwa aktika ziara ya wilaya ya Monduli Desemba 4, 20, 16. Kushoto
kwake wajane wa marehemu, Napono Sokoine (wpili kulia) na kulia ni
Nekiteto Sokoine . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokwenda nyumbani kwa
aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine, Monduli Juu kuisalimia familia
akiwa aktika ziara ya wilaya ya Monduli Desemba 4, 20, 16. Kushoto
kwake wajane wa marehemu, Napono Sokoine (wpili kulia) na kulia ni
Nekiteto Sokoine . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo.(Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)
Yusuf Manji Atii Sheria Bila Shuruti,Alipewa saa 24 kuondoka kwenye jengo la PSPF Plaza (Quality Plaza)
Mfanyabiashara
Yusuph Manji jana alitii sheria bila shuruti kwa kuhama kwenye jengo la
Quality Plaza akitekeleza amri ya Mahakama ya kumtaka kurejesha jengo
hilo ambalo ni mali ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).
Mbali
na kutekeleza amri ya kuhama baada ya kupewa notisi ya saa 24
iliyomalizika juzi, pia anatakiwa kulipa malimbikizo ya deni la pango la
Dola za Marekani 6.1 milioni (zaidi ya Sh13 bilioni), ambazo kama
asipozilipa mali zake zitakamatwa.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Mahakama Kitengo cha Ardhi kutoa hukumu ya
kumtaka Manji kuondoka kwenye jengo hilo pamoja na kuilipa deni la
pango.
Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga hakupatikana kupitia simu yake ya mkononi.
Viongozi
wa kampuni za Manji waliokuwa wakisimamia uondoaji wa vifaa
uliomalizika jana asubuhi, walikataa kuzungumza na waandishi wa habari
waliofika kufuatilia tukio hilo.
Tangu
juzi chini ya usimamizi wa kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart,
Manji na kampuni zake walikuwa wanaondoa vifaa mbalimbali vilivyopo
kwenye jengo hilo na kuhitimisha shughuli hiyo jana.
Meneja
Uendeshaji wa Yono Auction Mart, Atukuzwe Mhugo alisema kampuni ambazo
walikuwa wakizisimamia kuondoa vifaa ni Quality Group Co Ltd, Gaming
Managemeti Ltd, Q Consult Ltd na Quality Logistics Co Ltd.
Hata
hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya Yono, Scholastica Kenyela
alisema tayari wameshaziondoa kampuni za Manji kwenye jengo hilo.
Kenyela
alisema mteja wao ambaye ni PSPF alichukua uamuzi huo baada ya Manji
kushindwa kulipa kodi ya pango ya zaidi ya Sh13 bilioni.
“Sisi
tumetimiza wajibu wetu, ukienda pale utaona tayari tumeshafanya kazi
yetu kwa sababu alipewa notisi ya saa 24 awe ameondoka,” alisema.
Ofisa
Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi alisema masuala yote
yanayohusiana na jengo hilo kwa sasa yako chini ya Yono Auction Mart. “Sipo Dar es Salaam na sitazung- umzia chochote kuhusu jengo hilo wenye mamlaka ni Yono naomba uwatafute wao,” alisema.
Waziri Mkuu afanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Mount Meru,Akerwa na Msongamano Katika Wodi ya Wazazi
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa jana alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali
ya Mkoa ya Mount Meru ambako kulikuwa na tuhuma za kuibwa watoto,
lakini alishuhudia wazazi watatu wakilala kitanda kimoja.
Ziara hiyo ilitokana na taarifa alizolalamikiwa na wananchi juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kwamba hospitali hiyo ina matukio ya wizi wa watoto wachanga.
Hata hivyo, jana baada ya kufika katika hospitali hiyo, Majaliwa alishuhudia msongamano katika wodi ya wazazi na kuagiza kuboreshwa hospitali za pembezoni.
Majaliwa aliagiza uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha wanaondoa changamoto za ongezeko la wagonjwa na kuboresha huduma katika hospitali hiyo.
Akizungumzia
sakata ya kupotea kwa watoto katika hospitali ya mkoa alivitaka vyombo
husika kuendelea na uchunguzi kwa kuwa suala hilo tayari lipo mikononi
mwa vyombo vya dola.
Wiki mbili zilizopita mzazi, Walda Mussa alisema kuwa alijifungua mtoto katika hospitali hiyo lakini hadi alipotoka hakumpata.
Wiki mbili zilizopita mzazi, Walda Mussa alisema kuwa alijifungua mtoto katika hospitali hiyo lakini hadi alipotoka hakumpata.
“Nilikuja
hapa hospitali Oktoba 4 na Oktoba 7 nikajifungua kwa upasuaji
wakamchukua mtoto na kumpeleka chumba cha joto, akaja mume wangu akaenda
kumuona mtoto mzima, siku ya pili alienda kumuona mtoto pia akiwa mzima
lakini siku ya tatu, tulipokwenda wote mimi na mume wangu tuliambiwa
mtoto alifariki na hatujawahi kuona mwili wake,” alisema mwanamke huyo hivi karibuni.
KURASA ZA NDANI ZA MAGAZETI YA LEO JUMATATU DEC 05 2016
TANO BORA ZA MASWAYETU BLOG KWENYE HABARI ZA MICHEZO LEO..





TANO BORA ZA MASWAYETU BLOG KWENYE KATUNI ZA LEO..





KUMI BORA ZA MASWAYETU BLOG KURASA ZA NDANI MAGAZETINI LEO

1

2

3

4

5

6

7

8

9

10














