Sunday, 3 April 2016

TANZIA:MFANYAKAZI SEKRETARIETI YA AJIRA AFARIKI DUNIA HOSPITAL YA MUHIMBILI

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

TANZIA

Marehemu Victoria Rubambimpala  
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anasikitika kutangaza kifo cha Bibi. Victoria Rubambimpala, (Katibu Muhutasi) kilichotokea tarehe 1 April, 2016 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taratibu za Mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu, Goba-Dar es Salaa, kabla ya kusafirishwa kwenda Ngara Mkoani Kagera kwa ajili ya maziko.
"Mungu ailaze roho ya mrehemu mahala pema pepon, 
Amen"

Share:

Mtu mmoja auawa kikatili na kutelekezwa porini mkoani Morogoro

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Wananchi wa kijiji cha Dete kata ya Tununguo wilaya ya Morogoro wamemtaka mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Stephene Kebwe kufika kijijini hapo kujionea utendaji kazi wa askari polisi wa kituo cha Ngerengere kufuatia mtu mmoja kuuawa kikatili na watu wasiojulikana bila askari wa kituo hicho kutoa msaada wowote kwa wananchi.

Wakizungumza kwa jazba wakati wa kuondoa mwili wa marehemu Abas Mwarabu aliyekutwa porini akiwa amefariki na kubaki fuvu na mifupa kutoka na kuchukua muda mrefu tangu alipo uawa wananchi hao wamesema endapo askari wa kituo hicho hawataondolewa wataandamana hadi kwa mkuu wa wilaya kupinga utendaji kazi wa askari wa kituo hicho.

Naye mwenyekiti wa kijiji hicho Fabiani Bayo akizungumzia tukio hilo amesema huenda mauaji hayo yametokana na ugomvi wa kimapenzi kwani alisha pelekewa kesi hiyo na kabla hawaja zungumza ndipo mauaji hayo yakajitokeza huku ndugu wa marehemu Ramadhani Rashidi akieleza masikitiko yao juu ya kukosa msaada wa jeshi la polisi katika kuutafuta mwili wa marehemu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrch Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema watu watatu wanashikiliwa na jeshi hilo akiwemo Juma Evanda ambaye ndie aliye husika kumuita marehemu nyumbani kwake wakati wa uhai wake huku akiwataka wananchi kuwasiliana naye moja kwa moja wanapo ona askari hawawatendei haki wanapo peleka malalamiko na tarifa zinazo hitaji msaada wa polisi.
Share:

Mtu Mmoja Auawa Kwa Kuchomwa Kisu Jijini Mwanza Kisa Kikiwa ni Wivu wa Mapenzi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mtu mmoja amefariki dunia, huku mwingine akijeruhiwa baada ya kuchomwa visu wakati wa ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alimtaja aliyeuawa kuwa ni Makororo Kitota (26) ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Iloganzala, alichomwa kisu shingoni na kifuani na kupoteza maisha palepale.

Alisema tukio hilo lilitokea Machi 30, mwaka huu saa nne usiku katika kilabu ya pombe za kienyeji.

Kamugisha alisema mtuhumiwa aliyefanya tukio hilo alikuwa na ugonvi wa muda mrefu na Kitota akimdhania kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe ambaye pia alikuwapo kilabuni hapo wakati wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, wanandoa hao walikuwa wametengana tangu Agosti 2015 kwa sababu hiyo hiyo kutokana na usaliti katika uhusiano wa kimapenzi.

Aliyejeruhiwa katika tukio hilo ni Nchama Wanda (33), mkazi wa Sabasaba wilayani humo aliyechomwa kisu tumboni na utumbo kutoka nje alipojaribu kuwaamulia wakati wakipigana.

Kamugisha alisema majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi na kwamba, hali yake siyo nzuri.

Alisema mke wa mtuhumiwa wa mauaji hayo anashikiliwa na polisi baada ya mtuhumiwa na mmiliki wa kilabu hiyo kukimbia kusikojulikana.

Kamanda huyo alisema jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watu hao ili kuwafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Share:

Magazeti ya Leo Jumapili ya April 3, 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 3/4/2016

Share:

Saturday, 2 April 2016

[PICHA]SHULE SEKONDARI BINZA (BINZA DAY) YAFANYA SHEREHE ZA MAHAFALI ZA KUWAAGA KIDATO CHA VI NA KUWAKARIBISHA FORM I 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
(Hawa ni baadhi ya waagwa wakiwa wamependeza kwelikweli)
Binza secondary school ni moja ya shule iliyopo mkoani simiyu wilaya ya Maswa,ambayo leo hii wamefanikiwa kufanya mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha  sita na kuwakaribisha kidato cha kwanza mwaka wa 2016 ambao wanatarajiwa kufanya mitihani siku chache zijazo.

Katika mahafali hayo Mgeni Rasmi alikuwa Ni mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki(CCM) MH.Nyongo amabaye aliwakilishwa vizuri na kikamilifu na Mwl.Kabarata-Headmaster Shishiyu sec school,ambae kiujumla alifanya kazi yake aliyoagizwa na Mh.Mbunge kwa ustadi wa hali ya juu.

Maswayetu blog team inapenda kuwapongeza wanafunzi wote waliofanya mahafali yao kidato cha sita na kuwapongeza kidato cha kwanza kuchaguliwa kujiunga na shule kongwe na nzuri ya binza iliyopo maswa mkoani Simiyu.

Tazama hapo chini Matukio katika picha

(Mgeni Rasmi mwalimu kabarata akiwa ktk meza kuu wakati mahafali yakiendelea)









Share:

New AUDIO | Kusini Allstars - Ngoma Ya Kimakonde | Download

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
DOWNLOAD via HULKSHARE
http://old.hulkshare.com/dl/tvhx104l5p8g/Kusini_All_stars-Cheza_kimakonde_SoNg_MaStEr_Produced_by_Aby_DaD.mp3?d=1
Share:

New AUDIO | Baghdad Ft. Profesa J Don Koli & Nikki Mbishi - Mtazamo (Remix) | Download

Share:

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WATANZANIA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA JESHI LA MAGEREZA 2016

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
(Jeshi la Magereza)

TANGAZO LA KUITWA CHUONI
Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania Bara anawatangazia wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Jeshi la Magereza baada ya Usaili kufanyika katika kambi mbalimbali za JKT.  Usaili huu ulihusu vijana waliohitimu Shahada ya Kwanza, Stashahada, Astashahada, Kidato cha Sita na Kidato cha Nne.
 
Wahusika wote wanatakiwa kuripoti katika Ofisi za Wakuu wa Magereza Mikoa mara wapatapo taarifa hii tayari kwa safari ya kwenda Chuo cha Mafunzo ya Awali kilichopo Kiwira Tukuyu Mkoani Mbeya.
 
Mafunzo yanategemewa kuanza tarehe 12 Machi, 2016 hivyo mwisho wa kuripoti chuoni ni tarehe 14 Machi, 2016.  Yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa tarehe iliyotamkwa kwenye tangazo hili hatapokelewa.
 
Wahusika wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
1.Walete vyeti halisi vya masomo na vya kuzaliwa, vikiwa na pamoja na nakala 5 za kila cheti.
2.Picha (Passport size) za rangi 5 za hivi karibuni.
3.Chandarua cheupe cha duara ft 31/2, shuka nyeupe mbili, mto wenye foronya nyeupe zisizo na maua/maandishi.
4.Fedha taslimu Tshs.90,000/=.
5.Kalamu za wino,  za risasi na madaftari ya kutosha.
6.Cheti cha afya kutoka kwa hospitali ya Serikali.
7.Nguo za kiraia za kutosha sweta, raba (Brown au nyeusi) na soksi
8.Kwa wale wenye kadi za Bima waje nazo na
9.Kila mwanafunzi atajitegemea kwa nauli ya kwenda.

Tangazo hili linapatikana kwenye mbao za matangazo zilizopo Ofisi za Magereza, tovuti ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.go.tz sanjari na blog ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.blogspot.com
 
Imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza.
 
SIGNED
Dr. J. A. Malewa  -  CP
Kny:  KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
 
 
<<<<<<<<BONYEZA HAPA KUONA MAJINA YOTE>>>>>>

<<<<<<BONYEZA HAPA KWA MAJINA YA NYONGEZA>>>>
Share:

Official VIDEO | Mh Temba x Jokate Mwegelo​ - Fundi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

https://youtu.be/FmNBsdof0io
Share:

NAFASI ZA KUJIUNGA NA NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA CHUO CHA MARIAN(MARUCO) 2016/17

Share:

SERIKALI KUPITIA WIZARA YA AFYA KUAJIRI WATUMISHI WA AFYA (AJIRA ZA AFYA 2015/16) 10000

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Serikali kuajiri watumishi wa afya 10,000

Serikali inatarajia kuajiri watumishi 10,000 wa sekta ya afya katika mwaka ujao wa fedha ili kukabiliana na upungufu wa wataalamu wa fani hiyo nchini.

Hayo yalisema jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla wakati akizindua majengo yatakayotumika kufundishia wakunga na wauguzi yaliyokarabatiwa na Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU).

Dk Kigwangalla alisema Serikali ina upungufu wa asilimia 51 ya wakunga na wauguzi na ili kukabiliana nao, imeamua kuongeza idadi ya wanafunzi katika vyuo vya afya.

“Nakipongeza Chuo Kikuu Cha Aga Khan kwa kuzalisha wataalamu wa fani ya ukunga na uuguzi kwa ngazi ya shahada na bado Serikali inahitaji kuwa na vyuo vingi vya afya ili kupunguza tatizo la uhaba wa wataalamu wa afya,” alisema.

Awali, Makamu wa Rais na Ofisa Mkuu wa Fedha wa AKU, Al-Karim Haji alisema chuo hicho kimepatiwa Sh2.9 bilioni na Benki ya Ujerumani (KFW) kwa ajili ya kukarabati vyumba na majengo ya kufundishia watalaamu hao.

“Lengo letu ni kuongeza ubora wa watumishi wa fani ya ukunga na uuguzi kwa sababu hapa nchini tumebaini kuwa kuna upungufu mkubwa wa vifaa na vyuo vya kisasa vyenye ubora wa kufundisha,” alisema Haji.

Alisema kupitia uboreshaji huo, AKU itachukua wauguzi na wakunga ambao wako kazini na kuwafundisha mara mbili kwa wiki ili waongeze ujuzi na kuwawezesha kupata shahada kwa wale wenye stashahada.

“Katika kipindi cha miaka 10, Chuo Kikuu Cha Aga Khan kimefanikiwa kuwafundisha manesi zaidi ya 600 katika ngazi ya stashahada na shahada,” alisema Haji.

Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dk Gerd Muller alisema walitoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya nchini.

Katibu Mkuu mstaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Dk Richard Sezibera alikipongeza chuo hicho kwa kuboresha sekta hiyo na mchango wake unaonyesha namna wataalamu wa afya watakavyopata elimu bora ambayo inakidhi viwango vya kimataifa.
Share:

Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa Naye Afikishwa Mahakamani Leo Kwa Tuhuma Za Rushwa

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa amepandishwa kizimbani mahakama ya Kisutu leo akituhumiwa kuomba rushwa ya Shilingi  milioni 30  akiwa kwenye Kamati za Bunge.
Ndasaa  anakuwa  mbunge  wa  nne  wa  CCM kupandishwa  mahakamani  kwa  tuhuma  za  rushwa  baada  Mbunge wa Mwibala, Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa  kupandishwa  mahakamani jana kwa tuhuma za kuomba rushwa ya milioni 30 toka kwa mkurugenzi wa Gairo  ili taarifa yake ipitishwe bila kujadiliwa.
Share:

Bosi wa Zamani wa TRA na Wafanyakazi wa StanBic Benki Wafikishwa Mahakamani

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA Dkt. Harry Kitilya na wenzake Shose Sinare na Sioi Solomoni wamefikishwa mahakamani (Kisutu DSM) leo kwa mashitaka 8 ikiwemo tuhuma za kujipatia fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6, mwezi Machi mwaka 2013, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic kwenda serikalini.

Watuhumiwa hao wamekana makosa na kurudishwa rumande hadi April 8, 2016

Share:

TAKUKURU Kuwafikisha Mahakamani Kamishna Mkuu wa Zamani wa TRA na Wafanyakazi Wawili wa Stanibic Benki

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo tarehe 1/4/2016 imewafikisha Mahakamani aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na Mwenyekiti wa ‘Enterprise Growth Market Advisors Ltd’ (EGMA), Bw. Harry Msamire Kitilya; aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Shose Mori Sinare pamoja na Aliyekuwa Mwanasheria wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Sioi Graham Solomon.

Washtakiwa wote wanashtakiwa kwa makosa ya:- Kula njama na kujipatia kwa udanganyifu kinyume na kifungu Na. 384 cha  Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E. 2002) ; Kughushi kinyume na kifungu Na. 333,335 (a) na 337 cha Kanuni ya Adhabu (Cap 16 R.E 2002) ; Utakatishaji wa fedha haramu kinyume na kifungu Na. 12 (a) 13 (a) cha Sheria ya ya Utakatishaji fedha Na. 12 ya Mwaka 2006 ‘Anti- Money Laundering Act’.

Mashtaka hayo yalisomwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mhe. Hakimu Emirius Mchauro. Kwa upande wa Jamhuri kesi hii inasimamiwa na Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Serikali Herman Tibabyekomia, Christopher Msigwa na  Mwendesha Mastaka wa TAKUKURU Stanley Luoga. Washtakiwa wanatetewa na Wakili wa Kujitegemea Ringo Tenga, Rosai Mbwambo, Semo na Nyaisa.

Washitakiwa wote watatu wamepelekwa rumande, wamekosa dhamana kwani  Kifungu Na. 148 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) Kinazuia utoaji wa dhamana kwa washtakiwa wa Utakatishaji wa fedha haramu. Kesi hii itatajwa tena tarehe 8/4/2016.

IMETOLEWA NA
OFISI YA AFISA UHUSIANO
TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA, MAKAO MAKUU
1 APRIL, 2016.
Share:

Bakwata Wakabidhi Msaada wa Madawati 500 kwa Serikali

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

BARAZA Kuu la Waislaam nchini (Bakwata) kwa kushirikiana na Shia wamekabidhi msaada wa madawati 500 kwa serikali ili kusaidia upungufu wa madawati katika shule za msingi na sekondari.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Bin Zuberi amesema kuwa katika msaada hawaangalii suala la dini kinachoangaliwa ni watakaolia madawati hayo ni watanzania.

Mufti Zuberi amesema kuwa wamechangia katika kusaidia serikali kauli mbiu ya elimu bure katika kuweza kusaidia watanzania wapate elimu.

Amesema kuwa wataendelea kushawishi waislaam katika kuendelea kuchangia elimu ili watoto wapate elimu iliyo bora kwa kuwa  serikali pekee yake haiwezi kutatua changamoto zote za elimu.
 
Mwenyekiti wa SHIA, Azim Dewj amesema kuwa amepeleka msaada huo katika bakwata ikiwa ni kuonyesha umoja na jinsi ya kusaidia serikali katika upande wa elimu.

Amesema kuwa ataendelea kushawishi matajiri wenzake kuangalia namna watakavyosaidia katika sekta ya elimu upande wa madawati kuwa kila mwaka kuweza kuchangia madawati 1000.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu amesema kuwa msaada wa madawati hayo ni mkubwa kutokana na changamoto iliyopo mbele yao.
 
Amesema kuwa idadi ya wanafunzi wa darasa la kwanza kuandikishwa umeongezeka  kutokana na mpango wa elimu bure  hivyo serikali kupata madawati ni jambo la furaha na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia madawati kutokana na mahitaji kuwa makubwa.
Share:

Rais Magufuli Amteua Hilda Nkanda Kuwa Kamishna Wa Kazi

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bi. Hilda Nkanda Kabisa kuwa Kamishna wa kazi.

Kabla ya Uteuzi huo, Bi. Hilda Nkanda Kabisa alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Bi. Hilda Nkanda Kabisa, anachukua nafasi iliyoachwa na Bw. Sauli Kinemela ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Siza D. Tumbo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC).

Kabla ya Uteuzi huo, Prof. Siza Tumbo alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) aliyebobea katika masuala ya Uhandisi Mitambo ya Kilimo.

Prof. Siza Tumbo anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Evarist Ng'wandu ambaye alistaafu kwa mujibu wa sheria.

Uteuzi huu wa watendaji wakuu wa taasisi za serikali umeanza tarehe 26 Machi, 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato

01 April, 2016
Share:

MSHAHARA WA RAIS MAGUFULI NI MILION 9,500,000/=

INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli jana alimpigia simu mtangazaji wa kipindi cha ‪Clouds360‬ cha ‪‎CloudsTv‬, Hudson Kamoga baada ya kusikia watu wanazungumzia kuhusu mshahara wa Rais.

Rais alisema mshahara alioukuta na ambao analipwa  ni milioni 9 na laki 5 (9,500,000)   na  wala  sio milioni 30  kama  wanavyodai wapinzani. Amelazimika kuyasema hayo wakati wa uchambuzi wa magazeti kupitia Clouds360.

Aliahidi akirudi kutoka likizo yupo tayari kuonyesha nyaraka za malipo ya mshahara wake.

Gazeti  la  Nipashe toleo  la jana  lilikuwa na habari  iliyowanukuu Tundu Lissu  na  Zitto Kabwe wakitaka Rais Magufuli ataje Mshahara wake na aweke wazi kama anakatwa kodi ili kuondoa sintofahamu iliyopo .
 
Hivi karibuni, Dk. Magufuli ameahidi kupunguza mishahara ya baadhi ya vigogo inayozidi shilingi milioni 15 ili mtumishi anayepata mshahara mkubwa zaidi usizidi kiasi hicho.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger