Friday 26 January 2024

FEZA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA WA ELIMU

...

 

........................

Shule ya Feza nchini imesema hivi karibuni imekuwa ikikumbana na changamoto kutoka shule za Serikali kutoka na mindombinu kuboreshwa hivyo kutumia kama chachu ya wao kufanya vizuri zaidi katika kuleta ufaulu.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam, Mwalimu Mkuu msaidizi wa Feza Shabani Mdoe, amesema hatua ya serikali kuboresha mazingira yake kumeifanya shule hiyo nayo kuendelea kuboresha mazingira yake hivyo kwa mwaka 2023 kuweza kufaulisha wanafunzi wao wote wa kidato Cha nne kwa daraja la kwanza.

Amesema kwa mwaka 2023  wanafunzi 76  wamefaulu kwa daraja la kwanza ambapo  zaidi ya wanafunzi 47 wamepata 1.7 ambapo ufaulu huo unatokana na jitihada za shule hiyo katika kufundisha kwa weledi.

Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne kwa mwaka 2023 wa shule hiyo tulipata wasaa wa kuzungumza nao ambao wamepata daraja la kwanza 1.7 wamesema kuwa ufaulu walioupata unatokana na jitihada za kusoma kwa bidii,kusali na mazingira yaliyo salama kujifunzia.

Shule za Feza nchini ni moja kati ya shule zinazofanya vizuri zaidi katika kufundisha  na mara zote zimekuwa ziliingia 10 bora hapa nchini Hali inayochangia sekta ya elimu nchini kukua zaidi.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger