Wednesday 10 January 2024

CMSA YATINGA ZANZIBAR KUTOA ELIMU YA UWEKEZAJI

...
Afisa uhusiano na elimu kwa umma kutoka CMSA, Stella Anastazi,akitoa elimu ya uwekezaji kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya biashara Zanzibar ( Zanzibar International Trade Fair).

************


MWANDISHI WETU.


KATIKA kuadhimisha Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya dhamana (CMSA) imetinga visiwani humo kutoa elimu juu ya masuala ya Uwekezaji katika Masoko ya mitaji.


Maonyesho hayo ya 10 ya Kimataifa ya Biashara Zanzibar ambayo yanafanyika Dimani Fumba visiwani humo yameanza rasmi Januari 7, mwaka huu ambapo
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Hussein Ally Mwinyi, atakuwa mgeni rasmi.


Akizungumza na wanahabari, Afisa uhusiano na elimu kwa umma, Stella Anastazi amesema, lengo kuu la kuja katika maonyesho hayo ni kutoa elimu juu ya masoko ya mitaji.


Stella amesema amefurahi kuona muitikio mzuri na mkubwa kutoka kwa watu mbalimbali waliotembelea banda la CMSA ili kujifunza.




"Nia na madhumuni ni kuleta elimu hii kwa wananchi wa Zanzibar, na pia kuwajuza maendeleo makubwa ambayo mamlaka imekuwa nayo mpaka sasa,"


Amesema imekuwa fursa kubwa kukutana na watu ambao wanaelimu juu ya mitaji hivyo hata kuwapa madini ya uwekezaji imekuwa rahisi tofauti na kukutana na mtu asiye na elimu ya masoko hayo.


Aidha Stella amesema ni wakati muafaka kwa wawekezaji kuwekeza kwani wao wanatoa ushauri zaidi na kujibu sintofahamu ambazo wananchi wamekuwa wakizipitia katika uwekezaji.


"Tumekuja na vipeperushi vingi vitazidi kumpa elimu muhusika ili kujua mambo mengi yanayohusu mitaji na masoko kupitia hivi vipeperushi pia vinampa mwongozo wa namna gani ya kuwekeza katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja na mambo mengi yanayofanyika CMSA,"amesema.


Aidha amewataka Watanzania kuwekeza ili kupata ongezeko la thamani ambayo ni faida kubwa sana kwao.


"Tuna kipeperushi kinacho toa elimu ya kujiepusha na uwekezaji wa upatu haramu ambao sio mzuri kwao maana akikosea anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria maana kuvunja sheria ya nchi ni kosa la jinai kufanya kosa hilo"amesema Stella.


Mmoja wa wananchi kisiwani Zanzibar Hamis Shaibu Hamad,amesema alikuwa akisikia mamlaka ya masoko ya mitaji lakini hakufahamu ni vitu gani vizuri vinapatikana huko ila baada ya kutembelea banda amefarijika kufahamu mengi.


"Unajua ukiwa haujapata elimu ya kitu husika unaweza kujikosesha fursa lakini mimi nimepata vitu vizuri kabisa kutika katika hili banda la CMSA nitakuwa balozi mzuri kwa wenzangu huko ili na wao waweze kuwekeza zaidi,"alisema Hamad.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger