Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) limeendesha Warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wabunge wa Bunge la Afrika juu ya Masuala ya Usimamizi wa Uhamiaji (Migration Governance) katika Bara la Afrika.
Warsha hiyo (Capacity building training workshop on labour migration governance and administration for members of Pan – African Parliament) imefanyika leo Jumanne Machi 14,2023 katika Ukumbi wa Bunge la Afrika, Midrand Afrika Kusini. Miongoni mwa sababu zilizotajwa kusababisha ongezeko la watu kuhama nchi zao ni pamoja na ukosefu wa Kazi na Ajira kwa vijana baada ya kuhitimu masomo ya Chuo katika nchi za Afrika hali inayochangia kuhamia maeneo ili kutafuta ajira.
Tazama matukio katika picha wakati wa warsha..... Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
0 comments:
Post a Comment