Wakazi wa kijiji cha Kibwera wilayani Geita mkoani Geita nchini Tanzania wamemuadhibu mwanamume mmoja kwa kuvuka mipaka ya maadili.
Mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina la Katayo Bote alinaswa na mke wa mtu mwingine wakirushana roho hali iliyowakasirisha wakazi wa eneo hilo.
Katayo alipigwa viboko hadharani na kutozwa faini ya shilingi Laki mbili kufuatia kisa hicho kilichowaudhi wenyeji. Emmanuel Ndalawa aliyeumia moyoni alisema alimfumania Katayo akimtafuna mke wake mdogo chumbani kwake.
Ndalawa alisema kwa siku nyingi, aligundua mpenzi wake alikuwa akionesha upendo usio wa kawaida kwake Katayo tangu walipohamia eneo hilo.
Ndalawa ambaye ana wake wawili, alisema alimkuta mke wake wa pili na mdogo akijivinjari na Katayo, baba mwenye nyumba waliyopangisha.
0 comments:
Post a Comment