Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 37, yuko taabani kufuatia kifo cha mpenzi wake ambaye alifariki dunia wakirusha roho kichakani katika eneo la Mbita, Kaunti ya Homa Bay nchini Kenya.
Marehemu aliyetambulika kwa jina la Milca mwenye umri wa miaka 48, aliangamia jioni ya Jumapili ya Machi 19, 2023 baada ya kuamua kuingia kwenye kichaka eneo la Got Rateng na mpenzi wake kumumunya uroda wakirejea nyumbani wakitokea kunywa pombe.
Akithibitisha kisa hicho, chifu wa eneo hilo Bernard Ouma alisema kuwa wapenzi hao awali walikuwa wameonywa dhidi ya kushiriki tendo la ndoa wakiwa wamelewa lakini walipuuza.
Kulingana na Ouma, mshukiwa alijaribu kuuzikwa mwili wa Milca na hivyo kupelekea kukamatwa kwake.
"Kuna wakati niliwaita na kuwaonya kuhusu kufanya mapenzi sehemu zisizo na staha hasa baada ya kunywa pombe, waliendelea na ninafikiri hilo linaweza kuwa chanzo cha maafa haya," alisema chifu Ouma.
Inaripotiwa kwamba mwanaume huyo alimrithi Milca baada ya kifo cha mume wake kama ilivyo utamadumi wa jamii ya Waluo ambapo mwanamke anaruhusiwa kurithiwa mumewe anapofariki dunia.
Kwa sasa mwanaume huyo anazuiliwa na polisi wa Homa Bay baada ya kukiri chanzo cha kifo hicho huku mwili wa Milca ukipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Rufaa ya Homa Bay, uchunguzi zaidi ukiendelea.
Chanzo - Tuko news
0 comments:
Post a Comment