Mohamed Salumu (44) mkazi wa Kijiji cha Olpopong kata ya Njoro wilayani Kiteto mkoani Manyara amenusurika kifo kwa kuchomwa mkuki kifuani wakati akizuia mifugo isiharibu mazao yake shambani.
Watuhumiwa hao waliamuru mifugo hiyo iharibu mazao hayo shambani ambapo jumla ya ekari 6 zimeteketezwa na mifugo hiyo.
Awali vijana hao walifika kwa mkulima huyo na kufungua uzio uliokuwa umewekwa hapo shambani na baada ya kuzuiwa mkulima huyo walimrushia mkuki ambao umemjeruhi kifuani na kwa sasa majeruhi huyo amelazwa hospitali ya wilaya ya Kiteto kwa matibabu zaidi.
Via EATV
0 comments:
Post a Comment