Zaidi ya vijana 2000 nchini wanatarajia kunufaika na ujenzi wa kiwanda cha Mkulazi kilichopo Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kwa kupatiwa ajira mbalimbali kulingana na ujuzi wao.
Hayo yamebainishwa Februari 14 mwaka huu na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Fatma Toufiq alipotembelea kiwandani hapo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho na kueleza namna ambavyo vijana watanufaika na ajira kupitia kiwanda hicho.
Amesema licha ya kiwanda hicho kutoa ajira kwa vijana kitasaidia kupunguza changamoto ya ukosefu wa sukari kwa matumizi ya binadamu na viwandani ambapo kitazalisha tani 50,000 kwa siku.
“kwa niaba ya kamati hii tumeridhishwa na ujenzi wa kiwanda hiki ambao umefikia asilimia 89, tunaamni kuwa kukamilika kwake mbali na kupunguza changamoto ya upungufu wa sukari pia vijana wetu watapa ajira na kujikwamua kiuchumi,"amesema.
Aidha Mwenyekiti huyo ampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha kwa ajili ya ujezi wa kiwanda.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce ndalichako amesema lengo la serikali ni kuhakikisha inaimalisha uzalishaji wa viwanda, kupunguza upungufu wa sukari nchini na kuttoa fursa kwa watanzania kupata ajira hususani vijana.
Aidha amewataka wakandarasi kukamilisha ujezi wa kiwanda hicho kwa wakati ili kianze kufanya kazi kwa wakati ifikapo Julai mwaka huu.
Naye, Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho Selestine Some amesema mradi huo hadi kukamilika utagharimu shilingi bilioni 344.47 na kufikia februari 28 mwaka huu jumla ya fedha zilizotolewa kama mtaji ni shiling bilioni 263.60 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 19.38 ni thamani ya ardhi na shilingi bilioni 127.00 fedha taslimu kwa ajili ya kazi ya kilimo cha miwa.
Hadi kufikia februari 2023 mradi wa mbigiri umetoa ajira kwa wafanyakazi 1,025 kati ya hao,wafanyakazi 340 wanafanya kazi mbalimbali za ujenzi wa kiwanda, 450 wanafanya kazi za mashambani na kitakapokamilika kitaajiri wafanyakazi zaidi ya 2315.
Hata hivyo kamati hiyo imetembelea kiwanda cha nyama cha ngulu hills na kukagua maendeleo ya kiwanda hicho na kukiri kuridhishwa na maendeleo ya kiwanda hicho yaliyofikia asilimia 98.
0 comments:
Post a Comment