Friday, 23 October 2020

Wafanyabiashara wakutana kujadili hali ya biashara katika mikoa yao.

...

Samirah Yusuph,
Simiyu.wafanyabiasha kutoka katika mikoa ya Mara, Kagera na Simiyu wamekutana mjini Bariadi kujadili hali ya mwenendo wa biashara zao kwa kipindi cha miaka mitano ya Rais John Magufuli.

Wafanyabiashara hao wameeleza namna ambavyo miaka hiyo imekuwa ya manufaa kwao kutokana na  kuboreshwa kwa mazingira ya kufanya biashara pamoja na usalama waa mali zao.

Wakizungumza katika kongamano hilo baadhi ya wafanya biashara wamesema kuwa kuimalishwa kwa hali ya usalama imekuwa ni neema kwao kutokana na hapo awali vitendo vya kuvamiwa na kuporwa bidhaa zao kiliwakatisha tamaa.

Hivyo wakashindwa kuwekeza kwa mitaji mikubwa,kwa sasa usalama umeimalika na umewafanya kuwekeza zaidi Alisema  Landeslaus Lutananukwa na kuongeza kuwa:

"Kutokana na hali ya mkoa wa Kagera kukatiza magari ya mizigo yalitekwa sana yalipo jaribu kukatiza yakiwa na mizigo nyakati za usiku lakini kwa sasa muda wote magari yanapita hakuna anaye weza kuteka usalama upo kila kona," alisema.

Huku wakieleza kuwa hata uzalishaji wa mazao ya biashara yameongezeka kutokana na uhakika wa upatikanaji wa masoko na namna ambavyo serikali imeboresha mifumo ya uuzaji na ununuzi wa nafaka na kuvipa fursa viwanda vya ndani pamoja na wawekezaji wazawa kuwa kipaumbele katika uwekezaji.

Wakitolea ushuhuda sekta ya uvuvi katika mkoa wa Mara walisema kuwa laiti kama serikali isingeweka mkazo wa kulinda na kuzuia uvuvi haramu kwa sasa kusingekuwa na upatikanaji wa samaki walio bora katika ziwa victoria.

"Kwa sasa samaki wanapatikana wa uhakika na ni wa kubwa wanaoingia katika soko la dunia hivyo ni fursa kwetu kuwekeza zaidi maana samaki wa afrika wamepewa kipaumbele zaidi na sisi tupo ukanda wa maziwa makuu tunasamaki wa kutosha," alieleza Aidan Siame kutoka Mara.

Ambapo aliongeza kuwa kuwatoa samaki kuwapeleka ulaya imekuwa ni rahisi zaidi kutikana na kuimarishwa kwa miundombinu ya usafirishwaji kama barabara na uwepo wa ndege za nyimbani zinazo beba mizigo moja kwa moja tofauti na hapo awali ambapo iliwabidi kupeleka mizigo Kenya ili Isafirishwe.

Jambo ambalo liliungwa mkono na Judith Lugembe ambaye alieleza kuwa licha ya uwepo wa miundombinu bora kwa sasa imekuwa ni rahisi sana kwa wajasiliamali kupata umiliki wa biashara kama kwa taasisi zanazohusika na mamlaka husikika kitendo kinacho wafanya kukuza mitaji yao na kuwa biashara kubwa.

"Ni rahisi sana kumkuta mjasiliamali ana cheti cha ubora (TBS) kwa sasa tofauti na hapo awali kwani leo tunakwenda kwenye maofisi na kufanyiwa kazi kwa muda tofauti na hapo awali ilikuwa njoo siku fulani," alisema.

Wakieleza Barabara ilivyokuwa changamoto kwao wafanyabiashara wa mkoa wa Simiyu walisema kuwa hali ya upatikanaji wa bidhaa imekuwa ni nyepesi kutokana na uwepo wa barabara zinazopitika vipindi vyote vya mwaka na hivyo kwao usafirishaji sio changamoto tena.
 
‘’mizigo inafika kwa haraka  kuliko huko nyuma kwa sababu barabara zinarahisisha usafirishaji, hata bandarini ambapo ilikuwa ni tatizo kwa sasa mizigo haikai muda mrefu kama huko nyuma,"Alisema Mwenyekiti wa wafanyabiasha mkoa wa Simiyu John Sabu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka alisema ni lazima kuweka kipaumbele kwa sekta binafsi ili kuilea na iweze kukua kwa sababu imebeba uthubutu wa kuchangia pato la taifa kwa kiwango kikubwa.

Mtaka alisema mazingira ya biashara kwa sasa yamekuwa huru na kuwataka viongozi wa serikali kuwalinda  wafanyabiashara ili waendelee kuwa huru katika uwekezaji.

Mwisho.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger