Mkurugenzi wa ufundi kutoka Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Osca Mirambo, akizungumza wakati kufunga mafunzo hayo ya ukocha kwa walimu 40 wa Michezo wa Shule za Msingi Mkoani Shinyanga
Walimu wa michezo kutoka Shule za Msingi manispaa ya Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na viongozi kutoka TFF, Mara baada ya kuhitimisha mafunzo ya ukocha.
Na Marco Maduhu -Shinyanga.
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), limetoa mafunzo ya ukocha kwa walimu wa michezo 40 kutoka Shule za Msingi Mkoani Shinyanga, kwa ajili ya kukuza vipaji vya mpira wa miguu kuanzia ngazi ya chini (Grass Roots).
Mafunzo hayo yametolewa kuanzia Oktoba 19 mwaka huu na kuhitimishwa leo Ijumaa Oktoba 23,2020 ambapo walimu hao walikuwa wakifundishwa namna ya kukuza vipaji vya wanafunzi katika mpira wa miguu pamoja na kuzijua sheria 17 za mpira huo.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkurugenzi wa ufundi kutoka Shirikisho hilo la mpira wa miguu (TFF) Oscar Mirambo, amesema mafunzo hayo ya ukocha wanayatoa kwa walimu wa michezo wa Shule za msingi kutoka mikoa nane, kwa lengo kuu la kuibua vipaji vya wachezaji kuanzia ngazi ya chini.
“Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) tumeanzisha programu hii ya kutoa mafunzo ya ukocha kwa walimu wa michezo wa shule za msingi (Grass Roots), lengo ni kukuza vipaji na kupata wachezaji wazuri ambao watalitangaza taifa katika ulimwengu wa soka,”alisema Mirambo.
“Baada ya kuhitimisha mafunzo haya pia tutatoa vifaa vya michezo kwa walimu wote 40 ili wapate vitendea kazi, ambavyo wataanza na vyo ku-kochi wanafunzi, na pia tutakuwa tukifuatilia maendeleo ya koje ya kuinua vipaji vya wanafunzi,”aliongeza.
Kwa upande wake mgeni Rasmi Afisa elimu wa Shule za Sekondari Manispaa ya Shinyanga Lucas Mzungu, akizungumza kwenye kuhitimisha mafunzo hayo alimpongeza Rais wa (TFF) Wallace Karia, kwa kuanzisha programu hiyo ambayo itakuwa ni chachu kubwa ya kupata wachezaji ambao watainua Soka la nchi, pamoja na kuchezea nje ya nchi.
Naye Katibu wa Chama Cha Mpira wa Miguu mkoa wa Shinyanga (SHIREFA), Stephen Mihambo, alisema wamefurahishwa sana na mafunzo hayo, ambayo pia yatasaidia Mkoa wa Shinyanga kuinuka kwenye mpira wa miguu, sababu ya kuwa na wachezaji wazuri waliofunzwa toka ngazi ya chini na wenye vipaji vizuri.
Nao baadhi ya walimu wa michezo waliopewa mafunzo hayo ya ukocha akiwemo Ruth Mgombele kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, walisema watakwenda kuyafanyia kazi pamoja na kuibua vipaji vya wanafunzi, ambavyo mara nyingi hua vimejificha na wamekuwa wakikosa mtu wa kuviibua.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mgeni Rasmi Lucas Mzungu ambaye ni Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Manispaa ya Shinyanga, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo ya ukocha kwa walimu wa michezo wa Shule za Msingi mkoani Shinyanga leo Ijumaa Oktoba 23,2020. Picha zote na Marco Maduhu
Mkurugenzi wa Ufundi kutoka Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Oscar Mirambo, akizungumza wakati kufunga mafunzo ya ukocha kwa walimu 40 wa Michezo wa Shule za Msingi Mkoani Shinyanga.
Mkufunzi wa Grass Roots kutoka TFF Raymond Gweba, akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo ya ukocha kwa walimu wa michezo wa Shule za Msingi Mkoani Shinyanga.
Katibu wa Chama cha Mpira wa miguu mkoa waShinyanga (SHIREFA), Stephen Mihambo, akiipongeza TFF kutoa mafunzo hayo, ambayo yatakuza mpira wa miguu mkoani Shinyanga.
Mwalimu wa michezo Ruth Mgombele kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, akishukuru kupewa mafunzo hayo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye ufungaji wa mafunzo ya ukocha kwa walimu wa michezo wa Shule za Msingi Mkoani Shinyanga.
Wanafunzi wakiwa kwenye ufungwaji wa mafunzo hayo ya ukocha.
Wanafunzi wakiwa kwenye ufungwaji wa mafunzo hayo ya ukocha.
Wanafunzi wakiwa kwenye ufungwaji wa mafunzo hayo ya ukocha.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za msingi manispaa ya Shinyanga wakipokea Jezi za mpira kutoka kwa Mkurugenzi wa ufundi TFF Oscar Mirambo, (kulia) na kushoto ni Mgeni Rasmi Lucas Mzungu afisa elimu Sekondary manispaa ya Shinyanga.
Zoezi la kukabidhi Jezi likiendelea.
Mgeni rasmi Lucas Mzungu ambaye ni Afisa elimu Sekondari manispaa ya Shinyanga akitoa Vyeti kwa walimu 40 wa michezo wa Shule za Msingi mkoani Shinyanga ambao wamehitimu mafunzo ya ukocha kutoka TFF.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la utoaji vyeti likiendelea.
Zoezi la ugawaji vyeti likiendelea.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.
0 comments:
Post a Comment