Friday 19 July 2019

Iran Yakana Marekani Kuitungua Ndege Yake Isiyo Na Rubani

Iran imekanusha madai ya Rais Donald Trump wa Marekani kwamba meli ya kivita ya nchi yake imeharibu ndege isiyo na rubani ya Iran karibu na Ghuba ya Uajemi baada ya kuitishia meli hiyo, tukio ambalo linaonesha ongezeko jipya la wasi wasi kati ya nchi hizo chini ya mwezi mmoja baada ya Iran kuitungua ndege kama hiyo ya Marekani katika eneo na kumfanya Trump kukaribia kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya kijeshi. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ameandika katika ukurasa wa Twitter kuwa Iran haijapoteza ndege yoyote isiyo na rubani katika ujia wa maji wa Hormuz ama kwingine kokote. 

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif amesisitiza hakuna ndege isiyo na rubani iliyopotea hadi sasa.

Trump jana alisema meli ya USS Boxer ilichukua hatua za kujihami baada ya ndege isiyo na rubani ya Iran kukaribia karibu yadi 1,000 kutoka meli hiyo na kupuuzia miito kadhaa ya kuondoka.


Share:

Hatimaye Jaguar Katua Nchini....Tazama Hapa Alichokisema


Mbunge wa Starehe nchini Kenya, Charles Njagua maarufu Jaguar yupo nchini kuanzia jana. Huku akieleza kuwa atakuwa Tanznaia hadi Jumapili Julai 21, 2019.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana Julai 18, 2019, Jaguar amesema amekuja Tanzania kwa kuwa hana tatizo na Watanzania na kauli aliyoitoa hakuwa amewalenga wao, bali wanaofanya biashara kinyume na taratibu za Kenya.

“Nimekuja kutembea Tanzania naipenda Tanzania na kama unavyojua ile kauli ambayo watu walishindwa kuielewa, nilikuwa namaanisha wanaofanya kazi kinyume na taratibu,” amesisitiza.

Msanii huyo wa wimbo wa 'Kigeugeu' amesema kwamba anapanga kukutana na wabunge marafiki zake wa taifa hilo kama vile Profesa J na Sugu pamoja na wasanii tofauti.

Juni 25, 2019 mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki kupitia mitandao ya kijamii video yake ilisambaa akieleza kuwafukuza wafanyabiashara wa kigeni wakiwemo Watanzania ndani ya masaa 24 kurudi kwao la sivyo watawapiga na kuwarudisha nchini mwao


Share:

Irene Uwoya na Steve Nyerere Wahojiwa na Jeshi la Polisi

Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Camilius Wambura, amethibitisha kumuita msanii wa filamu nchini,  Irene Uwoya na Steve Nyerere, kufuatia kitendo alichokifanya cha kuwarushia pesa, wanahabari katika  mkutano uliofanyika mapema mwa wiki hii.
 
Kamanda Wambura amesema, walimuita na kumhoji siku ya Julai 17, ambapo alidhaminiwa na kutoka kwa dhamana huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi.

''Waliitwa kuja, walionekana kwenye clip moja, Yule Irene alionekana anatupa fedha, kwa wanahabrari, na alihojiwa na kudhaminiwa na uchunguzi mwingine unaendelea'' amesema Kamanda Wambura.

Ikumbukwe kuwa  siku ya Julai 15, Irene Uwoya, alionekana katika baadhi ya video zilizosambaa mitandaoni, akirusha fedha kwa wanahabari, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni udhalilishaji na Irene alikiri kukosea na kuomba radhi kupitia ukurasa wake wa Instagram.


Share:

Serikali Kuanza kusajili nyaraka za ardhi ndani ya mkoa husika badala ya utaratibu wa mwanzo wa kusajiliwa ndani ya kanda

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi, amesema serikali itaanza kusajili nyaraka za ardhi ndani ya mkoa husika, badala ya utaratibu wa mwanzo  wa kusajiliwa ndani ya kanda zilizokuwa zimetengwa.
 
Waziri Lukuvi amesema  lengo ni kupunguza ucheleweshaji wa usajili wa nyaraka hizo na kuepusha usumbufu kwa wananchi.

Waziri Lukuvi ametoa kauli hiyo leo   Julai 18,2019 Jijini Dodoma wakati akifungua, mkutano wa wataalamu wa sekta ya ardhi, wanaokutana jijini  Dodoma, kutathmini wapi walipo na malengo ya sekta hiyo, sambamba na kuwaje uwezo wataalamu  hao namna bora ya ufanyaji  kazi na namna ya kutatua changamoto zilizopo.
 
Amesema wamekusudia kuhamisha ofisi za kusajili nyaraka za ardhi kutoka katika kanda, na kuzirudisha ndani ya mikoa husika, ili kurahisisha zoezi hilo, na upatikanaji wa nyaraka hizo kwa wakati,  na tayari wakuu wa mikoa wameridhia na kutoa majengo yatakayotumika kama ofisi za wizara za usajili ndani  ya mikoa.
 
“Serikali imeamua kuunda ofisi za ardhi ngazi ya mkoa  na sio kanda kama ilivyokuwa awali.
 
Hii ni kupunguza gharama ,hivyo michoro yote ya ardhi sasa inapitishwa mkoani,taarifa za uthamini wa ardhi  ambazo zilikuwa zinapatikana makao makuu sasa atateuliwa mthamini mkuu kila mkoa,Idara zote za ardhi zipangwe upya na wenye tabia za ovyo hawatapangwa”amesema.
 
Aidha Waziri Lukuvi amesema katika  kuhakikisha wananchi wanyonge wanapata huduma stahiki, amepiga marufuku wakuu wa idara za ardhi kupokea tozo ambazo hazistahili, pamoja na utumiaji wa madalali ndani ya ofisi za umma.
 
Amemtaka katibu mkuu wa wizara hiyo Doroth Mwanyika, kuhakikisha anapanga safu ya wakuu wa idara  haraka watakao kwenda kufanya kazi katika ofisi za wilaya na ofisi za mipango miji na orodha hiyo ipite mikononi mwake kabla ya wahusika kupewa barua za uteuzi.
 
Pia  Waziri Lukuvi ametoa maelekezo kwa maafisa  ardhi kutojihusisha na kampuni binafsi  za upimaji ,kutopokea au kutoza fedha  kinyume na taratibu katika upimaji wa ardhi,kutojihusisha na madalali wasiolipa kodi,kila wilaya kuhimiza kukusanya kodi,pamoja na kuwa na bei elekezi  katika upimaji wa ardhi.
 
“Tabia chafu ya kupokea na kuingiza  fedha bila utaratibu maalum Dodoma inafanyika sana,maafisa  ardhi mnawajua  matapeli lakini mnashirikiana nao ,Pia nawaagiza vibali vya ujenzi visitolewe zaidi ya  wiki moja na kwa viwango vilivyokubaliwa .Nimekuta baadhi ya halmashauri mtu anatozwa zaidi ya laki tano ili apate kibali cha ujenzi huu ni unyonyaji,Nitakula sahani moja na kila ,mtu ,bado kuna madudu mengi sana kwa watumishi wa ardhi   Double Location bado yapo”.amesema.
 
Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi amewasimamisha kazi  watumishi wa Ardhi ambao ni Manase Kastory aliyekuwa afisa ardhi Mikindani   Lindi na alihamishiwa Sengerema Mwanza ambapo waziri Lukuvi amesema afisa wa ardhi huyo  alifanya uhuni wa uchakachuaji wa michoro ya ardhi  Mikindani.
 
Maafisa ardhi wengine wanaochunguzwa ni afisa ardhi Rufiji,na afisa ardhi Kilwa aliyejulikana kwa jina moja la Sultan  ambaye amedhulumu Tsh.Mil.35 .
 
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Wizara hiyo Doroth Mwanyika, amebainisha malengo ya kukutana katika mkutano huo.
 
Na kauli mbiu ya mkutano huo ni “Mabadiliko katika sekta ya ardhi kwa maendeleo ya taifa letu”.


Share:

Serikali Kuyafuta Makampuni Binafsi Ya Ulinzi Yanayoajiri Vikongwe, Askari Feki Wasiopitia Mafunzo, Kulipa Mishahara Finyu

Na Felix Mwagara, Mwibara (MOHA)
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Serikali itayafuta makampuni ya ulinzi binafsi nchini ambayo yanaajiri askari vikongwe pamoja na wasiokuwa na mafunzo ya askari wa akiba (mgambo) wala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
 
Lugola amesema Wizara yake haiwezi kucheza na masuala ya ulinzi na usalama wa nchi kwa kuyaacha makampuni hayo yakiendelea kuajiri vikongwe ambao hawezi kushika silaha za moto na pia mara kwa mara wanasinzia kiasi kwamba muda wowote wanaweza wakanyang’anywa silaha na majambazi ambao wanazitafuta silaha kwa ajili ya kufanyia uhalifu.
 
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kata ya Nansimo, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda Mkoani Mara, leo, Lugola amesema kutokana na upungufu wa askari, Serikali iliruhusu kuwepo na makampuni binafsi ya ulinzi kwa ajili ya kusaidia masuala ya ulinzi na usalama nchini, lakini baadhi ya makampuni hayo yanavunja sheria kwa kuajiri walinzi wasiokuwa na mafunzo yoyote, askari waliostaafu ambao wamechoka na hawawezi kufanya kazi hizo na pia wanalipwa mishahara midogo au kutokulipwa kabisa.
 
Amesema kwa miaka ya hivi karibuni Serikali imeendelea kuwa na utaratibu wa kuhakikisha kwamba kwa wale wanaopita katika Jeshi la Akiba ambao wanaitwa Mgambo, na wale wanaopitia katika Jeshi la Kujenga Taifa, maeneo hayo mawili yasaidie kuzalisha askari ambao watachukuliwa na Makampani ya Ulinzi ili waweze kufanya kazi kwasababu wanauzoefu wamefundishika, wanajua jinsi ya kubeba na kutumia silaha za moto, namna ya kufanya doria pamoja na kulinda mali na maisha ya wananchi.
 
“Lakini niendelee kusikitika, baadhi ya makampuni, tumeshuhudia, yanaendelea kuajiri askari ambao wamechoka, askari ambao wamestaafu kwa mujibu wa umri wao, kwa maana hawawezi kufanya kazi tena hizi za kiaskari, lakini wanaajiriwa tena katika makampuni haya ya ulinzi, lakini pia tumeshuhudia unashtukia tu asubuhi mwananchi uliyemuona jana mtaani, na unamjua kabisa huyu mtoto wa fulani, hana mafunzo yoyote ya askari wa akiba, hana mafunzi yoyote ya Jeshi la Kujenga Taifa, ambapo vijana wanafundishwa uzalendo, uadilifu, lakini unamuona ghafla amebeba bunduki, amevaa sare za kampuni ya ulinzi, ana kirungu na anasema mimi nimepata ajira pale mjomba kanipeleka,” alisema Lugola.
 
Amesema yeye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, na kupitia Jeshi la Polisi nchini, haiwezekani masuala ya ulinzi na usalama ukachezewa, ambapo Ulinzi unahitajhi watu wenye mafunzo, watu wakakamavu, watu ambao hawana maradhi, na pia unahitaji watu ambao wanaweza wakafukuzana na uhalifu lakini baadhi ya makampuni hayo yanaajiri watu ambao hawana sifa hizo.
 
Lugola alisema, kutokana na changamoto hiyo, Serikali inakaribia kukamilisha kuwepo na sheria ya makampuni hayo ya ulinzi, ambayo itasimamia vizuri makampuni yote nchini, na sheria hiyo itaenda kudhibiti pia masuala ya ajira askari hao.
 
“Unaona mzee anatoka kazini asubuhi na bunduki yake kachoka hatua ishirini tu ameona mti pale kuna kivuli anafika hapo anaanza kusinzia mzee wa watu na bunduki, hata yunifomu zenyewe hazimkai vizuri, kachokaa, eti huyo ni askari wa kampuni binafsi ya ulinzi, haiwezekani, silaha hizi zinahitaji umakini katika kubeba na katika kutumia, na wahalifu nao wanazitafuta silaha za namna hii, wakigundua mahala fulani kuna walioajiriwa ni wachofu, wapo hoi bin taabani hao ndio wanaonyang’anywa bunduki,” alisema Lugola.
 
Amesema amelielekeza Jeshi la Polisi, wahakikishe kuwa Makampuni hayo yanaajiri askari ambao wanasifa za kufanya kazi hiyo, pamoja na wahakikishe wanaajiri askari wenye sifa na kuwalipa askari hao vizuri, kwa kuwa baadhi ya wamiliki wa kampuni hizo wamekua wakiwatapeli, kutokuwalipa, na wengine wanakopwa na ofisi zao.
 
“Askari gani wanakopwa, hawalipwi, huyo ni askari wa namna gani, matokeo yake askari huyo ambaye ana dhana ya moto anaweza kushawishika akafanya matumizi ya silaha ambayo hayaruhusiwi, au mali za wananchi zikaporwa kwasababu huyo ameshakata tamaa, kwahiyo niwatake makapuni yote ya ulinzi ambao askari wao watanilalamikia mimi au watamlalamikia Inspekta jenerali wa polisi kwamba hawalipa askari wao, hatuwezi kukubali kuwa na askari wanaofanya shughuli za ulinzi na usalama ndani ya nchi hii ambao hawalipwi, nitahakikisha makampuni hayo nitayachukulia hatua ikiwa ni pamoja na kuhakikisha yanafutwa kwenye madaftari ya makampuni ya ulinzi nchini,” alisema Lugola.
 
Aidha, Waziri Lugola katika ziara anayoendelea nayo jimboni kwake, kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, pamoja na kuchangia ujenzi wa madarasa ya shule za msingi na sekondari, zahanati, pia aliwataka wananchi wa jimbo hilo, kufanya kazi kizaelendo kujenga miundombinu, na kutofikiria kazi za maendeleo zinafanywa na Serikali pekee.


Share:

Katibu Mkuu Ofisi Ya Waziri Mkuu Akutana Na Wakuu Wa Taasisi Kujadili Namna Bora Ya Utekelezaji Wa Mpango Kazi Wa Mwaka 2019 - 2020

NA; MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe amekutana na Wakurugenzi wa Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kwa lengo la kujadili kwa kina maeneo watakayo shirikiana kwa pamoja katika mpango kazi wa mwaka 2019 – 2020 na kutoa maelekezo juu ya namna bora ya kuhudumia wananchi kulingana na huduma zinazotolewa na taasisi hizo.

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mkutano uliopo jengo la PSSSF Jijini Dodoma, alisema kuwa Mwaka wa fedha 2019/2020 ni muhimu kukubaliana kwa pamoja maeneo ambayo yatatekelezwa kwa ushirikiano ili kuimarisha utendaji wa shughuli mbalimbali.

“Lengo kuu la kukutana kwetu hapa ni kuangalia utekelezaji wa shughuli zilizopangwa kwenye mpango kazi wa kila Taasisi katika mwaka huu wa fedha, na kubaini namna bora ya kutekeleza maeneo hayo kwa ufanisi,” alisema Massawe.

Katibu Mkuu aliongeza kuwa kupanga na kukubaliana maeneo ya ushirikiano katika utekelezaji wa mpango kazi kutasaidia kuongeza tija katika utendaji wa kazi na majukumu ya kila siku.

 “Ninapenda kuona tunakuwa mfano wa kuingwa kwa kujijengea mwenendo mzuri wa kushirikiana katika utendaji ili kufanikisha shughuli nyingi kwa wakati mmoja,” alisisitiza Massawe

Aidha, alitoa wito kwa wakuu hao kuzingatia suala la mawasiliano na uhusianao kwa wadau na wateja wanaowahudumia ikiwemo kufanyia kazi malalamiko yanayotolewa kwa wakati.

Kwa Upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda alieleza kuwa ushirikiano na taasisi nyingine na wizara ni fursa pekee itakayo wawezesha kutekeleza dhamira na mikakati waliyopanga ili kuleta maendeleo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba alisema kuwa yapo maeneo mengi ya kushirikiana kwa pamoja na mpango kazi wa mwaka ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio yatakayo wasaidia kuwa na ushirikiano endelevu katika maeneo mbalimbali.

Kikao hicho kiliudhuriwa na Wakurugenzi na Wataalamu wa Mipango na Bajeti kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).


Share:

Ukweli Kuhusu Samaki Mtu Wa Baharini.

IMESIMULIWA  NA DOKTA.  MUNGWA  KABILI,   SIMU  0744 -  000  473.

Nimeulizwa  kuhusu  swali  hili  mara  nyingi sana. Watu  wengi sasa wanataka  kusikia  kutoka  kwangu  kuhusu  viumbe  hawa  wa  kipekee.

Kwa  sababu  siwezi  kumjibu  mtu mmoja  mmoja  leo  nimeamua  kutoa  majibu  ya  ujumla  kwa  watu  wote.

SAMAKI   MTU   NI  NINI?
Samaki    mtu  ni jinni  wa  baharini  ambae  hujidhihirisha  katika ulimwengu  wa  nyama  kupitia  ‘ masafa’  ya  umbo  la  mchanganyiko  wa  samaki  na  mwanadamu.

 Kuna  sababu  kubwa  sana  na  ya  msingi  kwa  nini  jinni  huyu  hujidhihirisha katika  umbo  la  samaki  na  mtu.

Labda  tu  kwa  wale  wasio  fahamu, majini  wanapo  amua  kujidhihirisha  katika  ulimwengu  wa  nyama na damu  huwa  wanafanya  hivyo  kwa  kutumia  ‘masafa’  ya  wanyama  mbalimbali  kama vile   nyoka, paka, nge nakadhalika. Ndio  maana  nyoka  wengi  wana  tabia  za  kupotea  potea  kila  wanapo  onekana.  Mnaweza  kuwa  mmekaa nyumbani  akatokea  nyoka  mkaanza  sekeseke  la  kumpiga, mara  kaingia  uvunguni  mara  ghafla  haonekani, mkiona  hivyo  basi  kuna  uwezekano  mkubwa  sana  nyoka  huyo  alikuwa  jinni.  Haya  sasa  tuendelee  na  samaki  mtu.

SAMAKI  MTU  WANAPATIKANA  WAPI ?
Samaki mtu  wanapatikana  baharini.

UMESEMA SAMAKI   MTU   WANAPATIKANA   BAHARINI  LAKINI  MBONA  KILA MARA  HUWA  TUNAENDA  KUOGELEA  BAHARINI  NA  HATUJAWAHI  KUONA  SAMAKI  MTU  HATA  SIKU  MOJA ?

Huwezi  kuwaona  samaki  mtu  ufukweni.   Ndani ya  bahari Samaki  mtu  hupatikana  kwenye  maeneo  yenye  vina  virefu. Hata siku  moja  huwezi  kumuona  samaki  mtu maeneo  ya  ufukweni.  Majini  wote  wa  baharini  wenye  nguvu  za  juu au  wale  walio  katika  daraja  la  juu, huwa  wanapatikana  kwenye  sehemu  zenye  vina  virefu.

 Kamwe  huwezi  kuwaona  ufukweni.   Hata  hivyo, majini  walio  katika  koo  nyinginezo za  majini  wanaweza  kuonekana  ufukweni  kwa  sababu  maalumu  sana  lakini  sio  Samaki mtu.

Samaki  mtu  hawezi  kuonekana  ufukweni  hata  itokee  nini!!!   Na  akitokea  ufukweni  labda  uwe  ni  ufukwe ulio  kwenye  kisiwa  kilichopo  kati  kati  ya  bahari kwenye  kina  kirefu na  pili  katika  kisiwa  hicho  kusiwe  na  shughuli  yoyote  inayo  muhusisha  mwanadamu.  Ipo sababu  ya  msingi  sana  ambayo  ina mfanya  samaki  mtu  asionekane  ufukweni hasa  hasa  katika  ufukwe  ambao  una tawaliwa  na  pilika  pilika  za  mwanadamu.

UMESEMA   SAMAKI   MTU  HAWEZI  KUONEKANA  WALA  KUTOKEA KWENYE  UFUKWE  WENYE  SHUGHULI  NA  PILIKA  PILIKA  ZA  BINADAMU.  SABABU   NI   NINI ?

Kuna  sababu  kuu  mbili  katika  hili, lakini  kabla  sijaanza  kuelezea  sababu  hizo  ngoja  nikukumbushe  kitu kimoja  muhimu  sana.  Baharini  wanaishi  majini  waswafi  tu. Baharini  hakai  jinni mchafu  wa kisheitwani. Baharini  hakikai  kitu  chochote  kichafu.  Ndio  maana  mtu  akifariki   baharini  basi  mwili  wake  unatupwa  nchi  kavu. 

Uchafu  ninao  uzungumzia  hapa  ni  uchafu  wa  kiroho yani  kitu  chenye  nguvu  hasi.   Hata  ndugu  zangu  wavuvi  wakiwa  kwenye  shughuli  zao  baharini  wanajua  kwamba  hawatakiwi  kuingia  kwenye  shughuli  wakiwa  wachafu  ( Mfano  wakiwa  na  Janaba  nakadhalika ).  Sio  hivyo  tu, bali  hata  lugha  wanayo  takiwa  kutumia  wakiwa  baharini  inatakiwa  kuwa  lugha  swafi  na  yenye  staha. Hakuna  lugha  za  matusi  wala  maneno  ya  hovyo  baharini.  Walio diriki  kuzunguma  maneno  ya  hovyo  wakiwa baharini  walipata  habari  yao.

Baharini kila  kitu  ni  kisafi.  Hata  kwa  wewe  menye  nuksi, balaa  na  mikosi  ukienda  kuoga  maji  ya  baharini  utaondosha  nukushi  zako  zote, kwa  sababu  hakuna  nguvu  hasi  inayo  weza  kukatiza  baharini.

Sasa  basi  kama  nilivyo  sema  hapo  juu  kwamba  baharini  hakikai  kitu  kichafu.  Samaki  Mtu  ni  jinni  wa  baharini. Ni  jinni  mswafi. Hakai na  kitu kichafu.  Sio  tu  kwamba  ni  jinni  wa  baharini  bali  pia  ni  jinni  anae  pendwa  na  majini  wa  baharini  kuliko  jinni  mwingine  yoyote  yule.

Kila  jinni  wa  baharini  anampenda  jinni  huyu.  Ni  jinni  mwenye  kuwavutia  sana  majini  wa  baharini. Popote  anapokuwa  anatembea  jinni  huyu  huwa  anafuatwa  na  jinni kutoka  katika  kila  koo  ya  majini  wanao  patikana  baharini.

Kwa  hiyo  popote  anapokuwa  jinni  huyu  huwa  ana  ambatana  na  majini wa  aina  zote  wa  baharini.  Ni  mfano wa  ndege  wa  porini   aitwae Msese  (Yule  mwenye  mkia  mrefu)   ambae  kila  mahali  anapokwenda  hufuatwa  na  kundi  la  ndege  lakini , Samaki  Mtu ni  zaidi  ya  Msese  kwa  sababu  Msese  hufuatwa  na  ndege  lakini  sio  ndege  wote.

Ni  kama  ndege  mmoja  wa  porini  anae  patikana  kwa  wingi  huko  kusini  mwa  Tanzania. Ndege  huyo  anapo taka  kujenga  kiota  chake, kila  ndege  unae  mjua  wewe  hupeleka  jani  kwa  ajili  ya  kujenga  kiota  cha ndege  huyu  mwenye  maajabu. Ninaposema  ndege  wote namaanisha  ndege  wote,  kuanzia  ndege  warukao  mchana  hadi  wale  warukao  usiku.

Kwa  wanyama  wanao  patikana  nchi  kavu, jinni  huyu  naweza  kumfananisha kidogo na  mnyama  aitwae Ngekewa( Mnyama  wa  porini  anaependwa  na  kuhusudiwa  na  wanyama  wote )

SABABU KWA NINI  SAMAKI  MTU  HAWEZI  KUONEKANA  UFUKWENI, HASAHASA  KWENYE  UFUKWE  WENYE  SHUGHULI  NYINGI  ZA  MWANADAMU.

Katika  ulimwengu  wa  kiroho, samaki  mtu  ni  kiumbe mwenye  uhusiano  mkubwa  sana  na  mwanadamu. Na  ndio maana  anapo  jidhihirisha  katika  ulimwengu  wa  nyama  hujidhihirisha  katika  umbile  la  mwanadamu  na  samaki. Kuna  maana  na  sababu  kubwa  sana katika  hili.

Katika  uliwmengu  wa  kiroho   lipo  jambo  moja  la  rohoni  ambalo  samaki  mtu  anafanana  sana  na  binadamu.  Nalo  ni  asili  ya   NAFSI  zao.    Asili  ya  nafsi  ya  mwanadamu  ni  UMEME-SUMAKU.  Yani  ni  umeme  wenye  sumaku  yenye  uwezo  wa  kuvuta  na  kukusanya  vitu  mbalimbali.   Ndio  maana  kijana mwenye  tabia  nzuri  anapo  anzisha  urafiki  na  kundi  la  vijana  wenye  tabia  mbaya  baada ya  muda  Fulani  na  yeye  ataanza  kuwa  na  tabia  mbaya  kwa  sababu  nafsi  yake  itakamatana  na  nafsi  za  vijana  hao  wenye  tabia  zisizo  faa (  Ndio  maana  mzazi  unashauriwa  kuchunga  sana  aina  ya  marafiki  wanao  ongozana  na  mtoto  wako  )

Hii ni kwa  sababu  nafsi  za  mwanadamu  zina  tabia  ya  KUKAMATANA  NA  KUSHIKAMANA. Na  ndio  sababu  wapenzi  wakiachana  nafsi  zao  huwa  zinapata  tabu  sana.  Humuwia  vigumu  sana  mtu  kuishi  bila  mpenzi  wake  ambae  wamezoeana na  nafsi  zao  zimekatana.

Vivyo  hivyo  na   kwa samaki  mtu. Asili  ya  nafsi  ya  samaki  mtu  ni  UMEME-SUMAKU. Nafsi  hii  inaweza  kukamatana  na  nafsi  ya  mwanadamu.

Samaki  mtu  anapokuwa  katika  mazingira  yenye  watu, nafsi  yake  huvuta  na kukamata  MAWAZO na  FIKRA  za  watu  wote  waliopo  katika  eneo  hilo  kwa  wakati  huo  jambo  ambalo  humletea  shida  sana kwa   sababu  nafasi  ya  mwanadamu  inatawaliwa  na  mambo  ambayo  hayatakiwi  kukaa kwenye  nafsi  ya  samaki  mtu.

Nafsi  ya  mwanadamu  inatawaliwa  na  mambo  makuu  yafuatayo:

1.     MAWAZO  MACHAFU  : Asilimia  kubwa  ya  mambo  anayo  yawaza  mwanadamu  ni MAWAZO  MAOVU.  Uzinzi, uasherati, husda, kijicho, usengenyaji, wivu  nakadhalika.  Haya  ni  mawazo  machafu  ambayo  hayatakiwi  kukaa  ndani  ya  nafsi  ya  Samaki  mtu  wala  nafsi  ya  kiumbe  yoyote  wa  kiroho  aishie  baharini.

Na  sababu  nimesha  ielezea  hapo  juu. Baharini hakikai  kitu  kichafu. Nafsi ya  samaki  mtu  haikai  na kitu  kichafu.   Kwa  kuwa  Samaki  Mtu  hapendi  na  hawezi  kukaa  na  vitu  vichafu. Vitu  vinavyo weza  kunajisi  nafsi  yake, kiumbe  huyu  hukaa  mbali  kabisa  na  mahali  wanapo  kaa  wanadamu  kwa  sababu  ya  kulinda  usafi  wa  nafsi  yake.

Samaki  mtu  hujisikia  vibaya  sana  kuona viumbe  wanao  fanana  na  wao  ( Yani  sisi binadamu )  na  ambao  wapo  katika  daraja  la  juu  sana  la  kiroho  miongoni mwa  viumbe  wanaoishi  duniani ( Binadamu  ndio  kiumbe  wa  Mwenyezi  Mungu  alie  katika daraja  la  juu  kabisa  la kiroho  miongoni  mwa  viumbe  wote  walioumbwa nae )  akiwa  amebeba  mambo  machafu yasiyo endana  na  hadhi  yake  ya  kiroho.

Mfano  wake  ni  sawa  tu  na  wewe  mwanaume  rijali  ambavyo  huwezi  kukaa  sehemu moja  na  wanaume  mashoga  na  kusikiliza  mambo  wanayo  yaongea. Watazungumza  mambo  yatakayo  ichefua  sana nafsi  yako. Utahuzunika  sana  kuona  wanaume  kamili kama  wewe  wakiwa  wanawaza  mambo  yaliyo  kinyume.   Na  kitu  kikubwa  utakacho  weza  kukifanya     ni  kuondoka  katika  eneo  hilo.  Hutotaka  kabisa  kukaa  karibu  na  watu  hao.   Ndivyo  ilivyo kwa  samaki mtu.

2.     MAWAZO   YA  MAHANGAIKO  NA  HUZUNI  YA  MWANADAMU Nafsi ya  mwanadamu  pia  imetawaliwa  na  huzuni  nyingi. Magonjwa  yasiyo  pona, maradhi ya  kichawi, ugumu  wa  kupata  rizki, matatizo  katika  ndoa , hofu, mashaka nakadhalika   ni  mambo yaliyo  tawala  nafsi  za  wanadamu.  Samaki  mtu  anapokaa  katika  eneo  lenye  watu  wengi  huweza  kuvuta  na  kukamata  mawazo  haya  ya  huzuni  yaliyo  tawala  nafsi  za  wanadamu.

Mawazo  haya  kwanza  humtia  huzuni  sana  kiumbe  huyu  kuona  viumbe  wanao  fanana  na  yeye  wakiwa  katika  mahangaiko  na  mateso  makubwa.  Huzuni, hofu, mashaka  na  kadhalika  ni  mambo  ambayo  hayatakiwi  kukaa  kwenye  nafsi ya  Samaki  Mtu  kwa sababu  kiumbe  huyu  ameumbwa  kuwa  na  furaha  wakati  wote. Huzuni  hizo  za  wanadamu  huchefua  nafsi  yake na  kuisononesha.  Kuepukana na  kadhia  hiyo, kiumbe  huyu  hapendi  kabisa  kukaa  karibu  na  wanadamu.

Mfano  wa  huzuni  na  sononeko  analo  lipata  hapa  ni  hapa  ni  ule  ambao  unaupata  wewe  mwanadamu  ( mwenye  moyo swafi )  ukimuona  binadamu  mwenzako  akiwa  kwenye  matatizo  makubwa. Mfano imetokea  ajali watu  wamepondwa  pondwa na  gari wamekufa  vibaya.  Kuna  watu  yakitokea  matukio  kama  haya  huwa  hawataki  hata  kuangalia na  kama  ni  kwenye  TV huwa  wanazima kabisa.

Mfano  mwingine  ni  kuona  maiti  za  binaadamu  wenzako. Watu  wengi  wana  hofu  ya  kutazama  miili  ya  marehemu  na  ni  wachache  wanaweza  kusogea  na  kukaa  sehemu  ambazo  kuna  miili  ya  watu  walio  kufa.

Kuona  maiti  ya  mtu  unaempenda  sana. Watu  wengi  hushikwa  na  huzuni  sana  pindi  wanapo  ona  maiti  za  watu  wao  wa  karibu. Huhuzunika  sana  hutamani  wasione  kabisa.    Ndivyo  ilivyo  kwa  samaki  mtu. Ndio  maana  hawapendi kukaa  karibu  na  mahali  walipo  binadamu.

UMESEMA  SAMAKI  MTU  WANAPATIKANA  KWENYE  VINA  VIREFU  BAHARINI  LAKINI  MBONA  HUWA  TUNAPITA  KWENYE  MAENEO  HAYO  LAKINI  HATUWAONI?

Huwezi  kumuona  Samaki  Mtu  kwa  sababu yupo  katika  ‘masafa’ tofauti  na  masafa  uliyopo  wewe.  Hwezi  kumuona  kwa  macho  ya  nyama  na  damu.

Viumbe  tuliopo  duniani  tunaishi  katika  masafa  tofauti  tofauti.  Ndio  maana  viumbe  wengine  mfano  majini hawaonekani  kwa  sababu  wapo kwenye  masafa  tofauti  na  binadamu  ingawa  tunaishi  nao  katika  dunia  hii  hii.

Mfano  wake  ni  sawa  na  redio  yako .  Ukiwa  na  redio  yako ukiweka  mfano masafa  namba  moja  unapata  matangazo  ya  redio  Fulani, ukiweka  masafa  namba  mbili  unapata  matangazo  ya  redio  nyingine  nakadhalika  nakadhalika.

Ndivyo  ilivyo  kwa  binadamu  na  majini. Tunaishi  nao majumbani  mitaani, tunapishana  nao barabarani, njia  panda, vyooni, makaburini  nakadhalika  lakini  huwezi  kuwaona  kwa  macho  ya  damu  kwa  sababu  wao  wapo  kwenye  masafa  ya  juu  kuliko  masafa yako  mwanadamu.

Vivyo  hivyo  kwa  samaki  mtu.  Huwezi  kumuona  kwa   macho  ya  damu  na  nyama  kwa  sababu  yeye  ni jinni  na  yupo  Kwenye  masafa  tofauti na  masafa  ulyopo  wewe.

JE  NIKITAKA  KUMUONA  SAMAKI  MTU  NINATAKIWA  KUFANYA  NINI ?

Ukitaka  kumuona  samaki  mtu  kwanza  unatakiwa kuwa  katika  masafa  yake . Yani  kuwa  na  uwezo  wa  kuona  vitu  visivyo weza  kuonekana  kwa  macho ya  nyama  na  damu.  Unaweza  kupata  uwezo  huo  kwa  kufanya  mambo  yafuatayo :  Kwanza  hakikisha  una  moyo  mswafi. Yani  ndani  ya  nafsi  yako  usiwe  na  wazo  lolote  hasi. Uzinzi, uasherati,. Husda, kisasi, kinyongo  nakadhalika.  Pili  usiwe  na  uchungu  wala  huzuni  ya  kiwango  chochote  ndani  ya  nafsi  yako.  Uwe  na  moyo  wenye  furaha  wakati  wote. Tatu  usiwe  na  tamaa  ya  kupata  chochote . Yani  lengo  lako  liwe  tu  unataka  kumuona tu jinsi  alivyo  na  sio  unataka  kumuona  kwa  ajli  ya  kupata  faida  yoyote  kutoka  kwake.

Baada  ya  hapo  uende  kwenye  kisiwa  kilichopo  baharini . Kisiwa  kiwe  kwenye  kina  kirefu  na  kusiwe  na  shughuli  zozote  za  binadamu katika  eneo  hilo.  Baada ya  kufika  kwenye  kisiwa  hicho, utafunga  na  kufanya  dua  ya  kuomba  kumuona  kiumbe  huyu. Ikiwa  ni  bahati  yako   kiumbe  huyu  atakutokea  na  utamuona. Na  asipo  kutokea  laivu  basi  anaweza  kukutokea  katika ndoto.

Kama  unaona  itakuwa  vigumu  kwenda  kwenye  kisiwani  unaweza  kufanya  ombi  maalumu  la  kumuona  Samaki  huyo katika  ndoto.  Utatakiwa  kutimiza  vigezo  vyote  nilivyo  vitaja  hapo  juu  yani  uwe  na  moyo  mswafi, usiwe  na  huzuni ( uwe  na  furaha wakati  wote ) na  usisukumwe  na  tamaa  ya  kupata  kitu  chochote  kutoka  kwa  samaki  huyo.

Kila siku  utakuwa  unaenda  ufukweni. Utakuwa  unaingia  kuogelea  kama  waingiavyo  watu  wengine  na  ukiwa  ndani ya  maji  uwe  una fanya  maombi  yako  yani  uwe  unaomba  kuonyeshwa  Samaki  Mtu  kupitia  ndoto.

Ufanye  hivyo  bila  kuchoka  wala  bila  kuwa  na  haraka  ya  kupokea  majibu  yako.   Baada  ya  muda  Samaki  huyu  atakutokea  katika  ndoto. Utamuona  Katika  ndoto.   Kama  ni  bahati  yako  basi  atakutokea  katika  ndoto  baada  ya  muda  mfupi  lakin,  Inaweza  kukuchukua  siku  arobaini, inaweza  kuchukua  miezi  mitatu, miezi  sita, mwaka  mzima, miaka  mitatu hata  Zaidi  ya  hapo.  Utakacho  takwa  kufanya  ni  kuwa  mvumilivu.  Na  kadri  utakavyo  kuwa  mvumilivu  ndivyo  utakavyo  kuwa  katika  nafasi  nzuri  ya  kumuona  samaki  huyo.

·       Je  Samaki  Mtu  wanaongea ?
·       Kama  wanaongea  huwa  wanaongea  lugha  gani ?
·       Ni kweli  samaki  mtu  huwa  wanasuka  nywele  zao ?
·       Ni kweli  samaki  mtu  huwa  wana  wabembeleza  na  kuwanyonyesha  watoto  wao ?
·       Je  kuna  uhusiano  wowote  ule  wa  vinasaba  vya  kiroho kati  ya  Samaki  Mtu  na  Mwanadamu ?

·       Kuna  dawa  moja  ya  asili  inajulikana  kama  AMBARI  NYEUPE  YA  BAHARINI.  Dawa  hii  inatumika kufungua  vifungo  vya  aina  zote na  kuwafukuza  majini  wabaya  mwilini,kwenye  biashara  na  kwenye  miji . Lakini  pia  dawa  hii  inatumika  katika  tiba  ya  kurefusha  na  kunenepesha  maumbile  ya  kiume. Kuna  watu  wanasema  dwa  hii  inatokana  na  nyangumi  na  wengine  wanasema  dawa  hii  inatokana  na  Samaki  Mtu.  Je  Ukweli  ni  upi ?

Yote  haya  nimeyaelezea  kwa  undani sana kwenye  kitabu  changu kiitwacho  " MESENJA  WA  BAHARINI "  ambacho  kitakuwa  mitaani  kuanzia  tarehe  01  SEPTEMBA 2019.  

Kitabu  kitapatikana  nchi nzima  kwenye  maduka  ya  kuuza  vitabu  pamoja  na  kwenye  vibanda  vya  wauza  magazeti.  Nchi jirani  kitabu  hiki  kitapatikana  pia  Mombasa, Nairobi na  Lamu  nchini Kenya.

Mbali  na  kuelezea  kwa  kina  kuhusu  Samaki  Mtu,ndani  ya  kitabu  hiki utapata  kujua  kuhusu  vitimbi  mbalimbali vinavyo watokea  binadamu  wakiwa  baharini  pamoja  na  mambo  yote  muhimu  yanayo  husiana  na  ufalme  wa  baharini.

IMESIMULIWA  NADOKTA.  MUNGWA  KABILI.  ANAPATIKANA  KUPITIA  SIMU  NAMBA  0744 -  000  473.


Share:

Wafugaji Njombe waulalamikia uongozi wa kiwanda cha maziwa

Na. AMIRI KILAGALILA-NJOMBE
Licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais DR.John Pombe Joseph Magufuli ya kuhakikisha inatimiza ndoto za kuifikia Tanzania yenye uchumi wa viwanda, huko mkoani Njombe wafugaji wa vijiji vya kilenzi na Uwemba wameulalamikia uongozi wa kiwanda cha maziwa Njombe kwa kukwamisha maendeleo yao.

Wafugaji wa kijiji cha kilenzi wakizungumza na MPEKUZI wamesema wanakosewa haki kwa kupata malipo yao kwa muda usio mwafaka ukilinganisha na muda waliopeleka maziwa katika kiwanda hicho.

“Nina masikitiko kwamba kiwanda kinakokwenda sio kwenyewe kwasababu wakati wapo wale weupe kiwanda kilikuwa kinaenda vizuri sana,lakini pengine viongozi wetu wanamsikilizaje Rais wetu?, yaani badala ya kiwanda kukisimamia vizuri ili kiwasaidie wananchi hilo hakuna” wamesema Ditrick Mlyuka na Azakia Ndawala wafugaji

Aidha baadhi ya wafugaji wa kijiji cha Uwemba wameonyeshwa kusikitishwa na kiwanda hicho kutoa bei mbili tofauti.

“Tuna masikitiko makubwa sana kwa kuwa utakauta kiwanda kimoja kinatoa bei mbili,kwa mfano kijiji cha utalingolo wanapewa shilingi mia saba kwa lita,sisi hapa uwemba tunapewa shilingi mia tano sitini nayo tunapata sio kwa muda muafaka yaani karibu vipindi vitatu”wamesema wananchi

Kwa upande wake meneja wa kiwanda cha maziwa Njombe ndg.Edwirn kidehele amekiri kucheleweshwa kwa malipo kwa wafugaji hao.

“Malipo tumeanza kulipa lakini mfumo mzuri wa kulipa vizuri nafikiri mpaka mwishoni mwa mwezi huu wa saba,hiyo mifumo yote itakuwa vizuri, sasa hivi tumeanza kupata oda kubwa kwa hiyo mzunguko wa fedha utakuwa mkubwa”alisema Kidehele

Kipaumbele cha Serikali ya awamu ya tano ni kuona tunafikia Tanzania ya viwanda vivyo hivyo kwa wafugaji hawa wanasema kwamba wanatamani kuwa mchango mkubwa wa kuifikia Tanzania ya viwanda, lakini wanasema endapo tatizo hili lisipotatuliwa huenda viongozi wa viwanda wakawa ndio chanzo cha kutofikia lengo la serikali.


Share:

Aweso Anusa Harufu Ya Rushwa Na Upigaji Dili Mradi Wa Maji Masange Kondoa Uliogharimu Zaidi Ya Tsh.mil.433

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amesema  Wizara yake itashirikiana na TAKUKURU  ili kujiridhisha  katika  utekelezaji mradi wa Maji kijiji cha Masange Wilayani Kondoa mkoani Dodoma Uliogharimu zaidi ya  Sh.Milioni 433  baada ya kupewa majibu yasiyojitosheleza na Mkandarasi wa Mradi huo.
 
Naibu Waziri Aweso ameyasema hayo   Julai 18,2019 katika kijiji cha  Masange Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo alipofanya ziara ya kukagua na kujionea mradi wa Maji kijiji cha  Masange uliogharimu kiasi cha Sh.Milioni  mia nne  thelathini na tatu,laki mbili,themanini na nane elfu,mia tano ,arobaini nane[433,288,548].
 
“Haiwezekani  tukauziwa mbuzi kwenye gunia,lazima kukagua na kujionea,baada ya kupewa majibu ya kusuasua hivyo TAKUKURU tutashirikiana nao  kubaini ubadhilifu,na mkandarasi asilipwe mpaka tufanye uchunguzi tujiridhishe”alisema Aweso.
 
Hali hiyo imekuja baada ya Mkandarasi wa mradi huo wa Maji kampuni ya Best One kwa kushirikiana na wataalam wa sekta ya Maji wa halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kutoa majibu yasiyoridhisha kuhusu matumizi ya fedha zilizotumika katika mradi huo .
 
 Mhe.Aweso amepiga simu mbele ya wananchi kuulizia taratibu za upatikanaji wa Gari la kuchimba visima .
 
Mbunge wa Kondoa ambaye  pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango  Dokta.Ashatu Kijaji amesema yupo tayari kufanya  kazi hata saa sita usiku na walichomwagiza wananchi wake ni kutatua kero ya Maji .
 
Wananchi wa Mtaa wa Masange wamesema adha kubwa inayowakabili ni maji hivyo ni  vyema serikali ikafanya mchakato haraka  kutatua kero hiyo.
 
Awali ,akisoma taarifa ya Mradi wa Maji wa Masange mbele ya Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso,Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji vijijini[RUWASA]Wilaya ya Kondoa Mhandisi Falaura Seleman Kikusa  amesema mradi wa Maji Masange ulianza tangu tarehe 15,Disemba,2014 na kuzinduliwa rasmi tarehe  13,Septemba ,2016 kupitia  mbio za Mwenge wa  Uhuru huku ukigharimu zaidi ya Tsh.Milioni 433 .
 
Aidha amebainisha kuwa muda wa utekelezaji wa Mradi huo kwa mujibu  wa Mkataba  ni kipindi cha miezi mine  kuanzia tarehe 15,Disemba,2014,hadi 15,Machi,2015 hivyo kutokana na changamoto mbalimbali hususan kuchelewa kwa malipo ya madai ya mkandarasi,mradi uliongezewa muda wa utekelezaji   na kukamilika rasmi mnamo tarehe 7,Juni,2018.

Mhandisi  Kikusa ameendelea kufafanua kuwa upatikanaji wa Maji katika kijiji cha Masange haukidhi mahitaji halisi ya maji kwa wakazi wa kijiji hicho kwani huduma ya maji imekuwa ikipatikana kwa mgao  kwa vitongoji kwa masaa manne hadi matano.
 
Amesema chanzo cha kuwepo kwa hali hiyo unatokana na changamoto kadhaa ikiwemo kuongezeka kwa wakazi  pamoja na kukua kwa mji  wa Masange ,Uwezo wa chanzo cha Maji [lita   119,577.6 kwa siku]kuwa mdogo ikilinganisha na mahitaji halisi ya Maji ya sasa [zaidi ya lita 141,560  kwa siku]  na changamoto  nyingine ni usimamizi usio mzuri kutoka kwa timu ya mhandisi .
 
Hata hivyo mkandarasi   wa mradi hadi kufikia sasa alishalipwa kiasi cha sh.347,421,000  kati ya gharama 433,288,548 na zilizobaki kwa mujibu ya makubaliano ya mkataba ni Tsh.120,609,648.


Share:

Rais Magufuli Aiagiza Wizara Ya Katiba Na Sheria Kupitia Magereza Yote Nchini Ili Kuwaachia Wafungwa Wasiostahili Kifungo.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameagiza Wizara ya katiba   na sheria kuendelea kupitia Magereza yote nchini ili kuweza kuwaachia wafungwa wasiostahili kifungo.
 
Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo  Julai 18,2019  wilayani Kongwa   mkoani Dodoma wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.
 
Mhe.Magufuli amesema baadhi ya wafungwa wamekuwa wakifungwa kwa kusingiziwa hivyo ni wakati sasa Umefika Kwa  Wizara kupita  kila gereza na kuchunguza uhalali wa kifungo ili kila mtu apate haki yake kwani serikali ya awamu ya tano ni Wanyonge.

Hivyo ,Rais Magufuli amesema serikali yake hawezi kutawala  kwa kuonea watu  wanyonge huku pia akisisitiza  Umuhimu wa viongozi  wa dini kuliombea taifa la Tanzania .

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amekumbusha Umuhimu wa  kufanya kazi kwa bidii huku akisema asiyefanya kazi na asile na Serikali yake haiwezi kugawa chakula kwa mtu Mzembe.


Share:

Waziri Mkuu: Wezi Wa Nondo Tani 5 Wasakwe Mara Moja

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah awasake na kuwatia mbaroni watu waliohusika na wizi wa tani tano za nondo na kisha wakatoroka.

Alitoa agizo hilo jana jioni, (Alhamisi, Julai 18, 2019) wakati akizungumza na wafanyakazi na wananchi mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi ya kimataifa ya Moshi, katika kata ya Ngangamfumuni, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi za siku nne, alisema mradi huo ni maalum kwani uko miongoni mwa miradi ambayo Serikali imekuwa ikiweka utaratibu wa kupelekea fedha kwenye miradi iliyotengwa na Halmashauri.

“Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 9 za kuanzia mradi huu lakini inasikitisha kuona kwamba wanaMoshi mnahujumu kwa kuiba vifaa vya ujenzi. Ninazo taaarifa kuwa hapa zimeibiwa tani tano za nondo na zimeshakamatwa.”

“Ni aibu, ni aibu kwa wana-Moshi. Ninyi wenyewe mnauhujumu huu mradi. Manispaa iweke utaratibu wa ulinzi ili vifaa vingine visipotee zaidi. Mkuu wa Wilaya chukua hatua ya kuwafuatilia wote waliohusika,” alisema.

Kupitia maswali aliyouliza, Waziri Mkuu alibaini kuwa walinzi wawili waliokuwepo siku ya tukio walitoroka ndipo akaamua kumwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa, awasake na kuhakikisha wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Ujenzi wa stendi hiyo kubwa unafanywa na mkandarasi mkuu ambayo ni kampuni ya CRJE ya China akishirikiana na wakandarasi wasaidizi watano na unatarajiwa kukamilika Januari 2021. Hadi kukamilika, ujenzi huo unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 28.8.

Ikikamilika, stendi hiyo ambayo itakuwa na ofisi, maduka, migahawa na hoteli, itakuwa na uwezo wa kuhudumia mabasi 300 kwa siku ambayo yataingia na kutoka. Kati ya hayo, mabasi 72 yanaweza kuegeshwa kwa wakati mmoja. Pia kutakuwa na maegesho ya ya magari binafsi 218, teksi 34 na bajaji na bodaboda 20.

Wakati huohuo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah amethibitisha kukamatwa kwa watu watano ambao wanatuhumiwa kuhusika na wizi wa tani tano za nondo katika eneo la ujenzi wa stendi hiyo lililopo Ngangamfumuni.

“Hawa watu tumewakamata jana jioni, na kati ya walinzi waliotoroka, tumemkamata mmoja wao tayari akiwemo mkazi wa Rau, Daudi Audifasi mwenye miaka 48 ambaye anadaiwa kutoboa ukuta wa uzio kwa chini, na kukutwa na nondo nyumbani kwake ambako ni mita 10 kutoka eneo la tukio.”

Amesema tukio hilo, lilitokea Julai 6, mwaka huu majira ya saa 2 asubuhi ambapo walinzi wa eneo hilo ambao ni Maxshield company walitoroka baada ya tukio hilo. Kamanda Issah alithibitisha kwamba nondo hizo zimekamatwa na ziko polisi.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 


Share:

Kufikia Julai 30 Wakulima Wote Watakuwa Wamelipwa Fedha Za Pamba

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Geita
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa hadi kufikia Julai 30, 2019 wakulima wote wa Pamba nchini watakuwa wamelipwa.

Hivi karibuni kumetokea hali ya sintofahamu kuhusiana na suala ununuzi wa zao hilo baada ya kutangazwa kwa bei elekezi ambayo ni sh. 1,200 kwa kilo moja katika mikoa yote inayozalisha zao hilo.

Alisema kuwa miongoni mwa changamoto za wanunuzi ni dhamana ya serikali katika taasisi za kifedha. Ambapo tayari serikali imeridhia kuwadhamini ili kununua zao hilo.

Waziri Hasunga ametoa kauli hiyo leo tarehe 19 Julai 2019 wakati akizungumza kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika katika Wilaya ya Mbogwe, Bukombe na Geita wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Mhe Hasunga alisema kuwa Serikali imeamua kuingilia kati suala la ununuzi wa zao la pamba kutokana na kusuasua kwa soko lake kwa kutoa dhamana ili kuwawezesha wanunuzi kukopeshwa fedha na benki mbalimbali kwa ajili ya kununulia pamba kutoka kwa wakulima.
  
Wakati huo huo Mhe Hasunga aliwasihi wakulima wa zao hilo la pamba na wakulima wa mazao mengine nchini wahakikishe mara baada ya kuuza mazao yao wanatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kununulia pembejeo watakazozitumia katika msimu ujao.

“Pamoja na kwamba mtalipwa fedha nzuri iliyopangwa na serikali ya shilingi 1200 lakini nawakumbusha kuwa serikali sasa haitawakopesha pembejeo hivyo ni vyema mkatenga fedha ili kununua pembejeo hizo” Alikaririwa Mhe Hasunga

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga alisema Serikali itahakikisha inaendelea kutafuta masoko ya mazao hayo ndani na nje ya nchi ili kuwawezesha wakulima kuwa na uhakika wa masoko kwa mazao yao na hivyo kujiongezea tija.

Pia, alisema mbali na kutafuta masoko, Serikali imedhamiria kufufua viwanda mbalimbali vya nguo hapa nchini ili kuwawezesha wakulima wa zao la pamba kuwa na soko la uhakika.

“Kuhusu suala la maghala tunatambua tatizo hilo na tutahakikisha tunayaboresha ili pamba iweze kuhifadhiwa katika mazingira bora” Alisema

Akizungumzia kuhusu changamoto ya viuatilifu, Waziri Hasunga alisema Serikali itahakikisha vinapatikana kwa kuzingatia eneo husika ili kuweza kudhibiti wadudu waharibufu.

Sambamba na hayo Mhe Hasunga ametoa miezi miwili kwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Shinyanga (SHIRECU) kuhakikisha kuwa kinafufua kiwanda cha kuchakata Pamba Kilichopo katika Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita na kufikia mwaka 2020 kianze kufanya kazi.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger