Friday 1 February 2019

NYOKA WA AJABU AUA WATU WATANO SUMBAWANGA..HUUA SIKU ZA JUMAPILI

Na Gurian Adolf -Sumbawanga

Maofisa Maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, wameamua kushirikiana na mtaalamu wa tiba za jadi wa kijiji cha Kinambo, Tarafa ya Milepa, kumsaka nyoka wa ajabu anayedaiwa kuua watu watano kwa nyakati tofauti kijijini hapo. 

Diwani wa Kata ya Milepa wilayani Sumbawanga, Aporinali Macheta, alisema jana kwamba, nyoka huyo aina ya koboko anadaiwa kugonga na kusababisha vifo vya watu watano katika kipindi cha miaka minne tofauti.

Alisema jambo la kushangaza ni kwamba nyoka huyo amekuwa na kawaida ya kugonga watu kila mwaka katika moja ya siku ya Jumapili. 

Alisema siku kama hiyo ya Jumapili mwaka 2016 nyoka huyo aliwagonga watu wawili ambao walifariki dunia muda mfupi baadaye.

Alisema kuwa msako dhidi ya nyoka huyo umeanza baada ya juzi kumgonga na kumsababishia kifo Ndoti (60), mkazi wa Kijiji cha Kinambo, ambaye alifariki muda mfupi baada ya kugongwa na nyoka huyo.

Alisema nyoka huyo anapatikana katika mti mmoja wa mwembe ambapo baada ya kumgonga mtu hutokomea porini.

Macheta aliongeza kuwa baada ya tukio hilo wanakijiji walimwandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuomba wataalamu wa Maliasili ambao walifika kijijini hapo jana. 

Alisema walifika na kuanza kuendesha msako dhidi ya nyoka huyo kwa kumtumia kijana aitwaye Seif Sikanda, ambaye ni mtaalamu wa tiba za asili.

“Msako wa nyoka huyo unaendelea, lakini leo (jana) tulifanikiwa kumuua kwa risasi nyoka mdogo mwenye urefu wa futi saba aina ya koboko... tunaendelea kumsaka yule mkubwa ambaye ndio tishio la maisha ya wananchi wa kijiji hiki,” alisema. 

Ofisa Mtendaji wa kijiji hiko, Richard Sungura, alisema pamoja na nyoka huyo kumgonga na kusababisha kifo cha Ndoti, pia amesababisha vifo vya Elezina Kasele (68), Saise Shigela (21), John Mboganzuri (63) na Benedicto Kasele (14). 

Alisema nyoka huyo pamoja na kuua watu hao kwa nyakati fofauti, pia amekuwa aking’ata mifugo kama ng’ombe, mbuzi na mbwa. 


CHANZO- NIPASHE

Share:

MBUNGE ATUPWA JELA KWA KUCHAPISHA UONGO TWITTER

Mbunge na aliyekuwa waziri wa zamani wa michezo Ivory Coast, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela, baada ya kusambaza taarifa za uongo kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Alain Lobognan aliandika katika ukurasa wake wa Twitter tarehe 9 Januari kuwa mkuu wa upelelezi ametoa tamko la kukamatwa kwa mbunge mwenzake, taarifa hiyo ilizua gumzo na fujo kwa miongoni wa wafuasi wa mbunge huyo.

Lakini mkuu wa upelelezi alikanusha kutoa tamko hilo kama alivyoandika Lobognan katika ukurasa wake wa Twitter.

Mbunge huyo ambaye yupo katika mgomo wa kula siku zaidi ya kumi sasa anasema kuwa kesi yake imeingiliwa kisiasa.

Mwanasheria wake bi Affoussiata Bamba Lamine, amesema kuwa wana mpango wa kukata rufaa.

Ameongeza pia kuwa kesi ya mteja wake imeingiliwa kisiasa, na kusema kuwa analengwa kwasababu ya ukaribu wake waziri mkuu wa zamani na alikua pia kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro.

Kwasasa ni spika wa bunge, mwezi uliopita kiongozi huyo alitangaza kuachia madaraka kama spika.

Wachambuzi wanasema kuwa huenda ameanza kujiandaa na kugombea urais mwaka 2020.
Chanzo - BBC
Share:

Picha : WATAFITI WATAKIWA KUONGEZA NGUVU KATIKA UTAFITI WA UGONJWA WA MALARIA


Mtaalamu wa magonjwa ya Damu, Vinasaba na Saratani Professa Lucio Luzatto wa Chuo cha MUHAS akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wageni waalikwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia.
Wageni waalikwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akiwasiliasha mada ya 'Malaria kwa akinamama wajawazito na Watoto' katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mtaalam wa Masuala ya Dawa wa Chuo cha MUHAS, Prof. Omary Minzi akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Wageni waalikwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Andrew Barnabas Pembe akifuatilia kwa makini mada.
Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha MUHAS, Dkt Bill Ngasala akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia.
Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Julie Makani (kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya ugonjwa wa Siko Seli unavyoendana na ugonjwa wa Malaria.
Mtafiti wa Malaria wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu kilichopo Bombo Hospitali, Tanga, Deus Ishengoma akizungumzia ukata wa fedha unavyonyongonyesha tafiti bunifu.
Mmoja ya mdau wa masuala ya afya akiuliza swali.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma MUHAS na Mloganzila, Hellen Mtui akitoa shukrani zake za pekee kwa wote walioweza kushiriki katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Muhadhara huo, Prof. Lyamuya akihitimisha kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Utafiti umeonyesha ugonjwa wa Malaria kwa akinamama wajawazito na watoto umepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na awali.

Kwa upande wa Zanzibar ugonjwa wa Malaria umepungua kwa kiwango kikubwa hivyo ni vyema Tanzania Bara kuendelea kupambana ili ifikapo 2030  tatizo la ugonjwa wa Malaria kwa jamii umalizike.

Hayo ameyabainisha Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma  wakati akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni 'Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya malaria Tanzania' lililofanyika jijini leo Dar es Salaam.

Amesema kuwa kadili mama mjamzito anavyotumia vizuri dawa za kujikinga na ugonjwa wa  Malaria wakati akiwa amepata ujauzito ndivyo anavyoweza kuepukana na ugonjwa huo.

"Kawaida mama mjamzito anapofika wiki ya 13 huwa anapewa dawa za kuzuia Ugonjwa wa Malaria kwa ajili ya yeye na kumkimkinga mtoto, hivyo akizitumia sawa sawa kwa kufuata maelekezo ya dokta pindi anapojifungua huwa salama," amesema.

Prof Kamuhabwa amesema kuwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyofanyika katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam imeonyesha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria yamepungua chini ya asilimia moja jambo linaloletea faraja kubwa.

"Tafiti ni jukumu letu kubwa na tunaangalia magonjwa ya kipaumbele katika nchi na Malaria ni ugonjwa wa kipaumbe maana unaathiri akinamama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 5 hivyo hatuna budi kupambana zaidi" amesema.

Amesema kwa sasa MUHAS wanaendesha tafiti nyingine ya dawa mbadala ya Malaria kwa akinamama wajawazito na watoto maana dawa ile ya awali SP imeonyesha kuwaletea sugu akina mama.

"Tunafanya tafiti huko Rufiji ya dawa mbadala ya kuzuia maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria ambapo Shirika la Afya Duniani limetutaka tufanyie utafiki katika nchi mbali mbali dunia japo wenzetu Kenya na Uganda matokeo yameonyesha dawa hiyo inafanya vizuri lakini kabla hapa kwetu hatujaanza kuitumia lazima nasi tufanye utafiki ila matokeo ya awali yanaonyesha dawa hii inafanya vyema.

Dawa wanayoifanyia utafiti inamchanganyiko wa mseto na dawa nyingine ili kupata mbadala na kuachana na SP kwa ajili ya kinga ya akina mama wajawazito na watoto ila tunamalizia utafiti ili tuje tutoe matokeo ifikapo machi mwaka huu.

Kwa upade wake Mtafiti wa Malaria wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilichopo Bombo Hospitali, Tanga, Deus Ishengoma ameiomba serikali kuwasaidia watafiti ili waweze kuibua tafiti zinazotoa majibu tofauti kwa jamii ambapo ka sasa ambapo tafiti nyingi zimekuwa zikigharimiwa na mashirika ya nje jambo linalowanyima uhuru kwa kufanya tafiti za kigunduzi.

"Serikali iliahidi kutoa asilimia moja ya pato la Taifa ili kuwawezesha watafiti nchi nzima ili waibue tafiti za kigunduzi, lakini mpaka leo kimya... tambueni fedha tunazopewa na mashirika ya nje zinakuwa zimelenga kile wanachokitaka wao na tufanye tofauti na tungewezeshwa kufanya tafiti za kigunduzi zingeleta tija kwa jamii, mfano kubuni mbinu mpya za kukabili Ugonjwa wa Malaria katika maeneo yenye Malaria kubwa kule Kanda ya Ziwa, Kigoma na Kusini mbinu ziwe tofauti, vile vile maeneo yenye maambukizi kidogo kama Dodoma, Kilimanjaro, Arusha na  Manyara na kuelekea ukanda wa nyanda za juu kusini mwa Tanzania napo kukawa na mbinu tofauti," Amesema Ishengoma.

Pia ameomba jamii kutumia vema vyandarua wanavyopewa ili kuzuia wasiumwe na mbu na kuachana na mila potofu zinazoweza kudhoofisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria ikiwemo kusema kuwa vyandarua vinazalisha kunguni, vinapoteza hamu ya unyumba kwa wapenzi na wengine wanafugua kuku.

Awali akifungua kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambapo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, Prof Andrew Barnabas Pembe amewaomba watafiti kujitokeza kwa wingi kufanya tafiti zitakazoleta matokeo Chanya katika jamii yetu.

"Niwaombe watafiti wote kujitokeza kwa wingi kuungana na Chuo chetu Cha MUHAS ili tufanye  tafiti zenye tija ili kuweza kutatua matatizo mbali mbali kwa jamii," amesema.

Kongamano hilo la pili limehudhuriwa na watalaamu kutoka Wizara ya Afya, Shirika la Afya Duniani (WHO), SIDA Tanzania, Kituo cha Utafiti Ifakara, Mradi wa Taifa wa kuzuia Malaria pamoja na Vyuo mbali mbali na wadau wa Afya.
Share:

CHADEMA WAMJIBU NDUGAI,WADAI ANAONGOPEA BUNGE NA UMMA WA WATANZANIA


Ndugu wanahabari na watanzania wote, bila shaka mmemsikia Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai tarehe 31 /01/2019 akitoa taarifa bungeni au kile alichakuwa akikiita kuwa ni ufafanuzi juu ya malalamika ya malipo ya matibabu ya Mh Tundu Lissu (MB) wa Singida Mashariki na Mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.


CHADEMA tunalazimika kumjibu Spika Ndugai kwa kuwa bila haya na kwa makusudi ameamua kuliongopea Bunge na umma wa Watanzania. Mh Tundu Lissu ametibiwa na Chama chake CHADEMA, wanachama mmoja mmoja,mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, watanzania waishio ndani na nje na sambamba na hilo wabunge mmoja mmoja walichangia takribani Tsh 43 millioni kutoka katika posha zao kama walivyofanya watanzinia wengine.

Mh Lissu ni Mbunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa mujibu wa sheria ya bunge anastahili kulipwa mshahara wake wa kibunge na posha mbalimbali na pia kutibiwa na Bunge. 

Takribani Tsh. 207 million alizopatiwa Mh Lissu ni stahikl zake halali za kibunge na si pesa ya Matibabu kama Spika alivyoliongopea bunge na umma wa Watanzania. 

Spika amedai kuwa anazo nyaraka za uthibitisho wa malipo ya matibabu tunamtaka atoe hizo nyaraka hadharani .

Sisi Chama,Familia na Mh Lissu mwenyewe wote tuna nyaraka zote za Matibabu kwa kila hatua. Tunalitaka Bunge kulipia Matibabu ya Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa ni haki yake kisheria na si huruma kama anavyojaribu kuonyesha

Share:

Thursday 31 January 2019

SIMBA YAMUUZA KICHUYA MISRI



Kichuya (kushoto) akiwa na Okwi

Baada ya jana klabu ya Simba kuweka wazi kuwa ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu ya Pharco ya Misri juu ya uhamisho wa Kichuya, hatimaye leo dili hilo limekamilika na Kichuya sasa si mchezaji wa Simba tena.

Akiongea na www.eatv.tv Mtendaji mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema Kichuya amesaini mkataba wa miaka 4 na klabu hiyo pamoja na malipo mazuri ambayo hata Simba hawakuwa wanamlipa.

''Kichuya ni kijana wetu na klabu imefaidika naye sana hivyo tunafurahi amepata timu ya daraja la pili na itamlipa vizuri na sisi kama Simba tumepata maslahi mazuri kwahiyo tumemuuza'', amesema.

Kichuya ambaye alisajiliwa na Simba akitokea Mtibwa Sugar atacheza ligi kuu ya Misri licha ya kuwa amesajiliwa na Pharco ambapo kwa mujibu wa Magori ni kwamba tayari timu hiyo imemtoa kwa mkopo katika klabu ya Enppi inayoshiriki ligi kuu.

Tayari Kichuya amesharipoti katika timu ya Enppi na kesho Februari 1, 2019 ataanza mazoezi na timu yake ya Enppi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Misri dhidi ya Al Ahly utakaochezwa Jumanne Februari 5, 2019.

Enppi inashika nafasi ya 14 kati ya 18 zinazoshiriki ligi kuu. Timu hiyo imecheza mechi 20, imeshinda 4, sare 9 na kufungwa mechi 7.
Chanzo - EATV
Share:

YANGA SC YAITOA BIASHARA UNITED KWA MATUTA, YATINGA 16 BORA ASFC


Yanga SC imefanikiwa kwenda hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.

Waliofunga penalti za Yanga SC ni Heritier Makambo, Paul Godfrey, Ibrahim Ajibu, Thabani Kamusoko na Matheo Anthony, za Biashara United zilifungwa na Lenny Kissu, George Makang’a, Derick Mussa, Kauswa Bernard, wakati Tariq Seif akapaisha ya nne.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Martin Saanya aliyesaidiwa na Abdallah Rashid na Rashid Zongo, Biashara United ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza 2-1.

Waziri Junior alianza kuifungia Biashara United kwa penalti dakika ya pili tu kufuatia beki Andrew Vincent ‘Dabte’ kumuangusha kwenye boksi George Makang’a.

Yanga SC wakasawazisha kwa penalti pia iliyopogwa na mshambuliaji wake Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe dakika ya saba kufuatia Frank Sekule wa Biashara United kumuangusha Nahodha, Ibrahim Ajibu.

Na Biashara United wakapata bao la pili dakika ya 41 kupitia kwa Innocent Edwin aliyemlamba chenga nzuri beki mkongwe Kelvin Yondan kabla ya kumchambua kwa shuti la kitaalamu kipa Ramadhani Kabwili.

Kipindi cha pili Yanga SC waliingia na mchezo wa kushambulia zaidi kusaka bao la kusawazisha na wakafanikiwa kupata bao la pili dakika ya 73 kupitiakwa mshambuliaji wake Heritier Ebenezer Makambo aliyemalizia mpira ulipanguliwa na kipa Nourdine Balora baada ya krosi ya Mrisho Khalfan Ngassa.
 
Kocha Amri Said ‘Stam’ alichukizwa na kipa wake, Nourdine Balora baada ya bao hilo na akamtoa nafasi yake ikichukuliwa na Hassan Robert.

Kocha huyo alionekana akitoleana maneno makali na kipa huyo kabla ya kumsemea kwa refa Saanya aliyemuinua kwenye benchi na kumuamuru atoke kwenye eneo hilo. 

Yanga SC sasa itamenyana na Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi ambayo iliitoa Mighty Elephant.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ramadhani Kabwili, Paulo Godfrey, Gardiel Michael, Kelvin Yondan, Andrew Vincent ‘Dante’, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Mrisho Ngassa, Pius Buswita/Thabani Kamusoko dk60, Heritier Makambo, Amiss Tambwe/Matheo Anthony dk76 na Ibrahim Ajibu. 

Biashara United; Nourdine Balora/Hassan Robert dk76, Taro Ronald/Kauswa Bernard dk67, George Makang’a, Waziri Junior/Tariq Seif dk63, Juma Mpakala, Frank Sekule, Innocent Edwin, Lenny Kissu, Wilfred Nkouzima, Derick Mussa na Abdulmajid Mangalo.
Share:

TGNP MTANDAO YATOA MAPENDEKEZO MANNE TUKIO LA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE

Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao Lilian Liundi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UKATILI DHIDI YA WATOTO HAUKUBALIKI, HAUVUMILIKI, TUWALINDE WATOTO.

TGNP Mtandao kwa kushirikiana na wadau wa haki za wanawake, watoto  na usawa wa kijinsia tunatoa salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza watoto Mkoani Njombe kutokana na matukio ya mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikina. 


Vitendo hivi ni vitendo ambavyo havikubaliki katika jamii kwani ni kinyume cha Azimio la ulimwengu juu ya haki za binadamu (Universal Declaration of Human Rights) la tarehe 10 Desemba 1948. Kifungu cha 3 kinachotamka kwamba “Kila mtu ana haki ya kuishi, haki ya uhuru na haki ya kulinda nafsi yake. Na ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977)  Ibara ya 14 imetamka juu ya Haki ya kuishi sambamba na sheria ya Haki ya kuishi ya mwaka 1984.

Jamii inawajibu wa kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia. Hii ni kwa mujibu wa sheria ya mtoto na. 21 ya mwaka 2009 na mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA), unaolenga kupunguza kiwango cha ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii yetu kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Matukio kama haya yamesababisha vifo vya wananchi (wanawake, wanaume, wazee na watoto) wasio na hatia kama vile mauaji ya vikongwe, watu wenye ualibino na sasa yanafanyika kwa watoto ambao hawana ulemavu.

TGNP Mtandao, tunatambua jitihada za serikali ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa katika kukabiliana na suala hili, na kamati ya kuchunguza mauaji haya tayari imeundwa. Kwetu sisi tunaona ni jitihada nzuri pamoja na kwamba upelelezi unaendelea, tunashauri yafuatayo:-

⇰ Kamati iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, ilete majibu hayaka iwezekanvyo, na taarifa ya uchunguzi ifanyiwe kazi kwa wakati ili kutokomeza kabisa mauaji haya.

⇰    Serikali na vyombo vya dola visimamie kikamilifu sheria ya kudhibiti uchawi na. 12 ya mwaka 1998(The Witchcraft Act). Ambayo imeainisha adhabu kwa watu wanaoendesha vitendo vya kishirikiana vinavyoweza kudhuru wengine.

⇨ Tunalitaka jeshi la polisi  na vyombo vingine vya dola kuhakikisha watoto wanakuwa salama kwa kuimarisha ulinzi katika maeneo yote yanayotajwa kuwa sio salama katika mkoa wa Njombe ili kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo kikamilifu.

    Tunaitaka jamii kutoa  ulinzi wa mtoto kwani ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha ustawi wa watoto. Pia, serikali na wadau kuzijengea uwezo kamati za ulinzi wa watoto ili waweze kutimiza majukumu yao ikiwemo kubaini maeneo hatarishi katika kijiji/ mtaa na kupanga mikakati ya kupunguza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Imetolewa na

Lilian Liundi
Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao.
Januari 30,  2019.
Share:

KIKOSI CHA INTELIJENSIA CHAINGIA RASMI NJOMBE KUONGEZA NGUVU YA UPELELEZI WA MAUAJI

Na.Amiri kilagalila Kamishna wa operesheni na mafunzo ya jeshi la polisi nchini NSATO MARIJANI akiwa na wataalamu wengine wa intelijensia wamefika mkoani Njombe ili kuungana na jeshi la polisi mkoani humo katika kupambana na mauaji dhidi ya watoto wadogo. kikosi hicho maalumu kimewasili mkoani Njombe Ikiwa ni siku moja imepita tangu naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi amuagize IGP SIMON SIRRO kutuma kikosi maalumu cha kiintelijensia kuongeza nguvu katika uchunguzi wa watekaji na wauaji wilayani Njombe. Akizungumza katika mkutano wa dharura na wananchi katika kituo kikuu cha mabasi…

Source

Share:

TUNDU LISSU AMJIBU NDUGAI " BUNGE HALIJAWAHI KUNILIPA HATA SENTI MOJA'

Tundu Lissu amesema Bunge la Tanzania halijawahi kutoa hata senti moja kugharamia matibabu yake.

Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Januari 31, 2019 saa chache tangu Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kusema Desemba 2018, Lissu alikuwa amelipwa Sh207.8 milioni zikiwa stahiki zake na Sh43 milioni zilizotolewa kama mchango wa matibabu kwake.

Lissu amekiri kulipwa Sh43 milioni zilizotolewa na wabunge wenzake kama mchango wao na kwamba kiasi kingine alicholipwa kinachofanya jumla ya fedha hizo kufikia Sh250 ni mishahara na stahiki zake, lakini siyo gharama za matibabu.

Ametoa sababu tatu ambazo Spika Ndugai alizitoa Aprili mwaka jana, kwamba Bunge haliwezi kulipia gharama za matibabu yake.

Lissu amezitaja sababu hizo kuwa hawajapata barua ya kibali ya madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili; hawajapata barua ya kibali cha Katibu Mkuu Wizara ya Afya; na tatu hawajapata barua ya kibali cha Rais (John) Magufuli kuidhinisha malipo hayo.

“Sasa anaposema wamenilipa pesa hizo anapaswa kuulizwa, je, ni lini walipata barua hizo tatu za vibali?” amehoji Lissu na kuongeza:

“Ukweli pekee uliopo ni kwamba Bunge halijawahi kunilipa hata senti moja ya gharama za matibabu yangu. Hata senti moja!”

Na Kalunde Jamal, Mwananchi 
Share:

BAWACHA TAIFA WALAANI VITENDO VYA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE

Baraza la wanawake Chadema Tanzania (BAWACHA) wameungana na watanzania wengine hususani wananchi wa mkoa wa Njombe kulaani vitendo vya mauaji ya watoto yaliyotokea hivi karibuni mkoani humo . Katika taarifa iliyotolewa na mwenyekitiki wa Baraza hilo Taifa HALIMA MDEE imeeleza kuwa Kwa kipindi cha takriban mwezi mmoja sasa kumekuwa na habari za kutisha kutoka mkoani Njombe ambapo vyombo vya habari mbalimbali vimeripoti kuwepo kwa mfululizo wa mauaji ya watoto wapatao 10, ambao wametekwa na kuuwawa kwa kuchinjwa katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe na Halmashauri ya Wilaya…

Source

Share:

MALORI 8 YALIYOSHEHENI MBAO NA MKAA YAKAMATWA NA TRA NJOMBE KWA KUKWEPA KODI

Na Amiri kilagalila Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Njombe inayashikilia Magari makubwa 8 yaliyosheheni mizigo ya Mbao kwa makosa ya kukwepa kulipa Kodi. Akizungumza na waandishi wa habari mapema siku ya leo katika kituo cha ukaguzi wa Magari kilichopo kibena njia panda ya kuelekea lupembe halmashauri ya mji wa Njombe,meneja wa TRA mkoa wa Njombe MUSA SHAABAN alisema kuwa malori hayo yanashikiliwa kwa makosa makuu mawili ikiwemo kuto kuwa na risiti za manunuzi. “Haya malori tumeyakamata kwasababu kuu mbili na sababu ya kwanza tumekagua risiti za manunuzi sasa…

Source

Share:

WEMA SEPETU NA DIAMOND PLATNUMZ USO KWA USO.. WAZUA GUMZO LA AINA YAKE


Msanii wa Bongo Fleva, Wema Sepetu na Diamond Platnumz leo Alhamisi Januari 31, 2019 wamekuwa kivutio katika viwanja vya Leaders Club ambako mkutano kati ya wasanii na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda unatarajiwa kufanyika.

Diamond amewasili viwanja hivyo majira ya saa 9:15 alasiri akiwa katika gari jeusi aina ya BMW X6 huku akiwa amevalia kanzu nyeupe na kilemba.

Akiwa amesindikizwa na walinzi wake, Diamond alipofika alielekea kushoto mwa jukwaa na kusalimia baadhi ya wasanii kabla ya kuelekea jukwaa kuu ambapo Wema na wasanii wengine walikuwa wamekaa.

Alianza kumsalimia ofisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara , meneja wake Babu Tale na kisha kumkumbatia mrembo huyo kwa takribani dakika moja kabla hajaenda kusalimia wasanii wengine akiwemo King Kikii, Masanja Mkandamizaji na wengine.

Tukio hilo lilionekana kuwavutia watu waliofika katika viwanja hivyo wakiwemo waandishi wa habari ambao kila mmoja alikuwa akipambana kupata picha.

Na Nasra Abdallah na Hellen Hartley, Mwananchi 
Share:

MABINTI WACHAPANA MAKONDE BAADA YA JAMAA KUWAAMBIA ANAOA MREMBO MWINGINE

Picha haihusiani na habari hapa chini
Mabinti wawili wanauguza majeraha ya kuwekeana baada ya kutwangana makonde wakizozania jamaa mmoja eneo la Kithyoko Kaunti ya Machakos nchini Kenya waliyekuwa wakimmezea mate.

 Inadaiwa kwamba jamaa huyo aliwaalika kwake na kuwaarifu kuhusu mipango yake ya kutaka kuoa karibuni kwani tayari alikuwa amepata binti wa kumuoa. 

 “Mimi nimewaita hapa tukae kama marafiki, lakini cha muhimu ningependa kuwaalika rasmi kwenye harusi yangu itakayofanyika karibuni,” jamaa huyo aliwaambia. 

Katika ripoti ya Taifa Leo la Alhamisi, Januari 31 inadaiwa kuwa, kusikia maneno ya jamaa huyo, mabinti hao walianza kukunja sura zao kwa mshtuko mkubwa huku kila mmoja wao machozi yakimlengalenga. 

 “Loh! Unamaanisha nini? Una hakika unajua unachosema wewe?” Mmoja wao aliuliza kwa mshangao huku ameikunja sura.

 “Najua kila mmoja wenu alitarajia mazuri kutoka kwangu. Lakini poleni sana kwa kuwa hivi sasa nina mchumba nitakayefunga naye pingu za maisha karibuni. Sasa komeni kujipendekeza kwangu na kila mtu ajitafutie maisha yake,” jamaa alisema.

 Inadaiwa mabinti hao walishindwa kujizuia na ghafla wakaanza kutwangana mangumi huku kila mtu akimlaumu mwenzake kwa kumharibia asiolewe na jamaa huyo.

 “Ni wewe… balaa hii yote ni wewe,” mmoja wa mabinti hao alimwambia mwenzake akimwonyesha kidole.

Inaelezwa kuwa binti mwenzake alimjibu kwa maneno ya kukera huku akimkejeli mwenzake aliyekuwa amemwonyesha kidole. 

 “Chunga mdomo wako. Si ulikuwa ukiringa utaolewa naye. Umekula hu!” alisema na wote kupigana na kuangushana hadi sakafuni huku jamaa akiwatenganisha.

 “Tokeni hapa sasa mumezidi. Nimewaambia msijipendekeze kwangu tayari nina mchumba wa kuoa. Sijui mnapigania nini sasa. Hebu! Kila mtu nje mkapiganie huko,” jamaa huyo aliwavuta na kuwaondoa nje kisha akaufunga mlango wake.

 Mabinti hao walizozana nje kwa muda kabla ya kila mtu kushika hasini zake na kutokomea baada ya majirani na watu kujikusanya kuangalia sinema ya bure. 

Via Tuko 
Share:

NDUGAI : NI VYEMA WATANZANIA WAKAJUA HUYU MWENZETU 'ZITTO KABWE' NI MUONGO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amemtaka Mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe amwogope Mungu na aache kuwa mwongio kwenye taarifa zake ikiwa ni pamoja na tuhuma za upotevu wa Shilingi trilioni 1.5.

Akizungumza bungeni leo Alhamisi Januari 31, 2019 Ndugai amesema licha ya uongo huo ni mapema mno kumpeleka kiongozi huyo wa ACT katika Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Amesema Zitto amekuwa akiandika kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Ndugai kuikalia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu upotevu wa Sh1.5 trilioni, jambo ambalo si kweli.

Ndugai amebainisha kuwa taarifa za mbunge huyo kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli na ni uongo mtupu

“Kwa mfano, aliandika katika mtandao wake kuwa nilipokea ripoti ya CAG tangu Januari 8, 2019 nikaikalia wakati mimi nimepokea taarifa hiyo Januari 16, 2019 na Januari 18, 2019 niliwapa kamati ya PAC. Ni vyema Watanzania wakajua huyu mwenzetu ni muongo,” amesema Ndugai.

Amesema Bunge liliweza kujadili habari za Sh300 bilioni kwa nguvu iweje washindwe kujadili kuhusu Sh1.5 trilioni ambazo ni nyingi.

Hata hivyo, amesema CAG, Profesa Mussa Assad alishaulizwa mbele ya Rais John Magufuli kuhusu fedha hizo na kubainisha kuwa hakuna upotevu wa kiasi hicho na hata kamati ya PAC ilishasema hakuna upotevu, lakini anashangaa kuona Zitto analisambaza jambo hilo.
Share:

KESI YA MBOWE NA MATIKO YAPANGIWA HAKIMU MPYA


Kesi inayowakabili baadhi ya viongozi wakuu wa Chama na Wabunge 7 wa Chadema, imeendelea leo ambapo imepangiwa Hakimu mpya anayejulikana kwa jina la Kelvin Mhina.

Hatua hiyo ya kesi hiyo Na.112/2018 kupangiwa Hakimu mpya imekuja baada ya aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Dar es salaam, Wilbard Mashauri kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kuteuliwa na Rais Januari 28,2019.

Wakati akiwa Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri aliwafutia dhamana viongozi wawili wa CHADEMA, M/Kiti , Mbowe na Mbunge Esther Matiko kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa na Mahakama.

Katika kesi hii ya viongozi wa CHADEMA, Hakimu mpya Kelvin Mhina, ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 14, 2019 itakapotajwa tena baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kutoa taarifa kwamba kesi hiyo ilienda kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanasubiri uamuzi wa mahakama ya rufaa.

Ameeleza kwamba upande wa mashtaka ulikata rufaa kupinga dhamana hivyo kesi hiyo itaanza kusikilizwa Februari 18, 2019.

Hata hivyo, Mbowe na Matiko bado wanaendelea kusota rumande kutokana na kufutiwa dhamana.

Chanzo - EATV
Share:

MBUNGE WA CHADEMA GODLESS LEMA ATANGAZA KUJIUZULU


Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA), Godbless Lema.


Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa endapo Spika wa Bunge Job Ndugai atalithibitishia bunge kuhusu kauli yake dhidi ya matibabu ya Lissu, yeye atakuwa tayari kujiuzulu.

Lema ametoa kauli hiyo kwenye ukurasa wake wa 'twitter' ambapo amejibu kauli iliyotolewa na Spika akiwa bungeni leo ambapo amesema kuwa mpaka sasa bunge limegharamia shilingi milioni 250 katika matibabu ya mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

"Bunge halijawahi kumlipia Mh Lissu pesa kwa ajili ya matibabu, alichokisema Mh Spika Ndugai ni upotoshaji kwa jamii na Mungu. Chama kitatoa tamko juu ya hili. Spika akiweza kuthibitisha hili, mimi nitajiuzulu Ubunge, mshahara wa Mbunge sio hisani ya Spika", ameandika Lema.

Akizungumza bungeni leo, Januari 13 Spika Job Ndugai amesema hadi sasa Bunge limeshamlipa Tundu Lissu shilingi milioni 250 kwa ajili ya matibabu yake.
Share:

NDUGAI SASA KU- DILI NA TUNDU LISSU "ADAI AMELIPWA MIL 250 KUTOKA BUNGENI"


Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuanzia sasa ataanza kumjibu mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kwa kuwa ana amini amepona na kwamba tayari ameshalipwa Sh250milioni kutoka bungeni.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Januari 31, 2019 bungeni mjini Dodoma baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Amesema hadi mwishoni mwa Desemba 2018, Lissu alikuwa amelipwa Sh207.8milioni pamoja na Sh43 milioni zilizotolewa kama mchango wa matibabu ya mbunge huyo.

Amesema kwa ujumla hadi sasa Lissu amelipwa Sh250milioni kutoka bungeni.

“Siku za mwanzo sikutaka kujibu maana niliamini kumjibu mtu aliyelala kitandani siyo vizuri kwani kuna vitu huenda vingekuwa vimempita, lakini sasa naamini ni mzima hadi anafanya ziara nje. Nalisema hili akijibu nakuja na mkeka hapa,” amesema Ndugai.

Amesema mbunge huyo amekuwa akilalamika kila wakati kuwa Bunge halimjali kitu ambacho hakina ukweli ndani yake na hakuna madai kama hayo.


Na Habel Chidawali, Mwananchi
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger