Wednesday 31 August 2016

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 31.8.2016

Share:

Tuesday 30 August 2016

Walimu 22 Azania Sekondari Waondolewa Baada ya Shule Kuwa ya Mwisho Matokeo Kidato cha Sita

Walimu 22 wa Shule ya Sekondari ya Azania Manispaa ya Ilala, akiwamo Mwalimu Mkuu, wamehamishwa kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha sita.
Chanzo hicho cha habari kiliongeza kuwa kati ya walimu hao, 17 walikuwa wanafundisha kidato cha tano na sita huku wanne kidato cha kwanza hadi cha nne na mmoja aliyekuwa mkuu wa shule hiyo.
Taarifa hizo ziliongeza kuwa kati ya walimu 17, wengi wao walikuwa wanafundisha mchepuo wa ECA ambao wote wamehamishwa na kupangiwa shule nyingine huku wengine wakihamishiwa shule za kata na kupangiwa kufundisha kidato cha kwanza, pili na tatu. Awali, walimu hao walikuwa wakifundisha kidato cha tano na sita.

Hivi karibuni Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), lilitangaza matokeo ya kidato cha sita na shule hiyo kongwe ikajikuta imo katika kundi la shule 10 za mwisho zilizokuwa na matokeo mabaya.
Share:

SCHORALSHIP NCHINI MEXICO KWA WATANZANIA,HASA WALIOMALIZA FORM SIX MWAKA HUU 2016

http://kurasampya.com/wp-content/uploads/2016/07/kurasa-Mpya-620x400.png
Share:

Aliyedaiwa kuuawa na polisi azikwa saa 4.00 usiku

 
Mwili wa marehemu Stanslausi Kalinga (42) aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi ulizikwa saa 4.00 za usiku nje kidogo ya Mji wa Mlowo baada ya ndugu zake kukubali yaishe.
Marehemu ambaye ameacha mke na watoto wanne alifariki akiwa mikononi mwa polisi jambo lililosababisha vurugu kutoka kwa wananchi ambao walitaka mwili uzikwe na polisi wenyewe.
Wananchi hao walisusia mwili tangu Agosti 27 hadi juzi usiku ambapo mwili ulirudishwa kutoka Hospitali ya Rufaa Mbeya ulikopelekwa kwa uchunguzi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Ernest Paringo.
Hata hivyo hakuna majibu ya uchunguzi yaliyotolewa licha ya ndugu wa marehemu kushiriki katika kuufanyia uchunguzi mwili huo.
Share:

Tahadhari dhidi ya Taarifa za uongo kuhusu kutangazwa kwa Orodha ya wanafunzi waliodahiliwa kwa mwaka wa masomo 2016/2017

kurasa Mpya

Tahadhari dhidi ya Taarifa za uongo kuhusu kutangazwa kwa Orodha ya wanafunzi waliodahiliwa kwa mwaka wa masomo 2016/2017
tcu new
Share:

Wanafunzi hewa 4,445 wabainika Kahama




NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jaffo, amesema Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, ina wanafunzi hewa 4445 ambao wanasoma katika shule za sekondari za serikali kinyume na utaratibu.

Jaffo aliyasema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri za Msalala na Mji, juzi, katika ziara ya kushitukiza, ambapo aliwaasa kufanya kazi kwa weledi kwa kufuata sheria na taratibu za kuwahudumia wananchi.

Alisema kuwepo kwa idadi hiyo kubwa ya wanafunzi hewa katika shule za sekondari kunatokana na maofisa elimu kutokujua takwimu za wanafunzi na kuongeza kuwa, muda mwingi wamekuwa wakikaa ofisini bila ya kutembelea maeneo ya kazi.

Naibu Waziri huyo alisema, takwimu za utengenezaji wa madawati, zimekuwa kinyume na ilivyotarajiwa, hali ambayo imesababisha kuchelewa kumalizika kama iliovyokuwa imepangwa na Rais John Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, Naibu Waziri huyo aliwaonya watumishi hao kutotumia fedha vibaya zitakazotolewa na wizara hiyo, kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya barabara katika halmashauri ya mji wa Kahama.

Mbunge wa Jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa Halmashauri ya Mji wa Kahama, ina changamoto nyingi zikiwamo za miundombinu ya barabara, kuzidiwa kwa wagonjwa wanaotoka katika wilaya 16 katika hospitali ya halmashauri ya mji pamoja na upungufu wa watumishi.

Alisema Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama, imezidiwa na wagonjwa ambao wanatoka katika sehemu mbalimbali zilizopo jirani, hali ambayo watumishi wake wanapata wakati mgumu katika kutoa huduma na wakati mwingine kushindwa kutoa huduma kwa wakati.
Share:

Lipumba Aendelea Kung'ang'ania Uenyekiti Wake CUF


Katika hali isiyokuwa ya kawaida Prof Lipumba ameendelea Kung’ang’ania kiti cha uenyekiti wa chama chake cha CUF na kusema kikao kilichokaa jana visiwani Zanzibar na kufanya maamuzi ya kuwasimamisha uanachama, hakikuwa halali na kilikuwa nje ya katiba ya CUF, sababu mojawapo ikiwa ni kuwekwa kando kwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya.

“Kikao hicho  hakikuwa halali, haiwezekani Baraza Kuu linakaa halafu Naibu Katibu Mkuu Bara hajui, wala hakujulishwa, na bado kuna wajumbe wengine hawakuhusishwa” Alisema Prof Lipumba

Lipumba aliongeza kuwa ni kweli alijiuzulu uenyekiti, lakini baadaye aliamua kuandika barua kwa Katibu Mkuu ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu na sasa yeye ndiye Mwenyekiti halali wa chama hicho.

“Nilimuandikia barua ya kurudi kwenye nafasi yangu, akasema anasubiri ushauri wa kisheria, lakini hadi sasa hakuna kitu, hiyo inamaanisha kuwa sasa mimi naendelea na nafasi yangu, na niko ngangari kama mwenyekiti” Alisema Prof Lipumba.

Aidha aliongeza kuwa alitaka kujieleza katika mkutano mkuu mbele ya wanachama, lakini mkutano ule ukavurugwa.

Kuhusu kuwepo kwa tofauti kati yake na Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, Prof Lipumba amesema kuwa huenda kuna tofauti kwa kuwa mara nyingi huwa hamuelewi jinsi anavyokiendesha chama bila kifuata misingi ya kidemokrasia.

“Katibu Mkuu anamdharau na hampi heshima yake Naibu Katibu Mkuu Bara, mara nyingi huamua mambo yake bila kushirikisha viongozi wengine, halafu sasa anataka kufukuza wanachama, huwezi kuwa na chama halafu ufukuze wanachama, wanachama wanatafutwa duniani kote, halafu wewe unawafukuza, hizo ni dalili za uongozi wa kiimla, kuongoza chama unapaswa kujali demokrasia na siyo kuwa dikteta ndani ya chama” Amesema

Kuhusu Julius Mtatiro kuwa mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uongozi, Lipumba amesema kuwa hatambui maamuzi hayo, na wala hamtambui Mtatiro kama kiongozi wa chama hicho bali mjumbe wa Mkutano Mkuu, nafasi ambayo yeye ndiye aliyempa.

“Mtatiro hawezi kuwa mwenyekiti, mimi ndiye mwenyekiti wa chama, Mtatiro alishindwa hata kuongoza mkutano mkuu, ukavurugika, hawezi, simtambui”
Share:

MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI TAREHE 30.8.2016



Share:

Mtoto wa Shule Alivyofumaniwa na Mwanaume wa zaidi ya Miaka 60 Tanga

August 29 2016 Kupitia Hekaheka ya Clouds FM Geah Habib ametuletea Hekaheka iliyotokea Tanga ambapo mzee mmoja kafumaniwa na mkewe akiwa na mtoto wa shule wa miaka 14.

Mjomba wa mtoto ameeleza kuwa mtoto amekuwa akijiandaa asubuhi na mapema sana na anaaga anaenda shule lakini anapitia kwa huyo mzee na baadaye muda wa saa moja anaena shule……

Mahusiano yameanza tangia January, mpaka sasa hivi ni mwezi wa nane na sisi mpaka tumekuja kugundua ni baada ya kutokea ugomvi, mke wake yule mzee amempiga na kumng’ata mtoto ameumia na sisi ndio tukajua hilo suala.

Mtoto wangu ana miaka kumi nne na mzee huyo ana kama 60 mpaka 70 maana ni babu kabisa, sisi halikuwa hatujui tulikuwa tunajua anaenda shule na alikuwa anamuaga bibi yake maana anakaa na bibi yake kwamba wanatakiwa kuwahi namba kumbe asubuhi anaanza kwanza kwa huyo baba.

Jumatano asubuhi walipokutana na huyo baba kupewa hela mara mke wa huyo baba akatoa akaanza kumshambulia na kumng’ata
Share:

DALADALA LAGONGA MAGARI MATATU MAJI MATITU TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM


Wananchi wakiangalia ajali iliyosababishwa na daladala lenye namba za usajili T 397 BVB linalofanya safari zake kati ya Temeke na Gongo la Mboto kwa kuyagonga magari mengine matatu eneo la Maji Matitu Temeke Dar es Salaam leo asubuhi. Katika ajali hiyo dereva wa gari dogo namba T 628 DFE alijeruhiwa.
Gari dogo namba T 628 DFE lililogongwa na daladala hilo likiwa limeharibika.
Daladala hili likiwa limegonga gari namba T 458 CAN.
Kuku waliokuwa kwenye moja ya gari lililogongwa wakiondolewa kuku kadhaa walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Askari wa Usalama barabarani akiangalia ajali hiyo.
Daladala uso kwa uso na gari dogo.

Na Dotto Mwaibale

MKAZI wa Chamazi ambaye ni mwanamke amejeruhiwa baada ya gari lake dogo alilokuwa akiendesha kugongwa na daladala lenye namba T 397 BVB linadodaiwa kuiba njia.

Ajali hiyo imetokea Maji Matitu Temeke jijini Dar es Salaam leo asubuhi ambapo daladala hilo pia liliyagonga magari mengine matatu na kuzua kizaazaa katika barabara ya Charambe kwenda Chamazi.

Mkazi wa eneo hilo Hamisi Juma aliyeshuhudia ajali hiyo amesema ni mungu kasaidia kutokea kwa vifo kwani ajali hiyo ilikuwa ni mbaya sana.

" Saa 12 na dakika 55 nikiwa nasubiri gari kwenda kazini niliona daladala lililokuwa likitoka Charambe kwenda Chamazi lilikuwa likipita upande ambao si wake likiwa katika mwendo wa kasi na ghafla lililigonga gari dogo namba T 628 DFE ambalo ligeuka na kulala katika mtaro" alisema Juma.

Alisema baada ya kuligonga gari hilo liliyaparamia magari mengine madogo mawili likiwepo lililobeba kuku na kuyasukumia kwenye mtaro.

Aliongeza kuwa baada ya kutokea tukio hilo dereva wa daladala hilo alikimbia na kulitelekeza gari lake.

Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T 628 DFE, T 397 BVB, T 451 CQB na T 458 CAN.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ili kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda baada ya simu yake kuita bila kupokewa alipopigiwa simu mara kadhaa.
Share:

UVCCM Waahirisha Maandamano Yao, Watii Agizo la Jeshi la Polisi


Agosti 22, 2016 Umoja wa Vijana wa CCM tuliutangazia umma na dunia kwamba ifikapo Agosti 31 mwaka huu tutaitisha maandamano ya amani nchi nzima yenye lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli kwa utendaji wenye tija, ufanisi na uliorudisha imani na matumaini kwa wananchi.


Msimamo na dhamira ya kufanya maandamano hayo ya amani yenye maudhui na kusudio hilo, bado uko pale pale ingawaje si kwa tarehe tuliopanga na kutangaza awali yaani Agosti 31 mwaka huu.


Jumuiya yetu kama mjuavyo ni ya Vijana wa CCM, (UVCCM) inapata malezi kwa karibu mno na Jumuiya ya Wazazi ya CCM. Wiki ya jana Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Nd. Abdallah Bulembo alikutana na waandishi wa habari akitutaka UVCCM tuahirishe maandamano ya Agosti 31 mwaka huu hadi wakati mwingine.


Kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, Jumuiya ya Wazazi ndiyo Msimamizi wa Malezi, Maadili na Adabu kwa Vijana wote nchini, sisi UVCCM tunaamini kuwa sikio halishindani na kichwa, mtoto ni mtoto kwa Wazazi wake hakui, hana jeuri wala ubishi.


Mtoto au watoto wanaokaidi amri, ushauri au maelekezo ya Wazazi wao huitwa watukutu, wenye viburi, manunda na wasioambilika. UVCCM si watukutu, hatukufunzwa tuwe wabishi, wakaidi na wenye viburi. Tumezingatia kutii maelekezo, makatazo na maonyo , tumeambiwa tuahirishe maandamano yetu nasi tumekubali na kuheshimu mambo tuliyoaswa.


Sambamba na hilo tumepata majibu ya barua yetu tuliyomwandikia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP Ernes Mangu) inayotutaka tuache kufanya maandamano yetu kwa sababu Polisi wamezuia mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa na maandamano nchi nzima.


Jambo jingine ambalo limetufanya pia tuahirishe maandamano yetu ya Amani ni taarifa ya kintelejinsia iliowasilishwa na Kamati yetu ya Usalama na Maadili ya UVCCM mbele ya kikao cha Sekreteriet yetu, nayo ilipendekeza suala hilo liahirishwe kwa wakati huu hadi muda mwingine.


Pia jambo jingine ambalo limefanya maandamano hayo tuyabatilishe ni kulipisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) ambalo litakuwa katika shughuli za maadhimisho miaka 52 tokea kuanzishwa kwake.


Wanajeshi wetu watakuwa katika kazi mbalimbali za kijeshi kwenye kambi zao na mitaani kufanya usafi wa mazingira, hivyo isingependeza na wala si heshima wakati sisi tukiandamana, wao wakifanya kazi muhimu kila mmoja wetu zinazomgusa badala yake ni vyema kuwaunga mkono jambo wanalolifanya la usafi wa mazingira.


UVCCM tumekubali, hatutaki kuingia katika uvunjaji wa sheria hasa baaada ya kutakiwa kuahirisha na mamlaka za Kisheria hadi wakati mwingine muafaka na si wakati huu.


Tunaelewa kwamba uamuzi wetu wa awali wa kutaka kuandamana kwa amani hata kama tungenyimwa kibali ungetugharimu, ungetusababishia madhara na pengine hasara, kwa wakati huu na kuona jambo lenyewe ni la kuipa Ari serikali katika kuhimiza Uwajibikaji, Utendaji na Usimamizi bora wa Uendeshaji wa masuala ya kiutawala.


Tulishusha maagizo kwa Makatibu wetu wote wa Mikoa yote 32 na Wilaya 171 ya Kichama tukiwataka waandike barua katika Ofisi za Ma RPC na OCD, washirikiane ili kuratibu maandamano na kuyafanikisha kama tulivyokusudia.


Watendaji wetu wa ngazi husika wamefuata maelekezo, wametii taratibu zetu za kiutendaji na leo tumewajulisha tena wasitishe maandamano hadi tutakapowapa tena maelekezo mengine. Tunawahimiza na kuwataka ni vyema kutii mamlaka za Kikanuni na Kisheria.

UVCCM kwa wakati huu tumeamua kuachana na maandamano badala yake tunajikita katika matayarisho ya kuwapeleka Vijana wetu wakashiriki katika Mafunzo ya Siasa, Utawala, Uongozi, Ufundi na Ujasiriamali yatakayoanza kufanyika katika Chuo chetu kilichopo huko Ihemi Mkoani Iringa ambapo kitakuwa kielelezo na alama nzuri ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa vitendo.

Tumewataka Makatibu wetu wa Mikoa na Wilaya kuendelea na zoezi la Uratibu na Uhakiki kwa Vijana ambao watateuliwa kushiriki Mafunzo hayo huko Ihemi.

UVCCM tunarejea kusema tena kwamba dhamira ya maandamano yetu ya kusifu Utendaji wa Serikali ya awamu ya tano iko pale pale ila tutapanga tarehe nyingine katika wakati ujao badala ya kufanyika Agosti 31 mwaka huu kama tulivyotangaza hapo awali.

UVCCM tunawataka Vijana wote kuendelea kuheshimu Tunu ya Amani Umoja na Mshikamo wetu kwa Taifa.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)

KAIMU KATIBU MKUU.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger