Friday 29 July 2016

Mkapa ahimiza sera zinazotekelezeka


RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amezitaka nchi za Afrika kuhakikisha zinatoa kipaumbele katika uongozi unaojali masuala ya utawala bora, uzalendo na sera zinazotekelezeka ili kuweza kupata maendeleo endelevu.
Kwa mujibu wa Mkapa pamoja na marais wengine wastaafu wa nchi za Afrika, endapo nchi hizo zitashindwa kutumia njia sahihi kufikia malengo yake ya maendeleo zitajisababishia kuwa nchi zisizo na usawa katika mgawanyo wa mali na migogoro.
Akizungumza katika Kongamano la Viongozi wa Afrika lililofanyika jijini Dar es Salaam jana, Rais Mkapa alisema ni lazima Waafrika wajitume na kujiletea maendeleo yao wao wenyewe na kusisitiza kuwa hakuna mtu yeyote wa mataifa ya nje atakayewasaidia.
Alisema ni wakati muafaka sasa kwa Waafrika kuungana na kutumia uwezo walionao kuhakikisha ajenda ya Umoja wa Afrika (AU) ya kutafuta na kutumia rasilimali zinazopatikana Afrika ifikapo mwaka 2063 inafanikiwa.
“Kaulimbiu ya mwaka huu, inasema namna Sekta ya Biashara inavyoweza kuleta mageuzi Afrika kwa haraka. Kama mnavyojua katika ajenda yetu ya 2063 tumejiwekea malengo ya kuhakikisha nchi za Afrika zinakua kiuchumi na kuwa na maendeleo endelevu…lakini ili haya tuyafanikishe ni lazima tutegemee zaidi ushiriki wa Waafrika,” alifafanua.
Alitolea mfano kipindi cha uongozi wa Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere kwamba aliweka msisitizo katika masuala ya watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora ili kuwapatia maendeleo Watanzania.
“Ardhi tuliyonayo inaweza kutumika kwa manufaa yetu, watu tulionao tunaweza kuwahamasisha kuwajibika, sera nzuri zinaweza kusaidia kusukuma watu kuleta maendeleo lakini pia utawala bora unatengeneza njia kwa maendeleo endelevu,” alisema Mkapa.
Naye Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Wachimba Madini cha Afrika Kusini na mtoa mada mkuu katika mkutano huo, Sipho Nkosi, alisema Afrika imekuwa na maendeleo mazuri ya kibiashara kwa muda mrefu na kusisitiza kuwa kwa mwenendo uliopo, bara hilo litaleta mageuzi makubwa duniani.
Nkosi ambaye ni bilionea wa tatu kwa utajiri Afrika Kusini, alisema kila nchi ya Afrika ina wajibu kutengeneza mazingira mazuri na fursa kwa wafanyabiashara Waafrika ili kuwajengea uwezo na kuwapa nafasi ya kuwa sehemu ya mafanikio ya nchi yao.
Kwa upande wake, Rais mstaafu wa Msumbiji Joaquim Chissano, alisisitiza umuhimu wa kutafuta mbinu bora za kisasa za kutumia ardhi ili iweze kuleta maendeleo katika nchi hizo za Afrika badala ya kutegemea zaidi mikakati na mbinu za nchi za Magharibi.
Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika, Frannie Leautier, alisema nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na ukosefu wa viongozi wenye mikakati na uwezo wa kuziletea mabadiliko ya kiuchumi hali inayosababisha nchi hizo uchumi wake kukua taratibu.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, alisema viongozi wanaochukia ubinafsi ndio chachu katika kuwawezesha Waafrika kukua kimaendeleo.
Share:

Asilimia 60 ya waajiriwa hawana mikataba ya kazi


KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimezindua Ripoti ya Haki za Binadamu na Biashara kwa Mwaka 2015 ambacho kimebainisha kuwa asilimia 60 ya wafanyakazi nchini hawana Mikataba stahiki ya kazi, jambo linalosababisha serikali kupoteza mapato ya kodi.
Aidha ripoti imebainisha Mikataba mingine iliyopo kuwa na upungufu mwingi ikiwa ni pamoja na miongoni mwao kuandikwa kwa lugha isiyoeleweka na mingine kuandikwa kwa ufupi na kushindwa kujumuisha mambo ya msingi.
Nalo Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), limekiri kuwepo kwa matatizo hayo kwa wafanyakazi lakini likafafanua kuwa wengi ni waoga kufukuzwa kazi, hivyo wanashindwa kujitokeza hadharani na kueleza yanayowasibu.
Akizungumzia ripoti hiyo wakati wa uzinduzi jijini Dar es Salaam jana, Mtafiti wa Taarifa wa LHRC Clarence Kipobota alisema miongoni mwa wafanyakazi ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa kukosa Mikataba halali ya kazi ni pamoja na waandishi wa habari pamoja na madereva.
Alisema kutokuwepo pia kwa vyama vya wafanyakazi katika maeneo ya kazi, kumekuwa kukichangia wengi wao kukosa makubaliano ya pamoja.
“Hali ya ajira na mahusiano kazini inakabiliwa na changamoto kubwa, wengi hawana Mikataba na matokeo yake Serikali inakosa kodi ambayo ingekatwa katika Mishahara inayofahamika kama PAYEE,” alisema Kipobota huku akiitaka Tucta kusaidia kumalizwa kwa tatizo hilo.
Aidha alisema utatuzi wa masuala ya kazi unaofanywa na Tume ya Usuluhishi wa Migogoro sehemu ya Kazi (CMA) umekuwa hauna kasi kama inavyotakiwa kumalizika ndani ya siku 60 ambapo mashauri mengi huchukua muda mrefu.
Alisema asilimia 57.5 ambayo ni sawa na mashauri 30,095 ndio ambayo yamesikilizwa tangu mwaka 2006 hadi 2015.
Kuhusu suala la ardhi alisema ardhi za vijiji zinaendelea kuchukuliwa ambapo wawekezaji wa ardhi wamekuwa wakichukua eneo kubwa na kuliacha bila kuendelezwa huku wananchi wakiendelea kuhangaika jambo linalozalisha migogoro ya wakulima na wafugaji.
Share:

Chadema yakosa pa kushika


SIKU moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza nia ya kufanya mikutano ya hadharani nchini kote kuanzia Septemba Mosi kutokana na sababu mbalimbali, taasisi na wadau mbalimbali wamelaani mpango huo.
Akizungumzia hilo, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema amepokea kwa masikitiko makubwa tamko hilo, huku Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikijitokeza na kulaani mpango huo.
Wengine waliopinga mpango huo ni wasomi wakiwemo Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayejipambanua katika siasa za upinzani, aliyewahi kuwa mwanachama wa Chadema, Dk Kitila Mkumbo na wachambuzi wa Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Benson Bana na Dk Bashiru Ally.
Msajili vyama vya siasa alaani
Akizungumzia tamko hilo la Chadema, Jaji Mutungi alisema limejaa lugha ya uchochezi, kashfa, kuudhi na lenye kuhamasisha uvunjifu wa amani.
Alisema kimsingi Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu (2) (c) inakataza chama cha siasa kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia malengo yake kisiasa.
Alisema aidha kifungu cha 9 (2) (f) kinakataza chama cha siasa kuruhusu wanachama au viongozi wake kutumia lugha ya matusi, kashfa na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au kupelekea kutokea uvunjifu wa amani.
Alisema pia kanuni ya Maadili ya Vyama vya Siasa, Tangazo la Serikali namba 215, linakataza chama cha siasa kutumia lugha za matusi, kashfa, uongo na uchochezi.
Alisema Kanuni ya 5 (1) (d) inakitaka chama cha siasa kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni uongo, kuhusu mtu yeyote au chama cha siasa chochote. “Hivyo tamko la Chadema ni ukiukwaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
Aidha, hii si mara ya kwanza kwa Chadema kutumia lugha za namna hii za kuhamasisha uvunjifu wa amani.
“Natumia fursa hii kukemea tamko hilo hadharani, kwa mujibu wa kanuni ya 6 (2) ya Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa, pia nawaasa Chadema wasiendeleze tabia hii,” alisema Jaji Mutungi.
Alisema dhamana aliyopewa kama Msimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa kazi yake ni kuviasa vyama vyote vya siasa vitimize wajibu wao kwa weledi kama taasisi za kisiasa.
“Ni vyema viongozi wa vyama vya siasa wakaonesha taswira stahiki ya wanasiasa wakomavu, au vyama vya siasa vya kutolea mfano ndani na nje ya mipaka yetu, kwa kuzingatia sheria za nchi katika kuendesha shughuli za kisiasa. “Vyama vya siasa viepuke vitendo, kauli au matamshi yenye mlengo wa kusababisha uchochezi au kufarakanisha umma na serikali yao. Navisihi kuzingatia utaratibu wa mawasiliano kwa mujibu wa sheria zilizopo, aidha uvumilivu wa kisiasa katika azma za kudumisha ukuaji wa kidemokrasia nchini haukwepeki,” alisema Jaji Mutungi.
CCM wajibu mapigo
Katika hatua nyingine CCM imeionya Chadema kuacha kupotosha umma na kutaka kuwaaminisha wananchi uongo wanaoutunga ili kujaribu kupata wafuasi.
Aidha, imewataka Watanzania kupuuza maandamano yaliyopangwa kufanywa na Chadema kwa kuwa ni ishara ya kuchochea uvunjifu wa amani, huku ikiwataka viongozi hao wanaoshinikiza maandamano kuandamana na familia zao.
Msemaji wa CCM, Christopher ole Sendeka alisema Dar es Salaam jana kuwa tamko lililotolewa na Chadema la kupanga kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima kuanzia Septemba Mosi mwaka huu, limejaa uongo na ubabaishaji na linaonesha kuwa wapinzani wamekosa ajenda na njia pekee wanayoona inafaa ni kutunga utapeli, uongo na uzushi.
Alisema kimsingi hoja walizotumia kufikia uamuzi wao bila kuzirudia zimejaa upotoshaji na uongo uliokithiri.
Alisema kwa mfano chama hicho kimekuwa kikidai serikali imezuia mikutano yote ya vyama vya siasa huku wakijua jambo hilo si kweli. “…Wamekuwa wakisema hivyo huku wakijua kuwa ni uongo kwani serikali haijazuia mikutano. Kwenye majimbo wabunge wao wako huru kufanya shughuli zao, tumeona wabunge wakifanya mikutano kwenye majimbo ikiwemo wa upinzani,” alisema Ole Sendeka.
Alisema vyama vya siasa kufanya shughuli zao kwa mujibu wa Katiba si kosa na wala si jambo ambalo limezuiliwa na ndio maana imeshuhudiwa vyama vya siasa vikifanya mikutano yao ya kikatiba bila tabu.
Ole Sendeka alisema jambo lingine ambalo ni hoja za uongo na uzushi ni kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ni ya kidikteta, na alihoji udikteta wanaousema Chadema ni upi? “Ni huu wa kushughulikia watumishi hewa, ni huu wa kuwabana wakwepa kodi, ni huu wa kupunguza na kudhibiti safari za nje, ni huu wa kubana matumizi ya serikali, ni huu wa kufukuza wazembe na wabadhirifu kazini? “Hivi udikteta huo ni huu wa kushughulikia mafisadi na mpaka kuanzisha Mahakama yao?” Alihoji Msemaji huyo wa CCM.
Alisema CCM inaamini Watanzania wengi wanaunga mkono hatua zinazochukuliwa na Rais John Magufuli na serikali yake, lakini kama hatua hizo Chadema inaona ni udikteta bila shaka wao ni sehemu ya mfumo mbovu na ndio maana wako tayari kuleta vurugu.
Wasomi UDSM wafunguka
Wakitoa maoni wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mkumbo, Dk Bashiru na Bana walikosoa mpango huo wa Chadema. Profesa Mkumbo alisema vyama vya siasa vina wajibu wa kulinda misingi ya demokrasia lakini pia vina haki ya kupigania kufanya shughuli za siasa ingawa si kwa mapambano.
Alisema ni muhimu vyama vya siasa kujenga amani ya nchi lakini akasema ni muhimu pia kwa Jeshi la Polisi kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu kupinga mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa.
“Pande zote mbili yaani Jeshi la Polisi na vyama vya siasa vipeane nafasi kila mmoja, bila kuvuruga shughuli za maendeleo, kulindwa kwa demokrasia na kuiendeleza,” alisema Profesa Mkumbo.
Naye Dk Bashiru alisema kauli ya kufanya mikutano nchi nzima ni vyema ikafafanuliwa, kuhojiwa au kutafsiriwa na taasisi za kidemokrasia ikiwemo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambayo inasiamamia sheria za vyama vya siasa.
Alisema taasisi hiyo itoe ufafanuzi kwa kuzingatia sheria ili kuongoza kauli na vitendo vitolewavyo na vyama vya siasa katika kukuza demokrasia, pamoja na kuangalia matakwa ya wanasiasa ili isiwe ni kuvuruga misingi ya mamlaka.
Alisema hakuna mahali utaratibu, sheria na kanuni zinafuatwa kiholela, na kwamba uholela haujengi demokrasia bali ni chanzo cha chuki na hata kuumiza, hivyo yawepo mazungumzo ili kufikia muafaka na kama yupo asiyeridhika aende Mahakamani.
Kwa upande wake Dk Bana alisema kukaidi agizo linalotolewa na vyombo vya dola sio jambo jema na kwamba ni vyema kuheshimu ikiwa ndio njia ya kukuza demokrasia. Alisema kama chama hicho kinaona hakiridhiki na maagizo hayo wanaweza kutafuta ufumbuzi wake kwa kwenda Mahakamani ili kuitafuta huko.
Akizungumzia sakata hilo, Dk Bana alisema mpango huo si suluhisho la maridhiano ya kisiasa na badala yake utaleta vurugu na kuchochea uvunjifu wa amani.
Alisema Chadema wanapaswa kuachana na mpango huo na badala yake waombe kuonana na Rais Magufuli na viongozi wengine wa Serikali ili kuwasilisha hoja zao kuhusu mambo wanayoona hayaendi sawa, akisema Rais Magufuli ni msikivu.
‘Kutumia ubabe hakuwezi kuzaa mwisho mwema kwao, wangeweza pia kulitumia Bunge lakini walilikwepa, hivyo si njia za kiungwana kufanya mikutano hiyo kwa nchi nzima na watambue kuwa hawatoungwa mkono,” alisema Dk Bana.
Kuhusu kumwita kiongozi wa nchi dikteta, Dk Bana alihoji kama kitendo cha kutumbuliwa kwa majipu na mafisadi kimewaudhi au walitaka atumie sindano kubwa ama ndogo ili aweze kutimiza azma hiyo na wao waweze kufurahia.
Alisema Watanzania wameshaona mwanga wakitambua kuwa Rais Magufuli ndiye kiongozi wamtakaye na anaongoza serikali waitakayo na hivyo ni vigumu kuwaaminisha vinginevyo kama wanavyotaka kufanya Chadema.
Habari hii imeandikwa na Oscar Mbuza, Lucy Lyatuu na Katuma Masamba
Share:

Waziri Mkuu atoa saa 48 wafanyakazi 80 kutimuliwa



WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa saa 48 kwa Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kuwa amewaondoa kazini watumishi 89 wanaofanya kazi katika halmashauri hiyo kwa Mikataba.
Amewatahadharisha pia watendaji wa halmashauri zote nchini kutotumia fedha za miradi zinazopelekwa na serikali kinyume na malengo kutokana na kuimarishwa kwa mfumo wa ufuatiliaji wa matumizi yake na thamani ya miradi itakayojengwa.
Aliyasema hayo alipozungumza na watumishi na watendaji wa manispaa hiyo, huku akiweka bayana kwamba halmashauri hiyo inaongoza kwa kuwa na watumishi wa Mikataba, jambo ambalo ni kinyume cha taratibu za utumishi.
Akiendelea na mkutano huo, ghafla Waziri Mkuu alimsimamisha Kaimu Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Zaituni Hassan na kumuuliza idadi ya watumishi wa Mikataba katika halmashauri hiyo ambapo ofisa huyo alijibu kuwepo kwa watumishi 89.
Jibu hilo lilimfanya Waziri Mkuu kuhoji sababu ya kuwepo kwa idadi kubwa hiyo na kujibiwa kuwa hatua hiyo ilitokana na wengi wao kukosa sifa za kuajiriwa huku akisema wengi wao ni madereva.
Zaituni aliendelea kumwambia Waziri Mkuu kwamba mwaka jana Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilitangaza nafasi za kazi na kuwataka watumishi hao kuomba lakini walishindwa kufikia vigezo vilivyowekwa na kusababisha halmashauri kuendelea kuwatumia bila kuwaajiri.
Pamoja na maelezo hayo, Waziri Mkuu alieleza kushangazwa na hatua ya kutokuwepo kwa madereva waliohitimu Kidato cha Nne ambao wangeweza kuajiriwa, hata hivyo Ofisa Utumishi huyo alimwambia waliopo wana elimu ya Kidato cha Nne lakini hawana vyeti vya mafunzo ya udereva kutoka Chuo cha Elimu na Mafunzo Stadi (VETA).
Majaliwa alieleza kuwa wanaotakiwa kuajiriwa kwa Mikataba ni walimu wa Masomo ya Sayansi na watendaji wa mitaa hivyo kama madereva hao hawana sifa ni vyema wakaondolewa kwa vile wanaziba nafasi za watu wenye sifa za kuajiriwa.
Alisema kutokuajiriwa ni moja ya sababu za kuwepo watumishi hewa hivyo alisema hadi kufikia Julai 30, mwaka huu, Ofisa Utumishi huyo awe amejiridhisha kuhusiana na sifa za watumishi hao ili wasio na sifa waondolewe na wenye sifa waajiriwe huku akisema zoezi hilo lifanyike katika idara zote.
Alimtaka kuanza taratibu za kumuomba Katibu Mkuu wa Utumishi kibali cha kuwaajiri watumishi hao na kusema ametoa nafasi hiyo kwa kuwa watumishi wengi katika halmashauri hawana mwelekeo mzuri kutokana na kutoajiriwa, hivyo wasio na sifa waondoke ili watafutwe wenye nazo.
Akizungumzia fedha zinazopelekwa katika halmashauri, Waziri Mkuu alisema kila fedha inayoingia katika halmashauri itakuwa na maelekezo ya matumizi na Mkurugenzi atalazimika kutoa nakala ya maelezo hayo na kumpatia Mkuu wa Wilaya ili ajue matumizi ya kila shilingi na thamani ya miradi.
Alisema baada ya kumaliza uteuzi wa viongozi mbalimbali, sasa Serikali inaanza kupeleka fedha za maendeleo katika halmashauri zote ili utekelezaji wa shughuli za maendeleo uendelee.
Share:

Thursday 28 July 2016

Breaking news:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WA SPECIAL DIPLOMA UDOM-MSINGI WAMECHAGULIWA KWENDA VYUO MBALIMBALI VYA UALIMU JULY 28 2016

WANACHUO 1168 WA PROGRAMU YA STASHAHADA YA UALIMU WA E. YA MSINGI KUTOKA UDOM KWENDA VYUO VYA UALIMU 
Tokeo la picha la moe.go.tz 


Wanafunzi 1168 wa programu ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi, wenye ufaulu wa Daraja la II-III wamepangiwa kuendelea na masomo yao katika vyuo vya ualimu kwa gharama zao wenyewe. 

Share:

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis Aanguka Akiendesha Ibada Kanisani..Tazama Video Hapa



Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amepata ajali ya kuanguka ghafla alipokuwa akitembea kuelekea kwenye jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuendesha ibada, Czestochowa nchini Poland.
Papa Francis mwenye umri wa miaka 79 alisaidiwa kwa haraka na wasaidizi wake na kufanikiwa kuamka na kuendelea na safari hadi kwenye kiti kilichoandaliwa.

Papa Francis alikosa kukanyaga vyema kidato kimoja na akaanguka katika madhabahu matakatifu zaidi nchini humo, madhabahu ya Jasna Gora.

Papa, mwenye umri wa miaka 79, mzaliwa wa Argentina, alionekana akitembea akiwa anatafakari sana, na hakugundua kulikuwa na kidato kimoja kabla ya kufikia altare, shirika la habari la AP limeripoti.

Mapadre waliokuwa karibu naye walikimbia na kumsaidia kuinuka.

Misa iliendelea kama ilivyopangwa na papa alihubiri kwa muda mrefu mbele ya maelfu ya waumini waliokusanyika Jasna Gora katika jiji la Czestochowa, kusini mwa nchi hiyo.

Ibada hiyo ilikuwa ikirushwa moja kwa moja kupitia vituo mbalimbali vya runinga na kuangaliwa na mamilioni ya watu.

Shirika la habari la AFP linasema aliinuka upesi, na hakuonekana kuumia hata kidogo.

Alipoulizwa iwapo Francis aliumia baada ya kuanguka, msemaji wa Vatican Greg Burke ameambia wanahabari “papa yuko salama”.

Papa amewahi kuteleza na hata kuanguka mara kadha awali, na kila mara huwa anainuka peke yake au kusaidiwa na mmoja wa wasaidizi wake, shirika la AP linasema.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Papa Francis anasumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kama Sciatica, ugonjwa ambao wakati mwingine hushusha maumivu ya ghafla kwenye miguu kutoka mgongoni.
Angalia Video hapa

Share:

Rais Magufuli Atengua Uteuzi Wa Mwenyekiti Wa Bodi Ya Mfuko Wa Barabara


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) Dkt. James Munanka Wanyancha.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi iliyotolewa leo Mjini Dodoma imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo tarehe 28 Julai, 2016.
Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Joseph Odo Haule kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.
Uteuzi wa Bw. Joseph Odo Haule umeanza leo tarehe 28 Julai, 2016.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Joseph Odo Haule alikuwa Meneja wa Mfuko wa Barabara (Road Fund).
Wajumbe wengine wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wanaendelea katika nafasi zao.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
28 Julai, 2016
Share:

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO CHA MIPANGO DODOMA 2016/2017

Kindly view the link below and download selected candidates to join The Institute of Rural Development Planning (IRDP) – Dodoma Main Campus  for Certificate Courses 2016/2017
Selected candidates for Certificates Programmes (Certificate in Rural Develoment Planning & Certificate in Development Administration and Management) Academic year 2016/2017
Share:

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JULY TAREHE 28.7.2016


IMG_20160728_044116
IMG_20160728_044141
IMG_20160728_044159
IMG_20160728_044218
IMG_20160728_044241
IMG_20160728_044258
IMG_20160728_044320
IMG_20160728_044344
IMG_20160728_044403
IMG_20160728_044434
IMG_20160728_044458
IMG_20160728_044521
IMG_20160728_044538
IMG_20160728_044557
IMG_20160728_044719
IMG_20160728_044747
IMG_20160728_044811
IMG_20160728_044829
IMG_20160728_044853
IMG_20160728_044913
IMG_20160728_044949
IMG_20160728_045005
IMG_20160728_045031
IMG_20160728_045048
IMG_20160728_045253
IMG_20160728_045316
IMG_20160728_045343
IMG_20160728_045428
IMG_20160728_045459
IMG_20160728_045523
IMG_20160728_045553
IMG_20160728_045618
Share:

KOZI ZA SPECIAL DIPLOMA CHUO CHA UDOM ZIMEFUTWA RASMI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

 Logo
 Kozi mbalimbali zilizokuwa zikitolewa chuo kikuu cha udom miaka iliyopita zimefutwa .
Kozi hizo ni pamoja na special diploma programmes zilizokuwa zikitolewa UDOM,Kozi ambazo zimefutwa ni pamoja na zifuatazo,

Share:

HIZI HAPA KOZI ZA DIPLOMA & CHETI ZITOLEWAZO CHUO KIKUU CHA UDOM 2016/2017

Share:

UDOM:CALL FOR APPLICATIONS FOR ADMISSION INTO NON DEGREE (DIPLOMA AND CERTIFICATE) PROGRAMMES FOR ACADEMIC YEAR 2016/2017

Logo
Welcome to Online Application for Admission into Certificate and Diploma Programmes
UDOM invites applications from suitably qualified candidates for admission to the non-degree (Certificate and Diploma)
Programmes for academic year 2016/2017.
Programmes, entry requirements and how to apply are available on the following links:
All eligible applicants are highly encouraged to apply.
Share:

Wednesday 27 July 2016

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO CHA ST.FRANCIS IFAKARA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

TANGAZO KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO MWAKA WA MASOMO 2016/2017

WANAFUNZI WOTE WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CERTIFICATE), STASHAHADA (DIPLOMA) WANATAKIWA KUTHIBISHAKUCHAGULIWA KWAO KUPITIA BARUA PEPE YA CHUO (principal@sfuchas.ac.tz).
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger