Thursday, 10 April 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRILI 11,2025

Share:

UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA NEMC


Share:

JAMII IBADILI MITAZAMO UKATILI WA KIJINSIA : DKT. JINGU


Na WMJJWM- Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu ameitaka jamii kubadilika na kuachana na dhana ya kumdidimiza mtoto wa kike kwani dhana hiyo ni kikwazo cha maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Dkt. Jingu ameyabainisha hayo katika kikao kazi baina ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wizara za kisekta zinazoratibu Kupinga Ukatili wa kijinsia (GTAP)  na Umoja wa Ulaya  kilichofanyika jijini Dodoma Aprili 09, 2025.

Dkt. Jingu amewataka wadau hao kuongeza ufanisi na ufatiliaji wa programu hiyo ili kuweza kutimiza malengo yaliyodhamiriwa toka kuazishwa kwake ikiwemo kupunguza vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto, kwainua wanawake kiuchumi na kuhakikisha mabinti wanarudi shule.

“Tunaweza kujifunza mifano mizuri kutoka kwa  walioweza kudhibiti wanaokinzana na sheria  na taratibu za nchi hii  kwa kufuata nyanyo zao ili jamii iweze kutambua kuwa endapo mtu atakiuka  taratibu zilizopo atachukuliwa hatua stahiki  ikiwemo kifungo kwani majadiliano si suluhu ya kila kitu muda mwingine hatua kali ni muhimu “amesema Dkt Jingu.

Aidha Dkt. Jingu amepongeza hatua zilizofikiwa toka kuanzishwa kwa utekelezaji wa programu hiyo nchini ikiwemo kuongezeka  kwa idadi ya mabinti  walioweza  kurejea shuleni baada ya kukatishwa masomo, kuongezeka kwa nyumba salama kwa manusra wa ukatili lakini pia asilimia kubwa ha wanajamii kuamka na kuanza kuachana na vitendo vya ukatili.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Umoja wa Ulaya  Karina Dzialowska ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya katika kutengeneza mazingira salama na rafiki kwa mtoto wa kike kuweza kustawi na kuweza kufikia malengo yake.

“Tunatarajia hata baada ya programu hii kuisha Serikali itaendeleza kuweka juhudi na afua mbalimbali ili kuhakikisha wanawake wanaendelea kuwa salama  kwani bado kuna safari ndefu ya kuhakikisha watoto wa wanaondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia” amesema Dzialowska.

Utekelezaji wa Programu ya mabadiliko na Kupinga Ukatili  wa kijinsia (GTAP) iliyoanza mwaka 2022/2023 unatarajia kukamilika 2025/2026.

Share:

Wednesday, 9 April 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 10, 2025

Share:

NIMEBAINI SIRI NZITO KATI YA MKE WANGU NA BOSI WANGU!



Naitwa Salum kutokea Temeke, ni mume na baba watoto wa watatu, jamani nimeamua kuandika ujumbe huu baada ya Bosi wangu kuleta mambo ya ajabu sana, nayo ni kung'ang'ania kuzaa mtoto na mke wangu wa ndoa.

Hili ni suala ambalo lilighubikwa na usiri mzito ajabu, ila kwa uwezo wa Kiwanga Doctors ndipo nilipobaini mbinu hiyo chafu ya Bosi wangu, nakumbuka nafiki yangu mmoja alinipa namba ya mtaalamu huyo na kuniambia anaweza kumfunga mke wangu asiweze kutoka nje ya ndoa.

Nilifika ofisini kwa Kiwanga Doctors huko Migori nchini Kenya, alinipatia dawa na kuanza kuzitumia, niliendelea na shughuli zangu, wakati huo Bosi wangu alikuwa kila mara ananipa safari nyingi za kikazi ili apate muda wa kuendelea kumshawishi mke wangu.

Hata hivyo, mke wangu hakujua kama nimemfunga, wala Bosi wangu hakujua hilo, hivyo nilipokuwa napata safari za kikazi nilikuwa na amani tele na furaha zaidi hasa kutokana na kuongezeka ka fedha ambayo nilikuwa napatiwa kama posho ya kujikimu na safari.

Baada ya muda wa miezi kadhaa mke wangu aliniita chumbani na kuniambia Bosi wangu alikuwa akimtongoza na kumwambia anataka kuzaa naye kutokana anaona watoto wetu ni wazuri.

Mke wangu aliniambia kwa muda mrefu alifanya jambo hilo kuwa siri lakini anaona kadiri anavyofanya siri moyo wake unakosa amani kabisa.

Alilia sana na kuniomba msamaha kwa kutunza siri hiyo ya ajabu ambayo ingeweza kumfanya akazaa nje ya ndoa yetu ambayo imedumu kwa miaka nane sasa.

Hadi kufika hapo nikajua kabisa dawa ya Kiwanda Doctors kweli inafanya kazi yake ipasavyo. Kilichokuja kunishangaza ni yule Bosi wangu alikuja kufukuzwa kazi katika mazingira ambayo sikuwahi kuyaelewa hadi sasa na hapo ndoa yangu ikazidi kuwa na usalama zaidi.

Ni watu wengi hadi sasa wamepata uponyaji na furaha kupitia huduma za Kiwanga Doctors ambao unaweza kuwasiliana na kwa namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zao ambazo zimewasaidia wengi. 

Share:

MAONESHO YA MADINI MKOA WA LINDI KUFANYIKA JUNI 11 HADI 14, 2025


Na Regina Ndumbaro-Lindi.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainab Telack, ameongoza kikao cha kwanza cha maandalizi ya Maonesho ya Madini yaliyopangwa kufanyika kuanzia Juni 11 hadi 14, 2025 katika viwanja vya madini vilivyopo Ruangwa, mkoani Lindi. 

Maonesho hayo ni msimu wa pili kufanyika katika mkoa huo na yataambatana na mnada mkubwa wa madini. 

Kikao hicho kimefanyika Ruangwa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wawakilishi wa makampuni ya uchimbaji na uchenjuaji wa madini, wachimbaji wadogo, taasisi za Serikali na kifedha, pamoja na wadau wengine muhimu wa sekta ya madini.

Katika kikao hicho, Mhe. Telack amesema kuwa maonesho ya mwaka huu yatakuwa ya kipekee na tofauti na yale yaliyotangulia. 

Ametoa wito kwa kila mdau kushiriki kikamilifu kwa nafasi yake ili kufanikisha tukio hilo muhimu. 

Miongoni mwa waliokutana katika kikao hicho ni pamoja na wawakilishi wa Bodi ya Korosho, vyama vya ushirika kama Lindi Mwambao na RUNALI, ambao wote kwa pamoja wameonesha utayari wa kushiriki katika maandalizi na utekelezaji wa maonesho hayo.

Maonesho hayo yanatarajiwa kuwa jukwaa muhimu kwa ajili ya kutangaza fursa za madini zinazopatikana mkoani Lindi, kuimarisha usimamizi wa rasilimali hizo, na kuhamasisha uwekezaji endelevu. 

Lengo kuu ni kukuza uchumi wa wananchi wa Mkoa wa Lindi pamoja na Taifa kwa ujumla kwa kuhakikisha rasilimali za madini zinatumika kwa manufaa ya watu wote.

Mhe. Telack amesisitiza pia kuhusu umuhimu wa mnada mkubwa wa madini utakaoambatana na maonesho hayo, ambao utatoa nafasi kwa wachimbaji na wadau wa madini kuuza, kununua, na kuona vito mbalimbali vya thamani vinavyopatikana mkoani Lindi. 

Hii ni fursa muhimu kwa sekta ya madini kuonyesha thamani yake halisi na kuwavutia wawekezaji wapya ndani na nje ya nchi.

Share:

EVANCE KAMENGE ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA NKENGE UCHAGUZI MKUU 2025

Na Lydia Lugakila - Kagera

Evance Kamenge, Mkulima na mchumi kutoka Wilaya ya Missenyi, Mkoani Kagera, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Nkenge katika uchaguzi wa mwaka 2025. 

Hii ni hatua ya tatu kwake baada ya kushiriki katika uchaguzi wa mwaka 2015 na 2020 bila ya kufanikiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Manispaa ya Bukoba, Kamenge amethibitisha kwamba yuko tayari kuwasilisha ombi lake la ridhaa kwa wananchi wa Nkenge.

 "Niliwahi kugombea na sasa nataraji kugombea tena mwaka huu 2025," alisema Kamenge.

Kamenge ameeleza kuwa yeye ni sehemu ya mabadiliko na kwamba kuna umuhimu wa kuweka mikakati thabiti ya kuboresha hali ya maisha ya wananchi.

 "Mimi ni mkulima na ninaajiri watu, haya ninayoyasema yanatokana na hali halisi ya maisha ya familia yangu," amesema Kamenge.

Mwanasiasa huyo pia amesisitiza kwamba anapokusudia kugombea, anataka kuwa sehemu ya mapinduzi siyo mageuzi.

 Amesema kuwa ameona mambo mengi yanapaswa kubadilishwa ili kufikia maendeleo halisi huku akidai kutoridhishwa na hali ya maendeleo katika eneo hilo.

Aidha, Kamenge ameonesha kuwa ana imani kwamba viongozi wa sasa wanapaswa kutekeleza ahadi zao huku akiongeza kuwa anatazamia kuwaambia wananchi ukweli huo wakati atakapokuwa na afya njema.

Kamenge pia amegusia umuhimu wa viongizi kuwa waaminifu katika siasa, akitaja msemo ulioko kwenye kadi yake ya chama chake isemayo "Nitasema kweli daima, fitina kwangu ni mwiko." kauli ambayo imeonesh ya kukazia dhamira yake na kueleza haja ya kuwa na viongozi waaminifu na wanaojali maslahi ya wananchi.

Share:

Tuesday, 8 April 2025

WAZIRI DKT.GWAJIMA AAMSHA ARI YA WANAWAKE KUJIUNGA MAJUKWAA YA UWEZESHAJI WANAWAKE KICHUMI

•Apokea nakala 1000 za Mwongozo wa Uundaji na Uanzishwaji wa Majukwaa ya Uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi.

•Atambulisha Kamati ya Kitaifa ya kuratibu hamasa na elimu kwa Wanawake kujiunga na Majukwaa hayo.

Na WMJJWM- Dar es Salaam

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amewataka Wanawake kujiunga na Majukwaa ya Uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi Ili kuzifahamu fursa za kiuchumi zilipo nchini. 

Waziri Dkt. Gwajima ameyasema hayo Aprili 08, 2025 jijini Dar Es Salaam wakati akipokea nakala 1000 za Mwongozo wa Uundaji na Uanzishwaji wa Majukwaa ya Uwezeshaji wa Wanawake kiuchumi kutoka Benki ya Biashara Tanzania (TCB) na kuitambulisha 
Kamati ya Kitaifa ya kuratibu Hamasa na Elimu kwa Wanawake kujiunga na Majukwaa hayo.
 
Waziri Dkt. Gwajima amesema, lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona Wananchi wanazifahamu fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi likiwemo kundi la Wanawake.

Akizungumzia kwenye hafla hiyo, Waziri Dkt. Gwajima amesema, jukumu la Kamati hiyo ya kitaifa ni kuratibu Wadau wengine wote kushiriki kwenye zoezi hili endelevu la kuhamasisha na kutoa elimu kwa wanawake walio kwenye majukwaa ya uwezeshaji kiuchumi ili wafahamu faida za kujiunga kupitia Kampeni ya ‘Inuka-Imarika-Tusua Kiuchumi’.

“Natoa wito kwa  Wadau wote wa maendeleo kushirikiana na Kamati hii niliyoitambulisha rasmi leo Aprili 8, 2025 ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi mkubwa” amesema Dkt. Gwajima.

Ameongeza kwamba, Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa maendeleo imekuwa ikitekeleza jukumu la kuwawezesha Wanawake Kiuchumi ambapo, kutokana na uzoefu wa utekelezaji huo ilifanya mapitio ya Mwongozo wa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wa mwaka, 2022 na kutoa toleo la mwaka 2024 linaloendana na mahitaji ya sasa. 

Aidha Waziri Dkt. Gwajima ameishukuru Benki ya Biashara Tanzania kwa utayari wa kuchapisha nakala elfu moja (1000) za Mwongozo huo ambao usambazaji wake utaanza  rasmi  sambamba na kampeni ya hamasa na elimu na kufika ngazi zote hadi kata, vijiji na mitaa. 

"Nakala hizi zitasaidia ni nyezo muhimu katika uhamasihaji wa wanawake kujiunga katika majukwaa ya uwezeshaji kiuchumi" amesema Waziri Dkt. Gwajima

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia Badru Abdulnoor amesema, Wizara itaendelea kushirikiana na Wadau katika kuhakikisha Sera na Mipango ya Serikali kuhusu uwezeshaji Wanawake kiuchumi inatekelezwa. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) Adam Mihayo amesema, Benki hiyo imefanya maboresho katika afua zake za kuhakikisha inaendeleza juhudi  za Serikali katika kuwawezesha Wanawake kiuchumi na kwa mwaka 2024 Benki hiyo ilitoa shillingi bilioni 300 kuwawezesha Wanawake kiuchumi.

Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imedhamini uchapishaji wa Mwongozo wa Majukwa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi nakala 1,000 ili kuweza kutoa Elimu juu ya utekelezaji wa majukumu hayo nchini.

Share:

DAWA YA WANAUME WANAOKATAA MIMBA NA KUTELEKEZA WATOTO

Jina langu ni Wit kutokea Morogoro, kwa sasa ni mama wa familia nikiwa na watoto wawili lakini huyu wa kwanza nilimzaa kabla sijaolewa ila naishi naye na mume wangu hana shida yoyote. 

Hapo awali mimi nilizalishwa mtoto wa kwanza lakini mwanaume tangia mimba hakuwahi kunihudumia kitu chochote kile na hadi leo sijui yupo wapi mbaka mtoto ana miaka mitano na shule ameanza. 

Jambo hilo lilinipa hasira sana na kusema hata akija kumuona sitoongea naye, nitakuwa bubu tu maana haina maana unampa mwanamke ujauzito halafu unatokomea huko kusiko julikana bila kujali kiumbe chako. 

Jamani nilikaa nyumbani hadi nafikisha miaka 30, wazazi walinipambania sana pamoja na mwanangu mpaka akawa mkubwa. Lakini nikajikuta nimebeba mimba ya mwanaume mwingine. 

Nakawaza mama akijua anaweza kunifukuza, sasa nikawa nafikiria jamani wapi nitaenda?, ndipo nikakimbilia kwa Kiwanga Doctors ambaye alinifanyia dawa (get back your ex lover) ambayo ilinisaidia kumrudisha mtu huyu wa pili kwangu. 

Ni kama naye alitaka kunitelekeza nikiwa na hii mimba lakini kwa dawa hizo alirejea kwangu na kuja nyumbani kujitambulisha na kunioa. 

Baada ya kujifungua, niliweza kumchukua yule mtoto wangu kutoka kwa wazazi wangu na sasa anaishi naye. Ikiwa unapitia kitu kama hicho, ninakushauri kuwa fika au wasiliana na Kiwanga Doctors. 

Tiba zao zinafanya kazi haraka na wanaweza kukusaidia katika changamoto mbalimbali za kimaisha, kuanzia masuala ya uhusiano hadi matatizo ya kiafya kama kuchelewa kupata mtoto na mengine mengi. 

Hadi sasa wengine wengi wamepata uponyaji na furaha kupitia huduma zao. Basi wasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba +254 116469840 au tembelea tovuti yao.  

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger