Thursday, 5 December 2024
SERIKALI YASISITIZA KUIMARISHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KWA MAENDELEO YA UCHUMI WA TANZANIA
FDH YAIPONGEZA UNEP KUENDELEZA AGENDA YA MAZINGIRA KWA WENYE ULEMAVU
Na Dotto Kwilasa,DODOMA
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya kusaidia watu wenye ulemavu ya mkoani Dodoma ya Foundation For Disabilities Hope, Maiko Salali amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP kwa jitiada zake za kupaisha agenda ya ulinzi wa mazingira kwa watu wenye Ulbino nchini.
Salali, alisema kupitia ushirikano wa shirika hilo la UNEP na FDH wameweza kusukuma Mpango kazi wa kitaifa wa haki na ustawi watu wenye ulbino ambapo serikali ilisikiliza na kufanyia kazi maombi hayo na hatimaye mpango huo kuzinduliwa Disemba 03, 2024 katika siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu duniani.
“Kwa hapa Tanzania tuliazimisha katika ukumbi wa Dimond Jubilee Dar es salaam, FDH inaishukuru sana UNEP kwa jitiada hizi ambazo zimewezesha watu wenye ulbino nchini kupata mpango na nimatumaini yetu kuwa tunaendelea kushirikiana ili kuendelea kuhakikisha agenda ya mazingira na ulinzi wa mazingira kwa watu wenye ulemavu unakuwa kipaumbele muhimu
SERIKALI YA AHIDI KUWEKEZA KATIKA SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Wednesday, 4 December 2024
TEKNOLOJIA YA UHANDISI JENI (GMO) NI MKOMBOZI WA KUKUZA UCHUMI AFRIKA
Na Hellen Kwavava - Dar es Salaam
Imeelezwa kuwa Teknolojia ya Uhandisi jeni ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi,kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Sambamba na kupunguza kasi ya uzalishaji ya uzalishaji wa gesi joto afrika na duniani kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Profesa Pius Yanda kutoka Taasisi ya usimamizi wa maliasili,mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchi iliyopo Chuo kikuu cha Dara es salaam (UDSM) Katika Kongamano na maonyesho ya tisa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere(JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Profesa Yanda amesema katika mada yake kuhusu mchango wa sayansi, teknolojia na ubunifu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi aliweza kuelezea kuwa teknolojia hiyo ya Uhandisi Jes(GMO)imeanza kutumika kwa kiasi kidogo kutokana na kutokuwa na teknolojia ya kutosha kuweza kutumia.
"Uhandisi jeni unatumika kwenye maeneo mengi ikiwemo elimu, afya, kilimo na maeneo mengine hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha kuna ubunifu wa ziada kutumia teknolojia hii kwa kiasi kikubwa," amesema.
Aidha amesema kuwa ushirikiano na nchi zilizoendelea hususan katika utafiti, unaweza kuwa na ubunifu bora zaidi wa kukuza matumizi ya teknolojia hiyo kwa maendeleo ya Tanzania.
Amesema ubunifu wa ziada unahitajika ili kutumia rasilimali zilizopo kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
"Mabadiliko ya tabia nchi yanatuathiri zaidi Afrika na Tanzania hivyo, suala la kutumia bayoteknolojia kwa ajili ya kutengeneza uchumi, ni vema kuboresha ikolojia kwa kuboresha maisha ya watu, kipato na kuchangia uchumi wa nchi,"amesema Yanda .
Kuhusu matumizi ya nishati safi, Profesa Yanda amesema Tanzania itakuwa mstari wa mbele katika matumizi ya nishati hiyo kwa kuhakikisha jamii inayoishi vijijini waweze kushiriki katika mkakati huo.
“Utashi wa kisiasa unaoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan unaibeba Tanzania kuwa mstari wa mbele katika kuongeza matumizi ya nishati safi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi",amesema
Uhandisi Jeni ni teknolojia inayotumia michakato ya Kibaolojia kuzalisha mbegu za Mazao na Mimea na ina sifa ya kukinzana na magonjwa,kustahimili ukame na kupambana na wadudu waharibifu wa Mazao.