Saturday, 25 April 2020

DOWNLOAD - PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ...TUKUTUMIE HABARI ZOTE BURE KWENYE SIMU YAKO

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.


Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa
Share:

Video Mpya :NG'WANA ISHUDU - CORONA



Msanii wa Nyimbo za asili Ng'wana Ishudu kutoka Shinyanga anakualika kutazama video ya wimbo wake mpya unaitwa Corona...Tazama hapa chini


Share:

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO


Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.


FULL POWER

⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.

⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50

⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4

⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.

Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama

Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

MAREKANI YAENDELEA KUONGOZA DUNIANI KWA IDADI KUBWA YA VIFO VYA CORONA


Marekani imeendelea kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na corona Duniani ambapo hadi muda huu wamefariki Watu 52,217.

Marekani pia inaongoza  kwa visa, vimefikia 925,758  na wamepona 110,432.


Wakati huo huo Ofisi ya Bajeti ya Congress ya Marekani imetoa ripoti ikionyesha kuongezeka kwa asilimia 14 ya ukosefu wa kazi nchini humo.

Ofisi hiyo imesema kwamba ongezeko hilo la uhaba wa ajira limeripotiwa katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu wa 2020.

Hii ni katika hali ambayo mamilioni ya Wamarekani wamepoteza ajira  au wanakadiriwa kupoteza nafasi hizo za kazi katika miezi michache ijayo.

Alhamisi iliyopita, Wizara ya Kazi ya Marekani ilitoa ripoti yake ya kila wiki ikisema kuwa tayari watu milioni 26 wamepoteza nafasi zao za kazi katika kipindi cha wiki tano zilizopita kutokana na kuenea kwa kasi nchini humo virusi hatari vya corona.


Kuenea virusi hivyo katika pembe zote za nchi hiyo kumepelekea viwanda na vituo vingine vya uzalishaji ajira kufungwa na hivyo kuifanya nchi hiyo ikabiliwe na mgogoro mkubwa wa kiuchumi.


Share:

KIJANA ALIYEVUA NGUO ASAKWA NA POLISI KWA KUMUUA BIBI YAKE KWA KUMKATA SHINGO KISHA KUONDOKA NA KICHWA


Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linafanya msako mkali kumtafuta HAKIMU JAMES MWAKIFUNA miaka [20] Mnyakusa wa Kiwira kwa kosa la Mauaji ya maksudi ya bibi JUNE SANKANYE miaka [65] wa kijiji cha Nkunga Kata ya Nkunga  {T} Ukukwe.

Tukio hili lilitokea tarehe 23/04/2020 saa 05:00 Wilaya ya Rungwe.  Marehemu ambaye ni bibi mzaa baba wa mtuhumiwa walilala nyumba moja.  Huku mtuhumiwa akiwa sebuleni na marehemu amelala chumbani.  

Usiku muda usiojulikana HAKIMU JAMES MWAKIFUNA alichukua kitu chenye ncha kali na kumkata bibi shingo na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili na kisha kuondoka na kichwa cha JUNE SANKANE.

Mnamo tarehe 18/04/2020 mtuhumiwa HAKIMU J. MWAKIFUNA alianza kuvua nguo na kutembea na Panga huku akitaka kuua baadhi ya ndugu zake aliokuwa akiishi nao Kiwira kwa bibi mzaa mamaye – MONICA BUKUKU.  Kufuatia hali hiyo tarehe 21/04/2020 alifukuzwa na kwenda kwa marehemu ambaye ni bibi yake mzaa baba yake.

Baada ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa alitoboa ukuta wa nyumba ya marehemu na kuondoka na kichwa kwenda kusikojulikana.

Jeshi la Polisi linatoa rai ni tukio baya sana kutokea mkoani kwetu na kuwasihi wananchi na viongozi wote wa wananchi popote akionekana mtu mwenye dalili za upungufu wa akili apelekwe hospitali kupata matibabu.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA


Share:

MIKOA YA KANDA YA ZIWA YAKUBWA NA TETEMEKO LA ARDHI


Tetemeko la ardhi limetokea katika  Ukanda wa Ziwa Victoria na kuyakumba maeneo ya mikoa ambayo ni jirani na  Ziwa hilo  ikiwemo eneo la mpaka wa  Geita na Shinyanga.

Mjolojia Mwandamizi kutoka taasisi ya Jiolojia Bwana Gabriel Mbogoni amesema Tetemeko hilo lina ukubwa wa 4.6 katika Vipimo vya Richta.

Bwana Mbogoni amesema Tanzania imepitiwa na mkondo wa bonde la ufa la Afrika Mashariki ikiwa na mikondo miwili mkondo wa Mashariki na mkondo wa Magharibi hivyo matukio ya  mateteko ya ardhi kwenye mkondo wa bonde la ufa ni  lazima yotokee na kuwataka watanzania muda wote wawe kwenye hali ya tahadhari.

Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita Mponjoli Lotson amethibitisha kutokea kwa tetemeko katika mkoa wake ambaye amesema Tetemeko hilo limepiga hadi Chato lakini hata hivyo haijasaabisha Madhara.

Mkoani Shinyanga hasa katika Wilaya ya Kahama ambayo inapakana na mkoa wa Geita kupitia kwa Mkuu wa  wilaya hiyo Bw. Anna Mringi Macha amethibitisha kutokea kwatuki hilo huku akieleza kuwa pia halijaleta madhara.

Credit:ITV


Share:

ASIMULIA JINSI ALIVYOKAMATWA BAADA YA 'KUPOST FACEBOOK' KUWA ANA MAAMBUKIZI YA CORONA

Michael Lane Brandin aliambiwa kwamba ujumbe wake aliotuma kwenye mtandao wa Facebook utasababisha hisia tofauti.

Kile ambacho hakufahamu ni kwamba atakamatwa, atapoteza kazi na kushtakiwa kwa makosa ambayo huenda yakamfanya akajipata kizimbani.

Ilikuwa ni majira ya mchana mwezi Machi na mjadala kuhusu namna ya kukabiliana na Covid-19 ulipokuwa unaendelea kila mahali.

Hivyo yeye, akaamua kushiriki mjadala huo kwa kuandika.

Michael alituma ujumbe unaosema kwamba yeye amepatikana na virusi vya corona na madaktari walikuwa wamemuambia kuwa virusi hivyo vinaweza kusambazwa kwa njia ya hewa.

Kupitia mtandao wa Facebook, alichokutana nacho hakuamini, kuhurumiwa na mshtuko. Rafiki zangu walimtumia ujumbe kumuuliza kama yuko sawa, na akasema yuko sawa, katika ujumbe wake alikuwa anatania tu,' anasema.

Kipi kilikuwa kinaendelea kando na mtandao hangewahi kukifikiria.

Uvumi tayari ulikuwa umeanza kusambaa kama moto wa msituni katika kaunti yote ya Tyler. Kulingana na polisi katika mji wa Texas, tayari watu walikuwa wameanza kuwa na wasiwasi.

Huo ni wakati ambapo hakuna nchi yoyote ambayo ilikuwa imetoa amri ya kutotoka nje kwa raia wake na pia walikuwa wanapiga simu hospitali uuliza ikiwa taarifa hizo zilikuwa za kweli na kile ambacho wanaweza kufanya kujilinda.
Kibali cha kukamatwa

Polisi ikawasiliana na Michael na kumwambia kwamba arejee kwenye ujumbe wake wa Facebook na kuandika tena kwamba alichokisema hakikikuwa cha kweli na akafanya hivyo.

Hatahivyo, uvumi huo ulikuwa unaendelea kusambaa na ujumbe mwingine katika ukurasa wa Facebook ukawa unatoka kwenye akaunti ya Tyler ofisi ya Sheriff:

'Katika lalamiko rasmi kutoka idara ya makosa ya jinai, hakimu Jacques Blanchett alitoa kibali cha kukamatwa kwa Brandin kwa makosa ya kuzua taharuki kwa taarifa za uwongo.

Brandin akajipeleka kwa mamlaka.

'Nilijipeleka mwenyewe na baada ya mchakato wa kujiandikisha kukamilika, wakasema kwamba usiko huo nitalala jela kwasababu ni lazima nimsubiri hakimu siku itakayofuata.

Nilikuwa na wasiwasi kupita maelezo,' Brandin anasema.

Kwasasa amerejea nyumbani akisubiri siku ya kesi yake kusikizwa ambayo hadi kufikia sasa haijulikani kwasababu ya kusambaa kwa virusi vya coona lakini licha ya kwamba hali ilivyo kwa Brandin bado ni tete, anasema kwamba bado anahisia mchanganyiko kuhusu ikiwa anajutia kile alichofanya au la.Michael Lane Brandin

'Nina shahada ya uanahabari na nimesomea nyanja hiyo kuonesha vile ilivyo rahisi kwa yeote yule kutuma ujumbe mtandaoni na kusababisha wasiwasi.

Pia nilitaka kudhihirisha kwamba ni muhimu kwa watu kuelimika na kufanya utafiti wao kabla ya kukubali kwamba kila wanachokisoma mtandaoni ni cha kweli.

Lakini kwa ujumbe nilioandika Facebook, nimepoteza kazi, mafao yangu ya afya, na pia sikuweza kuanza shahada yangu ya uzamili kwa wakati niliokuwa nimepanga kwa ukosefu wa pesa na hilo limeniongezea mzigo wa kifedha kwa familia yangu kwasababu wote wananisaidia kulipa gharama zangu.

'Licha ya kwamba najutia, nililazimika kuandika barua ya kuacha kazi na kulala jela kwa usku mmoja na pia ama naweza kuambiwa nilipe faini au hata kuhukumiwa kifungo jela. Hayo sio mambo mazuri.'

Katika ofisi ya umma, wamesema wamelazimika kuchukua hatua hiyo kwasababu ya wasiwasi uliokuwa unaendelea kuhusu virusi vya corona Marekani

Marekani sio eneo pekee ambapo ambapo sheria mpya inamaanisha kusambaza taarifa kwa mitandao ya kijamii kuhusu virusi hivyo kunaweza kukufanya ukakamatwa.

Watu waliokamatwa kote duniani

Waliokamatwa kwa kusambaza taarifa za uongo ni taarifa zinazoripotiwa India, Morocco, Thailand, Kenya, Tanzania Cambodia, Somalia, Ethiopia, Singapore, Botswana, Russia na Afrika Kusini.

Katika baadhi ya matukio, uvumi unaweza kusambaa ukiwa na nia njema lakini waangalizi wa haki za Binadamu wametuambia wamesema kwamba wana wasiwasi kuwa janga hili limefanya mafia kuwa na nguvu mno kiasi cha kukandamiza wale wanaowakosoa.
Via BBC Swahili
Share:

IGP Sirro: Wanaotumia Mitandao ya Kijamii Kupotosha Kuhusu Corona Wachukuliwe Hatua Kali za Kisheria

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro   ameagiza kuchukuliwa  hatua kali za kisheria baadhi ya watu wanaotumia mitandao kwa nia yao ovu ya kupotosha kuhusu ugonjwa wa Corona

“Watu wa mitandao ni sumu sana…hasa wanapoitumia vibaya…maelekezo kwa makamanda hawa ni kuhakikisha kwamba akijitokeza mtu mmoja au kikundi cha watu wakafanya haya wanayoyafanya kwa ajili ya kuwaletea watanzania hofu…tuwashughulikie vizuri sana…” - Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro.

==>>Msikilize hapo chini


Share:

IGP SIRRO: Wale ambao wamefungiwa…wasitafute ugomvi na Watanzania

“Mkubwa wako wa nchi akishasema umekuwa ‘lockdown’ kwenye nchi yako…ustaarabu…ukae kwako…! mambo yakiwa mazuri si tutatembeleana..!

...wale ambao wamefungiwa wasitafute ugomvi na Watanzania…,” - IGP Sirro.

==>>Msikilize hapo chini


Share:

Wizara Ya Kilimo Kushirikiana Na Sua Kuzalisha Mbegu Bora Za Mazao

Wizara ya Kilimo imekubaliana na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine kuanza kuzalisha mbegu bora za mazao ya kilimo ili kujitosheleza na mahitaji ya wakulima nchini.
 
Makubaliano hayo yamebainishwa jana (24.04.2020) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya alipokutana kwa mazungumzo na Menejimenti ya Chuo hicho mjini Morogoro na kueleza kuwa nchi bado haijajitosheleza na mbegu bora.
 
“Tunahitaji ushirikiano wa kuzalisha mbegu bora za mazao ya kilimo kwa wingi ndani ya nchi ili kukidhi mahitaji ya wakulima ” alisisitiza Katibu Mkuu
 
 Wizara ya Kilimo inapenda chuo Kikuu cha Sokoine  kianzishe vitalu vya uzalishaji mbegu bora za mazao ya mboga mboga na matunda ili kupunguza utegemezi toka nje ya nchi.
 
“Ifike hatua nchi yetu kuwa na uhakika wa mbegu bora na hai.Hii itaongeza ajira kwa vijana na wakulima kupata manufaa” alisema Katibu Mkuu Kusaya
 
Kusaya alitaja maeneo mengine ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Sokoine kuwa ni  kuanzisha maabara bora ya kilimo ili kusaidia mapinduzi katika utafiti,uanzishwaji wa mashamba darasa kwa wahitimu wa masomo ya kilimo na kujenga maabara ya kisasa ya kupima ubora wa mazao yakiwemo mboga mboga na matunda kabla ya kusafirisha nje ya nchi ili kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo.
 
Pia uhamasishaji matumizi ya teknolojia ya bora ya uzalishaji kwa kutumia zana za kisasa na utoaji huduma za ugani na mafunzo ya muda mfupi kwa wataalam wa wizara  na wakulima kwa kutumia vyombo vya habari na TEHAMA
 
Ili kuwa na kilimo chenye tija na manufaa kwa mkulima ,Katibu Mkuu Kusaya amekiomba chuo cha Sokoine kusaidia jitihada za wizara kudhibiti visumbufu vya mimea na mazao kama viwavijeshi,ndege waharibifu wa kwerea kwerea,nzige wa jangwani,panya na magugu yanayoathiri mazao ya wakulima. 
 
“Tunahitaji sifa nzuri ya ubora wa mafunzo na wataalam wa  chuo kikuu cha Sokoine iendelee na kuwanufaisha wakulima kuongeza tija na uzalishaji  kwa kudhibiti visumbufu vya mazao yake. “ alisema Kusaya
 
Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya kilimo kuwa uzalishaji wa ndani wa mbegu bora umefikia tani 61,703 mwaka 2019
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine Prof,Raphael Chibunda alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kutembelea chuo hicho na kuwa wapo tayari kuanzisha mafunzo maalum ya muda mfupi kwa ajili ya kufundisha wataalam waliopo kazini na wale wanaopenda kujifunza kilimo cha kisasa.
 
Prof.Chibunda alisema SUA itaendeleza ushirikiano na Wizara ya Kilimo kupitia taasisi za utafiti wa Kilimo (TARI) na kampuni ya mbegu nchini (ASA) na Taasisi ya Udhibiti wa Mbegu Tanzaia (TOSCI) kuzalisha mbegu bora za mazao  kwa kutumia teknolojia na wataalam waliopo nchini.
 
“SUA ina msitu wa wataalam hivyo tunaahidi tutashirikiana na wizara ya kilimo kufanya tafiti za mbegu bora na pia kuzalisha mbegu hizo kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi. ” alisitiza Prof.Chibunda
 
Aliongeza kusema kina mkakati wa kuanzisha digrii maalum itakayosaidia kuzalisha wataalam wabobezi kwenye usimamizi wa sekta ya ushirika na kilimo nchini ili kuunga mkono jitahada za serikali kuwa na ushirika imara.
 
Katika hatua nyingine Prof.Chibunda aliomba Serikali iweke utaratibu wa kuratibu waduka ya pembejeo ili yawe na wataalam waliosomea kilimo na mifugo kwa ajili ya kutoa huduma za ushauri kwa wakulima.
 
Katibu Mkuu huyo wa wizara ya Kilimo alisema lengo la wizara yake ni kuhakikisha kunakuwepo sera nzuri na mazingira wezeshi ya kufanya kilimo kuwa ajira, uchumi na biashara kwa watanzania walio wengi.
 
Mwisho
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
MOROGORO








Share:

MBUNGE WA ZAMANI WA JIMBO LA PERAMIHO AFARIKI DUNIA


Na Magnus Mahenge, Dodoma
Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma, Dk Damas Mbogoro amefariki dunia katika hospitali ya Peramiho alikokuwa akihudumiwa.

Taarifa ya Spika Job Ndugai iliyosomwa bungeni na Naibu Spika wa Bunge, Dk Ackson Tulia ilisema mbunge huyo wa zamani amefariki jana katika hospitali hiyo. Dk Tulia alisema hayati Dk Mbogoro alikuwa Mbunge wa Peramiho kwa miaka 10 kati ya mwaka 1980-1995 baada ya kumaliza kipindi hicho alichukua jimbo hilo Prof Simon Mbilinyi na sasa lipo chini ya Jenista Mhagama.

Dk Mbogoro pia amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, pia amewahi kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku nchini. Dk Mbogoro ambaye kitaaluma ni mchumi pia amewahi kuwa Kimishna wa Mipango na Kamishna wa Sensa nchini.

Pia aliwahi kuwa Mwanzilishi wa Taasisi ya Wirima Community ambayo ndiyo chimbuko la Sekondari ya Wirima iliyopo katika eneo la Wino jimboni Peramiho. Baada ya kustaafu, Dk Ndumbaro alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) tawi la Songea.

Hayati Dk Ndumbaro atazikwa leo katika kijiji cha Wino katika Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.
Share:

THTU YATOA MAPENDEKEZO KADHAA YA KUKABILIANA NA ATHARI ZITOKANAZO NA JANGA LA CORONA


Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania(THTU) Dkt.Paul Loisulie (kushoto) akizungumza wakati akitoa taarifa yake kwa wanachama wake, wadau na umma wa watanzania wote nchini ikiwa ni sehemu ya kuungana na serikali katika kupigana vita dhidi ya Corona.
............................................................................................
“Ni Wajibu wa Kila Mmoja Wetu: Jilinde na Mlinde mwenzako, Timiza wajibu wako kwa,
pamoja tutazuia corona”
  1. Utangulizi
Ugonjwa wa corona (Covid 19) umeleta athari kubwa duniani katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii na kisiasa. Pia umeharibu utaratibu na mfumo mzima wa maisha ya kawaida katika nchi zote na kusababisha maelfu ya vifo duniani. 

Serikali na Wataalamu wa afya wameelekeza njia mbalimbali za kujikinga na kuepuka ugonjwa huu ambao mpaka sasa hauna tiba. 

Njia hizo ni pamoja kuepuka mikusanyiko, kutumia vitakasa
mikono, kunawa mikono kwa kutumia sabuni na maji tiririka, kutosafiri au kwenda sehemu yoyote yenye watu wengi isipokuwa kwa mahitaji ya muhimu, na kuwekwa
karantini kwa wale wote wanaohisiwa kuwa na virusi vinavyosababisha ugonjwa huo. 

Serikali ya Tanzania, kama zilivyo serikali nyingi duniani, imechukua hatua mbalimbali za kudhibiti njia za maambukizi ya ugonjwa huu zikiwemo zuio/katazo la shughuli nyingi zenye mikusanyiko mikubwa kama vile michezo, matamasha, makongamano na aina
nyinginezo zinazofanana na hizo.

 Pia shule zote za awali, msingi na sekondari pamoja
na vyuo ngazi zote zimefungwa kwa muda usiojulikana.

THTU inapongeza hatua zote za kiafya ambazo zimechukuliwa na serikali na wataalamu mbalimbali wa afya mpaka sasa na pia tunaunga mkono michango
mbalimbali ya mawazo ya kitaalamu inayotolewa na taasisi mbalimbali au mtu mmoja mmoja katika kukabiliana na janga hili.


 Hivyo basi, kwa kuzingatia hali hii inayoendelea
duniani kote na ndani ya nchi yetu, sisi THTU kwa kutumia kauli mbiu yetu ya “Nia na
1
Mwelekeo ni Kujenga Daima, Taifa Kwanza” tumeamua kutoa mchango wa maoni yetu
ya namna ya kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa corona pamoja na
ushauri wa namna ya kukabiliana na athari zilizojitokeza na zitakazojitokeza.
  1. Namna ya kuendeleza Mapambano dhidi ya corona;
  1. Kwa kuzingatia ukubwa wa nchi yetu na uelewa wa kila mwananchi mmoja
mmoja kuhusiana na ugonjwa huu, tunashauri kuongezwa kwa kampeni na
hamasa kubwa kwa mtu mmoja mmoja maeneo yote nchi nzima ili kuongeza
uelewa na umakini katika kudhibiti corona.
  1. Kuimarisha dhana ya serikali shirikishi kwa ngazi zote za Tawala za mikoa
(Mikoa na Wilaya) na serikali za mitaa (Halmashauri za Majiji, Manispaa, Wilaya,
mamlaka ya miji, kata na Vjiji/Mtaa) ili kuwezesha wananchi kuchukua hatua
stahiki za kujikinga na ugonjwa huu na pia kutoa taarifa pale wanapoona kuna
wananchi wenye dalili za ugonjwa huu.
  1. Viongozi wa dini zote wachukue hatua madhubuti ya kuwalinda waamini wao
kwa kutafuta njia mbadala ya kufanya shughuli za kiimani isiyohusisha
mikusanyiko. Ikiwezekana hatua zilizochukuliwa na Maaskofu wawili wa Mkoa
wa Kagera (Mhashamu Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la
Rulenge – Ngara na Mhashamu Askofu Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya
Karagwe) zifanyiwe kazi na viongozi wengine wa dini zote ili kuendeleza
mapambano dhidi ya corona. Sisi THTU tunaamini kuwa pamoja na maombi kwa
Mwenyezi Mungu kupitia Imani zetu za kidini, bado jitihada za kisayansi lazima
zichukuliwe na kila mmoja wetu.
  1. Katika kipindi hiki, tunapendekeza taasisi mbalimbali za serikali na zile za binafsi
kuruhusu baadhi ya wafanyakazi wao kufanya kazi kwa kutokea nyumbani ili
kupunguza mikusanyiko ya wafanyakazi maeneo ya kazi na kubaki na
wafanyakazi wachache sana ambao ni muhimu kuwepo ofisini ili kuendelea
kulinda utendaji wa taasisi hizo. Mfano, maeneo ya Vyuo Vikuu, vyuo vya kati na
shule, katika kipindi hiki ambacho wanafunzi hawapo, baadhi ya wafanyakazi
2
wangebaki nyumbani na kutumia mtandao wa intaneti kuwasiliana kwa shughuli
mbalimbali za kiofisi.
  1. Kwa siku za hivi karibuni, taarifa za serikali zimeonyesha kuwa maambukizi
yanaongezeka yakiambatana na vifo. Hivyo basi ni ushauri wetu kuwa hatua za
kupiga marufuku shughuli zote zinazohusisha mikusanyiko ya watu ziendelee
kuimarishwa kwani ushauri wa kitaalamu unaonyesha mikusanyiko ni njia moja
kuu inayosababisha kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa huu.
  1. Katika nyakati hizi ambazo kila mwananchi yuko katika jitihada za kulinda afya
yake na wale walioko karibu yake na kwa kuzingatia umuhimu wa huduma za
kiafya kwa kila mmoja wetu, tunashauri kuwa Taasisi mbalimbali ziepuke kutoa
taarifa au kufanya maamuzi yanayoleta au kuongeza msongo wa mawazo kwa
watu hasa katika nyakati hizi za janga la corona. THTU kwa masikitiko makubwa,
imeshtushwa na hatua zilizochukuliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) kupitia taarifa yao ya tarehe 14/04/2020 kuhusu wanufaika wa huduma za
bima ya afya ambao ni watoto wenye umri wa miaka 18 na kuendelea. Kwa
maoni yetu, taarifa hii imeleta usumbufu mkubwa kwa wanufaika wa bima ya
afya wakiwemo wanachama wa THTU ambao ni wachangiaji katika mfuko huo.
  1. Tunashauri kuwa ni vema Mfuko wa Bima ya Afya ukaonesha uungwana kwa
kusitisha uamuzi wao huo kama njia ya kuunga juhudi za kupambana na janga la
corona kwa kuwapa uhakika wanachama wake kuweza kupata huduma za afya
kwa wategemezi wao hao na hali ya nchi ikitengamaa wakae na wadau ili kujadili
namna njema ya kufanya mabadiliko hayo. Kila mmoja anaelewa mfumo wetu
wa afya ulivyo na namna ambavyo wananchi wengi wanaoishi na wategemezi
wao wanavyotegemea huduma za afya zilizopo. Kufanya maamuzi hayo katika
kipindi hiki ni kuwaongezea wanachama wa Mfuko huo msongo wa mawazo na
mzigo mkubwa wa kiuchumi katika nyakati ambazo hali ya kiuchumi ni mbaya
kutokana na athari za ugonjwa huu wa corona.
3
  1. Utengenezaji wa vitakasa mikono (hand sanitizers), barakoa na vifaa vingine
usimamiwe na mamlaka zinazohusika ili zikidhi vigezo vinavyotakiwa lakini pia
ziuzwe kwa bei ambayo watu wote wanamudu. Wafanyabiashara wasio
waaminifu wanaweza wakatumia mwanya huu kujinufaisha bila kujali uhai wa
watu.
  1. Mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu (LATRA) ikishirikiana na Jeshi la
Polisi kitengo cha usalama barabarani iongeze usimamizi wa maelekezo ya
wataalamu wa afya katika usafiri wa umma kipindi hiki cha hili janga.
Ikiwezekana kwa sasa jitihada kubwa zielekezwe kwenye usimamizi wa
maelekezo hayo ili kusaidia kupunguza maambukizi.
  1. Vyombo vya habari kwa ujumla wake (redio, televisheni na magazeti) pamoja na
mitandao ya kijamii vimefanya kazi nzuri mpaka sasa. Lakini tunashauri kuwa
ubunifu zaidi wa vipindi na makala ya kusaidia mapambano dhidi ya corona
uongezwe kwa kuongeza matanagzo yenye elimu ya kujikinga na ugonjwa wa
corona katikati ya vipindi vinavyopendwa na watu wengi. Utoaji wa taarifa sahihi
ni muhimu sana katika kipindi hiki. Vyombo vya habari vina nafasi ya pekee
kabisa katika hili.
  1. Ushauri wa namna ya kukabiliana na athari zinazotokana na janga la corona:
Pamoja na jitihada za kudhibiti na kutokomeza gonjwa hili la corona, ni ukweli
usiopingika kwamba tayari athari zimeshaonekana na nyingine zitaonekana siku zijazo.
Hatupaswi kuendelea kusimama katika taratibu za kawaida tulizozoea wakati corona
imeshavuruga taratibu hizo. Ni lazima tujipange na kutafuta utaratibu mbadala wa
kukabiliana na athari za sasa na zijazo. Tukitambua ukweli kwamba ni lazima maisha
yaendelee sambamba na mapambano ya huu ugonjwa, sisi THTU tunatoa
mapendekezo ya namna ya kukabiliana na athari kama ifuatavyo;
  1. Vyuo vikuu, taasisi za elimu ya Juu na vyuo vya kati vioneshe umahiri wao wa
kutumia fursa za TEHAMA kuhakikisha kwamba vipindi vinaendelea kwa yale
masomo yanayowezekana kwa njia ya mtandao. Hii ni njia mbadala ambayo
4
itasaidia taasisi hizi kupangilia vizuri mihula ya masomo pale ugonjwa huu
utakapodhibitiwa. Kukaa kusubiri tatizo liishe ndipo kuchukua hatua ni
kutojitendea haki wenyewe, kutoitendea haki jamii na nchi kwa ujumla. Wito wetu
kwa serikali ni kuwezesha taasisi hizi kuweza kufanikisha malengo haya na
kutoa msaada kwa taasisi za binafsi ambazo kwa wakati huu zinapitia wakati
mgumu sana kufuatia vyanzo vyao vikubwa vya mapato kusimama kutokana na
wanafunzi wengi kutolipa ada kwa wakati huu.
  1. Utaratibu ulioanzishwa na Taasisi ya Elimu Tanzania ya utoaji wa elimu
mtandaoni na kwenye televisheni uboreshwe zaidi kwa kuhusisha redio ili
kuwafikia wanafunzi wote nchi nzima. Ili kutoharibu mtiririko wa mihula,
wanaweza wakatafutwa walimu wa kila somo na kurekodi vipindi (mada zote)
ambazo zitarushwa kwenye redio zote nchi nzima na wanafunzi kutakiwa
kusikiliza na kufanya majaribio. Hili litasaidia kuwafikia wanafunzi wote nchi
nzima. Hoja ya msingi hapa ni kurasimisha utaratibu wa utoaji wa elimu kupitia
mitandao, vyombo vya habari (redio, televisheni na mitandao ya kijamii) hasa
wakati huu wa janga la corona.
  1. Makampuni ya simu yaliyopo Tanzania yanashauriwa kutafuta namna ya
kupunguza gharama za vifurushi vyao vya intaneti na pia miamala yao wakati
huu wa corona ili kuruhusu watu wengi kufanya malipo kwa kutumia mitandao ya
simu bila kuhofia gharama. Pesa ambayo huwa inatumika kutimiza azma ya
wajibu kwa jamii (corporate social responsibilities) inaweza kusaidia kutumika
kwa njia hii ya kupunguza gharama za miamala na vifurushi.
  1. Wizara zote zijielekeze katika kutengengeza taratibu na mazingira wezeshi
yatakayoendelea kulinda mazingira ya kiuchumi na kijamii kwa mwananchi wa
kawaida na pia kulinda shughuli za kiuchumi za biashara mbalimbali ili kulinda
ajira za wafanyakazi wengi.
  1. Taasisi za elimu ya Juu na vyuo vikuu vichukue hatua ya kufanya tafiti na
machapisho juu ya ugonjwa huu wa corona badala ya kusubiri machapisho na
5
tafiti kutoka vyuo vya Ulaya na Marekani. Hatua hii itasaidia sana kuwepo kwa
taarifa sahihi za dunia na za mazingira yetu pia.
  1. Ni wakati muafaka wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa kutekeleza dhana
ya Tanzania ya viwanda kwa kupambana kutengeneza bidhaa zitakazouzwa
ndani na nje ya nchi ili kuondoa upungufu wa bidhaa na huduma zilizokuwa
zinaletwa kutoka nje ya Tanzania kabla ya janga la corona. Tunashauri serikali
kufanya jitihada za makusudi kulinda viwanda vyetu vya ndani ili visifungwe na
hivyo kuhatarisha mapato ya ndani na ajira za wafanyakazi wengi.
4.Hitimisho
Mapambano dhidi ya janga la corona si ya serikali, mtu mmoja au kundi moja.
Tunahitajika kufanya kazi kwa ushirikiano kuanzia mtu binafsi mpaka jamii yote kwa
ujumla. Serikali na Wataalamu wa afya peke yao hawataweza kufanikisha vita dhidi ya
janga la corona kama jamii itaendelea kuishi maisha kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Pamoja na Imani zetu za kidini, maombi peke yake bila tahadhari haiwezi kudhibiti
corona. Ni vyema tufuate ushauri wa wataalamu, tuunganishe nguvu zetu pamoja. Huu
ni wakati wa kuchukua hatua zitakazoendelea kuimarisha umoja wetu watanzania,
kuelimishana, kupunguziana ugumu wa maisha na kupeana moyo huku tukipena taarifa
sahihi juu ya corona. Kwa pamoja tutashinda.
NIA NA MWELEKEO WETU DAIMA NI KUJENGA, TAIFA KWANZA
Dkt. Paul Loisulie
MWENYEKITI THTU TAIFA
6
Share:

MUME AMUUA MKEWE KWA KUMTWANGA RISASI..AJARIBU KUJIUA


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Koka Moita.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Elibariki Geofrey mkazi wa Chekereni wilayani Arumeru, kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Ester Elibariki, baada ya kumpiga risasi mbili kifuani na shingoni, kisha na yeye kujijeruhi nayo shingoni, na sasa anatibiwa kwenye Hospitali ya Mount Meru.

Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Koka Moita, ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa Aprili 23, 2020, majira ya saa 6:25 usiku, ambapo taarifa za awali zinabainisha kuwa mauaji hayo ya kikatili yamesababishwa na wivu wa mapenzi.

"Tukio hilo limetokea eneo la Chekereni, wilayani Arumeru, Mama aitwaye Ester Elibariki aliuawa kwa kupigwa risasi mbili na mume wake Elibariki Geofrey, mwili wa marehemu huyo upo katika Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya uchunguzi, uchunguzi unaendelea ili kubaini nini chanzo halisi cha tukio hilo, japo taarifa za awali zinaonesha kuwa ni wivu wa mapenzi" ameeleza Kamanda Moita.

Aidha Kamanda Moita akielezea maafa ya mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo, amesema kuwa katika Kijiji cha Morala Kata ya Songoro, kumetokea kifo cha mzee mmoja ambaye aliangukiwa na ukuta wa nyumba yake na kufariki pale pale.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi April 25

















Share:

Friday, 24 April 2020

Makubwa Haya!! WANANCHI WAVUNJA AMRI YA CORONA KUSHUHUDIA CHIFU MAARUFU AKIZIKWA NDANI YA GARI AKIWA AMEKAA KWENYE USUKANI

Mazishi ya Tshekede Pitso

Chifu Tshekede Pitso wa kijiji kimoja Jozanashoek Sterkspruit, Eastern Cape nchini Afrika Kusini amewaacha wengi vinywa wazi baada kuzikwa ndani ya gari lake alilopenda sana enzi za uhai wake la Mercedes Benz.

Inaelezwa  kuwa chifu huyo alikuwa ameagiza familia yake kuheshimu matakwa yake kwa kumzika ndani ya gari hilo lenye gharama ghali.

Chifu Pitso, ambaye alifariki akiwa na miaka 72, alivutwa na trela hadi katika kaburi lake akiwa amevalia suti nyeupe huku mikono yake yote ikiwa imeshikilia 'steering' kana kwamba alikuwa hai. 

Kulingana na binti wa chifu huyo, Sefora Letswaka, marehemu alipenda sana gari hilo la Mercedes Benz E500 licha ya kuwa lilikuwa limeharibika.

 "Kwa wakati mmoja baba yangu alikuwa mwanabiashara tajiri ambaye alikuwa na kundi la magari ya Mercedes. Miaka miwili iliyopita, alijinunulia Mercedes Benz iliyokuwa imetumika. 

Haikuchukua muda kabla ya gari hilo kuharibika, lakini muda wake mwingi alikuwa akiketi ndani ya gari hilo. Hakuwa analiendesha lakini hapo ndipo alikuwa anapata furaha na kusema wakati utakapofika angependa kuzikwa ndani yake. Tulimsikiza na kutimiza matakwa yake na ninatumai amefurahi," alidokezea Sefora.

 Baba huyo wa watoto sita alifanyiwa mazishi rasmi ya dini ya kikristu katika boma la familia hiyo Afrika Kusini. 

Mazishi ya mwanasiasa huyo wa Chama cha United Democratic Movement iliwashuhudia watu wengi wakihudhuria ambao waliamua kuvunja sheria ya kutoka nje kutokana na Janga la Corona. 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger