Saturday, 30 November 2019

Chuo Cha Mipango Chatakiwa Kufanya Utafiti Wa Umasikini Na Utekelezaji Miradi Ya Umma

Benny Mwaipaja, Dodoma
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amekitaka Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, kutafiti kwa kina namna wananchi wanavyoweza kuondokana na umasikini wa kipato pamoja namna Miradi mbalimbali ya Serikali inavyoweza kutekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia thamani ya fedha kuliko ilivyo sasa.

Dkt. Kijaji ametoa rai hiyo wakati akiwatunuku astashahada na shahada mbalimbali wahitimu 3,182 Wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kampasi ya Dodoma wakati wa sherehe za mahafali ya 33 ya chuo hicho.

Amesema kuwa matokeo ya tafiti hizo yataisaidia Serikali na Jamii kwa ujumla kupanga mikakati ya namna ya kukabiliana na umasikini wa wananchi hususan wa vijijini pamoja na kuharakisha maendeleo ya nchi kwa kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa na Serikali inakuwa na tija.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Kamishna Msaidizi wa Bajeti Bw. Pius Mponzi amemwahidi Dkt. Ashatu Kijaji, kwaniaba ya Baraza la Chuo hicho kwamba wataongeza jitihada katika eneo la utafiti na kuhakikisha kuwa matokeo ya utafiti huo yanawafikia wananchi kwa lugha rahisi

Naye Mkuu wa Chuo hicho cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya amesema chuo chake kimetimiza miaka 40 tangu kianzishwe na kimepata mafanikio makubwa kwa kutoa wahitimu mahili na wenye kukidhi mahitaji ya soko.

Amebainisha kuwa Chuo kimeongeza idadi ya kozi kutoka kozi moja mwaka 1980 hadi kufikia kozi 25 mwaka huu, huku idadi ya wanachuo wanaodahiliwa nayo imeongezeka kutoka wanachuo 13 mwaka huo hadi kufikia wanachuo zaidi ya elfu 11 mwaka huu.


Share:

Simbachawene: Matumizi Ya Nishati Mbadala Ni Kitu Cha Muhimu Kwa Maendeleo Ya Taifa

Matumizi ya nishati ya kuaminika na endelevu ni kitu kisichoepukika kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na kwa Taifa lolote duniani hasa tunapoelekea kufikia lengo la Uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025. Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene alipokua akizindua maonyesho ya  14 ya kitaifa ya nishati jadidifu yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja , jijini Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa changamoto kubwa iliyopo  ni kuhakikisha kuwa masuala yote yanayokwamisha upatikanaji rahisi, ueneaji na ongezeko la matumizi ya Nishati hizi kwa wananchi wote hasa walioko vijijini na hata mijini linashughulikiwa ipasavyo.  ”Ninawashauri muwe tayari kupeleka huduma zenu vijijini kwa kuanzisha matawi ya biashara zenu huko badala ya kunga’ng’ania mijini pekee” alisema Waziri Simbachawene.

Aidha alisititiza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inathamini juhudi  za uendelezaji na uhamasishaji wa matumizi ya Nishati jadidifu na udhibiti wa ubora wa vifaa na ufungaji wa mitambo mbalimbali, ili kuwa na Teknolojia endelevu katika ustawi wa Mazingira yetu. Pia amewaagiza TAREA kufanya utafiti kubaini kwa kiasi gani jamii ya Wananchi katika mkoa wa Dar es Salaam wanatumia nishati jadidifu.

“Naye Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Bwana Jeroen Verheul amemshukuru Waziri Simbachawene lakin pia amesema kuwa wataendelea kufadhili masuala mbalimbali  ya mazingira yakiwemo yanayohusu nishati mbadala kama ambavyo wamefanya kwa TAREA.

Akiongea katika ufungzi huo Katibu wa Jumuia ya Nishati jadidifu Makamu Mwenyekiti wa TARE Bwana Prosper Magali, alimshukuru Waziri Simbachawene kwa kufungua maonyesho hayo na aliongeza kuwa TAREA itaendelea kushughulika na  masuala ya nishati jadidifu lakini pia wanachukua maelekezo ya Waziri aliyowapa na kuyafanyia kazi.

Maonyesho hayo ya nishati jadidifu yameandaliwa na Jumuia ya nishati jadidifu (TAREA) ambapo hufanyika kila mwaka. Kwa mwaka huu maonyesho hayo ymefanyika katika viwanja vya mnazi mmoja na mgeni Rasmi akiwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene.


Share:

KAULI YA MWAKINYO BAADA YA KUMCHAPA MFILIPINO ARNEL TINAMPAY


Bondia Mwakinyo akimchapa konde la uso mfilipino Arnel

Bondia Hassan Mwakinyo amesema moja ya sababu iliyopelekea yeye kumshinda Bondia Mfilipino Arnel Tinampay, ni yeye kurusha ngumi nzito huku mpinzani wake akiwa anarusha ngumi nyingi zilizokuwa nyepesi sana.

Mwakinyo ametoa kauli hiyo, baada ya kuisha kwa pambano lake usiku wa kuamkia leo lililofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, ambapo alimchapa Mfilipino, huyo kwa alama 97-93, 98-92 na 96-96.

Mwakinyo amesema kuwa"sipigi ngumi nyepesi napiga sana madude, kilichomsaidia Mfilipino alishasoma, alikuwa ananificha ukitaka kufanya finishing na yeye anapiga."

"Najua kitu kikubwa kilichokuwa kinambeba alikuwa mvumilivu sana, ila pia Mabondia wengi huwa tunapigwa nje ya nchi kwa namna ambavyo hata yeye mwenyewe amepigwa" ameongeza Mwakinyo
Share:

Mahiga Awataka Wakuu Wa Magereza Nchini Kutumia Ujuzi Wa Wafungwa Kujiendesha Na Kutoa Mchango Wa Gawio Kwa Serikali

Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Balozi Dkt Augustine Mahiga amewataka Wakuu wa Magereza nchini kutumia nguvu kazi na ujuzi wa wafungwa walioko magerezani kubuni miradi mbalimbal ili kuwazalishia fedha zitakazowawezesha kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini.

Balozi Mahiga ameyasema hayo jana alipotembelea gereza la Kyela kujionea jinsi Taasisi za Haki Jinai zinavyotekeleza majukumu yake katika mahakama na magereza ikiwemo kutatua changamoto ya mrundikano wa mahabusu katika magereza pamoja na kuboresha mfumo wa utoaji haki na hali ya magereza kote nchini.

“Nguvu kazi za hawa wafungwa ni nyingi na wana ujuzi mbalimbali mnaoweza kuutumia kuanzisha miradi ambayo itawasaidia kupata fedha na mkaweza kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini, watumieni. Pale Dar es Salaam natazama yale majengo ya magereza mnajengewa na jeshi wakati mngeweza kujenga wenyewe.”

Kwa upande wake Mkuu wa Gereza la Kyela ASP. Nelson.M. Mwaifani amesema kwamba wao wamejitahidi kuhakikisha kwamba gereza hilo halina msongamano wa mahabusu na kwamba mazingira ya wafungwa na mahabusu ni mazuri salama kwa afya za watu hao kwani wana mabweni na magodoro yanayowatosha wafungwa na mahabusu wote waliopo katika gereza hilo. Pamoja na hayo ASP. Mwaifani amemwambia Waziri Mahiga aliyeambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Biswalo Mganga kwamba wameingia mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Kyela ya kuzoa taka ngumu, kuzibua mifereji na kufanya usafi katika hospitali ya Wilaya kwa makubalino ya kulipwa shilingi 6,700,000/- kwa mwezi.

Hata hivyo, Dkt. Mahiga alifurahishwa na uongozi wa gereza la Kyela chini ya ASP. Nelson.M. Mwaifani kwa kuwa wabunifu na kushirikiana vizuri na Halmashauri ya Kyela kiasi cha kufanikiwa kupata tenda ya kufanya usafi katika Halmashauri hiyo jambo linalowaingizia wastani wa cha shilingi milioni sita kwa mwezi. Aidha aliwataka wakuu wote wa Magereza nchini kuiga mfano huo na kwamba siku moja wawe sehemu ya taasisi za serikali zitakazotoa gawio mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Joseph Pombe Magufuli.

“Nataka siku moja gereza hili lichangie kwenye mgao wa pesa za Taasisi ya Mahakama kwaajili ya gawio la kwenda serikalini mbele ya Rais, nikisikia, nitafurahi sana. Nina uhakika hivi karibuni tutaulizwa mchango wenu ni nini kwenye gawio la serikali. Najua mnaweza kuwa vyanzo vingi vya kupata pesa hivyo ni matumaini yangu kuwa gawio lijalo Wizara yetu au Taasisi ndani ya wizara yetu itatoa kitu (‘very signficant’) kikubwa, na magereza nina uhakika. Kule sabasaba kila mwaka mnapata zawadi tena nzuri tu, mnaongoza, sasa hapa onesheni mfano mzuri.” Amesema Dkt. Mahiga.

Hivi Karibuni Mheshimiwa Rais Dkt. John Joseph Pombe Magufuli azitaka Taasisi za Umma zinazozalisha na kupata faida zitoe gawio kwa serikali na kuzipa siku 60 Taasisi,Mashirika na Makampuni ya serikali ambayo hajatoa yafanye hivyo ndani ya muda huo. Waziri Mahiga ameamua kutumia ziara yake ya siku saba pamoja na mambo mengine kuzipa changamoto Taasisi za utoaji haki jinai kuanza kufikiria namna ya kuweka mikakati madhubuti ili nazo zianze kutoa gawio kwa serikali. Ziara hii iliyoendelea leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela na Gereza la Kyela, itaendelea tena kesho katika Wilaya ya Mbarali jijini Mbeya.


Share:

ELIMU YA UMEME KWA WASIOONA YAIPA TANESCO TASWIRA MPYA


 MKUU wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare  akizungumza wakati wa uzinduzi wa wasrha hiyo kushoto ni  Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro William Masome
 Sehemu ya wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro.
 Sehemu ya wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro Mkuu wa Mkoa huo ambaye hayupo pichani

 wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro.
MKUU wa Mkoa wa Morogoro aliyevaa suti jeusi akiwa kwenye picha ya Pamoja na washiriki wa semina hiyo kushoto ni  Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro William Masome 

SHIRIKA la Umeme Nchini TANESCO limeendesha semina maalum inayohusu masuala ya Umeme kwa wanachama wa chama cha wasioona  Tanzania (TLB)  mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati wa uzinduzi  wa warsha hiyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Loata Ole Sanare amesema kuwa Tanesco  imeonyesha mfano mzuri wa kuigwa kwa kutoa elimu hiyo kwa watu wa kundi  maalum katika jamii.

Alisema pia kupitia hili shirika limetoa taswira kuwa mashirika ya Umma yanafuata muelekeo wa Raisi John Pombe Magufuli ambae ni  Raisi wa wanyonge na kwa kujali wateja wake hata wa Makundi maalum kwa kutoa elimuYa Umeme itakayowasaidia katika maisha yao ya kila  siku.

Mkuu huyo wa Mkoa  amewataka wasioona kutokuwa wanyonge kwakudhani kuwa  Serikali haiwatambui na kusema kuwa Serikali ipo pamoja nao na kuwakaribisha katika ofisi za Mkoa, muda wowote watakapokua na changamoto zozote.

Naye Kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro William Masome amesema Kuwa TANESCO chini ya Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Tito Mwinuka imetambua umuhimu wa watu wenye Ulemavu wa kutoona kupatiwa elimu ya Umeme ili waweze kutambua fursa  zitokanazo na umeme zitakazoweza kuwainua kiuchumi lakin pia kuwafundisha jinsi ya kutumia umeme vizuri (matumizi Bora ya umeme)ili wasilipe gharama kubwa
Kwenye kununua Umeme.

Naye kwa upande wake Mratibu wa idara ya maendeleo, Vijana na Chipkizi toka TLB , Bw.Kiongo Itambu ameishukuru TANESCO kwa kuwapatia elimu hiyo
Maalum ambayo itawasaidia hasa katika kujiepusha na matukio ambayo yanaweza kuathiri usalama wao.

Alisema kwani wameshajua athari za kukaa karibu na miundombinu ya umeme  na  kuahidi kushirikiana na TANESCO katika kuwafichua wanaolihujumu Shirika kwa kuiba umeme na kuharibu miundombinu ya Shirika.

Aidha Bw. Kiongo alimuhakikishia Mkuu wa mkoa kuwa wao kama watu wenye ulemavu ni kama watu wengine, ni mara chache kusikika wasioona ikiwa na sifa ya kuliibia shirika la umeme na watakuwa mabalozi wa kuhakikisha Tanesco haiujumiwi ili kukuza kipato chake kwa maendeleo ya Shirika na Taifa kwa ujumla
Share:

ACT- Wazalendo wataka vifurushi bima ya NHIF Visitishwe, Serkali Yawajibu

Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kusitisha vifurushi  vya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Tanzania (NHIF) kwa madai kuwa vinakandamiza wasiokuwa na uwezo.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dorothy Semu, alipozungumza na waandishi wa habari.

Vifurushi hivyo vilizinduliwa juzi jijini Dar es Salaam na uongozi wa NHIF, ukieleza kuwa vimegawanywa katika makundi matatu yaliyopewa majina ya 'Ninajali Afya', 'Wekeza Afya' na 'Timiza Afya'.

Kwa mujibu wa mpango huo mpya wa matibabu wa NHIF, watu wenye umri wa kati ya miaka 18 na 35 watalipia Sh192,000 kwa mwaka kuwa katika kifurushi cha Najali Afya Premium ama Sh384,000 cha Wekeza Afya ama Sh516,000 cha Timiza Afya.

Kwa wenye umri mkubwa zaidi wa kuanzia miaka 36 hadi 59 watagharimia matibabu ya mwaka mzima kwa kulipia Sh240,000 katika mpango wa Najali Afya Premium au Sh444,000 (Wekeza Afya) au Sh612,000 (Timiza Afya).

Watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea wataweza kugharimia matibabu ya mwaka kwa kulipia kati ya Sh360,000 na Sh984,000. Bei za vifurushi hivyo inaongezeka kulingana na idadi ya wanufaika kama mwenza na watoto hadi wanne.

Dorothy Semu alisema  kuwa kitendo cha serikali kujiondoa kwenye kuhudumia raia wake kwenye afya kwa kutangaza vifurushi vipya vya bima, ni kuwatenga wenye kipato cha chini.

Alisema gharama zilizowekwa katika vifurushi hivyo vipya zinajenga matabaka mawili katika utolewaji wa huduma za afya; la wenye nacho na wasio nacho.

“Binadamu hachagui kuumwa au aina ya ugonjwa ambao unapaswa kuugua, utaratibu huu wa vifurushi unachukulia kwamba suala la ugonjwa ni jambo la hiari, kwamba mtu anaweza kuchagua kuumwa ugonjwa huu ama kuukataa ule, hivyo atatibiwa kutokana na chaguo lake.

"Mtazamo wa namna hii ni hatari sana katika ujenzi wa jamii yenye utu, usawa na yenye haki. Duniani kote kuna bima aina mbili, ya binafsi na ya umma. Kiwango cha malipo ya kila mwaka kwa kila mtu ni tofauti kulingana na vigezo tofauti.

"NHIF kimsingi ni skimu ya bima ya afya ya umma, na kwa maana hiyo viwango vya malipo vinatokana na uwiano wa kipato cha mtu na mafao yanapaswa kuwa sawa kwa watu wote bila kujali kiasi cha mchango wanaotoa.

"Kitendo cha kutoa vifurushi vya malipo tofauti, na huduma kutolewa kwa kuzingatia kifurushi, ni kitendo cha kuifanya NHIF kuwa bima binafsi na 'kubidhaisha' afya ya Watanzania," alidai.


Chama hicho kilishauri kusimamishwa kwa huduma ya vifurushi hivyo vipya ili kupunguza matumizi makubwa ya rasilimali fedha.

“Kwa mfano, badala ya kuzuia wananchi wa kipato cha chini kupata huduma mbalimbali kama MRI na CT scan, serikali itoe ruzuku kwa wananchi hao kwa kuwalipia NHIF. Huu ndiyo wajibu wa serikali kutokana na kodi inazokusanya kutoka kwa wananchi,” alisema.


Hata hivyo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameyajibu madai ya ACT- Wazalendo kwa kusema kuwa   Vifurushi hivi ni kupitia utaratibu wa HIYARI  na sio lazima. Pia, havijafuta Bima ya Afya ya Jamii (CHF) .

"Tusifanye siasa kwenye hili.  Vifurushi hivi ni kupitia utaratibu wa HIYARI sio lazima. Pili, havijafuta Bima ya Afya ya Jamii (CHF) ambapo kiwango cha kuchangia kwa mwaka ni shilingi 30,000 kwa kaya ya hadi watu 6. Aidha, vifurushi vya watoto, Wakulima nk. bado vipo." Ameandika Ummy Mwalimu katika ukurasa wake wa Twitter wakati akipangua Hoja ya Zitto Kabwe



Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi November 30

















Share:

Friday, 29 November 2019

Credit Officer Job Opportunity at The Guardian Limited (TGL)

Credit Officer Job Opportunity at The Guardian Limited (TGL) OVERVIEW The Guardian Limited (TGL), widely acclaimed as the Home of Great Newspapers, is part of the IPP Group of Companies – one of Tanzania’s leading private sector entities with dignified presence in the print media as well as television and radio broadcasting. TGL currently publishes two upmarket daily… Read More »

The post Credit Officer Job Opportunity at The Guardian Limited (TGL) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Waziri Mhagama Ampa Miezi Miwili Mkandarasi Kukamilisha Hatua Ya Kwanza Kiwanda Cha Bidhaa Za Ngozi Cha Karanga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mgahama, amempa miezi miwili mkandarasi anayejenga Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga, kilichopo mkoani Kilimanjaro, kukamilisha hatua ya kwanza ya  ujenzi wa kiwanda hicho hadi kufikia tarehe 20 Januari mwaka 2020, ili ujenzi  hatua ya pili ya ujenzi wa kiwanda hicho uweze kuanza mara moja kwa ajili ya kuhakikisha kiwanda kinaanza uzalishaji wa bidhaa za ngozi.

Mkandarasi huyo ambaye ni Kikosi cha ujenzi cha Shirika la Uzalishaji la Magereza ameelekezwa kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ndani ya kipindi hicho kuhakikisha amejenga majengo manne, ikiwa ni jengo la kuzalisha bidhaa za ngozi na soli za viatu, jengo la mitambo ya umeme pamoja na ghala la vifaa vya ngozi.

Waziri Mhagama ametoa maelekezo hayo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho leo tarehe 29 Novemba, 2019, mkoani Kilimanjaro, ambapo amefafanua kuwa  kiwanda hicho ni muhimu kujengwa kwa haraka sana kwani kitaiwezesha Tanzania  kuufikia uchumi wa viwanda kwa kuwa bidhaa zitakazozalishwa na kiwanda hicho zina soko kubwa ndani na nje ya nchi hususani katika Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
 
“Sisi katika Afrika ni matajiri wa mifugo na bidhaa zinazolishwa na mifugo, lakini hapa nchini  hatuna kiwanda tunachoweza kutegemea katika bidhaa za ngozi, hivyo ni muhimu kuharakisha ujenzi wa kiwanda hiki ili tuweze kutengeneza ajira hapa kati ya elfu tatu hadi elfu nne na ukizingatia nguvu kazi ya nchi yetu asilimia 56 ni vijana.Kiwanda hiki kitakuwa muhimu sana kwa ustawi wa nchi” Amesema Mhagama.

Mhe. Mhagama amewataka watekelezaji wa Mradi huo  kuhakikisha wanakuwa na mpango kazi wa kukamilisha kazi hiyo na kuuwasilisha kwake, lakini pia kuwa  na mpango mkakati wa biashara utakao wezesha kusaidia kupatikana na masoko ya bidhaa hizo. Ameongeza kuwa atakuwa na watu wakufuatilia kwa karibu shughuli za ujenzi huo ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati. Huku akisisitiza Changamoto zozote za utekelezaji wa Mradi huo zizingatiwe ili pindi ukikamilika zisije anza kuibuliwa na kuweza kukukosesha mradi kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Ajira, vijana na Watu wenye Ulemavu), Andrew Massawe, amemuhakikishia Mhe. Waziri Mhagma kuwa, atafuatilia ushughuli za ujenzi wa mradi huo kwa  karibu ili kuhakikisha maelekezo yake yanatekelezwa kwa  kila hatua za ujenzi ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa muda uliopangwa.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, Hosea Kashimba amemhakikishia Mhe.Waziri Mhagama kuwa atahakiksha kuwa ujenzi huo unakuwa na ubora na unakamilika ndani ya muda aliouelekeza ili watanzania waweze kunufaika na  bidhaa za kiwanda hicho lakini pia waweze  kupata ajira za uhakika kutoka katika kiwanda hicho.

Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Viwanda vya ngozi Karanga unatekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),na Magereza kupitia wataalamu wake wa ndani na timu ya washauri elekezi wa viwanda TRIDO.

Mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga unatokana na Kampuni ijulikanayo kwa jina la “Karanga leather Industries Co Ltd” iliyoanzishwa mwaka 2017  kwa lengo la kutekeleza mradi wa viwanda vya bidhaa za ngozi katika eneo la gereza la Karanga , kampuni hiyo iliingia ubia kati  ya uliokuwa mfuko wa Pensheni PPF ambapo kwa sasa majukumu yake yamechukuliwa na PSSSF pamoja na Jeshi la Magereza kupitia Shirika la Uzalishaji. Malengo ya ubia huo nikuongeza wigowa uzalishaji wa bidhaa za ngozi na kuongeza thamani ya ngozi nchini.

MWISHO.


Share:

Waziri Mkuu: Madhehebu Ya Dini Yameisaidia Serikali Kupata Viongozi Wazuri

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema madhehebu ya dini yametoa mchango mkubwa katika kuwapata viongozi wa Serikali wanaofuata maadili mema na miiko ya uongozi.

Akizungumza  wakati alipofungua Msikiti wa Haq – Kionga ulioko Magomeni, jijini Dar es Salaam leo mchana (Ijumaa, Novemba 29, 2019), Mheshimiwa Majaliwa amesema imedhihirika kwamba waumini wazuri wa dini mbalimbali wamebainika kuwa ni viongozi wazuri na waadilifu ndani ya Serikali.

Amewasihi viongozi wa dini waendelee kuwafundisha maadili mema waumini wao ili Taifa liendelee kuwa na raia wema ambao baadhi yao ndiyo watakakuwa viongozi katika ngazi mbalimbali hapo baadaye.

“Nyumba za ibada ndiyo mahali sahihi panapojengwa maadili mema kwa watu wa rika zote, hivyo nawaomba Watanzania wawe waumini wazuri wa dini zao kwani kwa kufanya hivyo watakuwa pia ni raia wema,” amesema Mheshimiwa Majaliwa.

Amesema wazazi na walezi wanawajibika kuwarithisha watoto wao imani za dini vizuri kwani anaamini kwa kufanya hivyo watoto watajengewa misingi mizuri ya imani ya dini na maadili mema na watakapokuwa watu wazima watakuwa ni raia wema.

Mheshimiwa Majaliwa aliwasilisha mchango wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli wa sh. milioni 10 na yeye pia alichangia sh. milioni tano ili zisaidie katika awamu ya pili ujenzi wa msikiti huo.

Naye Sheikh Masoud Jongo ambaye alimwakilisha Sheikh Mkuu wa Tanzania katika ufunguzi wa msikiti huo, alisema uhuru mkubwa wa kuabudu uliopo nchini ndiyo sababu kubwa inayoifanya Tanzania iwe ni nchi ya amani na utulivu.

Sheikh Jongo amewaomba Watanzania wautumie vizuri uhuru mkubwa wa kuabudu uliopo nchini kwani ni nchi chache duniani zinazotoa uhuru mkubwa wa kuabudu kwa wananchi wake kama ilivyo hapa Tanzania.

Baadhi ya viongozi walioshiriki katika ufunguzi wa msikiti huo ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia na mbunge wa Kibaha Vijijini, Abuu Juma.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, NOVEMBA 29, 2019.


Share:

Picha : ABIRIA WANUSURIKA KIFO HIACE IKITEKETEA KWA MOTO STENDI YA MABASI SOKO KUU MJINI SHINYANGA


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Abiria ambao idadi yao haijajulikana wamenusurika kuungua baada ya gari aina ya Hiace yenye namba za usajili T998 AAP linalofanya safari zake Shinyanga kwenda Maswa kuteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokeo leo Ijumaa Novemba 29,2019 majira ya saa nane na nusu wakati abiria wakiwa wamepanda kwenye Hiace hiyo wakijiandaa kuanza safari kuelekea Maswa mkoani Simiyu.

Dereva wa Hiace hiyo aliyejulikana kwa jina Basu Gereja amesema chanzo ni kupasuka kwa Betri na kusababisha gari hilo kuwaka moto.

"Chanzo ni Betri kulipuka,tumefanya utaratibu wa kuwatoa abiria kwenye gari kisha kupiga simu Zimamoto kwa ajili ya msaada ambao wamefika na kusaidia kuzima moto huu,gari ilikuwa inatoka Shinyanga kwenda Maswa",amesema Basu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa dereva alikuwa amewasha gari akijiandaa na safari ndipo ghafla walipoona gari linawaka moto ndipo utaratibu wa kuwatoa abiria ukaanza kufanyika huku abiria wengine wakitokea madirishani kwa sababu mlango uligoma kufunguka.

Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga Edward Lukuba (Afisa Oparesheni Mkoa wa Shinyanga) amesema wamepata taarifa za kuteketea gari kwa kuchelewa na kukuta gari hilo linaungua na kufanikiwa kuzima moto huo huku akiwasisitiza wananchi kujitahidi kuwa wanatoa taarifa mapema pindi majanga yanapotokea.
Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiendelea kuzima moto uliokuwa unateketeza Hiace katika Stendi ya Mabasi Soko Kuu Mjini Shinyanga - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga Edward Lukuba (Afisa Oparesheni Mkoa wa Shinyanga) akiwa eneo la tukio


Share:

Arsenal yamfuta kazi Kocha Mkuu Unai Emery

UNAI Emery aliyekuwa kocha mkuu wa Arsenal amepigwa chini ndani ya kikosi hicho baada ya kudumu nacho kwa muda wa miezi 18 akiwa kazini.

Arsenal imefikia uamuzi huo baada ya jana kupigwa na Frankfurt bao 2-1, kwa mchezo wa saba mfululizo bila ushindi (sare 5 na  vipigo 2).
 

Arsenal imemtangaza Freddie Ljungberg kuwa kocha wa muda na kurithi mikoba ya Emery.


Share:

Viwanja Bei nafuu: Bunju na Mapinga (Kimele)

Kwa Mapinga vipo viwanja vya 20/25 bei milion 5, 20/30 bei milion 6, 20/40 bei milion 8, nusu eka milion 25 na eka milion 50

Kwa Bunju vipo viwanja vya sqm 1000 kwa milion 30.

Ukipata ujumbe huu mjulishe ndugu/jamaa/rafiki, na biashara hii haina dalali/udalali.

Mpigie mhusika: 0758603077


Share:

Harmonize Kumkabili Ali Kiba Disemba 8

Wasanii wa Tanzania, Alikiba na Harmonize watakutana katika jukwaa moja la tamasha la Fiesta litakalofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Desemba 8, 2019.

Waandaaji wa tamasha hilo Jumanne Novemba 26, 2019 wametangaza baadhi ya wasanii nchini watakaoshiriki Fiesta, wakiwemo wawili hao.

Kukutana jukwaani kwa wasanii hao kunasubiriwa kwa hamu kutokana na Harmonize kuachana na lebo ya Wasafi, hivyo mashabiki wengi kutaka kumshuhudia akitoa burudani nje ya lebo hiyo.

Alhamisi ya Oktoba 24, 2019, Harmonize alieleza jinsi alivyouza nyumba zake tatu na baadhi ya mali ili kuilipa lebo ya Wasafi Sh500 milioni kwa ajili ya kupata hakimiliki ya kutumia nyimbo zake na jina.

Alibainisha kuwa mkataba alioingia na lebo ya Wasafi inayomilikiwa na msanii Diamond Platnumz ilikuwa na kipengele cha kulipa kiasi hicho cha fedha ikiwa atavunja mkataba ili aweze kuendelea kutumia nyimbo pamoja na jina lake la kisanii.

Wakati akiwa Wasafi, Harmonize hakuwahi kushiriki tamasha la Fiesta tofauti na Ali Kiba aliyewahi kushiriki mara kadhaa.


Share:

Diamond Platnumz Ambwaga Ali Kiba

Shirika la Utangazaji CNN limetaja wanamuziki bora 10 barani Afrika, akiwemo msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz.

Orodha hiyo inamfanya Diamond kuwa msanii pekee kutoka Afrika Mashariki kuingia katika orodha hiyo ya wasanii wanaofanya vizuri katika muziki.

Wengine waliotajwa ni Burna Boy wa Nigeria ambaye pia ameteuliwa katika tuzo za Grammy zitakazofanyika Januari 2020 pamoja na Yemi Alade, Tiwa Savage na Wizkid wote wa nchi hiyo.

Mtunzi, mwanaharakati na mshindi wa tuzo ya Grammy kutoka nchini Benin, Angelique Kidjo pia amejumuishwa katika orodha hiyo.

Pia wapo waimbaji wa Afrika Kusini, Sho Madjozi, Busiswa Gqulu ambaye pia ni mwandishi wa nyimbo na mshairi, rapa wa Zambia, Mwila Musonda maarufu Slapdee.

Diamond ambaye ameingia katika tasnia ya muziki miaka 10 iliyopita amekuwa na mafanikio makubwa.


Share:

Mfumo wa vifurushi vya Bima ya Afya Wazinduliwa Rasmi...Elimu Kutolewa Nyumba Kwa Nyumba

Mfumo wa vifurushi vya Bima ya Afya umezinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam, huku Mwenyekiti wa Bodi ya Mfumo wa Bima ya Taifa (NHIF) Anna Makinda, akisema watu watafuatwa mpaka majumbani kupewa elimu ili wajiunge.

Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge, aliwataka pia watumishi wa vituo vya afya na hospitali, kuwa na lugha nzuri kwa watu wanaotumia bima hizo.

Alisema kuna baadhi ya wahudumu wa afya wamekuwa hawatoi kipaumbelea kwa watu wanaotumia bima ya afya na kuwataka waache tabia hizo.

“Utoaji wa huduma za afya sasa unaenda kwa ushindani, hospitali yenye wahudumu wa afya wanaotoa huduma nzuri ndio watakaopata fedha nyingi, mtu akiumwa atatamani kwenda kwenye hospitali inayotoa huduma nzuri.

“Wahuduma waendelee kuwa na bidii, kuna baadhi ya wahudumu wa afya wamekuwa na lugha chafu kwa wagonjwa hasa wanaotumia bima, hawa nawaambia waache tabia hiyo wagonjwa, wanahitaji lugha zenye faraja.

“Uzinduzi huu unaenda na ile azima ya Tanzania ya viwanda, utakuwa na msaada katika kuleta  afya njema kwajamii kwani bila afya njema hakuna uchumi wa viwanda, hivyo ni msaada mkubwa kwa wananchi wote, watumishi watapita majumbani kutoa elimu ya vifurushi hivi ili watu wengi wajiunge,”alieleza Makinda.

Kutokana na baadhi ya watu kuamini kuwa kukata bima ni kupoteza fedha, Makinda aliwaomba Watanzania waweke kipaumbele katika kupata bima ya afya kwa hiyari ili kuepuka gharama kubwa wanapougua.


Share:

Tanzania Communication Officer at Frankfurt zoological Society – Tanzania

Job Summary The Frankfurt Zoological Society (FZS) is an international conservation NGO based in Germany. FZS is active in biodiversity-rich areas on four continents. The Africa Program includes projects in five focal countries: Ethiopia, Tanzania, Zambia, Zimbabwe and the DR Congo. It is coordinated from the Africa Regional Office (ARO) based in Arusha, Tanzania. FZS seeks to improve… Read More »

The post Tanzania Communication Officer at Frankfurt zoological Society – Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger