Na.Amiri kilagalila Maambukizi ya virusi vya ukimwi mjini mafinga mkoani iringa yanahofiwa kuongezeka kwa kasi kutokana na kuadimika kwa bidhaa ya kujikinga na maabukizi. kondom za kike na za kiume zimeonekana kupungua mjini hapo huku zilizopo zikielezwa kupanda bei na kuuzwa kwa bei ya ghali kunzia shilingi elfu 1000 mpaka elfu 3000 hali inayopelekea badhi ya watumiaji kushindwa kumudu gharama na kuwa hatarini zaidi na kukumbwa na maambukizi ya VVU. “Utakuta ukienda duka hili hakuna kondom je mh.mwenyekiti tunawasaidiaje wanaouza hizi kondom kuzipata kwa uraisi na ongezeko ili zije kwa…
Friday, 15 February 2019
WEZI SUGU WATATU WAPEWA ZAWADI YA VALENTINE DAY
Wezi watatu sugu ambao wamekuwa wakiwahangaisha watu katika eneo la Barnabas, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya wameteketezwa moto hadi kufa Siku ya Wapendanao "Valentine Day", Februari 14,2019.
Kwa mujibu wa walioshuhudia tukio hilo, washukiwa hao walikiri mbele ya umma kuhusika katika matukio mbali ambayo yamekuwa yakishuhudiwa mara kwa mara katika eneo hilo na kuwakosesha wenyeji amani.
Kulingana na Joseph Maina ambaye ni mkazi, aliyezungumza na Taifa Leo, Alhamisi, Februari 14 wahalifu hao wamekuwa wakihangaisha raia kwa muda mrefu sana.
Polisi walifika baadaye na kuichukua miili yao baada ya waliokuwa wakishuhudia kusababisha msongamano mkubwa wa magari katika barabara kuu ya Nakuru-Nairobi.
“Hii sio mara ya kwanza kupata tabu mikononi mwa wahalifu, wanaotekeleza maovu peupe bila kuogopa idara ya usalama,” alisema.
Bw Maina alisifia hatua ya wananchi kuangamiza sehemu ya genge hilo kwani vyombo vya usalama vimekuwa vikishindwa kutoa msaada kwao.
Imeelezwa kuwa, wahudumu wa boda boda pia walieleza kuwa shida ambazo wamekuwa wakipitia, zimechangiwa sana na majambazi hao kwani huwashambulia kila mara na kuwanyang’anya pikipiki zao na huwa wamejihami kwa silaha hasa nyakati za usiku.
Wakazi wafika kwa wingi kushuhudia wezi watatu walioteketezwa moto hadi kufa katika eneo la Barnabas, Kaunti ya Nakuru.
Itakumbukwa siku chache zilizopita, mwendeshaji mmoja wa boda boda aliuawa katika hali ya kutatanisha na inasadikiwa waliouawa ni sehemu ya genge la majambazi waliohusika na mauaji hayo.
Wananchi walifika kwa wingi kushuhudia tukio hilo na waliwalaumu sana pilisi na wamiliki wa maeneo ya burudani kwa ongezeko la uhuni eneo hiulo.
Kamanda wa Polisi (OCPD) Kaunti ya Nakuru Samwel Obara hakufika kwa wakati ili kutoa taarifa yake kuhusiana na mauaji hayo.
KATIBU MKUU TAMISEMI ARIDHISHWA NA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA IGOMA NYAMAGANA
Hayo yamebainishwa wilayani Nyamagana kwenye ziara maalum ya Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi. Mhandisi. Joseph Nyamhanga, akiwa kwenye ukaguzi wa miradi ya maendeleo sekta ya Afya, Miundombuni ya Barabara pamoja na sekta ya Afya. Mhandisi Nyamhanga amepata fursa ya kutembelea ujenzi wa majengo sita ya mradi wa Kituo cha Afya Kata ya Igoma inayogharimu shilingi 400,000,000 za kitanzania. Akiwa eneo hilo hakusita kupongeza uongozi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuzingatia thamani ya fedha katika ujenzi wa majengo sita aliyozingatia ujenzi…
MKE AMUUA MUMEWE KWA KUMCHOMA KISU TUMBONI WILAYANI LUDEWA KUAMKIA VALENTINE DAY
Na Amiri kilagalila Mkazi wa kitongoji cha Ukindo kijiji cha Lugalawa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe aliyefahamika kwa jina la Osmund Joseph Mwinuka anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 37 amefariki dunia kwa kuchomwa na kisu maeneo ya tumboni na mke wake kwa sababu ya Mapenzi. Akizungumza na mtandaao huu kwa Njia ya simu mmoja wa mashuhuda aliyefika katika tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa jina lake,amesema kuwa mwanaume huyo fundi piki piki na mkulima wa kijiji hicho alichomwa na kisu na mke wake Anatoria Mtweve majira ya jioni baada ya…
VIJANA WAFARIKI WAKIOGELEA KWENYE LAMBO LA KUJENGEA BARABARA SHINYANGA
Picha haihusiani na habari hapa chini
Vijana wawili waliofahamika kwa majina ya Mateo Dase (22) mkazi wa Kadoto na Jonas Pigi (27) wote wakazi wa Kadoto wamefariki dunia baada ya kuzama kwenye maji katika lambo la kitongoji cha Kadoto wakiwa wanaogelea kwenye lambo lililotokana na uchimbaji wa kokoto zilizotumika kujengea barabara itokayo Mjini Shinyanga kwenda Bubiki - Kishapu.
Kwa Mujibu wa Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Februari 14,2019 majira ya saa saa tano asubuhi kijiji cha Kadoto, kata ya Mwalukwa, Tarafa ya Nindo, wilaya ya Shinyanga.
Kamanda Abwao amesema mazingira ya vifo hivyo ni kwamba Jonas Pigi alikuwa anafanya juhudi za kumuokoa Mateo Dase aliyekuwa ameshazama ndipo wote wawili wakazama.
"Juhudi za kuopoa miili ya marehemu kutoka kwenye lambo hilo zimefanyika kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na SHUWASA kwa kuyatoa maji kwenye lambo hilo, miili ya marehemu imekabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi",amesema.
Na Kadama Malunde - Shinyanga
MAJAMBAZI WAMKERA MBUNGE WA USHETU..WANAKATA MAPANGA NA KUIBA FEDHA
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, wilayani Kahama, mkoani Shinyanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, amekemea vitendo vya kiuhalifu vinavyoendelea katika Halmashauri ya Ushetu ambavyo vimepelekea kusababisha majeruhi na vifo Halmashaurini hapo.
Amezungumza hayo katika kata ya Mpunze iliyopo katika Halmashauri hiyo ambapo kabla ya kuzungumza nao Mbunge huyo alipita katika kituo cha afya cha Ukune kwa ajili ya kuitizama na kuipa pole familia moja iliyoivamiwa usiku na kikundi cha watu kisichojulikana ambacho kiliwashambulia familia hiyo kwa kukatwa mapanga na kuwaibia fedha.
Mbunge Kwandikwa, ameonesha kusikitishwa na matukio yanayoendelea katika kata hizo na kuwaahidi wananchi wake kulisimamia suala hilo kikamilifu.
"Hatuwezi kukubali hali hii kwasababu wananchi wanaogopa kufanya biashara na wengine wanaogopa kuzalisha hivyo suala la ulinzi lipo mikononi mwetu wenyewe ni lazima jambo hili tuliondoe", amesisitiza Mbunge Kwandikwa.
Ameongeza kuwa atafanya juhudi za kuweka Kituo cha Polisi maeneo jirani ili kuweza kuongeza hali ya usalama kwa wananchi na iwe rahisi kwao kuripoti kituoni hapo matukio yote ya kiuhalifu pindi yanapotokea.
Aidha, Mheshimiwa Kwandikwa, amewataka wananchi kutoa taarifa kwake na kwa vyombo vya usalama kwa yeyote wanayemdhani anajihusisha na vitendo vya kijambazi katika maeneo yao ya wanamoishi.
"Hatutovumilia hali hii naomba viongozi wanaouhusika na ulinzi mjipange kisawasawa kwani hata mimi saa hii niko tayari kazini", amefafanua Mbunge huyo.
Katika hatua nyingine, Mbunge huyo amewaeleza wananchi wake baadhi ya miradi inayoendelea kufanyika katika kata hiyo na kata zingine za Halmashauri ya Ushetu na kusisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu na kujitoa katika shughuli za kimaendeleo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Sabasabini, Bw. Emmanuel Makashi, amemshukuru Mbunge huyo kwa kulisimiamia suala la usalama katika kata za jimbo lake kwani limekuwa kero ambapo naye ni miongoni mwa waathirika wa kuvamiwa.
Mbunge huyo yupo mkoani Shinyanga kukagua hatua zilizofikiwa katika miradi inayoendelea kutekelezwa kama vile ujenzi wa hospitali ya wilaya, jengo la halmshauri, na barabara zinazoendelea kujengwa kwa kiwango cha changarawe ya Nyamilangano-Butibu yenye urefu wa kilomita 12.
CiC-TZ NA UTPC ZAWAALIKA WAANDISHI WA HABARI KUCHANGAMKIA FURSA YA MRADI WA MIAKA MITATU

Shirika la Children in Crossfire (CiC-TZ) ni shirika la kimataifa la misaada lenye makao yake nchini Ireland ambalo kusudi la kuanzishwa kwake ni kusimamia haki na mahitaji ya watoto wadogo ambao wapo kwenye jamii maskini duniani.
CiC-TZ kupitia mradi wake wa kuongeza uelewa na uwajibikaji katika upatikanaji wa huduma bora za Malezi, Makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (Early Childhood Development – ECD), limeingia makubaliano ya kimkakati ya miaka mitatu (2019 – 2021) na taasisi ya UTPC kupitia waandishi wa habari walioko kwenye klabu za waandishi wa habari nchini kote, kwa kuvishirikisha vyombo vya habari katika ngazi zote za mkoa na taifa.
Lengo maalumu la ushirikiano huu ni kuleta ufanisi kwa kuvishirikisha vyombo vya habari hasa katika ngazi ya mikoa na kitaifa kupitia UTPC na klabu zake katika kuimarisha na kuboresha uelewa na uwajibikaji katika eneo hili la malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (Early Childhood Development – ECD) ili kuwapa watoto nafasi ya kufikia uwezo wao kamili kwenye maisha.
Waandishi wote ambao ni wanachama wa klabu wanahimizwa kuomba maombi maalumu ya kushiriki kwenye mradi huu kama ambavyo maelekezo yalivyotolewa kwenye klabu za waandishi wa habari nchini kote.
Maombi yote yatumwe kwenye anuani ifuatayo.
(Unashauriwa kutumia baruapepe)
Mkurugenzi Mtendaji
UNION OF TANZANIA PRESS CLUBS (UTPC)
S.L.P 314
Mwanza
Email: utpctz@yahoo.co.uk
MASELE AJIGAMBA JINSI CCM ILIVYOSAMBARATISHA UPINZANI SHINYANGA
Mbunge wa Shinyanga (CCM), Steven Masele amesema mkoa wa Shinyanga ulikuwa ngome ya wapinzani lakini wamefanikiwa kuisambaratisha.
Masele alisema hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.
Alisema kwa kushirikiana na viongozi wa chama hicho wilaya na mkoa ndani ya kipindi cha miaka saba wamefanya kazi kubwa kuisambaratisha ngome hiyo na baadhi ya viongozi wa upinzani kuhamia CCM.
“Mheshimiwa makamu wa pili wa Rais waliokuwa miongoni mwa viongozi wa Chadema Shinyanga tuliokuwa tukipambana nao mwaka 2015 sasa hivi wamerudi nyumbani wamejiunga na CCM,” alisema.
Masele alisema baadhi ya waliowahi kuwa viongozi wa Chadema ambao wamejiunga na CCM ni Hassan Baruti ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa baraza la vijana la chama hicho wilaya na Ngassa Donald aliyekuwa katibu wa mkoa wa Chadema.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Balozi Idd aliwataka wana CCM waachane na makundi ndani ya chama na badala yake washirikiane ili kuleta maendeleo wanayohitaji wananchi.
“Wana CCM lazima kuwa na nidhamu maana hatutasita kuwachukulia hatua wanaojifanya mchana wenzetu lakini usiku wanageuka.”
“Bora tuwe na wanachama wachache lakini wenye nidhamu na uchungu na chama, uchaguzi uliopita wapo wengi waliokwenda upande wa pili lakini walijirudi na baadhi yao waliomba radhi baada ya kubaini kosa,” alisema Balozi Idd ambaye ni mlezi wa CCM mkoa wa Shinyanga.
Naye katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga, Haula Kachwamba alisema jumla ya wanachama 40 wa vyama vyama vya upinzani wamejiunga na CCM, huku watu wengine zaidi ya 300 wakichukuwa kadi za kuwa wanachama wa chama hicho.
Na Stella Ibengwe, Mwananchi
TAARIFA KWA UMMA : UKOSEFU WA MAJI MAENEO YOTE YA JIJI LA MWANZA NA VIUNGA VYAKE
TAARIFA KWA UMMA
Tumepokea taarifa kutoka TANESCO, kuwa Tarehe 16 Februari, 2019 kuanzia Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 11:00 Jioni watazima umeme kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo eneo la Chanzo cha Maji Capri-Point.
Kufuatia taarifa hiyo, tunasikitika kuwataarifu wateja wetu wote kuwa hakutakuwa na uzalishaji wa maji hadi hapo huduma ya nishati ya umeme itakaporejea katika hali yake ya kawaida.
Tunawashauri kutunza maji yatakayotosha katika kipindi hicho ambacho kutakuwa hakuna uzalishaji wa maji.
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza. Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia kituo chetu cha huduma kwa mteja kwa namba 0800110023 (Bure).
Imetolewa Tarehe 15 Februari, 2019 na: -
OFISI YA UHUSIANO
MWAUWASA
KUTANA NA MREMBO MWENYE MATITI MAKUBWA ZAIDI

Jina lake halisi ni Pamella Odame Watara mwenye miaka 22, alizaliwa na mama Mghana na baba Mkenya lakini kwa sasa anaishi nchini Ghana.
Pamella amekuwa kivutio kikubwa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo licha ya rangi na sura nzuri aliyojaliwa, Pamella pia amebarikiwa kuwa na matiti makubwa yasiyo ya kawaida, kitu ambacho kinamfanya kila anapopita aache gumzo.
Matiti hayo yenye size ya 34D ambayo ni moja ya size kubwa zaidi, yamekuwa yakimpa wakati mgumu kwa siku za nyuma kutokana na kuchekwa na wenzake, lakini sasa ameamua kuyatumia kama kitega uchumi na kumuingizia pesa.
“Nilipokuwa mdogo mama yangu alikuwa anayabana kwa nguo, walishanipeleka hata hospitali kutafuta suluhu kutokana na yalivyokuwa yanakua, nilikuwa naona aibu sana lakini ninavyokua nimezoea”, alisema Pamella alipokuwa akihojiwa na moja ya mitandao nchini Ghana.

Mara nyingi watu wenye matiti makubwa ya size hiyo huwa wamefanya upasuai wa kuyaongeza, na mara chache sana huwa ya asili kama yalivyo ya Pamella.
Hivi sasa Pamella amekuwa akitumika sana kama 'video vixen' kwenye kazi mbali mbali za wasanii nchini humo, akiwemo rapper mkubwa kutoka Ghana Sarkodie.
“Wakiniona nimetokea kwenye video hivi nikipita tu, watu hutaka kuangalia zaidi huyu msichana mwenye matiti makubwa”, amesema Pamella.
Hivi sasa msichana huyo anasoma katika chuo cha Wisconsin kilichopo Accra Ghana akijikita kwenye masuala ya Marketing, huku akijihusisha na masuala ya uanamitindo kwenye mitandao ya kijamii, na kumfanya aingize mkwanja mrefu zaidi.
AJIUZULU UBUNGE BAADA YA KUIBA MKATE

Darij Krajcic.
Mbunge mmoja nchini Slovenia amejiuzulu baada ya kuiba mkate maarufu 'Sandwich' katika duka moja kwa madai kuwa wahudumu wa sehemu hiyo walimpuuzia.
Darij Krajcic ameviambia vyombo vya habari vya ndani kuwa alipuuzwa na wafanyakazi wa duka hilo na walikuwa wakiendelea na shughuli zao na hakujulikana kama ameiba lakini baadae baadhi ya wanachama walisisitiza arudi kulipa pesa ya mkate huo.
''Nilisimama pale kwa dakika tatu, nikitaka wanihudumie", alijitetea Mbunge huyo.
Krajcic ameomba msamaha na kusema kuwa anajutia kitendo alichokifanya, baada ya suala lake la kuiba kusambaa baada ya kuwaambia wabunge wengine wakati wa mkutano wa kamati siku ya Jumatano ambapo siku ya Alhamisi spika wa bunge hilo Brane Golubovic, alikemea vikali kitendo cha mbunge kuiba, na kusema kuwa ni kitendo kisichokubalika.
HIKI NDICHO WANACHO KIWAZA WANAUME WENGI KUHUSU KUINGIA KATIKA MAHUSIANO /NDOA NA SINGLE MOTHER
Wewe ni Single Mother ? Upo katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume ? Au unataka kuingia katika mahusiano ya kimapenzi/uchumba/ndoa na mwanaume ambae si baba wa mtoto wako?
Basi kabla ya kufanya hivyo,unatakiwa kujua kitu gani wanacho kiwaza wanaume wanao ingia katika mahusiano na single mothers.
Pia unatakiwa kuyafahamu mambo wanayo yawaza wanaume wengi kabla ya kuingia katika ndoa na single mothers.
Mahusiano mengi ya single mothers yanashindwa kufika mbali kwa sababu single mothers wengi huwa wanaingia katika mahusiano na wanaume bila kuyafanyia analysis mambo haya muhimu kabisa kwa kila single mother kuyafahamu.
AFRICANDADAZ ime kusanya maoni kutoka kwa wanaume mbalimbali kuhusu uzoefu wao na mtazamo wao kuhusu kuingia katika mahusiano ya kimapenzi au ndoa na single mothers.
Maoni haya yamechukuliwa kutoka kwa wanaume mbalimbali wa hapa Tanzania na waliopo nje ya Tanzania. Baadhi ya mambo yanayo semwa na wanaume hawa kuhusu kuingia katika mahusiano ya kimapenzi au ndoa na single mothers yanatisha na kuogopesha sana.
Ni vyema kila single mother ambae anafikiria kuingia katika mahusiano ya kimapenzi au kuingia katika ndoa na mwanaume ambae si baba wa mtoto wake ayafahamu mambo haya.
Kusoma zaidi makala haya tembelea Kwa kubofya hapo chini :
TEHAMA YARAHISISHA MCHAKATO WA AJIRA SERIKALINI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi (aliyekaa mbele) akiongoza jopo la wajumbe wa usaili lililokuwa Dar es Salaam wakiendesha usaili kwa njia ya Video kwa mwombaji kazi wa nafasi ya Meneja wa bodi.
Muonekano wa uendeshaji wa usaili kwa njia ya Video
Wajumbe wa Jopo la Usaili wakiongozwa na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Waziri Kindamba (wa pili kutoka Kushoto) wakijadili jambo
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imezidi kuboresha huduma zake kwa kuanza kuendesha usaili wa mahojiano kwa njia ya mtandao (Video Conference) baada ya usaili wa kwanza kufanyika wiki hii kwa baadhi ya nafasi za Watendaji Waandamizi ambapo mmoja wa wasailiwa alikuwa mkoani Mbeya na wajumbe wa jopo la usaili wakiwa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wajumbe wa jopo la Usaili huo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw Waziri Kindamba amesema kuwa Sekretarieti ya Ajira ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zilizoamua kufanya mageuzi katika kuhakikisha inaboresha huduma zake kwa wadau ili kuweza kuwafikia popote pale walipo kwa kutumia teknolojia katika mawasiliano.
Amebainisha kuwa hatua waliyoichukua Sekretarieti ya Ajira ni jambo la kuigwa na taasisi nyingine, kwanza kwa kuwa wabunifu, pili kuokoa muda na gharama kwa wasailiwa kusafiri na mwisho kuonyesha uzalendo kwa kutambua na kuamua kutumia miundombinu ya TTCL kuendesha usaili wake kwa waombaji kazi walioko nje ya Dar es Salaam.
Kwa upande wake Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amesema kuwa taasisi yake imejipanga kuhakikisha inasogeza huduma karibu na wadau wake ikiwemo kurahisisha mchakato wa Ajira kwa lengo la kuongeza ufanisi.
“Sekretarieti ya Ajira imeshafanya maboresho mengi tangu tulipokabidhiwa jukumu hili la kuendesha mchakato wa ajira serikalini, awali tulianza kwa kwa waombaji kazi kutuma maombi yao kwa njia ya posta na badae tukabadilisha na kuanza kupokea maombi kwa njia ya mtandao, kwa sasa tumejikita zaidi katika matumizi ya TEHAMA, kwa kuanzisha mifumo mbalimbali ili kurahisisha utendaji wa kazi na kuongeza ufanisi” amesema Daudi.
Daudi amefafanua kuwa baadhi ya mifumo hiyo kuwa ni pamoja na mfumo wa wa kuendesha usaili kwa njia ya mtandao (video conference), mfumo ya upokeaji wa maombi ya kazi (Recruitment portal), mfumo wa kupanga wasailiwa waliofaulu usaili (Placement Management Information System) na mfumo wa kutoa taarifa kwa waliopotelewa na vyeti mbalimbali vya kitaaluma (Loss report management system) wakishakamilisha taratibu.
Ameongeza kuwa nia ya Sekretarieti hiyo kuendelea kubuni mifumo inalenga kuongeza ufanisi, kupunguza muda wa kufanya mchakato wa ajira kutoka siku 90 hadi siku 52 kwa ajira mpya na kwa wale wanaohifadhiwa katika kanzidata kutumia muda wa wiki moja kwa mwajiri kupata mtumishi anayemuhitaji.
Hatua hii inalenga kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi na kupunguza malalamiko ya ucheleweshaji wa michakato ya ajira na kuondoa hisia za upendeleo kwa kuwa anayepata kazi ni yule mwenye sifa na vigezo stahili na si vinginevyo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
MAMBA NA FISI WAUA WATU SITA SENGEREMA

Mamba na fisi wamekuwa tishio kwa watu wanaozunguka Ziwa Victoria katika Halmashauri ya Buchosa, Sengerema mkoani Mwanza.
Katika mwezi huu pekee, watu wanne wameliwa na mamba hivyo kufanya idadi ya walioliwa kufikia 13 huku wengine watano wakijeruhiwa tangu mwaka 2016. Fisi wameua watu wawili na kujeruhi wengine wawili.
Kaimu ofisa ardhi na maliasili Halmashauri ya Buchosa, Aliko Ndile alisema jana kwamba hatua za haraka zinahitajika ili kunusuru maisha ya watu.
Ndile aliyataja maeneo ambayo yameathiriwa zaidi na wanyama hao kuwa ni vijiji vya Kanyaku, Kisaba, Nyambeba na Izindabo cha Kata ya Buhama kisiwani Kome Mchangani.
“Kweli hali hii inatishia uhai wa binadamu, maana watu 16 sio mchezo kuliwa na wanyama hao,” alisema Ndile.
Mwenyekiti wa makambi ya Kome Mchangani, Ntabaguzi Angelo alisema mwezi huu umekuwa wa majonzi katika eneo hilo baada ya watu wanne kupoteza maisha kwa kuliwa na mamba wakiwa wanaoga ndani ya Ziwa Victoria.
Amiri Soko ambaye alimpoteza mtoto wake aitwaye Hussen (24) alisema mwanaye alimuaga anakwenda kuoga na wenzake katika mwalo wa Chilogo saa 10 jioni lakini hakurejea na watu walionusurika ndio waliotoa taarifa za kuchukuliwa na mnyama huyo.
Mmoja wa watu walionusurika kuliwa na mamba katika eneo hilo, Amina Salumu alisema wamezoea kuoga ziwani ndio maana inakuwa rahisi kuliwa na wanyama hao.
Katika kukabiliana na tishio la mamba, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buchosa, Crispin Luanda alisema wamechimba visima 14 kwenye maeneo ambayo watu wanaliwa na kujeruhiwa na wanyama hao ili wasiende ziwani.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole alisema ili kukabiliana na janga hilo, ipo haja ya kuweka sheria ndogondogo ya zuio la watu kuoga ziwani.
Na Daniel Makaka, Mwananchi
TAASISI BINAFSI NJOMBE ZAKWEPA KUTUMIA MASHINE ZA EFD,TRA YATOA ONYO
Na Amiri kilagalila Mamlaka ya mapato TRA mkoa wa Njombe imefanya oparesheni ya dharura ya ukaguzi wa mashine za kielektronic za kukatia risiti katika taasisi za shule , Zahanati pamoja na vituo vya afya na kubaini kuwa idadi kubwa ya taasisi hizo hazitumii mashine hizo na kutoa muda wa wiki mbili kwa taasisi hizo kununua mashine hizo vinginevyo zitapigwa faini ya kuanzia mil 3 hadi 4 kwa kuisababishia hasara serikali. Akizungumza mara baada ya kukamilisha zoezi la ukaguzi wa mashine hizo meneja wa TRA mkoa wa Njombe Musib Shaban amesema…
RAIA 13 WA ETHIOPIA WANASWA WAKIWA WAMEJICHA SHAMBANI MWANZA
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia raia 13 wa Ethiopia wakiwa wamejificha kwenye shamba la mkazi mmoja wa mtaa wa Nyaburogoya Kata ya Nyegezi jijini Mwanza.Miongoni mwao, watano wamekutwa na hati za kusafiria zilizotolewa na Ethiopia zilizogongwa muhuri na Idara ya Uhamiaji ya Kenya, lakini bila kugongwa mhuri na idara hiyo nchini.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Jumanne Muliro, alisema watu hao walikamtwa Februari 13, mwaka huu asubuhi, kufuatia taarifa za kiintelijensia kutoka kwa raia wema, na kwamba walipofuatilia walikuta ni kweli kisha kuwakamata13, ambao walitambulika kuwa ni raia wa nchi hiyo.
“Tunachoendelea nacho kwa sasa ni kutaka kujua hawa watu wamefikaje hapa nchini, wamesafirije hadi kupita mpakani na ni nani mwenyeji,” alisema Kamanda Muliro na kuongeza:
“Watakapobainika wanaowapatia mbinu za kuingia nchini bila vibali watachukuliwa hatua sitahiki za kisheria, ikiwamo kufikishwa kwenye vyombo husika.”
Aidha, alisema kutokana na watu hao kutokuelewa lugha ya Kiswahili wala Kiingereza, utaratibu unafanyika wa kumtumia mkalimani ili kubaini sehemu wanayotoka na wanapokwenda.
“Tunawashikilia katika kituo kikuu cha Nyamagana, taratibu zinafanyika za kuwafikisha katika idara ya Uhamiaji kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria,” alisema.
BENKI KUU YAZINDUA MFUMO WA MALIPO YA PAPO KWA PAPO
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezindua mfumo mpya wa malipo ya fedha kwa njia ya kielektroniki utakaowezesha utumaji wa huduma za kifedha kutoka katika taasisi moja kwenda nyingine.
Pamoja na kurahisisha utumaji wa fedha, pia utaondoa urasimu na udanganyifu kwa taasisi za fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua mfumo huo, Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa wa BoT, Benard Dadi, alisema mfumo huo pamoja na kurahisisha utumaji wa fedha, pia utasaidia benki hiyo kupata taarifa za kifedha katika kila benki badala ya kusubiri kupelekewa taarifa hizo na taasisi za benki.
Kwa mujibu wa Dadi, pia utasaidia kuonyesha kiwango cha mapato ambacho serikali inapaswa kupata kupitia taasisi za fedha.
Kadhalika, alisema pia utapunguza matumizi ya fedha taslimu na kuondoa usumbufu ambao umekuwa ukitokea wa kukosea taarifa za kifedha ikiwamo majina na taarifa nyingine muhimu.
“Mfumo huo utasaidia kuonyesha kila muamala unaofanyika katika kila kampuni nyingine, kwa hiyo kutusaidia kujua miamala ni mingapi kwa siku, kwa mwezi, kwa mwaka, kuleta udhibiti ndani ya BoT, badala ya kwenda kwenye kampuni kwenda kuomba taarifa, hizo taarifa tutakuwa nazo, tutajua serikali inapata ushuru kwa kiasi gani kwa usahihi zaidi bila kutegemea mpaka ifike mwisho wa mwezi ndio tupewe taarifa kujua serikali imepata ushuru kiasi gani,” alisema Dadi na kuongeza:
“Vyote hivyo vitarahisishwa sana kupitia mfumo huu na kufanyika miamala utakuwa unachukua muda mfupi ndani ya sekunde mbili au tatu kumfikia mteja na pia itasaidia kupunguza gharama. Mfumo huu unajengwa ndani ya miezi 18 na utatumia wataalamu kutoka BoT,” alisema Dadi.
Sosteness Kewe, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), alisema mfumo huo mpya utakuwa na manufaa makubwa kwenye uchumi wa nchi, wananchi wa kawaida, wafanyabiashara na wakulima kwa sababu utakapoanza kufanya kazi utasaidia kupunguza gharama za utumaji wa fedha pamoja na kutoa taarifa za watu wote wanaotumia huduma za kifedha.
Alisema taarifa hizo pia zitasaidia taasisi za fedha kuongeza ufanisi namna ya kuboresha huduma kwa wateja.
“Tunajua wengi tunatumia mfumo wa fedha taslimu ambao ni gharama kubwa, lakini mfumo huu wa kutuma pesa kwa haraka utaepusha mengi, kwa mfumo wa sasa unatakiwa uende benki ukachukue pesa au umtume mtu au umtume boda boda, lakini kwa mfumo huu ambao BoT umezindua utarahisisha miamala mbalimbali kulipa au kupokea pesa kiurahisi hasa wafanyabiashara, wakulima kufanya miamala kwa urahisi zaidi, hawatakuwa na haja ya kulipa fedha taslimu,”alisema Kewe.




