Monday, 28 January 2019

MAMA ACHINJA MWANAE AKIGOMBANA NA MUMEWE SABABU YA MCHEPUKO

Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Cecilia Paschal mkazi wa Kisimani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara anadaiwa kumuua mtoto wake mdogo mwenye umri wa miezi sita baada ya kuibuka ugomvi kati yake na mumewe uliosababishwa na wivu wa mapenzi.

Inadaiwa kuwa Cecilia alitekeleza tukio hilo la kumchinja mwanaye kwa kisu na kitu kinachodhaniwa kuwa ni kisu, kisha kutaka kujiua mwenyewe kwa kumeza dawa za aina mbalimbali.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa polisi Mkoa wa manyara, Augustino Senga alipozungumza na waandishi wa habari amesema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 20, majira ya saa 12 jioni.

“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi kwa sababu kabla ya tukio, inaelezwa alikuta namba ya simu ya mwanamke katika simu ya mumewe, baada ya kuona namba ya simu ya mwanamke huyo ikitumika kuwasiliana na mumewe kila wakati, Januari 19, ndipo ukatokea ugomvi kati yao,’ alisema Kamanda Senga.

Kwa mujibu wa Kamanda Senga, mume wa Cecilia aliamua kuondoka nyumbani mpaka alipojulishwa madai ya mwanaye kuchinjwa ndipo akarejea nyumbani. 


Alisema kuwa Mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Hai kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
Share:

WABUNGE CHADEMA WAMJIBU ASKOFU KAKOBE

Baada ya Askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship nchini Tanzania, Zachary Kakobe, kuwataka viongozi wa CHADEMA waliotoa maneno machafu kwa viongozi wa dini kutubu haraka iwezekanavyo, baadhi ya viongozi wamemjibu kwamba anapaswa kupuuzwa, yeye ndiye atakayetumbukia kwenye shimo. Wakati wa Ibada ya jana siku ya Jumapili, Askofu Kakobe alisema kwamba kuna baadhi ya viongozi wa siasa wa CHADEMA tena walioko katika baraza kuu waliwatukana viongozi wa dini kupitia mitandao ya kijamii, hivyo wasipotubu chama chao kitatumbukia kwenye shimo refu. Kupitia baadhi ya kurasa za mitandao ya kijamii ya…

Source

Share:

ASKARI WA JWTZ MATATANI KWA KUBAKA MWANAFUNZI

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kambi ya Suku Mikumi, wilayani Kilosa mkoani Morogoro, Godlisten Remngstone (46), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya mapenzi na binti wa miaka 17, mwanafunzi wa kidato cha nne.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa, alisema askari huyo alikamatwa Januari 23, mwaka huu, majira ya alasiri maeneo ya Kikwalaza, Mikumi Wilaya ya Kilosa.


Alisema kuwa askari huyo alikamatwa na wananchi na kufikishwa katika kituo cha polisi Mikumi baada ya kumwita mwanafunzi huyo na rafiki yake nyumbani kwake kwa nia ya kufanya naye mapenzi.


Katika tukio lingine Paulo Ilonga (68), anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwabaka watoto wawili wa familia moja mmoja akiwa na umri wa miaka minane na mwingine miaka tisa, wakiwa watoto wake wa kufikia.


Kamanda Mutafungwa alisema mtuhumiwa huyo aliwabaka watoto hao baada ya kuwatoa ndani walikolala na kuwapeleka nyuma ya nyumba, huku akiwatishia kuwapiga.


Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi linamshikilia Jafari Ramadhani (26), mkazi wa Kidudwe Turiani, kwa tuhuma za kumbaka mwanawe wa kumzaa mwenye umri wa miaka sita baada ya kumwita chumbani.


Tukio hilo lilitokea Januari 21, mwaka huu saa nne asubuhi katika kijiji cha Kidudwe Turiani, baada ya mama mzazi wa mtoto huyo kugundua kuwa mtoto wake amebakwa na hivyo kutoa taarifa polisi.


Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani uchunguzi na taratibu za kisheria utakapokamilika.

Credit: Nipashe
Share:

CHADEMA WATAKA ASKOFU KAKOBE APUUZWE

Baada ya Askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship nchini Tanzania, Zachary Kakobe, kuwataka viongozi wa CHADEMA waliotoa maneno machafu kwa viongozi wa dini kutubu haraka iwezekanavyo, baadhi ya viongozi wamemjibu kwamba anapaswa kupuuzwa, yeye ndiye atakayetumbukia kwenye shimo.

Wakati wa Ibada ya jana siku ya Jumapili, Askofu Kakobe alisema kwamba kuna baadhi ya viongozi wa siasa wa CHADEMA tena walioko katika baraza kuu waliwatukana viongozi wa dini kupitia mitandao ya kijamii, hivyo wasipotubu chama chao kitatumbukia kwenye shimo refu.

Kupitia baadhi ya kurasa za mitandao ya kijamii ya viongozi hao akiwepo Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa amendika kwamba, "Kama kweli Kakobe ameongea maneno haya , anapasawa kupuuzwa, yeye ndiye ametumbukia kwenye shimo, aliwahi kusema umeme hautawaka pale Serikali ilipopitisha nguzo za umeme nje ya kanisa lake, huyu, aliwahi kusema Mrema atakuwa Rais Huyu, can we trust him anymore,"?.

Ameongeza kwamba, "CHADEMA hatuombi kupendelewa na kiongozi yeyote wa dini, sisi tunataka, utu, demokrasia, utawala wa sheria, haki za binadamu, uhuru wa Mawazo, uhuru wa vyombo vya habari, tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya. Kiongozi yeyote wa Dini asiyetaka haya, amepungukiwa na utukufu wa Mungu".
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini nae amedai kuwa Waziri Hamisi Kigwangalla ndiye anayepaswa kumuomba msamaha Askofu huyo na kwamba yeye ndiye aliyewahi kumtukana.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kwamba, "ni sawa kuheshimu watumishi wa Mungu. Ni baraka zaidi watumishi wa Mungu kumheshimu Mungu kwa dhati, kwa maneno, matendo, tabia na misimamo yao juu ya haki/matendo mema. Utumishi haupimwi kwa idadi ya waumini wala nguo za kitumishi. Ndio maana imeandikwa tutuwajua kwa matendo yenu".
Share:

WATOTO 10 WAUAWA KWA KUKATWA KOROMEO,SEHEMU ZA SIRI,ULIMI NA MASIKIO


 Watoto 10 wenye umri kati ya miaka miwili hadi sita wamechinjwa na kukatwa koromeo, sehemu za siri, masikio na ulimi wilayani Njombe mwezi huu.

Kutokana na matukio hayo yanayodaiwa kuhusishwa na imani za kishirikina, mkuu wa wilaya hiyo, Ruth Msafiri ametoa amri kwa wazazi na walezi kuwapeleka na kuwafuata shule watoto wao. Pia, ameagiza watoto wote wilayani humo kuhakikisha kuwa wanatembelea kwa makundi.

Aidha, mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amesema, “Imani za ushirikina na malipizo ya visasi ndivyo vinaleta haya mambo, nimeagiza vyombo vya ulinzi na usalama hasa Jeshi la Polisi kupitia upya leseni za waganga wote wa jadi na kuwakamata wale wote wanaohusishwa kutoa maelekezo yanayosababisha vifo vya watoto na watu wazima kwa imani za kishirikina.”

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alisema taarifa alizonazo ni za matukio mawili ambayo polisi wanayafanyia kazi.

Lakini wakati Lugola akisema hayo, Msafiri alisema mtoto wa 10 aliokotwa jana akiwa amechinjwa na kunyofolewa viungo. Alisema watoto sita wamefanyiwa ukatili huo katika Halmashauri ya Mji wa Njombe na wanne wanatoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.

“(Kati ya) sita waliookotwa (wakiwa wamekufa) Halmashauri ya mji Njombe, wawili walipotea na kuokotwa wakiwa wameuawa misituni, wawili wameokotwa maeneo tofauti wakiwa wamekufa na hawakutambulika, wamezikwa na halmashauri,” alisema.

Na Herieth Makwetta na Bakari Kiango, Mwananchi 

Share:

RAIS MAGUFULI AMTEUA HAKIMU KESI YA MBOWE, MATIKO KUWA JAJI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemteua aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Dar es salaam Wilbard Mashauri kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo jana kupitia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwatangaza baadhi ya majaji wengine wa mahakama ya Rufani na mahakama kuu.

Miongoni mwa Majaji walioteuliwa ni Jaji Wilbard Mashauri ambaye ni Hakimu katika kesi inayowakabili viongozi 6 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lakini pia anasimamia kesi inamkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Jamal Malinzi.

Katika kesi ya inayomkabili Freeman Mbowe na Esther Matiko, akiwa Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri aliwafutia dhamana viongozi hao wawili kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa na Mahakama.

Kesi nyingine ambayo inasimamiwa na Wilbard Mashauri ambaye kwa sasa ni Jaji, ni kesi inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU, Godfrey Gugai ambaye anatuhumiwa kwa kutakatisha pesa pamoja na kumiliki mali ambazo haziendani na na kipato chake.
Share:

SERIKALI YAFUTA KODI YA PANGO LA ARDHI KWA TAASISI NA MADHEHEBU YA DINI

SERIKALI Imefuta kodi ya pango la ardhi kwa Taasisi na Madhehebu ya dini nchini kuanzia mwaka wa fedha wa 2018/2019.

Hatua hiyo imetangazwa jana Jumapili Januari 27, 2019 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi jijini Mbeya wakati wa ibada ya kuwaweka wakfu viongozi wa Jumuiya Kuu ya Kanisa la Kibaptisti Tanzania (BCT).

Lukuvi alisema Rais Magufuli ameiagiza wizara hiyo kutoyatoza kodi madhehebu ya dini kwa sehemu ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya kufanyia ibada.


"Rais ameagiza kuanzia Julai mosi mwaka huu wa fedha madhehebu ya dini yasilipe kodi ya ardhi kwa maeneo ambayo huduma za maombi na ibada zinatolewa, hata hivyo msamaha huu hauhusu maeneo ambayo kuna miradi ya kuingiza fedha ambayo tunajua madhehebu mengi yameanzisha," alisema Lukuvi.


Lukuvi alifafanua maagizo hayo tayari yametolewa kwa makamishna wa ardhi wa kanda na mikoa pamoja na maofisa ardhi wa majiji, manispaa na halmashauri nchi nzima.


Hata hivyo, Lukuvi ametoa nafasi ya kukutana na viongozi wa dini ambao wana migogoro ya ardhi kwenye maeneo ambayo wanatoa huduma.


"Najua kuna migogoro mingi kwenye maeneo ambayo mnatoa huduma hivyo nawakaribisha ofisini kwangu Dodoma na kama migogoro itakuwa mikubwa nitafika mpaka eneo la mgogoro," alisema Lukuvi.


“Wizara yangu imepewa jukumu la kutatua migogoro ya ardhi kabla ya mwaka 2020 na tusipotatua migogoro ya dini inaweza kupelekea uvunjifu wa amani nchini hivyo hatutaki kuifuga migogoro iliyopo,” alisema.


Awali, askofu wa kanisa la Baptisti nchini, Arnold Manase amesema kanisa lake ni moja ya madhehebu yanayoongoza kuwa na migogoro ya ardhi na baadhi ya waumini wa kanisa hilo.


"Kwa kuwa waziri mwenye dhamana upo naomba nafasi nije ofisini kwako nikueleze migogoro iliyopo ndani ya kanisa langu ili uangalie namna ya kuitatua maana migogoro imekithiri mpaka kufikia hatua ya kujenga makundi miongoni mwa waumini," alisema Manase.
Share:

HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 28,2019.

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 28, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

Sunday, 27 January 2019

Video : RAIS MAGUFULI ATUMBUA NA KUTEUA WENGINE..WAMO MAJAJI, MA DAS NA WAKUU WA WILAYA

Share:

WALIMU,WANAFUNZI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA WIZI WA MITIHANI KIDATO CHA NNE 2018

Watu18 akiwemo mkuu wa shule ya Shule ya Sekondari Tumaini Lutheran Seminary iliyopo wilayani Malinyi, Mkoa wa Morogoro, baadhi ya walimu, wasimamizi wa mitihani na baadhi ya wanafunzi wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Ulanga wakikabiliwa na makosa yanayohusu udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Willbroad Mutafungwa alibainisha hayo jana wakati akizungumzia hatua ambazo zimechukuliwa na polisi kutokana na sakata la wizi wa mitihani ya kidato cha nne 2018.

Sambamba na washitakiwa hao raia kufikishwa mahakamani, Kamanda Mutafungwa amesema pia wamemtia mbaroni askari mwenye namba G 7281 Konstebo Khamisi na kumfikisha mahakama ya kijeshi kufuatia tuhuma za kujihusisha kwake, kushiriki kwa kupanga njama na kufanya udanganyifu wa mitihani wa kidato cha nne wa shule hiyo.

Alibainisha kuwa askari huyo kulingana na kanuni za jeshi atafikishwa kwanza katika mahakama ya kijeshi ili taratibu nyingine ziweze kuchukuliwa na baada ya hapo atafikishwa mahakama ya kiraia kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kwa sasa wilaya ya Malinyi bado haina mahakama ya wilaya ambapo mashauri yake yanayohusiana na ngazi ya mahakama ya wilaya yanashughulikiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ulanga.

Hivi karibuni Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk Charles Msonde akizungumza Dodoma na waandishi wa habari wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne 2018 alisema baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali walifutiwa matokeo kutokana na kubainika kufanya udanganyifu kwa kuingia na notes ( nondo), kwenye chumba cha mtihani.

Dk Msonde amesema katika hali ya kusikitisha, uongozi wa sekondari hiyo yenye namba za usajili S0983, ulionekana kupanga mbinu za ushindi kwa kuandaaa miundombinu ya kufanya udanganyifu, jambo lililolifanya Baraza la Mitihani Tanzania kufuta matokeo ya wanafunzi 57.

Via Habarileo
Share:

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE 2018 ATEULIWA KUWA MKUU WA WILAYA


Thomas Absalom (aliyeshikilia Mwenge)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa wakuu wawili wa Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga na Mkuu wa Wilaya ya Tarime.


Nafasi ya Mkuu wa wilaya ya Mwanga, ameteuliwa Thomas Absalom na Mkuu wa Wilaya ya Tarime ameteuliwa ndugu Charles Kabeho.

Ndugu Charles Kabeho alikuwa kiongozi wa mwenge mwaka 2018 ambao ulizunguka nchi nzima kukagua na kuzindua miradi mbalimbali.

Pia Rais John Magufuli amewateua majaji 6 wa Mahakama Kuu, kuwa majaji wa Mahakama ya Rufani na mahakimu na wanasheria 15 kuwa majaji wa Mahakama Kuu.

Wateuliwa wote wataapishwa Jumanne, 29 Januari, Ikulu Jijini Dar es salaam.
Share:

KARIOBANGI SHARKS MABINGWA SPORTPESA...WAMEICHAPA BANDARI FC


Kariobangi Sharks

Klabu ya soka ya Kariobangi Sharks ya Kenya imefanikiwa kubeba ubingwa wa SportPesa baada ya kuifunga Bandari FC ya hukohuko nchini Kenya.

Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Kariobangi ilipata bao lake kupitia kwa Harrison Mwendwa katika dakika ya 61 ya mchezo, ambao mpaka unamalizika, Kariobangi Sharks imeondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bandari.

Hii ni mara ya tatu kwa timu za Kenya kushinda ubingwa huo, klabu ya Gor Mahia ikiwa imeshinda mara mbili mfululizo na Kariobangi ikishinda mara moja ambayo ni mwaka huu.

Bingwa wa michuano hiyo anajinyakulia kiasi cha Dola 30,000 huku mshindi wa pili ambaye ni Bandari FC akijinyakulia kiasi cha Dola 10,000, nafasi ya tatu ikenda kwa Simba ambayo inajinyakulia kiasi cha Dola 7,500.

Bingwa wa michuano hiyo, Kariobangi Sharks anapata nafasi ya kucheza na klabu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Uingereza EPL.
Share:

SIMBA MSHINDI WA TATU SPORTPESA..WAMEICHAPA MBAO UWANJA WA TAIFA

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba, leo wameibuka washindi wa tatu katika mchezo wa SportPesa Cup Uwanja wa Taifa kwa kushinda mbele ya Mbao kwa penalti 5-3.

Dakika 90 za mchezo huu ambao ulikuwa na kasi kwa timu zote mashabiki walishuhudia timu zikitoka suluhu na kupelekea mwamuzi kuamua ipigwe mikwaju ya penalti.

Simba walifunga penalti zote tano huku wapigaji wakiwa ni Emanuel Okwi, Pascal Wawa, Deogratius Munish, Nicholas Gyan na Clatous Chama.

Kwa upande wa Mbao waliofunga walikuwa ni Said Khamis, Vincent Philipo na Peter Mwangosi huku Rajesh Kotecha akikosa penalti ya nne.

Kwa matokeo hayo Simba wanakuwa washindi wa tatu wa mashindano ya SportPesa Cup huku Mbao wakishika nafasi ya nne.
Share:

Utafiti : WANAOCHORA TATTOO WANA MATATIZO YA AKILI..WENGI WAO NI WACHEPUKAJI

Na Hassan Daudi 
WAKATI uchoraji wa ‘tattoo’ ukizidi kujizolea umaarufu kila kukicha huku ikielezwa asilimia 40 ya vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 29 wanavutiwa na utamaduni huo, utafiti umeonyesha asilimia kubwa ya wanaochora huwa na matatizo ya afya ya akili.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Miami kwa kushirikiana na kile cha Florida, nchini Marekani ndio uliokuja na matokeo hayo mapya.

Taarifa zilizochapishwa na gazeti maarufu la mtandaoni la nchini Uingereza, Daily Mail zinaeleza utafiti huo ambao umechukua zaidi ya miaka miwili tangu ulipoanza Julai, 2016, ulihusisha watu 2,008 waliokuwa wameipamba miili yao kwa michoro.

Wasomi hao wa kutoka Miami na Florida walieleza kuwa katika watu hao 2,008, waliohojiwa asilimia 50 walisema wana michoro miwili hadi mitano, huku asilimia 18 wakisema wana sita na kuendelea.

Watu hao waliulizwa maswali kadhaa kuhusiana na afya zao na ndipo wengi walipoonekana kusumbuliwa na ugonjwa wa akili na wengine walikiri kusumbuliwa na tatizo la kukosa usingizi.

Aidha, kutokana na majibu yao kwa watafiti, ilibainika pia kuwa wengi wao walikuwa wakijihusisha na tabia zisizokubalika katika jamii, ikiwamo uvutaji sigara, unywaji pombe n.k.

Kupitia majibu ya watu hao, watafiti waligundua pia kwamba wanaopenda kuchora ‘tattoo’ huwa si waaminifu katika mahusiano yao ya kimapenzi. Kwamba wengi wao ni ‘wachepukaji’.

Utafiti huo wa Miami na Florida ni kama umegongelea nyundo ule uliowahi kufanywa na Chuo Kikuu cha Rochester Medical Center mwaka 2001, ambao ulieleza namna vijana waliochora ‘tattoo’ walivyo wepesi kuingia katika uvutaji wa sigara, kunywa pombe na kuacha shule.

“Utafiti wa mwanzo ulionesha kabisa namna ambavyo kuna uhusiano kati ya kuwa na ‘tattoo’ na kujikuta kwenye tabia za ovyo,” alisema mmoja kati ya watafiti wa Chuo Kikuu cha Miami, Dk. Karoline Mortensen.

Hata hivyo, tafiti zao hizo zinapingana na madai ya mwanasaikolojia, Heather Silvestri, aliyewahi kusema ipo michoro inayoweza kumjenga mtu kiakili inapokuwa mwilini mwake.

“Tattoo zinazohusiana na afya ya akili ni kama zile zinazokukumbusha magumu uliyopitia, zinakupa nguvu na kukufanya upambane zaidi,” alisema Silvestri.

Kwa upande wake, jopo la utafiti la vyuo vikuu vya Miami na Florida linaamini matokeo ya utafiti wake huu mpya utawaongoza wataalamu wengine wa afya kuibua maswali kwa wagonjwa wao wanaowakuta na ‘tattoos’.

Chanzo - Mtanzania
Share:

BOSI FEKI NECTA ASHTUKIWA AKIENDESHA UKAGUZI SHULENI

 
Akiwa ofisini kwake Januari 24 saa nne asubuhi, ofisa Elimu Taaluma Sekondari Mkoa wa Mara, Elisenguo Mshiu alipokea barua kutoka kwa katibu muhtasi wake iliyogongwa muhuri wenye maneno yaliyoandikwa ‘siri’.

Katibu muhtasi alimwambia mleta barua yupo nje na inatakiwa itekelezwe kwa kuwa ilielekezwa kwa ofisa elimu mkoa ambaye alikuwa nje ya ofisi kikazi. Baada ya kuipokea barua hiyo Mshiu alimpigia simu ofisa elimu mkoa kuruhusiwa kuisoma kwa ajili ya utekelezaji.

Ndani ilimtambulisha mleta barua kama naibu katibu mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Salum Athuman na anatakiwa kwenda wilayani Serengeti siku hiyo ili Januari 25 afanye ukaguzi sekondari za Serengeti Nuru na Twibhoki.

Barua hiyo ilisema ukaguzi wake ulilenga kujua kwa nini wanafunzi wa Sekondari ya Serengeti Nuru katika mtihani wa kidato cha nne 2018 wengi wamepata daraja sifuri na Twibhoki kuna walimu wengi kutoka Kenya. Hata hivyo, licha ya Mshiu kudai kuwa naibu katibu mkuu Necta aliyetajwa anamfahamu kwa sura kwa kuwa aliwahi kufanya naye kazi, hakuweza kushtuka baada ya kukutana na sura tofauti na anayoifahamu.



Bosi abanwa

Mleta barua alimbana Mshiu waondoke bila kupita popote hadi Serengeti akiahidi kuwa fedha za kujikimu njiani atampata.

Katika kuonyesha kubana matumizi, bosi huyo feki alimtaka ofisa elimu wapande bajaji kutoka mjini Musoma hadi stendi ya Bweri, na akamtaka alipe Sh3,000.

Vilevile, Mshiu aliagizwa kulipa nauli ya watu wawili ya Sh12,000 (yeye na mtu huyo) kutoka Musoma hadi Mugumu, Serengeti na baada ya kufika akatakiwa kulipia gharama za vyumba vya kulala.

Bosi huyo feki alimtaka watafute vyumba vya Sh10,000 kama njia ya kubana matumizi.

“Tulipofika Nyumba ya Kulala (Wageni ya) Buruna nililazimika kulipia vyumba viwili kila kimoja Sh15,000, (yeye) akawa namba saba mimi sita,” alisema Mshiu.

“Chakula niliona mfukoni hali mbaya, nikaagiza ugali mbogamboga na maziwa yeye akaagiza wali kuku, nikalipia.”

Vilevile, ‘bosi huyo’ aliagiza amtaarifu ofisa elimu sekondari wilayani humo, William Makunja juu ya uwepo wake na kazi iliyowapeleka. “Nilitoa taarifa na Januari 25 tulifika ofisini na kumkuta (Makunja) akijiandaa kwenda Musoma na kutukabidhi ofisa elimu sekondari taaluma, Enock Ntaksigaye akatupeleka kwa gari Nuru Sekondari.”

Aanza ‘ukaguzi’

Mkuu wa shule hiyo, Benjamin Ng’oina alisema alitaarifiwa na ofisi ya elimu sekondari Januari 24 jioni kuhusiana na ukaguzi na baada ya kukutana na ‘bosi huyo wa Necta’ alimpa ushirikiano.

Alisema baada ya kufika shuleni hapo, aliomba kufuli ili aifunge shule hiyo kwa madai kuwa walimu walichelewa kufika.

Mtu huyo alianza ‘ukaguzi’, lakini kadri muda ulivyokuwa ukienda walianza kumshtukia. “Kwanza barua yake inadai anakuja kukagua shule yetu kwa nini wanafunzi wamepata daraja sifuri, nilikataa kwa kuwa walisajiliwa wanafunzi 55, waliofanya ni 51, daraja la kwanza mmoja, la pili 10, la tatu 23 na daraja la nne 17, hakuna ziro. Nilianza kupata wasiwasi,” alisema Ng’oina.

Via Mwananchi
Share:

ANAYETUHUMIWA KUUA MKE WAKE AKUTWA CHINI YA UVUNGU WA KITANDA

Mkazi wa Busale, Zawadi Daudi (41) anayetuhumiwa kumuua mke wake, Hawa Kamwela (32), amekamatwa akiwa chini ya uvungu wa kitanda cha wazazi wake na jeshi la polisi kwa kushirikiana na raia wema.

Daudi anadaiwa kumuua mkewe baada ya kutakiwa afanye maandalizi ya kumpeleka shuleni mtoto wao, Siri Zawadi, aliyechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.


Baada ya kudaiwa kutenda mauaji hayo mapema wiki hii kwa kutumia panga, Daudi alikimbilia kusikojulikana na baada ya mwili wa marehemu kupelekwa mochwari, ndugu wa mwanaume na wa mwanamke walianza kugombania maiti na hatimaye upande wa mkewe kupewa haki ya kuuzika.


Sanke Mwakajila, mkazi wa Busale, alisema jana kuwa baada ya tukio hilo, wananchi walianza msako wa kimya kimya kujua mahala alipo mtuhumiwa na baadaye wakaenda kitongoji cha Kabale.


Alisema baada ya kufika kitongoji hicho, mahala alikozaliwa mtuhumiwa, walifika katika nyumba ya wazazi wake saa 10 usiku na baada ya kubaini kuwa amejificha katika nyumba hiyo, walipiga lamgambo (ngoma) kuwakusanya wanakijiji.


Mwakajila alisema baada ya wanakijiji kufika eneo hilo, walimwita mwenyekiti wa kijiji na diwani ili wahudhurie tendo hilo, ndipo walipoingia ndani ya nyumba na kuanza kupekua na kumkamata akiwa chini ya uvungu wa kitanda wanacholalia wazazi wake.


Aida Maonwa, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, alisema alipata mshtuko baada ya kupigiwa simu na wanakijiji wakimweleza kuwa mtuhumiwa amejificha kwenye nyumba ya wazazi wake na alipofika eneo la tukio, alikuta wamemtoa nje ndipo alipopiga simu polisi.


Alisema baada ya polisi kufika hapo alfajili ya jana, walimchukua mtuhumiwa huyo akiwa salama na sasa ametiwa mbaroni polisi wakiendelea na uchunguzi na kwamba anawapongeza wananchi kwa ushirikiano wao kwa kuwa hawakutaka kumpiga bali walitaka sheria ifanye kazi yake.


Adam Kapeta, Diwani wa Kata hiyo, alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kusema baada ya kukamatwa aliwasihi wananchi wawe watulivu na polisi walipofika walimchukua na kuondoka naye kisha wakaendelea na kuwahoji wazazi waliomhifadhi mtuhumiwa.


Baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo, alisema yeye na viongozi wengine wa kijiji na kata, wanapanga kwenda kuzungumza na wazazi wa mtuhumiwa kujua sababu ya kumficha mtoto wao ilhali wanafahamu kuwa amefanya mauaji.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, alikiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kuwapongeza wananchi kutokana na ushirikiano wao kwa jeshi la polisi na kwamba mtuhumiwa atapandishwa kizimbani baada ya uchunguzi kukamilika.
Share:

ASKOFU KAKOBE AWATAKA VIONGOZI WA CHADEMA WALIOTUKANA VIONGOZI WA DINI WATUBU


Askofu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship nchini Tanzania, Zachary Kakobe, amewataka viongozi wa CHADEMA waliotoa maneno machafu kwa viongozi wa dini kutubu haraka iwezekanavyo, la sivyo chama chao kitatumbukia shimoni.

Mchungaji Kakobe ametoa kauli hiyo leo kwenye ibada aliyokuwa akiendesha kanisani kwake Mwenge, Jijini Dar es salaam, ambapo amesema kwamba viongozi hao wanatakiwa wajue kuwa viongozi wa dini wana nguvu kuliko wanavyodhani, hivyo ni vyema wakaomba msamaha kwa walichokifanya, kwani kuwatukana viongozi wa dini ni utovu wa nidhamu ni kiburi.

"Baada ya kumalizika kwa mkutano kati ya Rais Magufuli na viongozi wa dini, kuna baadhi ya viongozi wa siasa wa CHADEMA tena walioko katika baraza kuu waliwatukana viongozi wa dini kupitia mitandao ya kijamii, wajue viongozi wa dini wana nguvu katika nchi hii kuliko wao wanavyodhani. 

Viongozi ambao wamewatukana viongozi wa dini kwenye mitandao ya kijamii wanapaswa kutubu haraka sana, wakikaidi agizo hilo chama chao kitatumbukia kwenye shimo refu ambalo hakitainuka tena, kuwatukana viongozi wa dini kwa sababu hawakuzungumza yale mliyotaka kuyasikia ni utovu wa nidhamu ni kiburi", amesema Askofu Kakobe.

Ikumbukwe kwamba wiki iliyopita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alikutana na viongozi wa dini zote Ikulu jijini Dar es salaam na kuufanya nao mazungumzo juu ya kero zinazowakabili katika maeneo yao, huku akiwaomba kuelimisha jamii na kuwa na hofu ya Mungu.

Via>>EATV
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger