Na.Amiri kilagalila Mkazi mmoja wa mtaa wa Kihesa mjini Njombe aliyefahamika kwa jina la Maria mgeni (26) amenusurika kifo mara baada ya kujaribu kujiua kwa kunywa sumu kutokana na kushindwa kuwasilisha baadhi ya michango ya wanachama inayokaribia kiasi cha shiringi laki sita Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Rashid Ngonyani,alisema kuwa binti huyo mfanyabiashara ndogo ndogo wa mboga mboga alijaribu kujiua kwa kunywa sumu ambayo bado haijajulikana pamoja na kujichana maeneo ya kitovuni na kitu chenye ncha kali. “Mnamo tarehe 25 mwezi…
Saturday, 26 January 2019
SBL YAZINDUA KAMPENI YA ‘USITUMIE KILEVI NA KUENDESHA CHOMBO CHA MOTO’
Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha, akizungumza na wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Mkadam Mkadam, akizungumza na wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Mkadam Mkadam, akizungumza na wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha,kushoto ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha na kulia ni Mrakibu wa Polisi Mwandamizi Audax Majaliwa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha(kushoto) akimshukuru Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mwanza Mkadam Mkadam alipozindua mafunzo kwa wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.
Mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha, akiwasilisha mada ya kuepuka kunywa na kuendesha kwa wadau wa usafiri jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Usinywe na Kuendesha.
**
Mwanza, Januari 25, 2019-Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kampeni inayolenga kutoa elimu kwa umma juu ya unywaji wa kistaarabu, ikiwa ni moja ya hatua muhimu inayochukuliwa na kampuni hiyo kuzuia ajali nyingi zinazosababishwa na madereva wanaoendesha wakiwa wametumia vilevi.
Kampeni hiyo inayobeba ujumbe wa, “Usitumie Kilevi na Kuendesha Chombo cha Moto’ imezinduliwa jijini Mwanza leo na ilianza na kongamano lililojadili unywaji wa kistaarabu ambalo liliwaleta pamoja wadau kama vile Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, Mamlakka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), madereva, abiria, na wadau wengine katika sekta ya usafirishaji.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika hoteli ya Gold Crest, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) mkoani Mwanza Mkaddam Hamis Mkaddam, alisema kwa kulishirikisha jeshi la Polisi kampuni ya SBL imeiunga mkono serikali katika kuelimisha umma juu ya unywaji wa kistaarabu na kusisitiza umuhimu wa kutatua tatizo hilo.
Mkaddam alisema baadhi ya watu na haswa madereva hunywa kiasi kikubwa cha pombe pasipo kujali madhara yanayoweza kusababishwa na kitendo hicho na kuonya kuwa vitendo vya aina hiyo vinaweza kusababisha ajali mbaya.
“Sote tunafahamu kuwa matumizi ya vileo yana uhusiano mkubwa na uendeshaji mmbovu ambao unaweza husababisha ajali mbaya za barabarani zenye athari kubwa kwa jamii zetu. Athari zake siyo tu zinawagusa watumiaji wa vilevi bali hata maisha ya wengine na kusababisha upotevu wa maisha na ulemavu kwa watu ambao wangeweza kuchangia uchumi wa nchi,” alisema Mkaddam.
Alisema pamoja na kusababisha vifo visivyotarajiwa na majeraha, unywaji usiokuwa wa kistaarabu una maadhara makubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwa kiasi kikubwa cha fedha kinatumika kwa ajili ya huduma, madawa na vifaa tiba kwa waathirika wa ajali za barabarani na hivyo kuwa ni mzigo kwa Serikali.
“Ajali hizi pia ni mzigo kwa vyombo vyetu vya utekelezaji wa sheria kwa kuwa maofisa wanalazimika kuzishughulikia wakati zinaweza kuzuilika ambazo zinasabishwa na madereva wanaondesha wakiwa wametumia vilevi,” Mkaddam aliongeza.
Akizungumzia namna kampeni hiyo itaisadia jamii, mkuu huyo wa usalama barabarani alisema, “sote kwa pamoja ikiwamo sisi polisi, madereva, jamii na wadau wengine tuna jumuku la kutafuta suluhisho la kumaliza tatizo la kutumia vilevi na kuendesha vyombo vya moto. Ninayo furaha kuona SBL pamoja na kwamba biashara yao ni kuuza vilevi, wameona wanawajibu wa kuhimiza unywaji wa kistarabu”.
Kampeni hii inalenga kuwafikia vijana na watu wengine na kuwaeliisha juu ya madhara ya unywaji usiokuwa wa kistaarabu huku ikiwataka kubadili tabia kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL John Wanyancha alisema kampeni ya unywaji wea kistaarabu inalenga kuielimisha jamii kuwa wanywaji wanapaswa kunywa kwa kiasi na kuhakikisha unywaji wao hauna madhara kwao na kwa watu wanaowazunguka.
“SBL imedhamiria kuungana na serikali na wadau wengine kuhakikisha kuwa jamii na haswa madereva ambao wanakunywa na kuendesha vyombo vya moto wanaelimishwa juu ya madhara ya vitendo hivyo na kutakiwa kubadilisha tabia,” alisema Wanyancha.
SHULE YASHANGAA KUSHIKA MKIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
Shule za sekondari Kwizu na Masjadi Qubah zilizo miongoni mwa 10 zilizofanya vibaya kitaifa mtihani wa kidato cha nne 2018, zimetaja sababu ya kutofaulisha vizuri, huku mkuu wa shule ya Kwizu, Peter Mngulwi akisema matokeo yamewashangaza kwa kuwa wanafunzi wao walijiandaa vizuri.
Mbali ya shule hizo, zingine zilizofanya vibaya kitaifa ni Pwani Mchangani (Kaskazini Unguja), Ukutini (Kusini Pemba), Kwediboma (Tanga), Rwemondo (Kagera), Namatula (Lindi), Kijini (Kaskazini Unguja), Komkalakala (Tanga) na Seuta (Tanga).
Wakati Masjadi Qubah na Mkwizu zikitoa ufafanuzi wa matokeo mabaya waliyoyapata, askari PC Hamisi wa Kituo cha Polisi Malinyi anashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kujihusisha na udanganyifu wa mitihani hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa aliliambia Mwananchi jana kuwa, askari huyo alishiriki kufanya udanganyifu huo wakati akisimamia mtihani katika Sekondari ya Tumaini Lutheran iliyopo wilayani humo.
Tuhuma za askari kujihusisha na udanganyifu zilitajwa pia juzi na katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde katika mkutano wake na wanahabari wakati akitangaza matokeo hayo.
Dk Msonde alisema walibaini udanganyifu uliohusisha utoboaji wa tundu katika ukuta ambapo mitihani hiyo ilikuwa ikipitishwa kwenda kwa walimu kupitia kwa wanafunzi wa kidato cha pili ili wakaifanye na kisha ilirejeshwa katika chumba cha mtihani na askari.
Katika matokeo hayo, Masjadi Qubah ndio imeshika mkia kitaifa huku Kwizu ikiwa ya tatu kutoka mkiani.
Akizungumzia matokeo hayo jana, mwalimu mkuu wa Sekondari ya Kwiuzu, Mngulwi alisema yamewachanganya na hawakuyatarajia.
“Matokeo yametuchanganya hatujui nini kimetokea. Wanafunzi walijiandaa vizuri sana na tulitarajia matokeo mazuri, nashindwa kuelewa shida ni nini. Niko kwenye state of shock (hali ya mshtuko),” alisema Mngulwi.
KIKWETE : VIONGOZI WA SERIKALI NI CHANZO CHA WAKIMBIZI
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema sababu zinazo sababisha ongezeko la wakimbizi duniani ni pamoja na viongozi wa serikali wa nchi husika.
Dkt. Kikwete ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na umoja wa Mataifa ambapo ameeleza kwamba mwaka 2018 idadi ya wakimbizi ilifika milioni 68.5 ambapo idadi hiyo ndio kubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote.
Rais Kikwete amesema kwamba baada ya vita kuu ya pili hii ndio idadi kubwa ya watu waliohama maeneo yao, wengine wakatoka nje ya nchi lakini wengine wakaishi ndani ya nchi lakini sio kwenye maeneo yale ambayo yalikuwa ni makazi yao.
"Kuna watu ndani ya nchi zao, viongozi ama wa serikali au wakati mwingine ni wa jamii, kwa sababu watu wanakimbia mateso, wakati mwingine ni uongozi, unakuwa na serikali ambayo ni katili lakini wengine ni sera za kibaguzi ndani ya nchi ambazo zinawabagua watu kama ilivyo Myanmar, wanawakana wale wenzao ambao wanateswa kwa misingi ya dini, makabila kwa hiyo hayo ndio miongoni mwa mazingira ambayo sio tatizo la kubuni, ni tatizo dhahiri" .
Hata hivyo mapema wiki hii, Baraza la wakimbizi duniani, WRC limetoa wito kufanyike mabadiliko katika mifumo ya suala la wakimbizi duniani kwa ajili ya kulinda maslahi ya watu waliolazimika kukimbia ikiwemo walio wakimbizi wa ndani na jamii zinazowahifadhi.
MATATANI KWA KUMBAKA NA KUMUWEKA KINYUMBA MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE
Mkazi wa kijiji cha Kateka, Kalambo mkoani Rukwa, Linus Mayaya (35) ametiwa matatani kwa kudaiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la nne kisha kumweka kinyumba.
Linus ameingia kwenye wakati mgumu kutokana na tuhuma hizo baada ya kumfuatilia kwa muda mrefu mwanafunzi huyo huku akimpatia fedha za chipsi na soda ili kuweka mazingira ya kumsogeza karibu ili kutimiza azma yake.
Tukio hilo la kusikitisha na kushangaza jamii, limetokea baada ya mama mzazi wa mwanafunzi huyo, kutoa taarifa polisi kutokana na mtoto wake kuachishwa masomo na kijana huyo kumweka kinyumba akimfanya mke hali akifahamu kuwa anastahili kupata haki yake ya elimu.
Oliver Edita, mama mzazi wa mtoto huyo, alisema baada ya kutomwona mwanawe kwa siku mbili, alimtafuta huku na kule kisha juzi akabaini kuwa amewekwa kinyumba na mtuhumiwa huyo.
Alisema baada ya kugundua hilo, alitoa taarifa kwa serikali ngazi ya tarafa na polisi ambao walimkamata mtuhumiwa akiwa na mwanafunzi ndani mwake.
George Kyando, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kusema jeshi lake limemnasa mtuhumiwa huyo ambaye anaendelea kuhojiwa katika kituo kikuu cha polisi wilaya na atafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika.
HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO JANUARI 26,2019.
Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 26, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.
HESLB Control Number For Employer & Beneficiary (GVT Payment)
HESLB Control Number For Employer & Beneficiary
The post HESLB Control Number For Employer & Beneficiary (GVT Payment) appeared first on Udahiliportal.com.
Necta Form Four Results 2018/19: Mpangilio wa ufaulu (Mikoa/manispaa/halmashauri)
The National Examinations Council of Tanzania (NECTA) is Government Institution which was established by the Parliamentary Act No. 21 of 1973. NECTA is responsible for the administration of all National Examinations in Tanzania.
You May Also Like
- Necta Results 2018: Waliofutiwa Matokeo- Form IV Results
- Necta Results: Shule zilizofanya vizuri & Tanzania One 2018
- NECTA Qualifying Test (QT) Results 2018/2019
- Matokeo ya kidato cha nne 2018/19 – NECTA Form four (CSEE) Results 2018/19
Necta Form Four Results 2018/19: Performance arrangements
Manispaa/Halmashauri
Mikoa
The post Necta Form Four Results 2018/19: Mpangilio wa ufaulu (Mikoa/manispaa/halmashauri) appeared first on Udahiliportal.com.
Friday, 25 January 2019
NAIBU WAZIRI WA NISHATI :KAZI YA KUSAMBAZA MIUNDOMBINU YA UMEME NI ENDELEVU, HAKUNA KIJIJI HATA KIMOJA KITAKACHORUKWA
Mkuranga,Pwani. Naibu waziri wa nishati, Mheshimiwa Subira Mgalu amewataka wananchi wa Mkuranga mkoani Pwani na kote nchini kutumia nishati ya umeme kama fursa ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii na hivyo kuboresha vipato vyao na Taifa zima kwa ujumla. Naibu waziri Mgalu,amesema hayo leo akiwa katika ziara yake wilayani humo ambapo pia amewasha umeme katika kijiji cha Oyoyo kilichopo kata ya Tengerea na kijiji cha Mbezi kilichopo wilayani Mkuranga tukio lililoshuhudiwa na wataalamu kutoka Tanesco, Rea na wananchi “Tunaendelea kusisitiza kuwa wananchi walio karibu na nguzo waunganishiwe, kwani hawawezi…
Tanzia : MUIGIZAJI WA FILAMU TANZANIA AFARIKI DUNIA
Marehemu Mama Abdul enzi za uhai wake.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifamba, amesema msiba wa muigizaji Mama Abdul ni msiba ni pigo kwenye kiwanda kizima cha filamu Tanzania na wasanii wanatakiwa kuungana kuifariji familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu.
Akiongea kwa njia ya simu Mwakifamba amesema amepokea taarifa za msiba huo akiwa safarini hivyo hajaongea na familia juu ya chanzo cha msiba huo lakini anafanya mawasiliano usiku huu ili kujua undani wake.
''Nipo safarini ndio nimefika usiku huu, kuhusu chanzo cha kifo chake bado sijawasiliana na familia lakini niwaombe tu wasanii wenzangu tuungane katika kipindi hiki kigumu cha kumhifadhi mwenzetu kisha mimi nafanya mawasiliano na familia na nitatoa taarifa rasmi'', amesema.
Kwa mujibu wa taarifa ya mapema iliyotolewa na Kamati ya Matukio Maadili na mikataba ya Chama cha waigizaji TDFAA (M) Kinondoni na Ubungo ilieleza kuwa msiba huo umetokea mchana leo nyumbani kwake Mburahati na msiba upo hapo nyumbani.
Aidha ilifananua kuwa taarifa juu ya taratibu za mazishi itatolewa baadaye baada ya kikao na familia, huku wasanii pia wakiombwa kushirikiana.
Baadhi ya wasanii walioonesha kusikitishwa na msiba huo ni pamoja na JB, Riyama Ally, Johari, Monalisa na wengine.
Mtangazaji, Zamaradi kupitia ukurasa wake wa Instagramu ameandika "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa SALOME NONGE maarufu kama MAMA ABDUL."
"Kwa wasiomfahamu kama uliwahi kuangalia filamu ya KIGODORO 'kantangaze' nilibahatika kufanya nae kazi enzi za uhai wake, lakini pia kwa ambao hawajabahatika kuona filamu hiyo unaweza kumuona kupitia tamthilia ya MWANTUM kwenye stesheni ya Magic Swahili DSTV," aliandika Zamaradi huku akimalizia hiv; MUNGU amuweke mahala pema peponi Mama Abdul' Inalillahi wainailaihi Rajiun'
Kwa upande wake mama yake mzazi Monalisa ambaye anajulikana kama Natasha Mamvi ameandika TANZIA;RAFIKI YANGU KIPENZI.MZAZI MWENZANGU.MWIGIZAJI MWENZANGU SALOME NONGE (MAMA ABDUL) AMEFARIKI. NI PENGO AMBALO HALITAZIBIKA KAMWE.RIP MAMA ABDUL.
Naye Monalisa ameandika," Mama Abdul Jamani, Pumzika kwa amani tutakukumbuka daima."
Joti naye ameandika R.I.P Mama Abdull.Mimi mwanao Sina cha kuongea zaidi ya kukuombea upate mwanga wa milele, Pumzika kwa amani mama."
Kuwa Mjanja..Download App mpya ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari za michezo moja kwa moja Kwenye Simu yako
MUIGIZAJI MAARUFU MAMA ABDUL AFARIKI DUNIA MASTAA BONGO WAONYESHA MASIKITIKO
Msanii wa Maigizo, Salome Nonge (Mama Abdul) amefariki dunia. Mama Abdul alishawahi kuigiza filamu ya KIGODORO ‘kantangaze’ iliyoandaliwa na Zamaradi Mketema. Mtangazaji, Zamaradi kupitia ukurasa wake wa Instagramu ameandika “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa SALOME NONGE maarufu kama MAMA ABDUL.” “Kwa wasiomfahamu kama uliwahi kuangalia filamu ya KIGODORO ‘kantangaze’ nilibahatika kufanya nae kazi enzi za uhai wake, lakini pia kwa ambao hawajabahatika kuona filamu hiyo unaweza kumuona kupitia tamthilia ya MWANTUM kwenye stesheni ya Magic Swahili DSTV,” aliandika Zamaradi huku akimalizia hiv; MUNGU amuweke mahala pema peponi Mama…
K SHARKS BALAA...WAICHAPA MBAO FC
Wawakilishi pekee wa timu kutoka Tanzania ambao wamebaki hatua ya nusu fainali kwa sasa ni Mbao wamecheza na K Sharks hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa Cup.
Dakika 90 zinakamilika kwa timu zote mbili kumaliza bila kufungana hali inayopelekea kumtafuta mshindi kwa mikwaju mitano mitano ya penalti.
Mbao FC 5 - K Sharks 6