Monday, 21 January 2019

Waziri Ummy Mwalimu ataka waganga Wakuu Hospitali za Serikali kuwa wabunifu.....Akagua ujenzi wa kitengo cha watoto JKCI

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  imewekeza kiasi cha Sh1.2 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa kitengo cha watoto katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Kujengwa kwa kitengo hicho kutaiwezesha JKCI kuwafanyia upasuaji wa kufungua vifua watoto 40 kwa mwezi kutoka 20 wa hapo awali pamoja na vyumba vinne vya madaktari wa kuona wagonjwa watoto wanaougua maradhi hayo kutoka kimoja cha awali.

Akizungumza baada ya ukaguzi wa kitengo hicho jana Jumapili Januari 20, 2019 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema Rais Magufuli tayari ameidhinisha Sh500 milioni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo ifikapo Januari 28, 2019.

Alisema kitengo hicho kinachotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu, kimegharimu Sh2 bilioni ambazo fedha nyingine Sh800 milioni zimetolewa na wafadhili Charity Baptism.

“Serikali awali iliweka Sh700 milioni na wiki hii mheshimiwa Rais ametoa Sh500 milioni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi ili watoto wahamie katika jengo hili,” alisema Waziri Ummy.

Ummy alisema mwaka 2018 JKCI ilifanya operesheni nyingi zaidi kwa watoto hivyo anategemea mwaka huu zitaongezeka zaidi, “Hii itakuwa wodi ya kwanza kwa ajili ya watoto pekee kwa Afrika Mashariki walio wengi wanachanganya watoto na wakubwa.”

Katika hatua nyingine, Waziri Ummy amewaagiza waganga wakuu na wakurugenzi wote wa hospitali za Serikali nchini kuwa wabunifu katika kutatua changamoto katika maeneo yao ya kazi kama anavyofanya Mkurugenzi wa Taasisi ya Moya ya Jakaya Kikwete(JKCI),Profesa Mohamed Janabi.
 
Ummy Mwalimu alisema Profesa Janabi amekuwa akifanya kazi kubwa kutafuta wafadhili mbalimbali wa kuiwezesha taasisi hiyo, kupata miundombinu, Vifaa tiba pamoja na wataalam kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kutoa huduma ya kitabibu na kutoa mafunzo pia kwa madaktari na wauguzi wa taasisi hiyo.

 
Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji JKCI, Profesa Mohamed Janabi aLIsema kitengo hicho kipya kilichoanzishwa pembeni mwa jengo hilo kitakuwa na vitanda 32 kutoka 11 vya awali.

“Watoto walikuwa na vitanda 11 pekee lakini kwa sasa tutakuwa navyo 32 na vitanda vya ICU vitakuwa 15,” alisema Profesa Janabi.


from MPEKUZI http://bit.ly/2FN6PBw
via Malunde
Share:

Waziri Wa Maji Prof. Mbarawa Aongoza Zoezi La Kuotesha Miti 600 Mji Wa Serikali, Ihumwa Dodoma

Watumishi wa Wizara ya Maji wamepanda miti katika eneo la Ihumwa kwenye mji wa serikali zoezi lililoongozwa na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa.

Jumla ya miti 600 imepandwa na watumishi wa Wizara pamoja na viongozi akiwemo Katibu Mkuu Profesa Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Emmanuel Kalobelo, Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo.

Profesa Mbarawa ameelekeza teknolojia ya kisasa ya umwagiliaji itumike ili miti yote ilipandwa ikue. Amesema kuwa zipo teknolojia mbali mbali za umwagiliaji ambazo wataalamu wetu wanatakiwa kuzijua na kuzitumia.

Zoezi la upandaji miti kwenye kiwanja cha Wizara liliwahusisha wataalamu wa misitu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambayo imetoa miti hiyo ikiwa ni kampeni ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa kijani.

Awali, Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Kalobelo alisema kuwa, tayari Wizara ya Maji ina kisima kitakachotumika katika umwagiliaji wa miti na bustani za wizara hivyo miti iliyopandwa itatunzwa kama inavyotakiwa.
 
Jumla ya watumishi 300 walishiriki zoezi la upandaji miti katika mji wa Serikali - Ihumwa kwenye kiwanja cha Wizara.


from MPEKUZI http://bit.ly/2MnSaht
via Malunde
Share:

TADB, NFRA Wawahakikishia Wakulima Soko la Mahindi

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), kwa kushirikiana na Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula (NFRA), wameingia makubaliano kuongeza thamani ya mnyororo wa thamani wa zao la mahindi kwa kuhakikisha wakulima wa zao hilo wanapata soko la uhakika ili waweze kunufaika na kilimo.

Akizungumza baada ya kumaliza kikao cha pamoja, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine, alisema wamekubaliana na NFRA kuhakikisha zao la mahindi linapata soko, jambo litakalompa uhakika mkulima kuendelea na kilimo cha zao hilo.

“TADB ilishatoa zaidi ya Sh. bilioni 3.4 kwa vikundi 22 vya wakulima katika kufanya kilimo cha kisasa cha zao la mahindi, hivyo kupitia kikao hiki tunawahakikishia wakulima wa mahindi soko la uhakika,” alisema Justine.

Alisema kwa msimu wa kilimo uliopita soko la zao la mahindi liliyumba, hivyo kupitia mazungumzo kati ya TADB na NFRA yataibua matumaini kwa wakulima wengi wa mahindi kwa kupata soko la bidhaa hiyo ambayo bei yake ilishuka kutokana na uzalishaji kuongezeka tofauti na mahitaji ya nchi.

“Pamoja na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kununua zaidi ya tani 36,000 za mahindi bado shehena nyingi za mahindi zipo kwa wakulima, hivyo kama wadau wa sekta ya kilimo ni wajibu wetu kuhakikisha shehena hizo zinapata soko,” alisema.

Justine alisisitiza kuwa ili kumfanya mkulima kuendelea na kilimo cha zao hilo ni lazima ahakikishiwe soko la bidhaa yake itakayompa hamasa ya kulima kwa tija ili aweze kupata mavuno kwa wingi na tija inayotakiwa sokoni.

“TADB itaanda mkakati wa pamoja na NFRA utakaoleta mabadiliko makubwa katika mnyororo wa thamani wa zao la mahindi nchini, hii ni kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika msimu wa kilimo uliopita ulifanya zao la mahindi kushuka thamani,” alisema Justine.
 
Kwa upande wake Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Vumilia Zikankuba, alisema wamefanya mazungumzo mazuri na TADB ambayo yatawasaidia kama wakala katika kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha zao la mahindi linapata soko.


from MPEKUZI http://bit.ly/2HoReKP
via Malunde
Share:

KCMC Yasitisha Kutoa Huduma ya Bima Kwa Makampuni Haya

Hospitali  ya Rufaa ya KCMC iliyopo mkoani Kilimanjaro imesitisha kutoa huduma kwa wafanyakazi wa makampuni saba yanayotumia bima za afya kutokana makapuni hayo kudaiwa zaidi ya shilingi bilioni 2.2.
 
Kwa mujibu wa Ofisa Habari na Mahusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo, hospitali hiyo imelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya makampuni hayo kushindwa kulipa madeni yake  yanayokadiliwa kufikia Sh. Bilioni 2.2.
 
Chisseo ameyataja Makampuni hayo kuwa  ni NSSF, AAR, Jubilee, Strategies, Ngorongoro, TPC na TANESCO ambapo amesema  baadhi yake yanadaiwa fedha za tangu mwaka 2016.
 
“Tuna mkataba na hizi taasisi, ule mkataba unaonyesha baada ya mwezi mmoja wawe wametulipa baada ya kutoa huduma kwa wanufaika wao, hadi sasa tuna madai ya tangu mwaka 2016 mpaka sasa.
 
“Kwa hiyo kwetu sisi tunapata mzigo mkubwa na wakumbuke
tumekuwa tuna jukumu la kutibu watanzania ambao hawana uwezo kupitia hiki hiki kiasi kidogo ambacho wananchi wamekuwa wanachangia,” alisema Chiseo.
 
Alisema uongozi wa hospitali umeshatoa taarifa kwa njia mbalimbali, hivyo ni wajibu wa wanufaika hao kwenda moja kwa moja katika taasisi na mashirika hayo kuwaeleza namna ambavyo wataweza kuhudumiwa baada ya huduma kusitishwa.


from MPEKUZI http://bit.ly/2T4Y0a1
via Malunde
Share:

CAG Kikaangoni Leo....Atua Dodoma Tayari Kwa Kuhojiwa na Kamati ya Bunge

LEO  macho na masikio ya Watanzania yatakuwa Jijini Dodoma ili kujua nini kitajiri katika mahojiano ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad  na Kamati ya Maadili ya Bunge.
 
Assad anafika mbele ya Kamati hiyo ya Bunge kutokana na wito uliotolewa na Spika wa Bunge Job Ndugai  January 7, mwaka huu kumtaka afike mwenyewe leo January 21 la sivyo Bunge linaweza kumfikisha mbele ya Kamati hiyo kwa pingu kuonesha kuwa wao sio dhaifu kama inavyodaiwa.
 
Aidha, mbali na CAG lakini pia Mbunge wa Kawe Halima Mdee (CHADEMA) naye ametakiwa kufika mbele ya Kamati hiyo kesho ili kuhojiwa pia kutokana na kile kilichodaiwa kuwa alinukuu maneno ya CAG. 

Chimbuko la sakata hilo ni mahojiano ya hivi karibuni wakati mkaguzi huo wa Hesabu za Serikali, alipokuwa akihojiwa na Mwandishi wa habari wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa (UN), Arnold Kayanda.
 
Kayanda alimuuliza CAG kuwa Ofisi yake imekuwa ikijitahidi kila mwaka kufanya ukaguzi na kutoa ripoti zenye kuonyesha kuna ubadhirifu lakini baada ya hapo wananchi hawaoni kinachoendelea.
 
CAG alijibu:”Hilo ni jambo ambalo kimsingi ni kazi ya Bunge. Kama tunatoa ripoti zinazoonyesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi, huo kwangu ni udhaifu wa Bunge. Bunge linatakiwa kusimamia na kuhakikisha pale panapoonekana kuna matatizo basi hatua zinachukuliwa.


“Sisi kazi yetu ni kutoa ripoti. Na huu udhaifu nafi kiri ni jambo lenye kusikitisha. Lakini ni jambo ambalo muda si mrefu huenda litarekebishika. Ni tatizo kubwa ambalo tunahisi Bunge linashindwa kufanya kazi yake kama inavyotakiwa.”
 
“Sitaki kuwa labda nasema hili kwa sababu linahusisha watu fulani, lakini ninachotaka kusema ni kuwa Bunge likifanya kazi yake vizuri, hata huu udhaifu unaoonekana utapungua.”alisema
 
Kauli hiyo ndiyo iliyomuibua Spika Ndugai na kumtaka CAG Assad kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Bunge ili ahojiwe kuhusu kauli hiyo ambapo Spika alidai imelidhalilisha Bunge lake.
 
Hatua ya Bunge kumwita Profesa Assad kumhoji, iliibua mjadala mkubwa kwa madai kuwa Spika hana mamlaka ya kumwita CAG na kutaka ahojiwe. 

Mvutano huo ndio uliomfanya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) aandike barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA) Ma-CAG na Maspika wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), akiwataka waingilie kati sakata la Spika Ndugai na CAG Assad.
 
Zitto pia aliamua kufungua kesi mahakamani akishirikiana na wabunge wenzake wanne, wakiomba tafsiri ya Mahakama juu ya mamlaka ya Spika kwa CAG.
 
Hata hivyo, mwishoni mwa wiki iliyopita CAG Prof Assad alivunja ukimya kwa kusema kwamba yuko tayari kwenda kuhojiwa na Kamati ya Bunge kuitikia wito wa Spika.
 
Profesa Assad pia alisema neno ‘Udhaifu’ alililolitumia kulieleza Bunge, ni lugha ya kawaida sana katika taaluma yao ya ukaguzi.

“Ni wazi kuwa watu wengine wanaweza kuchukua tafsiri tofauti ya maneno kama haya. Yametokea malumbano makali na marefu katika nyanja zote za mawasiliano kuhusu rai, nafasi na maamuzi mbalimbali yaliyochukuliwa na viongozi.
 
“Januari 15, nilipokea wito wa kisheria ulionitaka kutokea mbele ya kamati ya Bunge tarehe 21 Januari mwaka huu, kwa mantiki ya kudumisha mahusiano mazuri kati ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali na Bunge, ninayo
nia ya kuitikia wito huo hapo tarehe 21” alisema.
 
Pia wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walikaa kwenye Kamati ya Wabunge wa CCM(Caucus) kulijadili jambo hilo na kwa umoja wao walimpongeza Spika Ndugai kwa uamuzi huo huku wakidai kwamba Zitto anataka kuigawa nchi.


from MPEKUZI http://bit.ly/2CybhRn
via Malunde
Share:

Rais Magufuli Ampongeza Felix Tshisekedi Kwa Kutangazwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC

Baada ya Mahakama Kuu ya Kikatiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kumtangaza Kiongozi wa upinzani, Bw. Felix Tshisekedi kuwa mshindi wa uchaguzi wa Urais, Rais John Magufuli amempongeza Rais huyo mteule na kumuahidi kuendeleza ushirikiano.

Rais Magufuli ametoa pongezi hizo  Januari 20, ambapo mbali na kumpongeza Rais Mteule amewapongeza pia raia wa Kongo akiwataka kuduisha  amani.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Magufuli ameandika, "Kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu ya Katiba. Ninampongeza Felix Tshisekedi juu ya uchaguzi wake kama Rais wa DRC.

"Ninapongeza pia Wakongo wote, ninawasihi kudumisha amani . Ninaahidi kuendeleza uhusiano wetu wa kihistoria na wa kindugu".

Katika uchaguzi huo uliofanyika Desemba 30 2018, Mgombea Martin Fayulu alidai kuwa ndiye mshindi wa kiti hicho cha Urais, amezitaka Jumuiya za kimataifa kutomtambua Tshisekedi, akidai kuwa yeye ndiye mshindi halali wa uchaguzi huo.


from MPEKUZI http://bit.ly/2W8TI3A
via Malunde
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya January 21


















from MPEKUZI http://bit.ly/2HoXNxb
via Malunde
Share:

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 20, 2019

Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Januari 21, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.

Source

Share:

Sunday, 20 January 2019

MIEZI MITATU MICHUNGU KWA TAKUKURU NJOMBE SASA IMEKWISHA.

Na Amiri kilagalila Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Njombe imefanikiwa kufuatilia na kukagua miradi mikubwa mitano ya maendeleo ukiwemo mradi wa maji wa Lugenge wenye thamani ya Tshs 3,642,817 355 bilioni. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe Charles Mulebya Alisema Kuwa Takukuru mkoa ndani ya kipindi cha miezi mitatu ya Octoba hadi Disemba 2018 waliweza kufuatilia na kukagua miradi mikubwa mitano ya maendeleo kwa lengo la kuhakiki ubora na thamani ya fedha za umma. Mulebya alisema licha…

Source

Share:

LISSU ATUHUMIWA JUU YA MBOWE KUTESEKA MAGEREZA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, amedai kushangazwa na kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kutumia nafasi yake ya Ustaafu wa Urais wa Chama cha Wanasheria kuwashawishi mawakili wajitoee katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Katika waraka aliouandika kupitia ukurasa wake wa Instagram, Paul Makonda amedai kwamba alitegemea baada ya Lissu kupona angerejea nchini ili kumsaidia Mbowe katika kesi na siyo kufanya ziara katika nchi za Ulaya kama afanyavyo sasa.

"Tulitegemea wewe kama Mwanasheria ungekuwa umerejea nchini na kumsaidia mbowe lakini uroho wa madaraka umekufanya kutumia matatizo yake kujiimarisha kisiasa na kutafuta uraisi", ameandika Makonda.

Makonda ameongeza kwamba, "Mbaya zaidi unajua Mwenyekiti wa chama ambaye kimsingi ndiye aliyekupigania kutafuta fedha, kukaa na wewe Nairobi na kuja mpaka Ubeligiji umeamua kumwacha ateseke na kutumia nafasi yako ya Urais ustaafu wa TLS kuwashawishi Mawakili wajitoe ili aendelee kuteseka huku wewe ukitumia fursa hii kutafuta uraisi. Hauangaiki wala hata haufikirii kwamba ni wakati muafaka kurudi kuja kumpa moyo kama ambavyo alifanya yeye. Kweli hayo ndio malipo unayompa Mbowe kwa kukuangaikia wewe upate matibabu bora".

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki amenza ziara yake katika nchi za Ulaya ambapo amesema ataeleza kile ambacho kilichomtokea Septemba 07,2017 maeneo ya nyumbani kwake area D kwa kupigwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana alipokuwa akitoka kwenye vikao vya bunge.

Hivi karibuni Lissu alipokuwa akizungumza na Shirika la Utangazaji la BBC, alisema endapo chama chake kitampa baraka ya kuwania nafasi ya urais 2020 yeye yupo tayari.
Share:

MAGUFULI AWAPONGEZA UPINZANI, AWAPA AHADI YA KUENDELEZA USHIRIKIANO

Baada ya Mahakama Kuu ya Kikatiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kumtangaza Kiongozi wa upinzani, Bw. Felix Tshisekedi kuwa mshindi wa uchaguzi wa Urais, Rais John Magufuli amempongeza Rais huyo mteule na kumuahidi kuendeleza ushirikiano.

Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo Januari 20, ambapo mbali na kumpongeza Rais Mteule amewapongeza pia raia wa Kongo akiwataka kuduisha amani.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Magufuli ameandika, "Kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu ya Katiba. Ninampongeza Felix Tshisekedi juu ya uchaguzi wake kama Rais wa DRC.

"Ninapongeza pia Wakongo wote, ninawasihi kudumisha amani . Ninaahidi kuendeleza uhusiano wetu wa kihistoria na wa kindugu" Rais Magufuli.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Desemba 30 2018, Mgombea Martin Fayulu alidai kuwa ndiye mshindi wa kiti hicho cha Urais, amezitaka Jumuiya za kimataifa kutomtambua Tshisekedi, akidai kuwa yeye ndiye mshindi halali wa uchaguzi huo.
Share:

RAIS MAGUFULI AMPA NYUMBA SHILOLE

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni mjasiriamali wa chakula, Zuwena Mohamed 'Shilole' amefunguka kuwa Rais Magufuli amechangia kukamilisha ujenzi wa nyumba yake.
Shilole amesema kuwa moja kati ya pesa alizopata na kuziwekeza katika ujenzi wa nyumba hiyo, zilitokana na kampeni za urais mwaka 2015 wakati wakimnadi mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM), ambaye ndiye rais wa sasa Dkt. John Magufuli.

"Nyumba yangu imejengwa na muziki pamoja na kampeni za kumnadi Rais Magufuli, maana tulikuwa tunalipwa na tulilipwa pesa nyingi ndipo niliamua kuwekeza kwenye nyumba yangu", amesema Shilole.

Shilole ameongeza kuwa, "Mimi ni mnyamwezi nimetoka Tabora kuja mjini kutafuta sijaja kuangalia maghorofa ya Dar, nilivyopata ile hela tu nikasema naenda kununua kiwanja moja kwa moja lakini wapo walionunua magari".

Shilole ni miongoni mwa wasanii wa kike waliofanikiwa kumiliki mjengo na kuuonesha kwenye ukurasa wake wa 'Instagram' mwaka uliopita, ambapo amesema kuwa mjengo huo aliujenga kidogo kidogo na unapatikana maeneo ya Majohe, Gongo la mboto jijini Dar es salaam.
Chanzo : Eatv
Share:

DKT SHEIN AWATAKA WAHITIMU WA CHUO KUTUMIA UJUZI WAO KUJIAJIRI

RAIS wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe.Dk Ali Mohamed Shein amewataka wahitimu wa Chuo cha Abdul Rahman Al Sumait kutumia ujuzi walioupata chuoni hapo kwa kujiajiri wenyewe bila ya kusubiri ajira kutoka Serikalini. Akisoma hotuba kwa niaba yake huko Chukwani, katika mahafali ya 18 ya chuo hicho, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma amesema tatizo la upungufu wa ajira si la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pekee bali ni kilio cha dunia nzima. Aidha Dk. Shein ameupongeza uongozi wa chuo cha Alsumait…

Source

Share:

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 198 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  
             
“Tuondoke”        
Jojo alizungumza huku akitangulia kutoka nje, hapakuwa na msichana hata mmoja aliye jaribu kumshika wala kumsogelea Jojo. Tukapandisha juu kabisa ya meli hii.

“Ninahitaji twende nyumbani sasa baba”
Jojo baada ya kuzungumza hivyo akanikumbatia kwa nguvu kisha tukajitosa kwenye bahari na nikajikuta nikianza kupiga kelele kwani kasi tunayo kwenda nayo chini kusema kweli inatisha na kuogopesa na ukitegema ni usiku  basi ujasiri ukaniisha kabisa.

ENDELEA
Tukazama ndani ya maji cha kushangaza sipati tabu ya aina yoyote kama binadamu wa kawaida akizama chini ya maji. Tukazidi kwenda chini sana hadi kwa mbali nikaanza kuona taa nyingi zinzo waka kwa haraka haraka unaweza kuzifananisha na jiji la New York nchini Marekani pale ifikapo majira ya usiku. Nikatamani kuzungumza kitu ila nikashindwa kabisa na kusahau hata kitu hicho ninacho hitaji kukuzungumza.

Tukafika hadi kwenye moja ya jumba la kifahari ambalo kuta zake zimejengwa kwa dhahabu tupu, hakuna sehemu ya jumba hili iliyo sakafiwa hata kwa saruji.

“karibu baba hapa ndipo kwa mama anapo ishi”
Jojo alizungumza huku akiniachia. Kusema kweli kuna mambo mengi sana dunia nilikuwa ninayasikia juu ya viumbe hivi vinavyo itwa majini ila kusema kweli leo ndio nimeamini kwamba kuna mji wa majini ambao wanaishi kama tunavyo ishi duniani. Nikiwa kama binadamu wa kawaida, lazima woga unitawale hata kama nimefanya mambo mengi maovu na ya kutisha ila huku nilipo kusema kweli ninaogopa sana.

“Usiogope baba, yangu kuwa na amani”
“Ila Jojo ninaoga”
“Hakuna anaye weza kukudhuru”
Wasichana wa huku kusema kweli ni wazuri kupindukia, wana kila aina ya sifa ambayo duniani huwezi kumkuta nayo mwanamke mmoja. 

Nilihisi kwamba Magreti ana wazidi wote ila hawa wa huku wana wazidi wote waliopo duniani. Kila tunapo pita mimi na Jojo, tunamwagiwa maua na wasichana hawa ambao wamajipanga pande mbili za barabara inayo ingia kwenye jumba hili la kifahari. 

Mlango ukafunguliwa na nikakuta ukumbi mkubwa sana na mbele kabisa kuna kiti kimoja ambacha mekaa Olvia Hitler huku pembeni yake kukiwa na wasichana wawiliw alio shika manyoya makubwa ambayo sifahamu hata ni ya mnyama gani ila wanampepea taratibu.

“Waooo karibu mume wangu”
Olvia Hitler alizungumza huku kinyanyuka kwenye kiti chake, akaanza kunifwata kwa mwendo wa taratibu huku gauni lake jeupe pee likiburuzika kwa nyuma. Tukakumbatia taratibu, marashi mazuri aliyo jipulizia Olvia Hitler kusema kweli yakanisisimua mwili mzima.

“Pole sana kwa tabu za dunia ambazo umepitia”
“Asante”
“Usiogope, hapa ndipo kwangu, karibu sana, nilimuachia maagizo Jojo wako kwamba akulete pale atakapo pata nafasi ya kukuleta hapa nyumbani”
“Nimekaribia”
Olvia Hitler akapiga kofi moja, wakaja wasichana wanne walio valia vizuri na wamependeza sana.

“Mpelekeni baba Jojo mukamuogeshe”
“Sawa malikia”
Wasichana hawa wakanishika mikono yangu na taratibu tukaondoka katika ukumbi huu, tukaingia kwenyemoja ya chumba kikubwa ambacho kina swimming pool kubwa ambayo maji yake yanafuka mvuke. 

Taratibu wakaanza kunivua koti langu la suti, wakafwatia shati, na kumalizia nguo zote za chini na nikabaki kama nilivo zaliwa. Wasichana hawa nao wakavua nguo zao na kuingia nami kwenye swimming pool hili kwa mara ya kwanza nilihisi labda maji yanaweza kuwa ya moto, ila mvuke vuke wake kusema kweli yameufanya mwili wangu kuhisi nguvu fulani ambayo katika maisha yangu sikuwahi kuihisi hii nguvu.

Taratibu wakaanza kuniogesha mwili wangu, hapakuwa na sehemu ambayo wameshindwa kuigusa, hata jogoo wangu mamemgusa kwa viganja vyao vilaini ila hapakuwa na hisia yoyote kwenye mwili mwangu. 

Wasichana hawa hawazungumzi chochote na mimi, baada ya kumaliza kuniogesha wakanitoa ndani ya swimming pool hili kisha wakanivisha vazi kubwa lililo pambwa mwa madini ya dhahabu kwenye maua mau yake. Tukarudi katika ukumbi huu, na nikapokelewa na tabasamu kubwa la Jojo na mama yake.

“Baba umebadilika kama sio wewe”
“Eti ehee”
“Ndio yaani umekuwa kama mfalme fulani hivi”
“Hahaa ila ni mfalme kwa maana mimi si malikia”
“Alafu kweli mama hapo umenena jambo la kweli”

“Inabidi mule sasa alafu nikawatembeze”
“Mukanitembeze wapi?”
“Inabidi uweze kufahamu mji huu viziri sana, pia ukaione familia yako sehemu walipo”
“Familia yangu?”

Niliuliza huku nikiwa nimejawa namshangao mkubwa sana.
“Ndio familia yako”
“Twendeni sasa hivi jamani nina hamu ya kuiona familia yangu?”
“Mmmmm acha papara baba, kula alafu tutakwenda sote watatu”
Sikua na jinsi ya kufanya zaidi ya kumsikiliza Olvia Hitler anacho kizungumza. Tukaingia katika chumba cha kupatia chakula na kuanza kupata chakula taratibu. Chakula cha huku kusema kweli ni kitamu sana na kinavutia ambacho duniani sikuwa kula. Tukamaliza kula chakula na tukaanza kutembea sehemu mbali mbali za huu mji nanikajionea mambo mengi sana ambayo kusema kweli dunia hakuna kabisa.

“Huu ndio ulimwengu, ambao hakuna binadamu anaye weza kuja pasipo ridhaa yetu”
“Ni pazuri sana”
“Kwenye huu mji wetu kuna sehemu mbili, moja ni hii ambayo unaiona ni nzuri sana na kuna nyingine ambayo ni mbaya sana. Huko ndipo jehanamu, sehemu ambayo wanadamu wakifa wale ambao ni wetu basi wanaletwa huku chini”
Olvia Hitler alizungumza huku akinitazama uosni mwangu.

“Sasa familia yangu ipo wapi?”
“Familia yako ipo huko sehemu ya pili, mtu ambaye hayupo kwenye sehemu hiyo ni mmoja tu ambaye ni mwanao wa kike, ila wengine wote wapo huku”
Nikajihisi tumbo langu kunika, ila nikajikaza.

“Huku tunapo elekea unatakiwa kuwa mkakamavu sawa Dany”
“Sawa”
Nilizungumza ila moyo wote umepoteza imani. Kufumba na kufumbua tukajikuta tukiwa ndani ya sehemu yenye giza kubwa ila mianga ya makaa ya moto inatufanya tuweze kouna watu waliomo ndani ya shimo kubwa huku miili yao wakiwa hawana nguo  hata moja. Watu wote waliomo kwenye hili eneo wanaonekana kupata maumivu makali ya moto unao waunguza. Katika kukatiza macho yangu huku na kule nikamuona mama yangu akiungua jhuku  akipiga mayowe ila hakuna anaye weza kumsaidia. Nikataka kumfwata na kumsaidia, ila Olvia Hitler akanishika mkono na kunizuia.

“Unataka kwenda wapi?”
“Kumsaidia mama yangu?”
“Huwezi kwenda, hili eneo ni la muumba wa kila kitu”
“Ina maana unataka kusema kwamba humu kunalindwa na Mungu?”
“Ndio, malaika wa Mungu wanalinda hili eneo”
“Hatuwezi kweli kuwasaidia, yaani hata kufika huku, hata Jojo mwenyewe hajawahi kufika, kwa nguvu zangu ndio mume weza kufika huku. Nikamuona mdogo wangu Diana akipata mateso makali sana huku mwilini mwake akitobolewa na funza wenye moto. Nikamuona baba yangu naye akiteseka sana huku adhabu yao yote ikiwa ni moja kwa wote. Kuna baadhi ya viongozi wa Tanzania na dunia nzima nikawaona nao wakipata adhabu kubwa.

“Mama hivi hawa si waliokuwa ni viongozi?”
“Jojo huku hakina kiongozi, mtu akifa kama ana dhambi zake, breki yake ya kwanza ni hapa. Anapata kibano kama hawa, hadi siku ambayo Mungu ataamua kuimaliza dunia”
“Mmmm hivi Olvia Dunia inaweza kuisha?”
“Sio leo wala kesho kwa maana hata sisi hatufahamu ni siku gani dunia itahukumiwa”
“Mmmmmm sasa hata sisi si tutahukumia?”
“Inategemea na itakavyo kuwa kwa maana katika hilo kusema kweli hata mimi sielewi itakuwaje”
Sikuzungumza kitu chochote zaidi ya kuwatazama wana familia yangu jinsi wanavyo pata mateso makali. Huruma ikanijaa moyoni mwangu na kujikuta nikimwahikwa na machozi usoni mwangu, Jojo na mama yake wakabaki kimya. Taratibu wakanishika mkono, kufumba na kufumbua tukatoka katika hili eneo na tukatokea katika eneo jengine kabisa ambalo limetulia sana na lina nyumba moja pamoja na miti mingi.

“Huku ni duniani au?”
“Hapana bado upo chini ya bahari”
“Hivi inakuwaje hadi munaishi kama hivi?”
“Kivipi?”
“Munaishi chini ya bahari?””
“Yote ni miujiza ya Mungu”
“Hata nyinyi muna muabudu Mungu?”
“Ilikuwa, ila si kwa sasa”

“Ilikua lini?”
“Kipindi hicho kabla haijatokea vita huko mbinguni”
“Ahaaa sawa sawa”

Tukaingia ndani ya hii nyumba, alama niliyo kutana nayo kwenye tambaa kubwa lililo ning’inizwa katika hili seble.

“Dany mume wangu unatakiwa kuweza kupata nguvu ambazo zitakusaidia kwa maisha yako yote”
“Nguvu za aina gani?”
“Hapa unapo paona ndipo anapo ishia baba yangu, ambaye hadi leo bado anahistoria kubwa kwenye dunia”
“Historia gani?”
Olvia hakunijibu chochote zaidi ya kuingia katika chumba kimoja kinacho nukia manukato mazuri sana. Sikuamini macho yangu kukutana na gaidi wa mika hiyo ya 1880’s ambaye ni Adolf Hitler ambaye hadi sasa hivi duniani hakuna mtu aliyeweza kudhibitisha kifo chake. Wapo walio seme kwamba alijitosa kwenye acid(tindikali), wapo walio sema amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha baada ya kushindwa vita ya pili ya dunia. Pasipo kuambiwa chochote, nikasalimia salamu yake ya kunyoosha mkono mmoja juu, mzee huyu akarabasamu sana na taratibu akanyanyuka kwenye kitanda alicho lala na kukaa kitako. Kwa ishara ya mkono akaniita na kuninyooshea mkono wake wa kulia, nikaushika taratibu.

“Kwa miaka mingi duniani, vizazi na vizazi nilikuwa ninatafuta mtu wa kumuachia uwezo wangu, sikumuona ila wewe sasa una uwezo huo kwani umeweza kuitingisha duani kama nilivyo itingisha mimi”

Adolf Hitler alizungumza huku akiendelea kuishika mikono yangu.

“Umeifanya dunia nzima kukujua, umewafanya waandishi wengi kukuandika kwenye vitabu ambavyo vitadumu miaka kwa miaka yote duniani. Utaelezewa kwenye kila historia ya kila kizazi kwamba alikuwepo gaidi anaye itwa Dany.”
“Kuanzia leo nitakupa jina la Hitler, utaitwa Dany Hitler, hakikisha kwamba jina hili unalikuza.”
“Sawa sawa mzee”
“Watu watakuogopa mara kumi ya wanavyo kuogopa hivi sasa. Utaishi karne kwa karne hadi pale atakapo tokea mtu mwenye uwezo wa kufanya zaidi ya kile ambacho umekifanya wewe ndipo utakapo kuwa tayari kumkabidhi nguvu hizi ninazo kupatia”
Jinsi mzee Adolf Hitler anavyo zungumza ndivyo jinsi nilivyo hisi kuna vitu vikiingia mwilini mwangu.

“Hadi leo nchi yangu ya ujerumani inaitwa ‘HE’. Ni mwanaume wa nchi zote duniani, hata Marekani yenyewe pia ni She. Hakikisha kwamba Tanzania unaifanya iwe He, iwe dume kama Ujerumani sawa”
“Sawa”
“Haijalishi utaifanya wewe mwenyewe, haijalishi ataifanya raisi yoyote ajaye. Ila hakikisha kwamba nchi yako, chimbuko lako linakuwa ni nchi kubwa sana ulimwenguni”
“Nimekuelewa mzee”
Nikahisi kitu kikubwa kikiupiga mwili wangu, nikajikuta nikinyong’onyea na kuishiwa nguvu kabisa na nikapoteza fahamu kabisa.                                                                                           ***

Nikayafumbua macho yangu na kujikuta nikiwa nimelala kitandani, pembeni yangu nikamuona Jojo akiwa amekaa huku akinitazama.

“Hei baba umeamka?”
“Yaaa nipo wapi?”
“Tumerudi duniani tayari”
“Kule nimeondokaje?”
“Tumeondoka siku nyingi sana, kwa maana sasa hivi ni miezi miwili imepita tangu tutoke kule nyumbani kwetu”
“Weeee acha kunitania”
Nilizungumza huku nikikaa kitako kitandani, mazingira ya chumba ninacho kiona kwenye macho yangu sikuwahi kuyaona kabisa.

“Jojo hapa ni wapi?”
“Nyumbani kwetu, nimetafuta nyumba nzuri nina imani kwamba utaipenda baba yangu”
Nikajitazama mikono wangua ambayo kwa kumbukumbu zangu za mwisho ninakumbuka nilishikana na mzee Adolf Hitler.

“Babu yako yupo wapi?”
“Tayari amepoteza maisha, tumemuhifadhi kule kule nyumbani kwetu”
Nikashuka kitandani na kumfanya Jojo naye kusimama, tukatoka chumbani humu na  kufika sebleni, nikalitazama hili eneo taratibu. Sikuhitaji kuishie hapa nikatoka nje na kuuona ufukwe wa bahari kwa mbali huku nyumba yetu hii ikiwa imezungumkwa na maua mengi sana.

“Jojo hapa ni wapi?”
“Tupo Tanzania kwenye visiwa vya Pemba, hapa ndipo makazi yetu yatakapo kuwepo miaka yote tutakayo ishi hapa duniani”
“Ila si hatari Jojo hili eneo?”
“Sio hatari baba, hapa tulipo hakuna binadamu wa kawaida anaye weza kufika katika hili eneo kabisa”
“Kwa nini hawawezi kufika?”
“Baba hili eneo lipo mbali sana na hakuna binadamu anaye weza kufika wao wapo huko mbali sana. Hapa tutakuwa tunafanya kazi zetu zote”
“Hivi kwa jinsi ninavyo tafutwa duniani, kweli hawatoweza kuja kunikamata hapa?”
“Hapana baba jiamini, ninamini mimi mwanao. Hapa ni salama kabisa kuliko hata kule kwenye meli ya Livna sio salama kuliko hapa”

Jojo alizungumza kwa msisitizo, tukaanza kulizunguka hili eneo, huku akinionyesha baadhi ya eneo la mazoezi alilo litengeneza.

“Baba kwa sasa una nguvu nyingi, ambazo unatakiwa kuanza kufanya mazoezi kuhakikisha kwamba unaweza kuzi contro nguvu zako na zisiweze kumdhuru mtu asiye na hatia”
“Mbona sihisi chochote”
“Ngoja?”
Jojo akanisukuma kwa haraka sana na nikajikuta nikianguka, hata kabla sijafika chini nikajihimili na kusimama haraka sana jambo ambalo si rahisi kwa hata mfanya mazoezi kufanya hivi”
“Baba una nguvu ya kuona kile ninacho kiona mimi, mambo yanayo weza kutokea miaka kwa miaka, pia unaweza kukwepa kitu chochoye kinacho kufwata kwa kasi ambayo binadamu wa kawaida hawezi kukiona.”
“Kama kitu gani?”
“Risasi ni moja wapo ya kitu ambacho unaweza kukikwepa haraka iwezekanavyo. Baba sasa huu ndio wakati wa kwenda kumtoa K2 madarakani, tummalize yeye pamoja na maadui wengine wote ambao waliweza kukuletea tabu wewe sawa”
Maneno ya Jojo yakanifanya nitabasamu kwani kwa uwezo nilio nao sasa K2 na wajinga wezake watajuta kunifahamu na watajutia ni kwa nini waliweza kuniharibia maisha ikiwemo kuwaua ndugu zao ambao nimewashuhudia wakipata mateso makubwa kuzimu, mateso ambayo K2 na wezake nao pia wanastahili kuyapata kwani ni haki yao.

  ITAENDELEA
‘Haya sasa Dany amepata uwezo mkubwa wa kufanya chochote juu ya maadui zake je kazi yale hiyo ataitendaje? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”


from MPEKUZI http://bit.ly/2QYhETf
via Malunde
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger