Tuesday, 24 June 2014
KANGA MOJA:HUYU HAPA YULE MAMA ALIEPIGWA RISASI WAKATI WAKISHIRIKI NGOMA HIZO
MAMA mzazi wa binti aliyesababisha wasichana wawili kujeruhiwa kwa
kupigwa risasi na polisi baada ya kushiriki ngoma maarufu ya Kanga Moko
iliyopigwa marufuku, huko Mwananyamala Kisiwani jijini Dar es Salaam,
amefunguka na kusema kuwa hakukuwa na sherehe yoyote nyumbani kwake siku
hiyo ya tukio.
Grace Loy (20), mkazi wa Mwananyamala Mchangani, aliyepigwa risasi katika paja la kulia wakati wa vurugu iliyotokea.
Mama huyo, Rehema Aziz alisema waliojeruhiwa walikuwa wakisherehekea
kuolewa kwa mwanaye aitwaye Aziza Aziz, ambao walikuwa ni marafiki zake
na walifanya hivyo kwa mujibu wa mila za watu wa Pwani, za kucheza na
kufurahi wakizunguka mitaani, lakini bila kufanya fujo yoyote.
KIWANDA CHA MAFUTA IRAQ CHATEKWA

Wapiganaji wa kisunni wamekuwa wakiteka miji nchini Iraq na kuwaacha maelfu bila makao
Monday, 23 June 2014
ANGALIA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA UFUNDI MWAKA 2014 ARUSHA TECHNICAL COLLEGE (ATC) ,DIT,WDMI, NA MIST
MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA MOJA ATELEKEZWA NA MAMA YAKE
VITUKO uswahilini! Mtoto wa mwenye umri
umri wa mwaka mmoja ambaye jina halikufahamika ameokolewa na Oparesheni
Fichua Maovu ya Global Publishers baada ya kudaiwa kutelekezwa kwa siku
nzima na mama yake mzazi, Mama Sofia.
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja aliyetelekezwa na mama yake
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja aliyetelekezwa na mama yakeMGIMWA ATUMIA USAFIRI WA BAISKELI KUWATEMBELEA WANANCHI WAKE,SOMA HAPA
Mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa akitumia usafiri wa Baiskeli kuwafikia
"KONDOMU" ZANASWA UKUMBI WA BUNGE,SPIKA ASHITUSHWA
Inaweza
kuonekana ni kituko cha aina yake, lakini ni kweli kimetokea kwenye
Ukumbi wa Bunge la Kaunti ya Nairobi na kuwaacha wabunge vinywa wazi.
Katika hali isiyo ya kawaida,
boksi la kondomu lilikutwa ndani ya ukumbi huo na kuwashtua wabunge wote akiwamo spika wa bunge hilo.
Mwakilishi
wa eneo la Karura, Kamau Thuo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuliona boksi
hilo na kuwashtua wabunge wengine hali iliyoibua mjadala mzito.
Kutokana
na sintofahamu hiyo Spika Alex Ole Magelo aliwataka wahudumu kufungua
boksi hilo kujua kilichomo ndani yake ndipo walipokuta kondomu.
MMUME WA FLORA MBASHA:MWAKA WA MAJANGA KWANGU NIMETAPELIWA HATI YA NYUMBA NA VIWANJA
MAJANGA! Siku
chache baada ya kuachiwa kwa dhamana katika kesi ya kudaiwa kumbaka
shemejiye, mwimbaji wa Injili na mfanyabiashara Bongo, Emmanuel Mbasha
amedaiwa kuibiwa hati za nyumba na viwanja.
Mfanyabiashara Bongo, Emmanuel Mbasha mume wa Flora Mbasha.





