Friday, 28 April 2023

CPB YATANGAZA FURSA KWA WADAU WA MAZAO

...



Baadhi ya wadau waliokusanyika katika kikao cha wadau wa mazao na CPB kilichofanyika Iringa janaa.
Mkurugenzi wa Biashara na Masoko  wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB)  Evans Mwaning'go akiongea na wadau wa mazao katika kikao kilichofanyika Jana Iringa

Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ( CPB)  Salum Awadh akiongea na wadau wa mazao
 katika kikao cha wadau na CPB kilichofanyika Iringa jana.

Na Mwandishi wetu, Malunde I Blog-IRINGA.

MWENYEKITI wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Salum Awadh ametangaza fursa mbalimbali zinazotolewa na CPB kwa wakulima na wafanyabiashara wa Mazao hapa nchini.

Ametaja baadhi ya fursa zinazotolewa na CPB ni pamoja kilimo cha mkataba ambacho kitaanzia na hekali 1000 na kuendelea.

Akizungumza katika kikao cha wadau kilichofanyika leo Iringa Awadh alisema Kilimo cha mkataba CPB kitakuwa na uwezo mkubwa kutoa maelekezo na ufuatiliaji kwa urahisi.

" Kilimo cha mkataba kitasaidia kuwa na uhakika wa wakulima watakaotuletea mazao, yatakuwa katika ubora"' alisema Awadh.

Mwenyekiti huyo amesema fursa zingine ni pamoja na kuhitaji Mawakala ambao wataingia nao mkataba kwaajili ya uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa CPB na kununua mazao kutoka kwa wakulima na wafanyabishara.

Awadh amesema CPB ni Shirika la Kibiashara la Serikali hivyo linafanya biashara kwa lengo la kuinua Uchumi wa Nchi lakini na mtu mmoja mmoja.

"Biashara ambayo CPB inafanya hatuwezi kumlalia mkulima au mfanyabiashara wa mazao, Sisi lengo letu, Sisi tupate na nyie mpate,alisema Mwenyekiti huyo wa Bodi.

Aidha Awadh amesema CPB ina maghala ambayo hutumia kuhifadhia mazao na bidhaa zao, hivyo wanafanya pia biashara ya kuhifadhi mazao katika maghala hayo ambayo yapo katika Mikoa mbalimbali.

vilevile Mwenyekiti huyo amesema kuwa CPB pia inatafuta masoko kwa Wakulima kama wanunuaji lakini kuwatafutia wakulima na wafanyabiashara kuwa inganisha na masoko ya nje.

" CPB inaongezea thamani mazao kwa kuchakata mazao kama Mpunga, Mahindi, Ngano, Alizeti na Siagi kupitia Viwanda vya CPB vilivyopo katika baadhi ya Mikoa ikiwemo Iringa,"amesema Mwenyekiti huyo akiwataka wafanyabiashara na wakulima wa mazao watumie fursa hiyo ili kuinuana kiuchumi.

Mwenyekiti huyo pia amesema katika kujiimarisha katika uchakataji wa mazao wanatarajia kujenga viwanda vingi zaidi katika Mikoa mbalimbali.

Ametaja Mikoa ambayo tayari kuna viwanda vya kuchakata mazao kuwa ni , Dodoma ambapo kuna kiwanda cha kuchakata Mahindi na Alizeti.

Mikoa mingine ni Arusha kuna kiwanda cha kuchakata Mahindi na Ngano, Iringa kiwanda cha kuchakata Mahindi, Mwanza kiwanda cha kuchakata Mpunga na Dar eslaam kuna Kiwanda cha kuchakata Siagi ya Korosho.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa  Iringa Elia Luvanda  ambaye alifungua kikao hicho aliitaka CPB kuangalia uwezekano wa kujenga kiwanda cha unga wa lishe kwaajili ya wanafunzi mashuleni.

"Unajua ukanda huu wa Nyanda za juu kuna tatizo la watoto kukosa lishe,hivyo niwaombe CPB mbali na kufanya biashara ya mazao,wajenge kiwanda cha kutengeneza lishe ili watoto wetu waondokane na utapiamlo', amesema Luvanda.

VvBjanaJG56ao katika kikao kilichofanyika Jana Iringa

Nnnnm
Hawa no wadau nbNnUeudJh katika kikao cha wadau wa mazao na CPB kilichofanyika Iringa janaa
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger