Friday 14 April 2023

WANANCHI WAMPONGEZA MBUNGE WA JIMBO LA KISHAPU BUTONDO KUTUMIA FEDHA VIZURI ZA MFUKO WA JIMBO KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

...

 

Wananchi wa Kishapu wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo kwa mgawanyo mzuri wa Fedha za mfuko wa jimbo kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kuangalia hasa sehemu zenye uhitaji.

Shukurani hizo wamezitoa leo mbele ya Katibu wa Mbunge kwenye hafla fupi ya kukabidhi Saruji pamoja na Bati kwajiili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Kishapu

Diwani wa Kata ya Kishapu Mhe, Joel Charles Ndettoson ameishukuru Ofisi ya Mbunge kwa kuendelea kuunga juhudi za wananchi wake kwa kuwapatia saruji mifuko 50 kwaajili ya ujenzi wa darasa katika shule ya Msingi Lubaga

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kupitia Mfuko wa Jimbo ameweza kusaidia kata ya Kishapu, hii ni awamu ya tatu sasa kwa awamu hii ameweza kutusaidia mifuko 50 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya msingi Lubaga, Mwaka jana alitupatia Bati 62 na Mifuko 50 ya Saruji, Mwaka juzi alitupatia Bati 100 kwa hiyo mfuko wa jimbo unaendelea kupunguza changamoto kwa jamii pia nimshukuru sana Mheshimia Rais kwa kuendelea kutupatia fedha kupitia mfuko wa Jimbo 

Naye Diwani wa Kata ya Lagana Mhe, Luhende Sana amesema kuwa Mfuko wa Jimbo umekuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi hasa wanapojitolea nguvu zao katika kunyanyua maboma na kuona juhudi zao zinaungwa mkono kupitia mfuko wa Jimbo kwenye hatua za ukamilishaji

Kwanza nimshukuru Mhe. Mbunge ndugu yangu Boniphace Butondo kwa kuona Lagana ni miongoni mwa kata ambazo zinasitahili kupata mgawanyo wa mfuko wa Jimbo hii inaleta hamasa kubwa sana kwa wananchi ambao wanajitolea nguvu zao pindi wanapoona hatua za ukamilishaji wa mabona unafanyika hii itasaidia sana kwa wananchi kuwa wazalendo katika kuchangia nguvu zao kwenye miradi ya maendeleo. Kwa kata ya Lagana tumepata mifuko 150 ya saruji pamoja na Bati 46

Aidha katibu wa Mbunge Ndugu, godfrey Nchimika ametoa wito kwa watendaji wote wanaohusika na Utekelezaji wa miradi kuwa wazalendo kwa nchi yao na hasa katika usimamizi wa miradi ili iweze kukamilika kwa wakati pamoja na utunzaji wa vifaa kwa uaminifu ili usitokee upotevu wa vifaa vya ujenzi.








Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger