*Matapeli kutuma ujumbe mfupi waibukia Viwanja vya ndege
Na Chalila Kibuda,
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imetoa wito kwa wadau wa posta wenye leseni kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu, kanuni na sheria pamoja na kuhuisha leseni zao ili wafanye kazi zao kwa ufanisi na kutambulika zaidi.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Meneja TCRA Kanda ya Mashariki Ikuja Jumanne katika utoaji mafunzo kwa wadau wa posta kupitia kampeni walioanzisha ya kutambua umuhimu wa kukata leseni na ambao bado wakate kwani itawasaidia kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi.
Aidha amesema kuwa elimu hiyo imekuja kutokana na uwepo wa malakamiko ya wateja kupotelewa na vipeto na vifurushi vyao kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha hivyo kutapeli watu na kushindwa kujua wamdai nani.
Hata hivyo amesema kupitia kampeni walioanzisha ya “Tumachapuchapu kwa Usalama “ itawezesha elimu kuwafikia wananchi wengi kupitia vipeperushi, vyombo vya habari, vituo vya usafiri na elimu zinazoendelea kutolewa na TCRA ili kupunguza wimbi la upotevu wa vipeto na vifurushi.
Ameongeza kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) haihusiki tu na usimamizi wa Mawasiliano bali pia wana kitengo cha posta ambacho hushughulikia utumwaji wa vipeto vyenye kilogramu 2 na vifurushi vyenye kilogramu 30 ndani na nje ya nchi kupitia kampuni zilizosajiliwa na mamlaka hiyo.
Amesema kuwa kuanzishwa kwa kitengo hich cha posta kumewezesha ongezeko la pato la taifa kkutokana na kusajiliwa kwa nakampuni hayo ya utumaji vifurushi na vipeto pamoja na kuongeza ajira kwa watanzania.
Kwa upande wao wada wa posta walioshiriki katika mafunzo hayo wamemshukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kwa kuwapatia elimu hiyo ambayo itasaidia kutatua changamoto mbalimbali walizokuwa wanakumbana nazo wakati wa utumaji wa vipeto na vifurushi.
Hatahivyo wameiomba Mamlaka hiyo kuendelea kushirikiana na wadau hao wa posta katika kukabiliana na wimbi la watu wasiofuata taratibu za usajili ambao huwasababishia usumbufu pindi mteja anapopoteza kipeto au kifurushi na kushindwa kujua amdai nani kwani aliowapa watume hawajasajiliwa.
Meneja wa Basi la Gallaxy Magreth Kibiki amesema kuwa wapo watu hawana mabasi lakini wanafanyabiashara ya kusafirisha vipeto na kuleta usumbufu kwao wakati mzigo umepotea na kudai walipwe wakati hawana stakabadhi ya malipo ya basi husika.
Kibiki amesema wananchi wanatakiwa kuwa na uangalifu wa kutuma mizigo kwenda katika kampuni ambazo zinafanya biashara kwa ya kusafirisha vipeto kwa njia ya halali.
Afisa Mauzo na Masoko wa ATCL Hellon anasema kuwa wanapata changamoto na matepeli wanawatumia ujumbe mfupi kuwatumia watu kuwa na mzigo ATCL wakiomba watume fedha ambapo waliotumiwa ujumbe wanatuma na kuanza kufatilia ATCL kupatiwa mzigo na kuleta usumbufu kwao.
Amesema kuna baadhi wanasafirisha mizigo kwenda nje wanatumia mwanya wa abiria wasio na mizigo hali amabayo ni changamoto kwa wenye leseni kukosa kufanya biashara na hao baadhi ya watu wanaotumia fursa isiyo halali kwao.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Kanda ya Mashariki Mhandisi Jumanne Ikuja akizungumza na waandishi habari kuhusiana na wasafirishaji wa vipeto kufuata sheria jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watoa huduma za vipeto wakiwa katika mkutano wa elimu ya utoaji wa huduma hiyo iliyoandaliwa na TCRA Kanda ya Mashariki.
Afisa Masoko na Mauzo wa ATCL Hellon akizungumza kuhusiana na matapeli wanaowatumia watu ujumbe wa mizigo wakati wao wakiwa hawajafanya huduma kwa mhusika ambaye alitumiwa ujumbe, jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Basi la Gallaxy Magreth Kibiki akizungumza kuhusiana na TCRA kuwasaidia kwa watu wanaofanya biasharara ya kusafirisha vipeto bila kusajiliwa, jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment