Monday, 10 April 2023

MWENYEKITI AUAWA BAADA YA KUNASWA NA MKE WA MTU MADAI WAKIELEKEA GESTI KUPAKUA ASALI

...
 

Na Daniel Limbe,Chato


WAKATI waumini wa dini ya kikristo duniani kote wakiendelea kusherehekea Sikukuu ya Pasaka,  wilayani Chato mkoa wa Geita kumetokea mauaji ya Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwabazengi, kata ya Muungano,Robert Msodock, baada ya kukutwa akiwa na mke wa mtu.

Imedaiwa kuwa chanzo Marehemu kuuawa ni wivu wa mapenzi, baada ya John Mbonge kumfumania akiwa na mke wake jana kwa kile kilichoelezwa kuwa walikuwa wakielekea nyumba ya kulala wageni kwenye kijiji cha Itale Branchi (Kahumo).

Habari zinasema kuwa marehemu amekuwa akifanya uzinifu na mke wa mtu tangu mwaka 2018 na kwamba kabla ya umauti huo tayari alikuwa ameshafumaniwa mara mbili.

Imedaiwa kuwa pamoja na fumanizi hizo,alikuwa akilipa faini ya fedha ikiwa ni adhabu ya kushiriki tendo la ndoa na mke wa mtu.

Katibu wa ulinzi wa Jadi, (Sungusungu) kijiji cha Itale Stoo, Enos Joseph,anakiri kuwa marehemu amekuwa akifumaniwa mara kwa mara na kwamba fumanizi lililosababisha kifo chake ni la awamu ya tatu.

"Ni kweli marehemu ameshafumaniwa mara mbili na hili tukio ni la tatu, baada ya kupewa taarifa za kuwa amefumaniwa jana, mimi na viongozi wenzangu wa sungusungu tulikwenda eneo la tukio kwaajili ya kumkamata, tulipofika pale tulimkuta amelala chini akiwa hai lakini hali yake ilikuwa mbaya sana,nilimuuliza kama ananijua akajibu ndiyo wewe ni Eno.

"Baada ya kunitaja jina nilimuuliza imekuwaje? akaniambia kutongoza wake za watu ndiyo imenifanya kuwa hivi, nikamuuliza tena simu yako iko wapi akasema John ndiyo kaichukua baada ya kunikatakata na mapanga, baada ya maneno hayo hakuongea tena tukamchukua na kumkimbiza hospitali ya wilaya ya Chato kwa matibabu"amesema Joseph.

Amesema wakiwa hospitalini hapo muuguzi aliyewapokea alimpima mgonjwa wao kisha kuwajulisha kuwa ameshafariki dunia baadae akapelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

Mwenyekiti wa kijiji cha Itale Stoo, Njingo Lubinza, amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo huku akidai limetokea akiwa safarini.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, ACP Safia Jongoamekiri kuwepo kwa tukio la mwenyekiti huyo kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kukutwa akiwa amesimama na mke wa mtu, huku akidai hajapewa taarifa za kifo cha majeruhi huyo.


"Nilipewa taarifa za mwenyekiti huyo kujeruhiwa vibaya upande wa paja la kulia,mkono na kichwani kutokana na wivu wa mapenzi na kwamba hali yake ilikuwa mbaya, taarifa za kuwa ameshafariki hizo nilikuwa bado sijatumiwa", amesema Jongo.

 Hata hivyo amesema kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo alikimbia baada ya kutenda kosa hilo na kwamba jeshi la polisi linaendelea kumtafuta.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger