********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Klabu ya Simba Sc imeshindwa kufanya vizuri katika mchezo wake wa pili Ligi ya Mabingwa Afrika mara baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy licha ya mchezo wa mwanzo kuondoka na ushindi wa mabao 2-0 ungenini.
Simba iliingia uwanjani ikiwa na faida ya mabao mawili mbele hivyo walikuwa wanahitaji sare ama ushindi wowote waweze kwenda hatua ya makundi.
Simba ilikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Larry Bwalya na kuwapeleka kipindi cha kwanza wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0.
Kioindi cha pili Simba Sc ilicheza mchezo ikiwa inaonekana kama imelizika kwa ushindi huo hivyo Jwaneng Galaxy wakapata bao dakika ya 47 ya mchezo na kuwaongezea motisha katika mchezo huo.
Simba Sc ilifanya mabadiliko ya wachezaji kadhaa ili kuona namna gani wanaweza kuondoka na ushindi katika mchezo huo bila mafanikio kwani Jwaneng Galaxy walipata bao lingine la pili dakika ya 68 ya mchezo.
Zilikuwa zimesalia dakika 4 pira kumalizika Jwaneng Galaxy wkaapata bao lingine dakika ya 86 ya mchezo na kuwahakikishia kwenda kwenye hatua inayofuata.
Mpaka mpira unamalizika matokeo kwa jumla yalikuwa 3-3, Jwaneng Galaxy wamesonga mbele kwa magoli mengi ya ugenini.
0 comments:
Post a Comment