Friday 29 October 2021

NYUKI WAKWAMA KWENYE MKONO WA MREMBO AKIWA NA MKOBA WENYE FEDHA NYINGI

...

Kulikuwa na tukio la kushangaza Jumatano, Oktoba 27,2021 mjini Machakos nchini ambapo kundi (bumba) la nyuki walipomvamia mwanamke punde baada ya kushuka matatu (gari la abiria).
 
Katika picha zilizozagaa mitandaoni, nyuki hao wanaonyeshwa wakiwa wamekwama kwenye mkono wake wa kulia wa mrembo huyo.

 Kulingana na walioshuhudia kisa hicho kisichokuwa cha kawaida, mara baada ya mwanamke huyo kushuka kutoka kwenye gari lililokuwa limetoka Kaunti ya Kitui, alivamiwa na nyuki hao.

Gazeti la Taifa Leo linaripoti kuwa polisi walijaribu kuwaondoa nyuki hao lakini juhudi zao hazikufua dafu walimkwamilia na hakuna hata mmoja aliyeng’oka mkononi mwake. 

Umati mkubwa wa watu ulikusanyika katika eneo la tukio kujionea maajabu wengi wakisema yalitokana na uchawi.

 Kisha baadaye mwanamke huyo aliondolewa katika eneo la tukio na dereva flani ambaye hakutambuliwa na kutoweka kusikojulikana.

 Hali hiyo iliwafanya wengi kushuku kuwa walikuwa pamoja huku wengine wakisema mkoba aliokuwa amebeba mrembo huyo ulikuwa umejaa pesa na ndiyo maana nyuki hao walitumwa kumlinda asipokonywe.

Baadhi nao walidai kuwa mkoba huo ulikuwa na mali ya wizi zikiwemo nguo na pesa.

Chanzo- Tuko News

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger