Thursday 28 October 2021

Kimenuka! RC MJEMA AAGIZA DIWANI NA AFISA MTENDAJI WA TINDE WASHUGHULIKIWE

...
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya afya ya msingi kuhusu tathmini ya utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko 19 leo Oktoba 28,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya afya ya msingi kuhusu tathmini ya utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko 19 leo Oktoba 28,2021. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ameagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kinidhamu Diwani wa Kata ya Tinde halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Jafari Kanolo na Afisa Mtendaji wa Kata ya Tinde Latifa Mwendapole kwa kufanya upotoshaji kuhusu Chanjo ya Uviko - 19.

Mhe. Mjema ametoa agiza hilo leo Oktoba 28,2021 wakati wa Kikao cha kamati ya afya ya msingi kuhusu tathmini ya utoaji wa chanjo dhidi ya Uviko 19 kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Amesema wapo baadhi ya Wanasiasa na viongozi ambao wapo mbele kusema chanjo ya COVID haitafanikiwa na kuhamasisha watu wasipate chanjo kitendo ambacho ameeleza kuwa hatakubali kuona kinaendelea mkoani Shinyanga . 

"Diwani  wa kata ya Tinde na Mtendaji wa kata yaTinde wanatukwamisha na kufanya upotoshaji kuhusu Chanjo ya Covid 19 hatua naagiza hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.
Naomba hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao, na hii iwe fundisho kwa watu wengine, hatuwezi kuona watu wanapotosha tukawaacha hivi hivi”,amesema Mjema.

“Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameleta chanjo ya UVIKO 19 ili wananchi wapate kujinusuru dhidi ya ugonjwa wa Corona. Mhe. Rais kaleta chanjo ili wananchi wawe salama. Rais anapotoa chanjo hizi, anapoleta chanjo anataka maendeleo”,amesema Mjema.

“Tumemaliza chanjo ya COVID awamu ya kwanza lakini awamu ya pili chanjo zingine zimeletwa, wale ambao hawajapata chanjo naomba wajitokeze wapate ili kujinusuru na Uviko 19”,ameongeza.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger