Friday, 29 October 2021

FACEBOOK YABADILI JINA SASA NI 'META'

...

Facebook imebadilisha jina lake la kampuni na kujiita Meta ikiwa ni mpango wake wa kujiimarisha sokoni.

Kampuni hiyo imesema ni heri kuweka huduma zake katika sehemu moja ili kuwavutia wateja zaidi katika mitandao ya kijamii katika vitengo vya uhalisia ulioigwa {Virtual Reality}.

Mabadiliko hayo hayatashirikisha mitandao ya watu binafsi kama vile facebook , Instagram na Whatsapp isipokuwa kampuni inayomiliki huduma hizo tatu..

Hatua hiyo inajiri kufuatia msururu wa habari zinazoipatia sifa mbaya Facebook , zinazotokana na nyaraka zilizovujishwa na wafanyakazi wake wa zamani.

France Haugen ameishutumu kampuni hiyo kwa kuzingatia sana kuhusu 'faida badala ya usalama wa wateja wake'.

Mwaka 2015, Google ilibadili jina la kampuni yake na kujiita Alphabet, hata hivyo jina hilo halijatambulika.

Mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg alitangaza jina hilo jipya wakati alipokuwa akizindua mipango ya kujenga "metaverse" - ulimwengu wa mtandao ambapo watu wanaweza kushiriki katika michezo, kufanya kazi , kuwasiliana katika mazingira yalioigwa na yasio na uhalisi kwa kutumia vitoa sauti vinavyovaliwa katika kichwa.

Amesema kwamba chapa iliopo haiwezi kuwakilisha kila kitu tunachofanya hii leo, sio tu katika siku zijazo na hivyobasi kuhitajika mabadiliko.

'Kwa muda sasa, natumai kwamba tutaonekana kama kampuni ya Metaverse na nataka kuongoza kazi yetu na utambulisho wetu katika kile tunachojenga' , aliambia mkutano uliofanyika katika video.

'Hivi sasa tunatazama na kuripoti kuhusu biashara kama kampuni mbili tofauti , moja ikiwa familia yetu ya programu na nyengine kuhusu kazi yetu katika mitandao tofauti katika siku zijazo'.

'Katika hilo ni wakati kupata chapa mpya ya kampuni ili kujumuisha kila kitu tunachofanya , ili kuonesha sisi ni akina nani na kile tunachotumai kujenga'.

Kampuni hiyo pia ilizindua nembo mpya katika makao yake makuu katika eneo la Menlo Park , California siku ya Alhamisi, ikibadilisha nembo yake ya thumbs-up "Like" na umbo la rangi ya bluu.

Bwana Zuckerberg alisema kwamba jina hilo jipya litatafakari nembo hiyo wakati unapokwenda, na kwamba wateja hawatahitaji kutumia facebook kutumia huduma nyengine za kampuni hiyo.

Jina Meta linatoka kutoka katika neno la Kigiriki 'meta' ikimaanisha 'zaidi'.

Kwa mtu kutoka nje , metaverse inaweza kuonekana kama mtindo mwengine wa VR lakini wengine wanaamini huenda ikawa ndio mpango wa siku zijazo wa intaneti.

Badala ya kuwa katika Kompyuta , watu katika metaverse watatumia Headset kuingia ulimwengu usio halisi na kuunganishwa katika mazingira yote ya kidijitali.

Inatumainiwa kwamba ulimwengu usio halisi wa VR huenda ukatumika kwa chochote kuanzia kufanya kazi , kucheza michezo pamoja na kujiunga na matamasha hadi kuwasiliana na marafiki na familia. Facebook imesema kwamba inalenga kuanzisha kuuza hisa zake chini ya jina jipya la MVRS kuanzia tarehe mosi Disemba.

Chanzo - BBC Swahili
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger