Wednesday 27 October 2021

BENKI YA CRDB YAKABIDHI PIKIPIKI KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA KAGERA

...

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera  Meja Jenerali Charles Mbuge ambaye ni mkuu wa mkoa huo katikati ya pikipiki akizungumza baada ya kupokea pikipiki kutoka Benki ya CRDB

 Na Ashura Jumapili, Kagera

BENKI ya CRDB mkoani Kagera wamekabidhi pikipiki tatu kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Kagera  Meja Jenerali Charles Mbuge ambaye ni mkuu wa mkoa huo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama mkoani humo.

Akiongea wakati akikabidhi pikipiki hizo Meneja wa Kanda ya ziwa wa Benki ya CRDB Lusingi Sitta amesema wamekuwa wakishirikiana na serikali kuboresha miundombinu ya usalama wa wananchi.

Sitta amesema wametoa usafiri wa pikipiki kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya ulinzi na usalama wa Wananchi Mkoani humo.

Amesema CRDB kama mdau mkubwa wa maendeleo ya serikali  wameamua waanze kutoa usafiri wa pikipiki ambazo zitasaidia kuimarisha ulinzi mkoa wa Kagera.

Amesema benki hiyo ipo karibu na uongozi wa mkoa na kumtaka mkuu wa mkoa popote panapokuwa na shida afike na watamjibu kwa wakati.

Amesema pia benki hiyo ipo karibu na wananchi kwa kutoa misaada mbalimbali ikiwemo ya fedha kwa wahitaji na huduma za mikopo kwa jamii yenye riba nafuu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge, amesema ameshapokea pikipiki nyingine saba na leo amepewa tatu ambapo moja amemgawia Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kagera.

Amesema pikipiki hizo zitasaidia askari kufika kwa haraka maeneo ambayo gari hazifiki baada ya kupata taarifa za matukio ya uhalifu.

Mbuge, amesema amani na utulivu unategemea jeshi la polisi kuimarisha ulinzi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Jumaa Awadhi , amesema anaishukuru  Benki ya CRDB kwa msaada huo.

Kamanda Awadhi, amesema bila kuwepo usalama uchumi wa nchi hauwezi kuwepo.

Alisema watatumia hizo pikipiki kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger