Wahitimu wakiwa kwenye mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata - SFS VTC
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumla ya Wasichana 125 wanaosomeshwa na Shirika la KIWOHEDE wamehitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata ( St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) Kahama mkoani Shinyanga.
Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC) yaliyotanguliwa na Adhimisho la Misa Takatifu ikiongozwa na Padre Vicent Mokaya yamefanyika leo Jumamosi Oktoba 2,2021 katika chuo hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele.
Akizungumza wakati wa Mahafali hayo Mgeni Rasmi Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga Paul Mangu Mabelele amelishukuru Ameyashukuru Shirika la KIWOHEDE na mashirika mengine ikiwemo FHI 360, Compassion, PACT na ETC kwa kazi nzuri wanayoifanya kuwezesha wanafunzi wa kike kusoma katika chuo cha Veta SFS VTC Mwakata hali inayokifanya chuo hicho kukua kwa kasi na kuwapa nguvu ya kuongeza udahili.
Mabelele ametumia fursa hiyo kuiomba serikali kuangalia njia bora zaidi ya kusaidia wanafunzi wanaotoka vyuo vya ufundi stadi VETA kwa kuwapatia vifaa vya kufanyia kazi badala ya kuwapa fedha za mikopo.
“Sisi watu wa VETA hatuoni tija kuwapa fedha wanafunzi hawa, badala ya kufanya kazi aliyoisomea anaanza kufanya uchuuzi. Tunaomba mtengeneze mpango mwingine, wanafunzi hawa wanaotoka VETA wapewe vifaa vya kufanyia kazi. Tunaomba mtupe vifaa kwani fedha zinaleta changamoto nyingi”,amesema.
Mtazamo wa kazi ambazo ni za wanaume tu siyo sahihi, hivyo sasa hakuna kazi ambayo haiwezi kufanywa na wanawake.
“Tunaomba pia wanafunzi wanapojiunga na masomo washauriwe kusoma pia masomo ambayo yanachukuliwa kuwa ni masomo ya wanaume tu, mfano fani ya ufundi magari na umeme. Tuangalia mazingira sawa, ili kila fani iwe na watu wa kuweza kuzifanya badala ya kusema kuwa baadhi ya fani ni kwa ajili ya wanaume tu”,ameongeza.
Mabelele amewataka wahitimu pindi wanaporudi kwenye familia zao wasiende kupumzika nyumbani kwani hali hiyo inadumaza taaluma yao.
“Msiende kupumzika nyumbani, ufundi usipoufanyia kazi unarudi nyuma, tumieni muda wenu vizuri.Mkitoka hapa nendeni mkafanye kazi. Huko mnakotoka kuna vijiwe, nendeni hata mkaombe kujitolea kufanya kazi na mafundi mahiri, watawajengea uwezo zaidi badala ya kukaaa tu nyumbani”,ameongeza.
Aidha amewataka wahitimu hao wawe mabalozi wa kuhamasisha jamii kupeleka watoto wao kwenye vyuo vya ufundi kwani takwimu zinaonesha vijana wengi wanamaliza shule lakini wapo tu mtaani hivyo ni vyema waende chuo kupata mafunzo hali itayowasaidia kujiari na kuajiri wengine.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la KIWOHEDE Justa Mwaituka amesema Shirika hilo linasomesha wasichana kutoka Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga na Ikungi mkoani Singida ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kuwezesha Wanawake na Wasichana Balehe ili kufikia usawa wa kijinsia kwa ufadhili wa UNFPA, UN Women na KOICA.
“Lengo la mradi huu wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2020 hadi 2022 unaotekelezwa katika halmashauri ya Msalala na Ikungi ni kupinga ukatili wa kijinsia,kuunda klabu za wasichana na kuimarisha kamati za ulinzi na usalama kwa wanawake na watoto”,amesema Mwainuka.
“Wasichana hawa 125 waliohitimu mafunzo ya VETA kati yao 75 wanatoka Halmashauri ya Msalala na 50 kutoka Halmashauri ya Ikungi. Hili ni kundi la pili la mabinti walionufaika na mafunzo ya Stadi za kazi kama njia ya kujikwamua kiuchumi, kupinga mimba na ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia”,ameeleza.
Ameongeza kuwa mara baada ya mabinti hao 125 kuhitimu mafunzo,mabinti wengine 125 kutoka Halmashari ya Msalala na Ikungi watajiunga chuoni hapo ikiwa ni awamu ya tatu kwa shirika la KIWOHDE kupeleka wasichana katika chuo cha SFS VTC Mwakata Kahama.
Amesema wasichana hao wanatoka katika vijiji sita vya kata tatu za Halmashauri ya wilaya ya Msalala ambazo ni Shilela, Lunguya na Bugarama na vijiji vinne kutoka halmashauri ya Ikungi kwenye kata za Irisia na Sepuka.
“Ninaushukuru sana kwa uongozi wa chuo cha SFS VTC kwa jinsi mmeweza kulea vijana, wamejiamini, wamejifunza mambo mengi ambayo yatawasaidia katika maisha yao. Tunawashukuru pia wadau tunaoshirikiana nao likiwemo shirika la FHI 360 ambayo tumefanya nayo kazi kwa muda mrefu”,amesema Mwainuka.
Afisa Maendeleo wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Friday Zacharia kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo amesema Shirika la KIWOHEDE limesaidia kupunguza mimba za utotoni na kujiajiri na kwamba halmashauri yao ipo tayari kuwakopesha vijana hao wakiwa kwenye vikundi ili kuwawezesha kiuchumi hivyo amewataka kutengeneza katiba za vikundi vyao
Afisa Mtendaji wa Kata ya Lunguya Lusajo Manase kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala amekishukuru Chuo cha SFS VTC kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa vijana akisema kinafanya kazi kubwa ya kusaidia mabinti kujiajiri na kujiinua kiuchumi.
“Shukrani zingine ni kwa shirika la KIWOHEDE kwa kazi kubwa ya kubaini mabinti na kuwawezesha elimu mabinti ili waweze kujitegemea na kujipatia mapato. Kazi ya serikali ni kuwawezesha kupata mikopo ili kuendeleza kile mlichokisoma. Sisi kama halmashauri ya wilaya ya Msalala, tunatoa mikopo ambayo haina riba kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu",amesema.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC)Padre Thomas Njue amelishukuru Shirika la KIWOHEDE kwa kukiamini chuo hicho na kuendelea kuwapelekea wanafunzi kila mara.
“Tunawashukuru kwa kutuamini hii ni awamu ya tatu mnatuletea vijana hawa ili waweze kufikia malengo yao. Sisi kazi yetu ni kuwalea hawa mabinti. Katika kipindi cha miezi 6 ya mafunzo wameimarika kimwili, Kiakili na kiroho. Tunawaomba KIWOHEDE waendelee kutuletea watoto”,amesema Padre Njue.
“Tunawapongeza vijana kwa kuhitimu mafunzo ya Miezi 6 na kumaliza mafunzo yao wakiwa salama, tumewafundisha mambo mengi, sasa mnamaliza Mnapokuwa nyumbani msikimbilie kuolewa, muda wa kuolewa bado sana, mnatakiwa muwe vizuri kwanza kiuchumi. Sisi kama chuo kama ulivyo utaratibu wa kuwafuatilia wanafunzi wetu kujua wanafanyeje, ili pale wanapohitaji msaada ili tuweze kuwasaidia”,amesema Padre Njue.
“Tusikae nyumbani na kukaa tu na kuolewa au kupachikwa mimba. Hili tulikatae , mimi napingana sana na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii”,ameongeza.
“Chuo chetu ni bora, chuo chetu kinasimamiwa na Kanisa hivyo watoto wakija hapa wanaimarika kiakili na kiroho. Naomba wananchi kukitumia chuo hiki kwa kuleta watoto wenu kwani jamii inayozunguka chuo ni wachache sana wanaleta watoto hapa”,amesema.
Akisoma Historia ya Chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 2003,Mwalimu Tawakal Seif amesema zaidi ya wanafunzi 5000 wamehitimu mafunzo mbalimbali na kuajiriwa na kujiajiri tangu kuanzishwa kwake huku ufaulu ukiongezeka kila mwaka na leo Wanafunzi hao 125 wamehitimu mafunzo ya fani mbalimbali ikiwemo ufundi umeme, Kompyuta, udereva, ushonaji, saluni na mapambo.
Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake,Minzula Shaban ameshukuru kwa mafunzo mazuri waliyojifunza chuoni huku akizitaja miongoni mwa changamoto zilizopo chuoni hapo ni vifaa vya kujifunzia na muda kujifunza kutotosha na changamoto ya mikopo pindi wanapomaliza masomo yao.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Padre Vicent Mokaya akiongoza Misa Takatifu wakati wa Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC) yaliyofanyika katika chuo hicho leo Jumamosi Oktoba 2,2021 ambapo jumla ya Wasichana 125 wanaosomeshwa na Shirika la KIWOHEDE wamehitimu mafunzo ya fani mbalimbali
Misa Takatifu ikiendelea wakati wa Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Misa Takatifu ikiendelea wakati wa Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Kwaya ikiendelea wakati wa Misa Takatifu katika Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Wahitimu wakiwa katika Misa Takatifu kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Wasichana 125 wanaosomeshwa na Shirika la KIWOHEDE waliohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata ( St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) Kahama mkoani Shinyanga wakiandamana kuelekea kwenye ukumbi wakati wa Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)

Wasichana 125 wanaosomeshwa na Shirika la KIWOHEDE waliohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata ( St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) Kahama mkoani Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele akizungumza kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele akizungumza kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mkurugenzi wa Shirika la KIWOHEDE Justa Mwaituka akizungumza kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mkurugenzi wa Shirika la KIWOHEDE Justa Mwaituka akizungumza kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi VETA wakimpongeza Mkurugenzi wa Shirika la KIWOHEDE Justa Mwaituka kwa kuwafadhili kusoma katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) Padre Thomas Njue akizungumza kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC)Padre Thomas Njue akizungumza kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Keki maaalumu kwa ajili ya Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele akimlisha keki mhitimu kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele akilishwa keki na mhitimu kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Wahitimu wakilishana keki kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Wasichana 125 wanaosomeshwa na Shirika la KIWOHEDE waliohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata ( St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) Kahama wakielekea jukwaa kuu kutoa burudani
Wasichana 125 wanaosomeshwa na Shirika la KIWOHEDE waliohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata ( St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) Kahama wakiimba na kucheza

Wasichana waliohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata ( St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) Kahama wakiimba na kucheza
Afisa Maendeleo wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Friday Zacharia akizungumza kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Afisa Mtendaji wa Kata ya Lunguya Lusajo Manase akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mratibu wa Mafunzo katika chuo cha SFS VTC, Charles Maganga akizungumza kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Wasichana 125 wanaosomeshwa na Shirika la KIWOHEDE waliohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata ( St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) Kahama mkoani Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Wasichana 125 wanaosomeshwa na Shirika la KIWOHEDE waliohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata ( St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) Kahama mkoani Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Wasichana 125 wanaosomeshwa na Shirika la KIWOHEDE waliohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata ( St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) Kahama mkoani Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Minzula Shaban akisoma risala kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Afisa mabinti balehe na kina mama vijana kupitia mpango wa DREAMS katika mradi wa EPIC unaotekelezwa na shirika la FHI 360, Agnes Junga akizungumza na Wasichana 125 wanaosomeshwa na Shirika la KIWOHEDE waliohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata ( St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) Kahama
Wasichana 125 wanaosomeshwa na Shirika la KIWOHEDE waliohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata ( St. Francis Vocation Training Center – SFS VTC) Kahama mkoani Shinyanga wakiwa kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Rais wa Serikali ya wanafunzo chuo cha SFS VTC Mwakata, Gasper John akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mwalimu Tawakal Seif akisoma Historia ya Chuo cha SFS VTC Mwakata Kahama kilichoanzishwa mwaka 2003
Wanafunzi wakitoa burudani ya Igizo kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Meza kuu wakiwa kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)

WAWATA na wazazi wakiwa kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)

Wanafunzi wa chuo cha SFS VTC wakiwa kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Wanafunzi wa chuo cha SFS VTC wakiwa kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Burudani ikiendelea
Wahitimu wakiimba wimbo kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Burudani ikiendelea
Burudani ikiendelea kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Burudani ikiendelea kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
WAWATA na wageni waalikwa wakicheza muziki kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Wahitimu chuo cha SFS VTC wakiwa kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Wahitimu chuo cha SFS VTC wakionesha namna ya kuunganisha umeme majumbani kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele (kulia) akikabidhi cheti kwa mhitimu kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)

Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele (kulia) akikabidhi zawadi kwa mhitimu kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)

Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele (kulia) akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi wa Shirika la KIWOHEDE Justa Mwaituka kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele (kulia) akikabidhi zawadi kwa Afisa mabinti balehe na kina mama vijana kupitia mpango wa DREAMS katika mradi wa EPIC unaotekelezwa na shirika la FHI 360, Agnes Junga kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Francis Vocation Training Center – SFS VTC)Padre Thomas Njue (kulia) akikabidhi zawadi ya cheti kwa Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele
Wanafunzi wa chuo cha SFS VTC Mwakata wakiwa kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)

WAWATA wakipiga picha na viongozi wa chuo kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele akipiga picha ya kumbukumbu na wadau na wafanyakazi wa chuo cha SFS VTC Mwakata kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele akipiga picha ya kumbukumbu na wadau kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele akipiga picha ya kumbukumbu Washereheshaji (Ma MC) kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele akipiga picha ya kumbukumbu na wadau Mabinti waliohitimu chuo cha SFS VTC Mwakata kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele akipiga picha ya kumbukumbu na wadau Mabinti kutoka Halmashauri ya Msalala waliohitimu chuo cha SFS VTC Mwakata kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo cha VETA Shinyanga, Paul Mangu Mabelele akipiga picha ya kumbukumbu na wadau Mabinti kutoka Halmashauri ya Ikungi waliohitimu chuo cha SFS VTC Mwakata kwenye Mahafali ya 17 ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Mwakata Kahama (SFS VTC).
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
0 comments:
Post a Comment