Saturday, 2 October 2021

MKUU WA MKOA AWASHTUA WAZEE WANAOITWA 'BABY' NA MABINTI WANAOWANYEMELEA KULA PESA ZAO

...
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Zuberi Homera amewatahadharisha Wazee kujiepusha na Mabinti ambao wanawanyemelea pindi tu wakipata viinua mgongo vyao baada ya kufanya kazi nzito kwa muda mrefu. Mhe Homera ameyasema hayo wakati akizungumza na Wazee katika Kijiji cha Ihahi Wilayani Mbarali.

"Mzee umefanya kazi kubwa, ukistaafu unakuta  Binti anakunyemelea, unamuacha Bibi pekee yake unakwenda kuchukua Binti mdogo. Wewe Babu ni Mzee lakini Binti anakuita Bebi! Bebi!, ujue hapo anataka hela yako. Hakuoni kama Wewe ni Bebi lakini pesa ile ndo Bebi. Anakuita Bebi si kwasababu ya ndevu na mvi ulizonazo, anakuita Bebi sababu ya pesa ulizonazo za kiinua mgongo baada ya kustaafu ualimu". Alisema RC Homera.

"Unamuacha Mzee mwenzako ambaye mlianza kuishi nae miaka ya 40 mmeishi pamoja, leo hii unamuacha na kwenda kuchukua Binti kadogodogo huko unakwenda kuishi nae. Matokeo yake unatengeza mazingira magumu kwa Bibi mwenzako na mwisho badala ya kuishi vizuri na yule Binti unaharibikiwa na kupoteza maisha". Aliongeza zaidi Mhe Homera. 

Mhe Homera ameendelea kuwaeleza Wazee hao kwamba vijana kwasasa ni Watukutu sana maana wakimng'ang'ania Mzee hawamwachi mpaka anapoteza maisha.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger