Saturday, 2 October 2021

Jeshi La Polisi Tabora Lawakamata Watuhumiwa 305 Kwa Makosa Mbalimbali

...


 NA LUCAS RAPHAEL,TABORA
Jeshi la Polisi mkoani Tabora limefakiwa kuwakamata watuhumiwa  305 wa kamakosa mbalimbali ya uhalifu kwa kipindi chaJanuari hadi  Septemba mwaka huu

Watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia misako mbalimbali inayoendeshwa na jeshi hilo katika wilaya zote 7 za Tabora ambapo watuhumiwa 127 wa kamaso ya vunjaji ,105 wa makosa ya mauaji na 73 ya ujambazi .

Akizungumza na waadishi wa habari ofisni kwake kamanda wa polis mkoani Tabora,Safia Jongo  alisema kwamba  matukio hayo yalikuwa ni kunzia januari hadi setemba mwaka huu .

Kamanda huyo alisema  wamefanikiwa kukamata silaha 54 ambazo ni AK.47 ,1,Gobole 30,Risasi 5,Shourtgun 13 na Bastola zilizotengenezwa kienyeji 11 na mitambo 5  .

Aidha alisema kwamba katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoani hapa lilimkamata mtuhumiwa mmoja katika kitongoji cha Miyenga Kijiji cha Mwakashidye kata ya Ibiri wilaya ya uyi Mkoani Tabora, akiwa na magunia ya bhangi 19 na vifurushi 3 vya akiwa na gunia moja la mbegu za bhangi ndani ya nyumba yake.

Hata hivo kamanda Safia Jongo   alisema mnamo tarehe 20 septemba mwaka huu katika Senta ya Mwanasi ndani ya hifadhi ya Igombe wilaya ya Uyuia Mkoani Tabora walifanikiwa kukamata watuhumiwa 3 wakiwa na gunia la bhangi.

Wakati huohuo jeshi la poisi mkoani hapa mnamo 18 septemba mwaka huu majira ya saa 15 .30 huko mtaa wa mlenda katika manispaa ya Tabora lilifanya upekuzi kwa mshitakiwa ambaye jina lake (limehifadhiwa ) walifanikiwa kupata silaha 1 aina ya Bastola ya Kimarekani yenye namba DAA317078 ambayo alikuwa akitumia katika matukio mbalimbali ya ujambazi wilaya za Kaliua,Urambo,Tabora na Nzega.

Kamanda huyo alisema alitoa onyo kwa waganga wa kienyeiji ambao hawana vibali vya kufanya shughuli zao lazima wafate utaratibu uliowekwa na serikali,kwani wao ndio chanzo cha kuleta mauaji kwa kupiga ramli chonganishi watakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Alitoa wito kwa wananchi waendelee kuwapa ushirikiano jeshi la polisi kwa kutoa taarifa sahihi za uhalifu ,kwani zoezi hilo la oparesheni ni endelevu na kuwataka wale wanajihusisha uhalifu msako unaebdelea juu yao.

Jeshi hilo lnaendelea kutoa tahadhali ya kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona (UVICO 19) kwa wavaa barakoa,kunawa mikono na sabuni kwa maji tiririka na kutumia vitakasa mikono na kuepuka mikusanyiko isikuwa ya lazima.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger